Close

IMANI IPI NI YA KWELI? IMANI IPI NI HAI? NA IMANI IPI IMEKUFA?


Watoto wa MUNGU aliye hai nawasalimu katika jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na mwenye imani mmoja tu iliyo hai ambayo asili ya imani yake ameipata kutoka kwa MUNGU aliye ndiye BABA yake na pia YESU huyu ndiye BABA yangu pia mimi Hebron. Leo nitaelezea kuhusu  imani ili mataifa mjielewe na mpone maana pasipo kuwa na imani hai hakika hautamuona MUNGU. Ukisoma katika kitabu kitakatifu cha neno la MUNGU, Waebrania 10:38; Neno la MUNGU linasema hivi “lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.” Hapa unaona neno linavyosema kuhusu imani ya kusita-sita ya kuwa ni adui wa MUNGU. Na ukisoma katika kitabu cha Waebrania 11:1,6 inaelezea vizuri kuhusu imani hai ilivyo na ni jinsi gani umuamini MUNGU, na zaidi imeandikwa kuwa imani huja kwa kusikia neno la MUNGU (hii ndiyo imani ya kweli na ndiyo iliyo hai).
Katika ulimwengu huu shetani amewapiga watu upofu na wakristo walio wengi zaidi wanaona wapo na imani hai pamoja na makanisa katika sehemu mbali mbali katika ulimwengu wote na kumbe tayari imani zao shetani ameshaziua katika ulimwengu wa roho na hata kimwili na madhara ya imani kuuliwa ni tayari umeshatekwa kwa shetani na hauna direction za MUNGU au kwa maana nyingine barabara ya kumuona MUNGU imeondoka mbele yako na kama haipo lazima unabakia barabara ambayo ni wrong way na hautafika kwa mhusika unayomtaka bali mwishoni utajikuta na kujuta upo kwa shetani pasipo kujua na hata leo hii wengi zaidi wapo kwa shetani, ila ntakufundisha ili upone hiyo ndiyo kazi aliyenituma YESU niwatoe katika  njia pana, niwaonyeshe njia yake yeye, atakayefuata na kutii atapona ila yeye atakayekaza shingo ajielewe jehanamu ndipo patakapokuwa ni makao yake, uamuzi ni wako sasa uamue leo ni imani ipi unayoitaka sababu wakristo wanaamini wanampenda sana YESU ila cha ajabu 98% ya wakristo wote katika uliwmengu wote imani zao ni mfu na wanajiona wapo salama, hata mimi kabla ya kufundishwa na YESU pamoja na serikali ya mbinguni nilijiona nipo sawa ila kumbe tayari nilikuwa nimewekewa pando la imani mfu  ikanifanya niende wrong way hadi pale aliponichomoa YESU peke yake katika mikono ya makanisa na watumishi waliomuasi MUNGU na kunitenga ndipo nikaujua ukweli na sasa ukweli huu ni lazima niwajulishe mataifa yote ili mpone au mtoke katika wrong way mkae katika njia sahihi aliyoitengeneza MUNGU peke yake.
IMANI HAI
Imani hai ni imani isiyotikisika na ni imani ambayo ipo sawa sawa na neno la MUNGU kiroho na kimwili na sheria zake bila kubadilishwa au kuabudu tofauti, kusujudu except MUNGU BABA, MWANA, na ROHO MTAKATIFU  peke yake, tena usimuabudu hata Maria nasisitiza sababu yeye siyo MUNGU ni mtu tu kama wewe, wala yeye hana umoja na wale watatu ambao ni MUNGU, YESU na ROHO na zaidi imani hai ipo katika mtumishi ambaye anafuata neno lilivyo na awe ameitwa  na MUNGU siyo amejiita na awe mtakatifu kweli kweli na anapokuwa hivyo na kanisa linaambukizwa imani iliyohai, sababu madhabahu inakuwa ndani ya kuhani, sasa jinsi kuhani alivyo ndivyo ilivyo na hali ya waumini.
IMANI ILIYOKUFA NI HII
Kwanza mtu anajiita yeye ni mkristo lakini hajaokoka, na pia unakuta mtu anasema anabatizwa ubatizo mmoja imani moja lakini siyo. Anabatizwa ubatizo wa maji ya kikombe? Je huu ndio ubatizo mmoja aliobatizwa YESU? Jibu siyo hivyo, hata hiyo imani tayari siyo hai tena, au mtu amebatizwa katika maji ya kisima maji mengi? Je nikuulize swali je YESU alibatizwa katika maji ya kisima? Jibu siyo hivyo, tayari hapo siyo imani moja tena haijalishi unajiita wewe ni mkristo. Yeye aliyeonyesha njia na akasema tufuate njia yake na imeandikwa katika Ufunuo 22: 18 atakayeongeza au kupunguza neno la MUNGU jina lake litaondolewa katika kitabu cha uzima. Na pia tujiulize biblia imeandika mtu hupokea imani kwa njia ya kusikia neno la MUNGU, sasa tujiulize maswali hizi aina za ubatizo umezisoma au kuzisikia katika neno la MUNGU? Jibu, hazipo, what do you think about your faith? Angalia unapewa pando la imani iliyokufa hivyo na wewe unatekwa na shetani haijalishi unasema shindwa shetani.
