Close

JE UNAJUA NI LINI? NA JE UNAJUA NI KWA NINI WATUMISHI WANATABIRI UONGO KUHUSU MWISHO WA DUNIA?

[ad_1]

Mataifa yote nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na ambaye yeye ndie atakayekuja kukamilisha tendo la mwisho wa dunia. Kama nilivyokwisha eleza ya kuwa lengo alilonituma YESU kwa mataifa yote ni waonyeshe njia ya kweli ili alipo yeye na wewe ufike na mwingine. Sababu sasa hivi hali ya injili ya neno la MUNGU limechanganywa na uongo na kubadilishwa ili watu watakapoamini uongo na kuufuata wasimuone MUNGU na wasiende mbinguni. Soma hili ninalowaandikia mataifa yote, ni mambo niliyofundishwa na YESU yeye ambaye ndiye kweli usije ukaona ni mimi Hebron, hapana, ni YESU ndani yangu aliyekasirika kwa nini watumishi wanawadanganya watu ya kuwa wanaijua siku ya mwisho wa dunia, wakiwemo wana sayansi na wanajimu?
Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo 24:3 “hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, tuambie mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, nay a mwisho wa dunia?” Hapa utaona wanafunzi waliuliza mambo mawili la kwanza ni kuja kwa YESU mara ya kwanza (unyakuo) na pili baada ya unyakup itapita miaka saba ya dhiki kuu ndio itatokea lile tendo la mwisho wa dunia.  Sasa nataka mfunguke ufahamu mataifa yote sababu mpaka sasa watumishi wanawadanganya watu eti kuwa sasa hivi tunasubiri mwisho wa dunia wakati ni uongo.
Kwanza ili ujue ni uongo kwanza unyakuo bado haujatokea, hili litakuwa ni tendo la kunyakuliwa watakatifu (watu waliookoka tu na kuzaliwa mara ya pili kwa maji mengi) na litafanyika kama vile mwezi baada ya unyakuo wale watakaobaki ni wenye dhambi peke yake wataiona dhiki kuu hii itakuwa ni miaka saba na hii haitakuwa siri katika ule mwisho wa dunia (Mathayo 24: 29-31) itakuwa ni wakati wa hukumu. Sasa watu wanadanganywa eti wajiandae na mwisho wa dunia badala ya kujiandaa na unyakuo kwanza. Nikuulize swali ni biblia gani wanayoisema ambayo inasema ni mwisho wa dunia unakuja kwanza? Badala ya unyakuo ambao ndio ujio wa kwanza wa YESU. Mimi nawasihi watu wote zaidi mjiandae kwa unyakuo sasa sababu ni wakati wowote hii ni siri ya MUNGU peke yake itakuwa ni lini na mwaka gani, mwezi gani ni yeye anajua peke yake.
Sasa wanadamu wamekuwa ni waongo hata wanajaribu kusema wanajua ni miaka gani na ni lini mwisho wa dunia? Nawatangazia hao watu ni waongo tena wanamkufuru ROHO MTAKATIFU na kuwapotosha watu wasijiandae na unyakuo sasa. Ukikuta mtumishi anaelezea au kuhubiri habari za mwisho wa dunia ni lini na anajua uelewe huyo ni MUONGO, anapotosha watu ndani yake ipo roho ya mpinga kristo na wengine hawajielewi wanaiga mapokeo ya elimu ya wanadamu pasipokujua. Watumishi hao wanakuandaa wewe ushiriki dhiki kii na usinyakuliwe na ndio sababu wao badala ya kuona unyakuo kwanza wao wanaona dhiki kuu, watashiriki na watakaa hapa hapa kipindi cha dhiki kuu na wateseke na kuteswa na mpinga kristo na watabakia hapa wanasubiri hukumu ile siku ya mwisho.
Natumaini unanielewa vizuri kuwa huu ni wakati wa unyakuo sawa sawa na katiba ya MUNGU isemavyo, kisha itakuwa dhiki kuu, halafu ndio mwisho wa ulimwengu. Haya yaliyotabiriwa vita, magonjwa haya yote yanaashiria dalili za kuja mwana wa MUNGU YESU WA NAZARETI kuja kulinyakua kanisa lake kwa mara ya kwanza kasha atakapilinyakua atapaa nao kwa miaka saba, hata wale waliokufa katika BWANA watafufuka wapae na kumlaki YESU mawinguni. Na wale ambao watakuwa wamekufa na dhambi watafufuka waishi tena kipindi hicho kitakuwa ni cha last game kama ukishinda hautahukumiwa. Na kama itakuwa ni kipindi cha dhiki hivi unaweza ukavumilia sababu utaambiwa ukimkiri YESU unakatwa mkono, sikio, miguu lakini haufi sababu mauti itafungwa. Je wewe upo tayari ubakie katika dhiki kuu? Kusubiria ule mwisho wa dunia? Jibu unapona, utoke, unyakuliwe, amua sasa uokoke na uyatoe mafikirio hayo katika moyo wako na kusubiria mwisho wa dunia badala ya unyakuo, kama hautaki unyakuliwe na YESU ujue mateso ya dhiki kuu yatakuhusu na je utaweza kuyavumilia? Jibu hautaweza.
