JE UNAFAHAMU BINADAMU AMBAYE NDIYE RAIS WA SERIKALI YA SHETANI?

[ad_1]

Nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO aliye hai ndiye BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE na ndiye mwana wa MUNGU wa pekee leo ninawafunulia jambo jipya ambalo ulimwengu wote haujui, ila mimi Hebron kwa neema ya YESU yeye aliyeniita nimtumikie na yeye aliyenituma niiharibu ufalme wa shetani na ni usimamishe ufalme wa MUNGU katika dunia yote, ufalme ambao ni kweli ya MUNGU yeye aliye hai na mwenye nguvu kuliko miungu yote. Wakati nilipotulia katika kuomba nikiwa peke yangu mara akaja malaika Mikaeli ambaye ndiye malaika mkuu wa MUNGU, ambaye yeye ndio kiongozi wa vita katika kuubomoa ufalme wa shetani na maajenti wake na wote, huyu ni malaika mkubwa hata mimi katika maisha yangu sikutegemea kama ningekuja kuwa karibu au hata na uhusiano na yeye sababu sikujijua kama ningekuja kuwa mtumishi wa MUNGU, ila nilifichwa mpaka wakati wake ulipofika MUNGU kwa kusudi lake likatimia.
Wakati wa kupigana akamkamata mtoto wa Adam wa kwanza kumzaa ambaye jina lake anaitwa KAINI, ilikuwa ni vita vikubwa sana katika ulimwengu wa roho. Akamleta mbele yangu akiwa tayari ameshamshughulikia na kumuamuru anieleze kila kitu, na kisha nibomoe hayo yote ambayo sitayataja hapa mpaka katika kipindi kingine nitakaporuhusiwa na YESU kuyasema. Ilikuwa ni vita vikubwa na kilio kikubwa katika serikali ya shetani. Na mimi nikamhoji KAINI, na kubomoa kazi zake zote. Sasa shetani alimpa KAINI cheo cha URAIS katika serikali yake na huyu ndiye mwanadamu ambaye shetani alimpa URAIS katika serikali yake, alimpa URAIS sababu yeye alikuwa ni mwanadamu ili aje  atawale wanadamu tena na kuwamwagia roho zake katika ulimwengu wote, ili watu wawe waasi kama Kaini. Na kila mtu yeyote aliye au anatenda uasi au dhambi ndani yake ipo roho ya Kaini na ndiyo maana watu katika ulimwengu huu hawaachi uasi ni sababu huyu aliyekuwa RAIS wa kuzimu yeye ndiye aliyekuwa anafanya hayo ili na wanadamu wamkosee MUNGU na kuwa na kiburi na kuimwaga hiyo roho katika makanisa na ndiyo maana makanisa yanaasi kila siku na mengine ni yeye ndiye anayesimamia hayo maelekezo kabisa, mfano kubatiza ubatizo wa maji ya kikombe, kuabudu sanamu, wakristo kukataa wokovu lakini wanajiita wao ni wakristo.
Hii yote ni Kaini ndiye amwagaye hiyo roho ya kuasi na watu wote walio hivyo waelewe wamejiunganisha na mtandao wa Kaini na laana zake ili alipo yeye na hao wamfuate wakati wa hukumu. Na ukisoma katika neno la MUNGU katika kitabu cha Mwanzo 4 chote utaona mtiririko ambao shetani aliutumia kumdanganya Eva mama yake na shetani aliendeleza kuwafuatia watoto wa Eva na Adam akamuingizia Kaini roho ya wivu na ukatili na kiburi, akamua Abeli na hata MUNGU alipomuuliza KAINI ndugu yako yupo wapi utaona Kaini akijibu kwa kiburi na kwa majibu yasiyofaa kujibiwa MUNGU, naye MUNGU akamlaani (Mwanzo 4:9-15).
Sasa hiyo roho iliyokuwa ndani ya Kaini bado ipo na inatenda kazi na ndiye anayeisambaza kwa wanadamu wote ili kilichompata yeye na kikupate na wewe, kama unakuwa hauelewi sasa uelewe. Unatenda dhambi, uchawi, unaua, zini, lewa, abudu sanamu, batizwa ubatizo wa maji ya kikombe na unajua ni dhambi, lakini unafanya tu. Hii ni sababu KANI amekushikilia na amekuwekea na roho yake na makanisa yamewekewa hiyo roho na ndio maana kanisa imekuwa ni nyumba ya biashara tu, neno la MUNGU linabadilishwa kweli haimo, hii ndiyo dalili watu  hao tayari Kaini amewaweka alama yake na ndiyo maana wanatenda dhambi bila hofu na ndiyo sababu dhambi katika ulimwengu huu inaonekana ni kitu cha kawaida. Hii ni sababu wanadamu wamejazwa roho ya Kaini. Swali kama na wewe umejazwa hiyo roho je utaenda mbinguni? Jibu, hauendi utafuata nyayo za Kaini.
Ni makanisa 98% all over the world yanafuata nyayo za Kaini badala ya kufuata nyayo za YESU ambaye ndiye dereva ameshikilia stelingi anaendesha YESU. Wamegeuka na kumfanya Kaini ndiyo dereva anayeendesha gari. Na waumini wanaposhiriki kila ibada japo hawajui na wanampenda MUNGU, matokeo yake wanaingiziwa hiyo roho ya Kaini na ndiyo maana makanisa kwanzia maaskofu mpaka viongozi wa chini ni watenda dhambi tena wazi wazi na hawana hofu na kumuogopa MUNGU hii ni sababu lipo pando la Kaini tayari na yeye ndiye aliyekuwa amepewa cheo cha URAIS na shetani. Katika makala mengine nitaelezea zaidi habari zake na kila mahali alipopita sawa sawa na MUNGU alivyonifunulia, habari hizi hata utafute katika biblia hautazipata, haya yalifichwa na sasa nimewapa picha kidogo.
NOTE:
Jichunguze je wewe hauna tabia za Kaini? Kiburi, wivu, makusudi, mchawi, mlevi, muabudu sanamu, mbatizwa wa maji ya kikombe, haujaokoka mpaka sasa na wala hauna mpango wa kuokoka?
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOZITENDA KWA KUJUA AU KUTOKUJUA, UNIANDIKE JINA LANGU  KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, NAOMBA UNIONDOLEE ROHO ZA KAINI NDANI YANGU NA NIKUTII WEWE NA KUKUSIKILIZA. AMEN.

NABII HEBRON.

[ad_2]