Close

BIBLIA YA SHETANI INATUMIKA KATIKA MAKANISA YA ULIMWENGU!!!

Kila mtu anajua biblia ni kitabu kitakatifu kilicho halilishwa na MUNGU peke yake na akalipiga muhuri ndicho kitumike kwa wanadamu na akaonya isibadilishwe jambo lolote wala kuongezewa (Ufunuo 22:18-19), na maneno tofauti na yaliyoandikwa katika biblia hiyo yasitumike na mwanadamu yeyote, biblia hii ndiyo katiba ya MUNGU aliyowawekea wanadamu wote na waifuate na siyo kitabu kingine chochote kile au imani tofauti na biblia takatifu.
Mpaka hapo umeelewa kuhusu biblia takatifu ya MUNGU aliye hai. Ila ujue pia ipo biblia ya shetani na biblia hiyo ya shetani imeandikwa na joka kuu na ndiyo inayotumika na kanisa la kuzimu na pia ndiyo biblia inayotumiwa na manabii wa uongo. Wanapewa katika ulimwengu wa roho na katika mwili utaona mtumishi anafundisha tofauti na biblia takatifu au Neno la MUNGU lisemavyo. Mfano katika biblia ya MUNGU ina sheria zake na biblia ya shetani inazo sheria zake ila zaidi katika biblia ya shetani inageuza vifungu vya mistari ya Neno la MUNGU na kwenda kinyume mfano ukisoma katika Wagalatia 1:6-8 utaona jinsi injili ilivyobadilishwa na ikawa ni ya namna nyingine, sasa hizi namna nyingine ndio imetoka katika biblia ya shetani ambayo haipo kimwili hapa ulimwenguni bali ipo kuzimu na mimi nimeiona kwa macho yangu baada ya YESU WA NAZARETI kunionyesha wakati akinifundisha neno lake na jinsi gani kweli ya MUNGU ilivyoachwa na makanisa yakageukia maneno ya biblia ya shetani, na kuwafanya mataifa wasimuone MUNGU katika maisha yao yote. Badala yake katika ule mwisho waingie katika uzima wa mauti ya milele sababu ndani ya mioyo ya watu ikiwa imejaa maneno ya biblia ya shetani watavuna uzima wa mauti.
Sasa uwaeleze Hebron watu wote wa mataifa na kuwafundisha waijue kweli yangu mimi YESU. Ni YESU niliyekufa kwa ajili ya mataifa yote na mimi ndiye neno na pasipo mimi hakuna atakayepona roho yake, na mimi ndiye chakula cha uzima yaani Neno langu ndiyo uzima. Sasa shetani amewapiga upofu watu akashirikiana na mpinga kristo wakaingiza biblia yao katika kanisa baadhi ya vifungu halafu mahali pengine ikafuatwa biblia sasa waeleze na mimi Hebron ninawaeleza ukweli wa Neno la YESU WA NAZARETI ili watu wote wamjue maana wengi wanaona wanamjua MUNGU kupitia Neno lake kumbe imekuwa kinyume, wanamjua shetani kwa kufuata biblia ya shetani.
Nitakutofautishia maneno baadhi yaliyopo katika biblia ya shetani na yanatumika makanisani na ukisoma katika biblia takatifu hayapo, na ukisoma jambo lolote linatumika katika kanisa lolote tofauti na biblia uelewe msingi wa kanisa hilo katika ulimwengu wa roho viongozi hao ndani yao ipo biblia ya shetani hivyo hayo yaliyo ujaza moyo wao ndio huyafundisha na kuwanajisi watu na wanapokea maneno ya shetani sasa na kuupokea uzima wa mauti ya milele pasipo kujua na kuangamia ila leo utapona.
KITABU CHA KUTOKA CHA SHETANI KILIVYOANDIKWA KUTOKA 20:1-26
1.     Joka kuu akanena maneno haya yote akasema. 2. Mimi ni bwana mungu wako niliyekutoa katika nchi ya misri katika nyumba ya utumwa. 3. Uwe na miungu mingi uiabudu nayo. 4. Ujifanyie sanamu za kuchonga kwa mifano ya vitu vilivyopo duniani 5. Na angani na chini ya maji uviabudu na kuvisujudia mimi ni shetani nisiye na wivu nawapenda wote waniabudio mimi kizazi cha kwanza hata cha nne nao. 6. Katika ule mwisho wataurithi uzima wa mauti niliyo nayo mimi shetani. 7. Ulitaje jina la mungu ovyo hata bila sababu. 8. Usiikumbuke siku ya sabato. 9. Fanya kazi siku zote. 10. Utamani vitu vya watu na pia mali zao hata wafanya kazi wao, usiwaheshimu baba yako na mama yako, uuwe, uzini, uibe, useme uongo.
