Close

JE UNAJUA KUWA MAKANISA YENYE BENDERA MAKANISANI YAPO CHINI YA UFALME WA GIZA!!!

BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote mnaompenda YESU na msiomjua pia nawasihi mumrejee yeye ni rafiki mwema na ni mponyaji na ndiye mfalme na yeye ndiye katika ile siku ya KIAMA yeye ndiye atakayekuhukumu kila mtu sawa sawa na matendo yake. Amenituma kwa ulimwengu wote niwaeleze habari zake na kuyafichua maovu ya shetani ambaye wengi hamuelewi na mnazidi kutekwa na shetani mkijua mpo na YESU kumbe mpo katika makanisa ya ufalme wa shetani na hii ni katika sehemu mbali mbali. Tafadhali unapopata ujumbe huu uwatumie na wengine na MUNGU atakubariki sana, utakuwa na wewe umeshiriki katika kazi ya YESU WA NAZARETI na atakukumbuka katika ufalme wake sababu watu watapona roho zao watakapo soma ujumbe huu.
Nitaelezea maana ya bendera kimwili, bendera ina maana ni ufalme fulani wa nchi fulani au taifa fulani au chama fulani na pale inapossimamishwa ina maana pale upo ufalme wake katika eneo lile, hii ni katika ulimwengu wa kimwili. Nitaelezea bendera za kiroho. Mtumishi yeyote ambaye MUNGU amemuita lazima anapewa bendera zake katika ulimwengu wa kiroho anampa bendera tatu, moja ikiwa ina ishara ya MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU. Mimi niliyajua haya wakati nilipotumwa na YESU na kunituma kwa mataifa yote, na bendera hizi hazionekani kwa hapa duniani kama bendera zilizopo hapa ulimwenguni, sababu kazi ya MUNGU inafanyika kwa roho na siyo kwa kimwili. Ila na shetani na yeye akabuni bendera zake ambazo njia aliyoifanya yeye ni wale watumishi anaowaita shetani yeye huwapa bendera zake ikiwa ni ishara ya ufalme wa giza na bendera hizi ni tofauti na bendera za nchi au vyama.
Bendera kuzijua kwa macho ya kibinadamu ni kazi ndogo sana, ila leo nitaelezea kwa ufupi kidogo sababu ile nitaendelea kuelezea hatua kwa hatua ili mfunguke fahamu zenu na muelewe hizo bendera kazi yake ni nini zinazowekwa makanisani na nyingine watumishi wanazitumia kama bendera zao katika misafara yao kuweka katika magari. Kwanza uelewe hata YESU alivyokuwa hapa ulimwenguni hakuwa na bendera yake kimwili na hata wale mitume wa YESU 12 hawakuwa na bendera zao kimwili na hata katika nyaraka za Neno la MUNGU Manabii hawakuwa na bendera makanisani. Bendera za watumishi wa kweli wa YESU zipo katika ulimwengu wa roho na hazionekani kama vile ilivyokuwa kwa YESU na kwa kina Yohana mbatizaji. Ila bendera anazowapa watumishi ambao baba yao ni shetani, bendera hizi lazima zionekane kimwili na zinaweza kuwa rangi tofauti na nyingine, na mengi ya misalaba kama red cross na nyinginezo nyingi.
Bendera hizo zinazo maana yake zinaashiria kwa shetani pale ndipo penye ufalme wangu yaani lusifa, zaidi hata biblia imeandika katika Zaburi ya 74:4-9 “watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako; waweka bendera zao ziwe alama. Wanaonekana kama watu wainuao mashoka, waikate miti ya msituni. Na sasa nakishi yake yote pia  wanaivunja-vunja kwa mashoka na nyundo. Wamepatia moto patakatifu pako; wamelinajisi kao la jina lako hata chini. Walisema mioyoni mwao, na tuwaangamize kabisa; mahali penye mikutano ya MUNGU wamepachoma moto katika nchi pia. Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii, wala kwetu hakuna ajuaye, hata lini?” utazidi kuelewa zaidi maana ya hizi bendera, bendera zinazozungumziwa hapa ni bendera ambazo watu aliowaumba MUNGU wanapokutanika wakidhani wanamfuata MUNGU wa kweli kumbe mahali hapo wanaumizwa na kupigwa nyundo kwenye ulimwengu wa roho, na ndani ya mioyo ya hao wenye bendera hizo wanajua wanachokifanya ili kuwatesa wana wa MUNGU, hivyo uelewe na ufunguke bendera za makanisa au za watumishi walizojitengenezea hao wanajua wanachokifanya hizo bendera zinaashiria ni ufalme wa shetani ndio unaotenda kazi hapo kama ulikuwa hauelewi, sasa elewa na utoke huko upone.
Amenituma nifichue uovu wao na mpate kupona msidanganyike tena. Ya Kaisari mpe Kaisari na MUNGU mpe MUNGU peke yake. Mpaka hapo umeelewa na umepata picha ya maana ya hizi bendera za makanisani na hata katika magari yao. KANISA LA YESU halina bendera za kimwili bali watumishi walioitwa na shetani wao hupewa bendera zake kimwili na ni lazima bendera hizo aziweke kimwili hapa ulimwenguni. Ili mapepo yaje kuwaangamiza wanadamu soma Zaburi 74 hayo mapigo ni mapepo na jeshi lake ndio huja kuziua roho za wana wa MUNGU. Epuka kanisa la jinsi hiyo na hata mtumishi wa jinsi hiyo, jibu umelipata sasa.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE NITOE HUKO NILIKOSHIKILIWA, UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE. AMEN.

NABII HEBRON.