Close

INJILI YA KENYA WATUMISHI WANATOZA USHURU WAUMINI NA KUPEWA RISITI OFFICIAL (HAWA NI WATUMISHI MATAPELI).

[ad_1]


Enyi wakenya kwa jinsia zote nawaandikia wosia huu mfunguke fahamu zenu. Mimi MUNGU amenituma kwa ulimwengu wote, ikifika muda wake nitakuja kimwili maana ni yeye ndiye atakayenileta niwaeleze habari njema na ukweli wake. Wengi mnampenda YESU ila mnaongozwa na yesu wa uongo kupitia watumishi. Injili hiyo mnayotozwa ushuru makanisani siyo injili ya kweli na hata hao wanaowachaji pesa ndiyo umwone mtumishi kwa private, nawatangazia msitoe tena. Pesa hizo kaleni na mfurahie maisha yenu, nitawaombea na MUNGU atawalinda nyie mnaoteseka na mnakiu ya kumtafuta YESU wa kweli.
Watumishi Kenya wacheni kumuaibisha YESU, jicho la MUNGU linawaangalia vilio vya wakristo wakenya vimefika kwa MUNGU kwa ajili wanavyotendewa makanisani na zaidi hakuna injili ya bure, hata kumuona mtumishi tu lazima utoe pesa na upewe risiti utasubiri siku ya kuitwa. Wengi wanachaji (Kshs 1000 au 2000) ndipo upate nafasi ya kumuona. Hawa wote ni waizi na siyo watumishi wa kweli. YESU alisema nimekupa bure, toa bure. Sasa huu siyo uvunjaji wa katiba ya MUNGU?
Nawaeleza ndani ya hao watumishi hayupo YESU wa kweli wala ROHO MTAKATIFU. Yupo yesu wa uongo na roho chafu kama walivyo kwa waganga wa kienyeji. Hivyo ukiona unadaiwa pesa ndiyo umuone mtumishi ujue hauendi kumuona YESU wa kweli unaenda kwa watoza ushuru, na wengi hawaendagi kwa YESU ila mnaenda kwa shetani au kristo wa uongo. Jambo hili pia lipo Tanzania ila huku halijawekwa wazi ni siri, atakueleza mchungaji mwenyewe bila aibu leta kiasi fulani, na Rwanda, Uganda katika Afrika mashariki, injili imekuwa ni biashara.
Ukikuta mtumishi anachaji pesa, kimbieni, hapo hakuna MUNGU, ni roho za shetani. Someni katika makala za Nabii Hebron mtapona roho zenu, na vitabu. Na pia fuatilia vipindi vya television vinafika katika nchi zote. Angalia time katika home page ya website www.prophethebron.org, angalia kwenye vipindi vya Television utapata muda na mtaujua ukweli na mtapona. Na pia karibuni watu wote, nimepata simu nyingi na meseji kutoka Kenya, mnalia kuhusu mateso ya kuchajiwa pesa.
Nawaombea, hao wanaoenda kinyume na Neno hiyo, nguvu inayotenda kazi ni nguvu ya shetani hata hiyo miujiza. Ila mwisho umefika, watakutana na MUNGU aliyewaumba aliye na uchungu sababu uchungu anaujua yeye aliyekuumba. Mrejeeni YESU, mkae kwa amani, msidanganyike tena. YESU siyo mnyang’anyi, mwizi, mfilisi. Hao wanajiita, wanatafuta pesa kwa kutumia jina la YESU. YESU hutoa Baraka bure, huponya bure, haangalii pesa yako. Anataka moyo wako tu ili aishi ndani yako, ila matapeli wanataka pesa yako tu, wakufilisi. Mfunguke sasa na MUNGU awaongoze msinaswe na makristo wa uongo.

NABII HEBRON.

[ad_2]