Close

HAYA NDIYO ALIYONIELEZA MAMA MARIA MAMA YAKE YESU WA NAZARETI ALIYE HAI

[ad_1]

SEPTEMBER 2013

Mnamo 2013, nilipokuwa katika maombi yangu binafsi na kuombea nchi ya Tanzania na mataifa yote yamrejee MUNGU ikiwa ina maana watu wote kwa rangi zote, ghafla nikapelekwa sehemu nyingine akaja Mama wa YESU WA NAZARETI akaniambia amani iwe nawe! Akajitambulisha akaniambia usiogope mwanangu mimi ni Mama yake YESU WA NAZARETI nimekuja kukutia moyo na kukuelekeza mambo ambayo alinieleza ambayo ni yangu peke yake. Akanishika mkono wangu na kulia na kuutikisa kwa furaha, akaniambia endelea kuifanya kazi aliyoianzisha mwanangu YESU, sasa hivi yeye yupo mbinguni na mimi pia nipo mbinguni. Nafurahi sana hata tunashangilia mbinguni maana wale watumishi ambao mwanangu aliwatuma wakaseme kweli ya MUNGU wetu wamemgeuka na kumfuata shetani wamebakia kutaja jina la mwanangu kwa mdomo tu ila ndani ya mioyo yao hawapo nae kabisa. Na sasa kazi ya MUNGU ilisimama kwa muda maana hakuonekana aliyemkubali 100% na sasa endeleza kazi ya MUNGU mpaka mwisho wake na kwa watu wote wa mataifa yote uyatende yale tu anayokueleza MUNGU na kukuongoza.
Akaniambia kipindi kile alivyokuwa na mwanae hapa duniani yeye aliangalia kusudi la MUNGU tu na alishinda na kipindi kile ilikua kimwili ila kwako wewe ni tofauti hautasulubiwa wala kuteswa na utapenya kila mahali atakapo MUNGU, wewe umeteuliwa uitetee injili na kuwakomboa watu wote wa ulimwengu. Akaniambia Hebron mimi ni binadamu tu kama wewe au wengine walioumbwa na MUNGU, mimi nilizaliwa na kufa kama binadamu wengine tu. Na mimi ninamuabudu MUNGU wangu kama wewe na kanisa lako mnavyomuabudu MUNGU aliye hai. Mimi niliishi maisha matakatifu na sasa nipo mbinguni na bado naendelea kumsifu na kumuabudu MUNGU wangu ambaye pia ndiye MUNGU unayemuabudu.
Akaniambia mwanangu Hebron nipo mbinguni nikitazama wanadamu moyo wangu unaniuma kwa ajili ya matendo wanayoyafanya, akaniambia wameacha kumuabudu MUNGU wananiabudu mimi mwanadamu kama wao. Waeleze ni machukizo makubwa mbele za MUNGU na waache kuniabudu mimi mwanadamu. Mimi sitaki kabisa niabudiwe, mimi siyo MUNGU, niliushinda ulimwengu kwa kuishi maisha matakatifu kama nilivyomfuata mwanangu njia zake hata mimi leo nipo nae huku mbinguni na bado namsujudia. Akasema kwa sauti ya uchungu na uliingia mpaka kwenye moyo wangu, mpaka leo hii ndio Napata amani baada ya kuandika kwa njia ya blog japo nilishautoa katika vipindi vya redio mbali mbali katika nchi ya Tanzania na Television.
Akaniambia imeandikwa usimuabudu au usiabudu kitu chochote tofauti na MUNGU peke yake. Waeleze ukweli waeleze wanapotea, watu wote wanaoacha kumuabudu MUNGU na kunitaja mimi, mimi siyo MUNGU wala sina mbingu yangu nipo kwa MUNGU wangu, nanachukia sana watu wanaponitaja na kuniabudu niwasaidie, niwajibu, niwaombee. Wanajiangamiza nafsi zao na kujichochea kwenda jehanamu.
Akaniambia Hebron wewe mwenyewe umepata neema kubwa sana ya kufundishwa na MUNGU mwenyewe, siku zote amekueleza ni yeye peke yake tu anayestahili kuabudiwa zaidi yake hakuna mwingine. Sasa tazama mwanangu Hebron kwa nini wanamkufuru MUNGU na ROHO MTAKATIFU? Nilikosa jibu japo nilikua najua hata ukimuabudu mama yake YESU ni dhambi.
a.      Akaniambia haya yafuatayo nitayasema ila hayo mengine sikuruhusiwa kuyasema. Hebron mimi nipo mbinguni nilikufa na kuzikwa nimeushinda ulimwengu na watu wote wafuate mfano wa YESU WA NAZARETI na uwaeleze kweli tupu maana neno lake limebadilishwa katika uliwengu wote ili watu wasiende mbinguni kama ilivyo hao ambao wananiabudu mimi Maria wasipoacha na kutubu tena na kuokoka wajue hukumu tayari ipo juu yao, ila wakitubu na kuokoka watapona, ila hao wote wanaoendelea kuniabudu mimi tayari hukumu ipo juu yao.
