Prophet Hebron

Written by Super User on .

Ndugu msomaji usiogope, huu ndio ukweli halisi alioniambia mwenye kanisa, yaani YESU. Mengi utayakuta kwenye vitabu nilivyoviandika, CD na DVD. Hakika utafunguka ufahamu wako utajua jinsi KANISA lilivyotekwa na shetani. Na zaidi, YESU alipokuwa akinifundisha, alinionyesha na kunifunulia ulimwengu wote, jinsi ulivyo kwa sasa, akasema watumishi ndio wanatumiwa 98% kuliharibu KANISA. Kwa mfano aliniambia, idadi kubwa ya watumishi wakubwa ulimwenguni ni member wa freemason, akaniambia hao sio watumishi wake.

Haijalishi wanalitumia jina lake, hao ni manabii wa uwongo, na asili yao ni manabii wa uwongo, na mengine mengi utayakuta huku kwenye website na kwnye blog; YESU ameshuka Tanzania kupitia watu wake ila wale waovu wataangamia tu, shimo la moto linawasubiri. Kuzimu nimeshafunga milango ambayo watumishi na wachawi waliyokuwa wanapitia kwenda kuchukua nguvu hamna tena na hawana msaada tena. Mwisho wao umefika. Na sasa utukufu wa KANISA la mwisho umetimia, kuzimu haina nguvu na hawaliwezi KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. YESU aliponipa ujumbe huu, nilikuwa kazini Serengeti katika kazi niliyokuwa nafanya ya utalii (Professional Driver Guide), niliogopa sana maana sikuwahi kumuona YESU “live live”. Siyo kitu cha kawaida, ukuu wake unatisha. Mengi utayakuta ndani ya website hii na nitaendelea na kila ujumbe anaonipa kukufikishia wewe kwa njia hii. Ufunuo wa Yohana 1:8

KUMBUKA, HUDUMA YA MAOMBI NA UPONYAJI NI BURE (Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma,toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. Mathayo 10:8)

Siku za ibada.

  • Jumanne saa tatu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana – Ibada ya ukombozi
  • Ijumaa saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni – Ibada ya majibu
  • Jumapili saa tatu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana.

 

Pia, mafundisho na vipindi vya Mtume na Nabii Hebron vinapatikana katika blog, youtube na redio mbalimbali.

Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo.

"Come unto me, all you that labor and are heavy laden, and I will give you rest. Take my yoke upon you, and learn of me; for I am meek and lowly in heart: and you shall find rest unto your souls."

St. Mathew 11:28