Nimeelezea kwa ufupi jinsi biblia ya shetani ilivyo na ina vitabu 66 hivyo hivyo na ukisoma biblia takatifu katika kitabu cha kutoka 20: 1-26 ukilinganisha utaona katika makanisa wanayatenda hayo yaliyoandikwa katika biblia ya shetani, mfano kuabudu sanamu, au kuvifanya vitu baadhi alivyoviumba MUNGU na kuviita mungu, mfano nyota, mwezi, jua au hata wanyama. Mahali popote wanaoenda kinyume na biblia wajijue ndani yao umo uzima wa mauti ya milele. Shetani hiyo ndiyo mbinu nyingine iliyojificha ambayo siyo rahisi kujua ila YESU amenionyesha na mimi niwaeleze watu maana wengi mnampenda mnahangaika sana mkiona MUNGU amewaacha. Laa si kweli, tatizo lipo kwa viongozi wa makanisa waliotekwa na shetani wakajifanya ni watumishi wa MUNGU na kumbe ndani yao wamejaa maneno ya shetani.
Katika biblia ya shetani katika kitabu chake cha Mathayo wa kuzimu 28:19 inasema hivi: enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wa shetani mkiwabatiza kwa ubatizo wangu wa maji ya kikombe kichwani tu na wa maji mengi ila yawe ni ya kisima tu yasiyotembea, na mkiwabatiza kwa ubatizo wa majina yenu kwa maji mengi ili uwe tofauti na ubatizo wa huyo wa juu, ili kuhakikisha watu wote wanakuwa wanafunzi wangu na ule mwisho nijumuike nao katika mateso ya milele.
NOTE:
Tazama sasa makanisani wanavyobatiza tofauti na yeye aliye njia ya uzima alisema tufuate kweli yake, na njia zake. Kwa kifupi katika point ya ubatizo utafunguka wazi wazi na hakuna cha kujificha au kubisha, tafuta katika biblia takatifu hakuna maelezo kama hayo kuhusu ubatizo alioagiza MUNGU. Sasa hayo yametoka katika kitabu cha biblia ya kuzimu ili shetani awavune watu kama vile alivyowavuna na anavyoendelea na anawatumia watumishi aliowawekea mafunuo yake na wale wote wanaotumia akili zao kuifanya kazi ya kanisa pasipo kuongozwa na MUNGU aliye hai au wale ambao ni wachawi.
Na hii ndiyo sumu inayoua roho za wana wa MUNGU na ili mpone kataeni hayo mafundisho kabisa maana ni ya shetani na mnapoyatenda tayari na nyie mmekuwa ni wa shetani na MUNGU analiangalia neno lake.
Mfano:
1.     Katika biblia ya shetani imeandikwa ndoa ifungwe kwa agano la shida na raha.
2.     Utoapo sadaka yako ijulikane umetoa kiasi gani na uandike jina, na utoe sadaka ya fungu la kumi, shukurani, ujenzi, ahadi, collect na nyingine zitakazotokea.
3.     Ili uponywe toa pesa au sadaka, hakuna cha bure hiyo ndiyo fomula ya shetani na hata waganga wanatumia biblia hiyo hiyo ya shetani maana ndio mungu wao.
Hivyo mfunguke, ukiona mtumishi au kanisa lolote lipo tofauti na biblia takatifu kineno na kimatendo au linachanganya Neno la MUNGU na uongo, ujue hilo kanisa au huyo mtumishi msingi wake ni neno la uzima wa mauti wa shetani na yeye ni agent wa shetani na ndiye mpinga kristo. Ili uendelee kufunguka endelea kufuatilia vipindi vyangu na endelea kusoma blog yangu na vitabu vyangu utapona roho na kuwa mwana wa MUNGU aliye hai.

NABII HEBRON.