b.     Akaniambia mimi Maria siyo sanamu mimi ni mwanadamu niliyoumbwa na MUNGU namtukuza MUNGU wangu, sistahili kuabudiwa wala kutukuzwa, hapo ulimwenguni wametengeneza vitu kwa mfano wangu na vingine vinatenda miujiza ya aina mbali mbali huo ni uongo, ni shetani wala siyo mimi. Pia nakueleza uelewe, mimi Maria sijawahi kuwatokea  watu katika ulimwengu huu, hao wote ni waongo ni mizimu ya shetani na mpinga kristo. Waeleze wanadamu na wamrejee MUNGU. Inasikitisha sana mimi Maria jina langu kufanywa MUNGU au tegemeo, mimi sina kitu chochote ni kama hao watu waliopo hapa duniani ila tofauti mimi nipo mbinguni, namuabudu MUNGU wangu.
c.      Akaniambia watu wengi wamepotezwa na shetani na hata watumishi aliowatuma mwanangu ambao wapo hai hata sasa wamekataa kusema ukweli, sasa Hebron usijidharau kama ulivyo, wewe siyo Yule wa zamani wewe umebadilishwa tayari kwa safari ya mbinguni na MUNGU yupo na wewe na serikali ya mbinguni. Waeleze ukweli, tokea nije mbinguni sijawahi kuja duniani wala kusema na mtu kwa maono au sauti, nasubiri mpaka ule mwisho wa ulimwengu atakapokuja YESU. Nimekujulisha uelewe na hayo mengine ni yako wewe kama wewe. Hivyo nawaeleza ulimwengu wote hapa na kusema mama yake YESU anaonekana hapa duniani ni uongo. Ila kinachoonekana ni mzimu wa Maria wa kuzimu siyo mama yake YESU WA NAZARETI.
Wapo YESU wa wawili:
1.     YESU WA NAZARETI aliyekufa na kufufuka yupo mbinguni hata na mama yake aliyemzaa.
2.     Yesu wa pili ni yesu kristu wa uongo, huyu yupo kuzimu na anaye mama yake wa kuzimu ambaye ndiye Maria mzimu au mzuka na ndio chombo cha mpinga kristo kuzimu, na sasa kinatawala ulimwengu.
Mama yake YESU wa kweli yeye anamheshimu MUNGU na anafuata sheria zake kama alivyofuata za mwanae ambaye ndiye Mfalme wa Wafalme na ni wapekee alikufa na kufufuka. Ila sasa elewa system ya mpinga kristo kuzimu inayo yesu wa uongo na pia yupo Maria wa uongo na Maria wa uongo ndiye anayemkufuru MUNGU aabudiwe yeye wakati yeye siyo MUNGU, tena anatengenezewa sanamu zake na watu humtolea sadaka. Sasa nawaeleza fungukeni mambo yameharibika.
MAMA YAKE YESU SIYO MUNGU WALA HAPASWI KUABUDIWA NA YEYE HATAKI, ila Maria wa kuzimu yeye ni mama wa mpinga kristo na anayeendeleza ya mtoto wake yesu wa uongo. Sasa amua leo, nakusihi usishiriki. Hiyo ni picha halisi 100% makanisa ya jinsi hiyo ni ya mpinga kristo siyo ya kuiendeleza injili ya YESU WA NAZARETI bali ni makanisa ya kuiua injili ya Neno la MUNGU, na kuwaingiza wanadamu wote wawe adui wa MUNGU na BWANA YESU wasiende mbinguni. Amua leo kumjua YESU WA NAZARETI na usiabudu hilo jina tena kama unataka uiponye nafsi yako. Kama unaabudu sanamu ujue nafsi yako ipo jela ya shetani. Mbinguni hakuna sanamu wala MUNGU siyo sanamu, YESU, ROHO MTAKATIFU wote siyo sanamu, sanamu haina uhai, haioni, haiongei. Ila MUNGU, YESU, ROHO MTAKATIFU wanao uhai, wanaishi milele
SALA YA TOBA
BWANA YESU WA NAZARETI NAOMBA UNIOKOE UANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE MIMI NI WAKO KWANZIA SASA NA DAMU YAKO INIFUNIKE NA NENO LAKO LIJAE NDANI YA MOYO WANGU NA LISITOKE MILELE.
AMEN.
SOMA:
Mathayo 7: 13-27
Mathayo 15: 7-9
Ufunuo wa Yohana 22:15
Kumbukumbu La Torati 32:39
Kutoka 20: 1- 20
NABII HEBRON.

[ad_2]