Close

ALIYEMSALITI YESU AKAMATWA KUZIMU NA KUBOMOLEWA MAKAZI YAKE

ALIYEMSALITI YESU AKAMATWA KUZIMU NA KUBOMOLEWA MAKAZI YAKE

[ad_1]



















ALIYEMSALITI YESU AKAMATWA KUZIMU NA KUBOMOLEWA MAKAZI YAKE (YUDA ISKARIOTI) ALIYEKUWA MWANAFUNZI WA YESU KATI YA WALE MITUME 12.

Marko 14:(10-43)
Nakusalimu katika jina la YESU KRISTO WA Nazarethi. Kama nilivyokwisha kukueleza katika vitabu, makala, CD na DVD, YESU amenituma kuupindua ufalme wa shetani akiniongoza yeye na Malaika mkuu na Wazee 24 na serikali yote ya mbinguni nikishirikiana nao. Katika maisha yote, sikuwahi kuongea ma MUNGU, nilikuwa nkiongea na YESU tu, ila kwa mara ya kwanza ni August 2012.
Niliogopa sana, nyumba ikatetemeka, na watu wa nyumbani kwangu hata waliokuwa wakipika muda wa saa mbili usiku walishukiwa na uwepo na kuhisi kuna jambo litatokea. Watu wote walitetemeka kila mtu kivyake, na ndipo sauti ikasema nami. Usiogope, mimi ni BWANA MUNGU wako, leo nimekuja kusema na wewe mwanangu usiogope. Ila wakati anaongea, yaani ile sauti tu, niliumwa tumbo na wiki hiyo kwa ajili ya mshtuko nilipungua mwili kama kilo tatu au nne. MUNGU anatisha ukuu wake, wala siwezi elezea.
Akaniambia, nilikuumba ili uje ufanye kazi hii ya mwisho. Akaniambia, mikono yako ni mikono yangu, na kinywa chako kinachoongea au kutamka itakuwa hivyo hivyo, akaniambia, nimekuja kukutia nguvu. Nakupenda maana nimemtii na nimekubali anitumie, kwa moyo mweupe, akaniambia, nipo na wewe milele, mimi ni alfa na omega. Akaja tena siku nyingine kuendelea kusema nami na kunipa maelekezo ya jinsi anavyotaka nifanye na kuharibu kazi ya muovu.
Mpaka leo, ameongea na mimi mara 13 kwa muda mrefu. Muogopeni MUNGU siyo wa mchezo kama mnavyofikiria na hata watumishi baadhi yao wanamchezea. Ole wako, na ninanukuu amesema NENO lake halitapita, lazima litimie tu. Mnamo saa mbili usiku 10-12-2012, Yule aliyemsaliti YESU yaani Yuda Iskarioti alikamatwa rasmi na ufalme wake aliopewa au kulipwa na shetani ulibomolewa rasmi na sasa hayupo tena, yupo kifoni na amezikwa pamoja na mke aliyepewa na shetani.
Yuda Iskarioti, iliandikwa ya kuwa YESU atazaliwa, na atasalitiwa na ikatimia kama ilivyo NENO la MUNGU lazima litimie. Huyu Yuda baada ya kufa, shetani alimpatia vyeo na ufalme, na aliendeleza kazi ya usaliti kwa wanadamu. Kwa YESU kama ilivyo hivi leo, alikuwa na jeshi kubwa la mapepo na anayaongoza na yanamtii yale anayotaka aharibu kanisa kama alivyofanya kwa YESU. Alipokuwa mwanafunzi wa YESU, alijifunza mengi kuhusu yale YESU aliyowafundisha waukomboe ulimwengu. Siri hizo alizipeleka kwa shetani, na shetani akampa mamlaka na nguvu ili yale mafundisho ambayo YESU ameagiza yafuatwe, yeye akawavuvia na kuwaibia watumishi na kuwawekea kinyume, mfano ubatizo wa kikombe (maji) kichwani tu ni Yuda kauleta ili kupinga ubatizo ya Yohana na mambo ya kufanya nyumba ya MUNGU soko na machafu yote yeye ndiye aliyekuwa akifanya kazi hiyo na kutumia hizo roho na kuwa mmiliki wa baadhi ya dini ulimwenguni mwote. Ukisoma kitabu cha Ufunuo wa Yohana 22:(18-20) wote wanaokwenda kinyume na YESU, ole wao; yaliyompata Yuda Iskarioti ujue na wewe ndivyo ilivyo. Angalia na ujiulize wewe wewe binafsi, ubatizo wa maji ya kwenye kichwa umeandikwa kwenye Biblia?  Jibu ni haupo. Nakujulisha wewe hujabatizwa, haijalishi una cheo gani katika kanisa au eneo lolote. Tafuta kwenye kitabu cha muongozo wa Mungu yaani Biblia au tuseme ndiyo katiba ya YESU. Ameniambia, waambie wabatizwe kwa maji mengi, soma katika kitabu cha “UBATIZO WA KWELI KWA LIMWENGU WOTE”, utafunguka vizuri.
Nimekueleza kwa kifupi tu, yaani YUDA ndiye mharibifu wa kanisa na mpaka sasa, 98% YESU haonekani ulimwenguni mwote imebakia 2% ndio anaonekana.
Huyu Yuda alizika Biblia na kufanya watu wasiielewe wakiisoma, hata watumishi, ila wapo wanaojua wapo ma-Yuda kuharibu kanisa na kuhakikisha watu wanaangamia kwa kupotea ili wasiende pazuri Paradiso. YUDA alifanya kazi hii kama mzimu, na huyu nilikuta anaongoza na  kumiliki baadhi ya dini kubwa za Kikristo na kuzipangia mafundisho kwa namna ya kubadili ukweli na kwenda kinyume.
Kwa mfano, imeandikwa usiabudu sanamu. Yuda ameingiza katika dini hizo ili kuwafanya wanadamu wapigwe kama yeye. Jambo lingine ni kwa wale wanaobatiza kwa maji mengi, akawaongezea wakubatize kwa jina la mchungaji, halafu BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU. Na wewe uliyefanyiwa hivyo hujabatizwa, ni ubatizo feki, wala mbinguni haupo, upo kwenye mafaili ya Yuda Iskarioti, na wewe hautaenda mbinguni, na pia uliyebatizwa kwa jina la mchungaji wewe ni wa huyo mtumishi, na zaidi amekushika maisha yako na fahamu zako, huendi popote!
Fuata ubatizo wa YESU, angalia kama huo uchafu ulifanyika. Ole ya MUNGU juu yako unayetesa wana wa MUNGU. Huyu Yuda baada ya YESU kufa, aliongozana na wale mafarisayo kushona lile pazia la hekalu. Ilikuwa na maana kuwafungia watu wasimjue YESU ila pazia nimelipasua upya na sasa watu wote, ulimwengu wote, hawatadanganyika tena, ni mwisho na YESU anawapenda sana.
Mnaowaomba watakatifu waliokufa, ni makosa. Hata wenyewe wanawashangaa! Nimeongea nao, yaani hawana furaha. Imeandikwa, muabuduni MUNGU peke yake tu, usiabudu hata alichokiumba yeye. Yuda akawabadilisha kanisa, likaanza kuwataja na kuwaomba baadhi “uniombee kwa baba”; funguka ufahamu wako! YESU alitutumia msaidizi ambaye ndiye ROHO MTAKATIFU tu. Sasa nikuulize swali, Je, hawa watu wanaowaomba si watu kama wewe? Niliongea na mama yake YESU, analia sana watu wanapomwabudu yeye na kuacha kumwabudu YESU, mnaofanya hivyo mmepotea, mwisho wenu ni kuzimu na kuchomwa moto. Ni mengi sana nitaendelea kukufundisha ili umjue YESU ambaye ndiye njia ya uzima na ukweli Yohana 14:6 (zaidi soma sura yote). Kwa huyo aliyekuwa msaliti, sasa amefungwa na ufalme wake umebomolewa, na siri zote nimemnyang’anya , sasa mtafunguka. Ila wachawi, freemason na wengineo mtambue hivi: yaliyompata Yuda Iskarioti yanakuhusu wewe pia, asema BWANA MUNGU wa majeshi.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA IBADA YA LEO (SIKU YA BWANA) TAR. 23-12-2012.