Hivi vitu mnavyoviona sasa katika ulimwengu huu haya ni matayarisho ya dhiki kuu je na wewe unayataka? Matayarisho haya hayatawadhuru wale ambao hawajamsaliti YESU WA NAZARETI na wameokoka, na msishangae hata majengo yakianguka katika sehemu mbali mbali, ni dalili za mwanzo wa kuja kwa mara ya kwanza YESU WA NAZARETI kulinyakua kanisa ambalo ni mtu aliyeokoka na kuzaliwa mara ya pili. Hivyo kuanzia sasa penda kufuatilia habari za unyakuo ili ukae vizuri na YESU akija akunyakue. Siyo vibaya kujua habari za mwisho wa dunia ni vizuri kabisa ila ninachotaka kwenu mtoe mawazo yenu katika elimu ya uongo mrejeshe katika elimu ya kweli ambayo ni unyakuo kwanza, na watakaobaki na dhambi wajue mateso ya dhiki kuu atapambana nayo, ni baada ya kupita miaka saba ndio sasa tendo la mwisho wa dunia litatokea, na watu kuchomwa katika ziwa la milele.
Hao wote wanaotabiri na kusema mwisho wa dunia umefika au ni mwaka Fulani au mwezi  Fulani, waulize swali je hivi YESU ameshanyakua wateule wake? Atabaki hana jibu, yeye ni muongo na ndani yake ni roho ya unabii wa uongo ili afundishe uongo na kutabiri uongo ili watakaoamini wawe wanatekwa fikra zao na fikra ikitekwa tu ujue YESU akija unyakuo hakunyakui sababu wewe fikra zako na nafsi yako inasubiri dhiki kuu, na hukumu. Sasa funguka leo na utubu na zaidi usome blog na masomo ya Nabii Hebron, blog hii inaitwa kwa jina la Hebron kama kivuli, hii ni blog ya YESU WA NAZARETI ajaye kulikomboa kanisa lake ili na wewe upone soma blog ya YESU ambaye inaitwa kwa jina la Nabii Hebron basi utapona na utakuwa huru.
Nimewaeleza mara nyingi ulimwengu umetekwa na shetani hata kanisa na watumishi utaona kabisa hawasemi ukweli idadi kubwa na kama hawasemi ukweli uelewe wazi kabisa ni roho ya Nabii wa uongo ndio itendayo kazi, ingekuwa ni roho ya kweli ya MUNGU angesema ni habari za unyakuo watu wajiandae na kuokoka na utakatifu. Sasa hizi roho zidanganyazo zinafundisha kinyume eti kwanza ni  mwisho wa dunia, je unyakuo utakuwa lini? Je neno la MUNGU ni uongo? Na je ni kwa nini YESU alisema kila kitu kitapita bali kila neno lililoandikwa katika biblia lazima litimie. Je hauoni YESU amepingwa na MUNGU amepingwa? Ila shetani anatukuzwa. Amenituma habari njema msidanganyike na usitishwe hakuna anayejua siku wala mwaka atakao linyakua kanisa lake YESU, bali akishalinyakua hapo itakuwa siyo siri tena itapita miaka saba ya dhiki kuu ikiisha tu ndio YESU atakuja tena kulitimisha tendo la mwisho wa dunia, wala siyo mtume yeyote, Nabii yeyote au chochote, ameteuliwa YESU peke yake na yeye atawachukua watakatifu peke yake, na baada ya unyakuo ndio dhiki kii itaanza. Wakati huo ataruhusiwa shetani atembee live live na mpinga kristo na kazi ya mpinga kristo atakuwa anahakikisha tu wale waliobaki na dhambi wmakatae YESU kabisa. Kutakuwa hakuna amani, itakuwa ni serikali ya shetani inatenda kazi.
Nitaelezea kwa ufupi hayo mateso kwa mfano baadhi, ukisema unaokoka au unampenda YESU, unaingizwa kwenye mafuta yanayochemka uchemke kama samaki na haufi unateseka tu, ila ukimkataa YESU ndio unatolewa je utaweza kuvumilia wakati huo? Jibu hapana. Utakatwa miguu, masikio, wengine watakatwa viungo vya sehemu za siri zinang’olewa na upanga, wengine miguu yote itakatwa na mikono na unabakia hapo chini hakuna msaada unabakia na maumivu miaka saba nab ado utateswa kila siku, je enyi wanadamu utaweza kuyavumilia hayo? Au utachemshwa kwenye maji ya moto kama vile mayai ya kuku na hautolewi mpaka umkane YESU, je utaweza kuyavumilia kwa miaka saba? Amua leo uokoke na ukae katika utakatifu na uishi maisha matakatifu yanayompendeza MUNGU ili MUNGU atakapomtuma mwanae YESU WA NAZARETI aje kuwanyakua watoto ambao MUNGU amependezwa nao na wewe uwe mmoja wapo. Nawaeleza hawa wanaowadanganya watu mwisho wa dunia ni siku Fulani, wasipo tubu na kuokoka leo wajijue jehanamu inawahusu pamoja na dhiki kuu. Ila lazima muelewe wengi wanaotabiri mwisho wa dunia ni lini hao ni wachawi, na siyo watumishi wanaoongozwa na roho wa MUNGU ndio sababu hawakiri kweli kama neno lisemavyo bali aliyepo ndani yao ni roho wa uongo ndio sababu wanatoa habari za uongo.
Omba toba wewe ambaye una dhambi, BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniandike jina langu kwenye kitabu cha uzima wa milele na uninyakue na mimi nisibakie katika dhiki kuu hapa duniani. Nibadilishe fikra zangu niujue kuwa ni unyakuo wa YESU WA NAZARETI kwanza, na mimi uninyakue YESU mwokozi wangu BWANA WA MATAIFA YOTE. Amen.
Karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, sikiliza vipindi vya television, radio na youtube. Fungua www.prophethebron.org utapata maelekezo zaidi. Na pia ulipokwama tuandikie kwa email yetu tutakuombea na kukuelekeza.
YESU WA NAZARETI AKUBARIKI.

NABII HEBRON.

[ad_2]