Jambo lingine imeandikwa usiabudu sanamu, lakini wakristo baadhi wanaabudu sanamu na wanamtaja YESU wakijua wanamuabudu YESU nawaeleza YESU hana ushirika na sanamu (tayari hao walio hivyo imani zao ni mfu na njia wanayoiendea ni jehanamu) amenituma YESU WA NAZARETI niwaeleze na niwafundishe mumjue yeye kikweli na mpokee imani ya kweli ili siku moja mfike alipo yeye na mje muurithi ufalme wake. Na wengine wanaweka sanamu kanisani wanawadanganya waumini wao hawaabudu sanamu eti wameweka kama tu vile mtu anavyoweka picha zake katika album, ni uongo biblia inasema hivi kumbukumbu zetu na zijulikane na MUNGU peke yake na zaidi ni ROHO MTAKATIFU peke yake atakayetushuhudia habari zilizopita na zijazo katika roho. Sasa ukiona hivyo uelewe kanisa la jinsi hiyo yupo roho mchafu na imani chafu ya shetani na unaposhiriki hapo na wewe inakuvaa pasipokujua na ni mpinga kristo huyo.
Jambo lingine nitaelezea kuhusu imani iliyokufa katika kanisa au kwa watumishi, ukisoma neno la MUNGU imeandikwa usijisumbue utakula nini utavaa nini. Hapa makanisa utayaelewa yaliyokufa imani na yenye imani inayosita-sita imani ambayo haina mwelekeo wa mbinguni, imani ya kwenda jehanamu, imani ya mpinga kristo. Ukikuta kanisa linafanya michango ili kujenga kanisa uelewe hawamuamini MUNGU kama anaweza kujenga na pia ukiona hivyo uelewe kuwa tayari hawapo na MUNGU aliye hai na kama kanisa likijengwa na nguvu ya imani mfu je nikuulize swali imani hai itakuja tokea hapo? Jibu hapana, hakuna ushirika kati ya nuru na giza. Ukiona mtumishi anaomba michango katika TV, RADIO au hata anaweka akaunti yake kwa internet ili uweke pesa, uelewe huyo ni mwizi na imani yake imekufa, na yupo kinyume na neno, usisumbukie lolote kama MUNGU amemuita amrudie yeye afungue njia au afanye. Sasa wengi hawajaitwa na wengi ni wachawi wakubwa na sababu aliyeko ndani yao ni shetani aliye maskini hivyo lazima anyang’anye wanadamu kwa kutumia njia hizo, ila MUNGU yeye siyo mnyang’anyi wala hachangishi.
Tazama hata nyakati zile YESU aliyakuta haya mambo ya biashara akawafukuza hekaluni ila leo yamejaa kila mahali, sasa pata picha je huku si kumkasirisha YESU na je wataweza kuizuia hasira ya YESU kwa jinsi wanavyolitumia jina lake kuibia watu pesa? Na kuwaingizia waumini imani mfu. Jambo lingine ukiona pastor amechangisha au analeta bahasha za sadaka nyumbani uelewe sasa imani yake ni ya kusita-sita na ndani yake hayupo tena MUNGU ajibuye kwa moto na watu mnaoshiriki mnakuwa mmenajisika na dhambi hiyo sababu huyo pastor ni kiongozi kipofu, sasa kipofu akimuongoza kipofu mwenzake wote wanaenda pamoja wasipopajua katika shimo.
NOTE:
Nawaeleza mlinde sana mlicho nacho asije mwizi akakuibia, linda imani yako, na usishiriki mahali popote unapoona pako kinyume na neno la MUNGU haijalishi mengine mwingine anafuata biblia na mwingine hafuati, MUNGU neno lake halichanganywi hata kidogo yeye ni kweli tupu.
TOBA:
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele nirejeshee imani iliyohai, iondoe imani mfu ndani yangu, unilinde milele na ROHO wako MTAKATFU aniongoze milele, Amen.
Nawakaribisha mataifa yote mnaomtafuta YESU wa kweli na mnampenda karibuni kanisani kwangu mtakutana na yeye live.

NABII HEBRON.