CHAPA YA MPINGA KRISTO (NAMBA 666) NI UBATIZO WA MAJI YA KIKOMBE KICHWANI (UFUNUO WA YOHANA 13:16-18).

CHAPA YA MPINGA KRISTO (NAMBA 666) NI UBATIZO WA MAJI YA KIKOMBE KICHWANI (UFUNUO WA YOHANA 13:16-18).

[ad_1]

HUYU NDIYE BABA YAKE WA KIROHO NABII HEBRON. (MOSES KULOLA- KULIA)

Naye atawafanya wote wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume au katika paji za nyuso zao. Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na aihesabu hesabu ya mnyama huyo. Maana ni hesabu ya kibinadamu, na hesabu yake ni mia sita sitini na sita.

Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron, huu ni wakati ambao YESU KRISTO wa Nazareti amewafunulia watoto wake wote katika ulimwengu wamjue yeye na wapone, japo sio wote watakaopona ndio maana kuna jehanam, na jehanam ipo kwa ajili ya wanadamu watakaomuasi MUNGU  au kwenda kinyume. Ila katika somo hili, nitaelezea kuhusu chapa ya namba 666 katika mkono na chapa ya namba 666 katika paji la uso.
Chapa ya namba 666 katika upaji wa uso ni ubatizo wa maji ya kikombe. Wanaomwagiwa wote wakiambiwa ndio ubatizo wa MUNGU. Huo sio ubatizo. Maana ya neno ubatizo ni kuzamishwa, sasa huku kumwagiwa maji kichwani na kwenye paji la uso ndio uambiwe ni ubatizo? Ubatizo huo ni uwongo 100%. Tafuta hata katika kitabu cha Biblia hautaona ubatizo uliofanywa kwa jinsi hiyo, na kama ulifanywa tofauti huo sio ubatizo. Haijalishi jina la YESU na ROHO MTAKATIFU linatajwa, huo ni ujanja wa kukupoteza wewe na kupigwa chapa katika paji lako la uso halafu unaambiwa huo ndio ubatizo.
Nimekwisha kukueleza maana ya neno ubatizo ni kuzamishwa. Sasa jiulize swali, je, kumwagiwa maji kichwani ndiyo umezamishwa? Jibu haujazamishwa, na kama haujazamishwa, ujue umepigwa chapa ya namba 666 ya mpinga KRISTO unatembea nayo bila kujua wala kupenda wewe mwanadamu. Zaidi soma kitabu cha Nabii Hebron (UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE) utajifunza mengi na kuelewa ili upone.
YESU ameniambia niwaeleze watu wote wa ulimwengu ukweli na wamjue yeye wapone. Injili ilianzia kwa watu weupe, ila imeharibikia huko na kubadilishwa na kuyasubirimapokeo ya wanadamu badala ya MUNGU kwa kubadilisha Neno la MUNGU alivyopanga na kupotosha ulimwengu. Na katika kitabu cha Ufunuo 22:18-20 ole wake atakayeongeza Neno la MUNGU katika kitabu hiki au kulipunguza.
Funguka ufahamu, huo sio ubatizo, unapigwa chapa ya mpinga KRISTO katika paji la uso wako kwa kudanganywa huo ndio ubatizo, huo sio ubatizo. Hiyo ni kazi maalumu kabisa ya kuwapiga chapa ya 666 wanadamu bila kujua na wengine hujua kabisa. Ikatae ubatizwe kwa maji mengi ufutwe hiyo chapa ya 666 katika paji lako la uso.
Jambo lingine, ni chapa ya namba 666 katika mikono ya wanadamu. Namba hizi ni pete zote za freemason wanachama, pete za kupewa na waganga wa kienyeji, pete za kutafutia bahati, riziki, pete za kukulinda kiuchawi, au upate madaraka fulani, hizo zote ndizo namba 666 ambazo wanadamu wamevaa chapa zake. Wengine wamenunua na kutoa makafara. Zaidi maana ya kuvaa pete hizo ni kuwa wewe unafunga ndoa na upo pamoja nao na umeolewa na shetani ndiye mume wako na mungu wako, hivyo anao uhalali wa kukumiliki. Funguka ufahamu hizo ndizo chapa namba 666 katika mikono ya wanadamu. Atakayeelewa aelewe, atakayekaza shingo yake kuwa ngumu atalia na kusaga meno.
Hata waliokufa na ubatizo huo na hayo mapete hawaendi mbinguni, wapo kuzimu wanateseka, nimewaona kwa macho yangu, YESU kanionyesha ni wengi hawahesabiki na wengi wao ni watu mashuhuri katika ulimwengu huu waliokufa; marais, viongozi wa dini, wanamuziki, wafanyabiashara, na walio kawaida katika maisha ya hapa duniani japo walifanyiwa mazishi ya kufana na ibada kubwa sana ila wamekataliwa, wanateseka mateso yasiyoelezeka na wanajuta hata wanatamani waje wawaambie watu wasivae hayo mapete na kupigwa chapa ya ubatizo kichwani. Ila haiwezekani. Jamani, watu wote badilikeni, mambo yameharibika; shetani analichezea pango la unyang’anyi (kanisa). Amelimiliki na kama amelimiliki hilo silo kanisa tena, linaitwa pango la wanyang’anyi. Funfuka ufahamu wako na wewe uliyeujua ukweli songa mbele usirudi nyuma, wafundishe na watu wengine wamjue YESU wa kweli, usiwe mchoyo wa kuwafundisha haya nikufundishayo ambayo mimi Hebron nafundishwa na YESU, ni ili ulimwengu umjue katika ukweli. YESU wa Nazareti amesalitiwa 98% katika ulimwengu mzima. Maneno hayo siyo yangu mimi Hebron, ni ya YESU pekee wala siongezi lolote. Akaniambia, msidanganyike na mtu yeyote anayejiita YESU na yupo hapa ulimwenguni. Huyo ni mwongo na ni adui yangu 100% wala simjui, ni kristo wa uwongo. Epukeni mtatekwa, ndani yao ni shetani yupo. Akaniambia mimi YESU nipokuwa hapa ulimwenguni (nilioa)? Nikamjibu hapana. Sasa mbona wengine wanajiita wao ni YESU na wameoa? Akaniambia ni uwongo mtupu, asije wadanganya mtu yeyote ajiite yeye ni YESU au ajiite MUNGU. Wakimbieni mpate kupona. Watu hao haijalishi wapo katika nchi gani, bara lolote, hao tayari shoka la MUNGU lipo juu yao ila muogope maana iliandikwa na lazima yatimie, na sasa yametimia maana Neno la MUNGU lazima litimie. Ujumbe huu ni wa YESU wa Nazareti, na mimi nimeufikisha kwako.

-Nabii Hebron.

[ad_2]