Bibi huyu akimshuhudia MUNGU kwa matendo makubwa aliyotendewa katika mwili wake. Kwa miaka mingi alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo, miguu na misuli ya mikono kukaza, lakini MUNGU amemponya leo kupitia mwili wa mtumishi wake Mtume na Nabii Hebron papo hapo.

Dada huyu alikuwa akiumwa na viungo kwa muda mrefu akiwa anaombewa na Mtume na Nabii Hebron.

Baada ya maombi, dada alijikagua mwili wake, kwa kufanya kitu ambacho hakuweza kufanya kwa muda mrefu, mojawapo ikiwa ni kuchuchumaa kama anavyoonekana katika picha, huku akibubujikwa na machozi ya furaha.

Mtume na Nabii Hebron akiwa kwenye maombi ya kukagua waumini mmoja mmoja, kiti baada ya kiti kwa maombi kuhakikisha hakuna adui aliyeacha uovu ndani ya wana wa MUNGU.

Waumini kwa pamoja wakimtukuza MUNGU kwa nyimbo za sifa na kuabudu kwa matendo makubwa na makuu ambayo MUNGU ameyatenda siku ya leo. Wagonjwa wengi wameponywa, wenye vifungo wamefunguliwa, waliozikwa nafsi zao wamefufuliwa na kupewa tena uhai na kumtumikia MUNGU.

 Kwa mawasiliano;

+ 255 759 610 820
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149


Email:

[email protected]


Imeandaliwa na Priscus & Dorcas Macrine,

KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

[ad_2]