Close

JE UNAELEWA KWA NINI MTUMISHI AU WA KANISA ANAKUWA NA BENDERA YAKE BINAFSI KAMA VILE YA RAIS??


Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI, nitaelezea maana ya mtumishi au mchungaji, Nabii, Mtume na wengineo wenye bendera zao binafsi ni jinsi gani ni jinsi gani imefikia mpaka akawa na bendera yake binafsi hata ukiona katika gari lake akitembea inapepea mbele ya gari lake na katika kanisa lake pia mtaikuta imewekwa mlingoti au na kama anayomakanisani sehemu nyingine hivyo hivyo ataziweka bendera nyingi kwa idadi ya makanisa yake. Bendera hizi ambazo utaiona ni special kwa mambo yake, kwanza kabisa mpaka uone mtumishi amekuwa na bendera yake uelewe amefikia kiwango kikubwa cha uchawi hivyo hupewa bendera hiyo na joka kuu ili awe na serikali yake huko duniani na anapokuwa na bendera hiyo anapewa mamlaka ya kuwateka waumini wake kwa nguvu za kipepo pamoja na watumishi wake wa chini na anawapa utawala, yeye anakua ni mfalme kwa upande wa shetani na majeshi ya shetani na mapepo huja kufanya kazi ya kuwasaidia kuwateka watu fikra zao na kuwanyang’anya nyota na kuwapofusha watu wasiende mbinguni.
Mahali pa namna hiyo nawaeleza ukweli halisi kama nilivyoelezea katika makala ya Nabii Hebron katika somo la bendera, soma utaelewa zaidi nini maana ya bendera kuwekwa makanisani. Ufalme wa MUNGU katika ulimwengu huu hauna alama, ufalme wa MUNGU upo katika roho tu, na ndio maana imeandikwa tunaenda katika roho na siyo katika mwili, bali ufalme wa shetani unaonekana kimwili na ndio sababu watumishi wanaotumiwa na shetani na wanapandishwa ngazi nyingine lazima hupewa bendera yake ili aanzishe serikali yake. Ni kama vile kiongozi wa nchi yeyote sababu anashinda kura na kuteuliwa kuwa kiongozi wa serikali lazima huwa na bendera yake kuashiria yeye ndie kiongozi mkuu wa serikali hiyo (kwa upande wa serikali za Kaisari hiyo ni sawa kabisa) ila kwa upande wa MUNGU hakuna kitu kama hicho cha mtumishi kuwa na bendera yake binafsi katika gari au kanisa. Hayo yote niliona kuzimu na niliona wanayopewa na lengo lao, akinipeleka YESU na  niliporudi ulimwenguni nikafunguka akili sababu hata mimi sikujua. Akaniambia, hao wanawapoteza watoto wangu na watoto wangu hawajui, nenda uwafungue macho, wahubirie wapone, waeleze mimi nilipokuwa hapo ulimwenguni nilionyehsa njia, kama ingekuwa ni mpango wa MUNGU, basi mimi YESU ningekuwa wa kwanza kuweka bendera katika punda au boti au katika gari la farasi. Mimi ndiye mfalme waeleze hao wote siyo watumishi wangu ni watumishi wa ufalme wa joka kuu amekuja kuupanda katika dunia, ni watumishi wa shetani na OLE wao wanaonitesea watoto wangu na kulibadilisha neno la MUNGU. Mimi YESU sina ushirika nao kabisa wala siwajui. Na mimi ninawafikishia ujumbe huo watu wote wa mataifa yote. Amua sasa upone na umrejee YESU ili utolewe katika hiyo serikali ya shetani iliyokuteka na wewe ukaona upo katika kanisa la YESU kumbe upo katika kanisa la mpinga kristo.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote asante kwa kujua ukweli wako, niponye roho yangu, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. ROHO MTAKATIFU uingie ndani yangu uniongoze peke yako. Amen.

NABII HEBRON.