Close

JE UNAJUA KUWA MTUMISHI YEYOTE AKIVAA KOFIA YA KIASKOFU, KICHUNGAJI, ANAKUWA NI ADUI WA MUNGU.


BWANA YESU asifiwe, kama kawaida naendeleza kusema ukweli kama alivyonituma YESU WA NAZARETI, mumrejee yeye na neno lake  wala usidanganyike na watu ambao tayari hata kimwili wanaonekana wameotea au ni vipofu na hata hao wanaowaongoza kwenda kwa YESU hawamjui YESU mwenyewe, sababu YESU ni neno. Ukisoma katika litabu cha 1 Wakorintho 11: 3,4,7 neno linasema hivi “3 lakini nataka mjue ya kuwa kichwaa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha kila mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni MUNGU. 4 kila mwanamume asalipo, au anapohutubu (kuhubiri), naye amefunika kichwa, yuaibisha kichwa chake. 7 kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa MUNGU.” Mpaka hapo ukiangalia neno la MUNGU kiwazi kabisa, na MUNGU haruhusu mtumishi yeyote kwa jina lake katika kanisa mtumishi mwanaume avae kofia yeyote au kufunika kichwa chake. Na MUNGU anakataa sababu utukufu wake unakaa katika kichwa cha mwanaume ambaye yeye humtumia. Sasa shetani ameliteka kanisa kwa njia hii ili kuuondoa utukufu wa MUNGU akabuni vazi la kofia wavae watumishi wakihubiri ili utukufu wa MUNGU usionekane bali utukufu wa shetani uonekane na uote mizizi pamoja na kuangamiza roho za watoto wa MUNGU.
Hivi umeshajiuliza wametoa wapi huu ujasiri wa kuingia na kofia kanisani wakati hata muumini akifika tu mlangoni kanisani tayari ana hofu anavua kofia, bali viongozi wanavunja katiba ya MUNGU wazi wazi. Na waulize swali je nyie mnaongozwa na biblia ipi inayoruhusu mvae kofia kanisani au mkiwaombea watu, jibu hawana. Ila ruhusa hii ipo katika biblia ya shetani soma katika blog ya Nabii Hebron kuhusu biblia ya shetani jinsi ilivyo utaelewa zaidi, ya kuwa ni nani anayewaongoza jibu ni mpinga kristo. Sasa kama kiongozi wa dini anavaa kofia ili watu wasione utukufu wa MUNGU, je watu watazamie kuona utukufu wa nini? Jibu ni wa shetani full, ila wewe hautaelewa kimwili mambo haya ni ya rohoni, sababu katika ulimwengu wa roho tayari shetani amewavalisha kofia ili kumzuia huyo mtumishi asije akatumiwa na MUNGU WA KWELI kabisa, ila ni shetani amtumie yeye peke yake awe mpinga kristo, hiyo ndiyo maana yake, na kitu chochote hadi kumtolea mtu au akifanye. Nahoji na wewe jihoji ndani yako ukiwa umetukiza ufahamu wako, je hii ni sawa mbele za MUNGU? Jibu siyo na zaidi Ufunuo 22:18 inasema ole wake atakayeongeza maneno ya kitabu hiki au kuyapunguza jina lake halitakuwepo katika kitabu cha uzima.
Haya jihoji tena sasa kama tayari hapa wameongeza yao na wao hawapo mbinguni, na kama hawapo mbinguni hawa si ndiyo viongozi vipofu? Na kama ni vipofu sasa hawaoni roho za watu zinauliwa na kupelekwa motoni na tena hata waumini wanampenda YESU WA KWELI na kumbe wanampenda yesu wa uongo, je utapona? Amenituma YESU WA NAZARETI na muda siyo mrefu atalinyakua kanisa lake. Funguka angalia usije ukakutwa upo katika mstari ya kristo wa uongo ukajuta na kulia, umeachwa haujanyakuliwa au hata kama ulikufa unakuwa umefia kwa bwana wa uongo na wewe hautaurithi ufalme wa MUNGU aliye hai.
Huu ndio wakati wako upone na inawezekana hata ni mtumishi na wewe unavaa kofia uliyopewa na dini yako kwa mapokeo ambayo hayatoki mbinguni bali ni mapokeo ya ulimwengu huu ambayo ni ya shetani unayorithi pasipo kujua, tubu na kumkiri YESU muda huu na uelewe wazi hapo ulipo ni mahali pa kristo wa uongo au mpinga kristo, sababu nyepesi kabisa ambaye hakuna kubisha. Angalia neno lisemavyo na wewe umeshiriki kumpinga, je hautakuwa adui wa MUNGU? Na kama ni adui wa MUNGU basi wewe ni rafiki wa shetani au ni mwanachama wake. Kama ulikuwa haujui umeujua ukweli, na wewe unayeongozwa na mtu wa jinsi hii ujielewe unaongozwa na watu ambao ni wapingaji wa neno la MUNGU na kumkufuru ROHO MTAKATIFU. Swali je kwa njia hii utafika mbinguni, jibu NO. ujumbe huu watumie watu wengine katika facebook, twitter, email na mengineyo ili huu uovu wa shetani uwekwe uchi na MUNGU ainuliwe juu na YESU juu pamoja na ukweli wake na watu wapone roho zao, badala ya shetani kuendelea kuziua roho kwa kudanganya watu.
TOBA:
BWANA YESU naomba unisamehe, sivai kofia kanisani tena na sishiriki ibada za kuvaa kofia mwanaume, najitenga kiroho na kimwili. Uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Asante YESU kwa kunifungua ufahamu na kukujua. Amen.
Mataifa yote karibuni katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, mje mponywe roho zenu na mkutane na YESU WA NAZARETI aliye hai na wa kweli na MUNGU awawezeshe kuja.

NABII HEBRON.