JE UNAJUA NJIA YA MBINGUNI?… NI IPI?

[ad_1]

Nawasalimu kwa jina la YESU aliye hai na anayetupenda na kutuonyesha njia ya mbinguni, ili alipo yeye na sisi siku moja tufike mbinguni (paradiso) na siyo peponi (peponi ni mahali pa mapepo, wala peponi siyo mbinguni), na hata mtu anayekufa halafu anatamkiwa uende mahali pema peponi, hii siyo sawa, hili neno silo la mbinguni, ni neno la kuzimu, na shetani anamshikilia mtu sababu amekiri mwenyewe anaenda peponi badala ya kukiri ukiwa hai unaenda mbinguni ukafundishwa kusema utaenda peponi hili ni neno potofu la kuua roho za wana wa MUNGU 100% hata YESU alipokufa pale msalabani alishuka kwanza kuzimu (peponi) akawanyang’anya funguo zote kisha akafufuka baadaye akapaa kwenda mbinguni. Sasa swali ni hili wewe utakapofika ule mwisho wako utaenda kwa mapepo (peponi) au mbinguni? Mamilioni ya watu wanapigwa upofu katika ulimwengu wote kwa kutoujua ukweli zaidi katika safari ya kwenda mbinguni au kuifuata njia ya kwenda mbinguni na matokeo yake watu wakiufuata njia ya jehanamu pasipo kujua, na wengine walijua kabisa wapo katika njia ya jehanamu na wanajiita wakristo na wameokoka.
Kazi yangu ni kusema ukweli alionituma YESU peke yake akiwamo na BABA yake. Hapa nitaelezea kuhusu njia ya mbinguni ikoje na utaijuaje hali upo bado hapa ulimwenguni njia hii ni YESU WA NAZARETI, yakupasa uishike njia hii ambaye ndiye yeye peke yake, tena uishike kiimani na kimatendo na kiutakatifu. Jambo la kwanza ni lazima uokoke hiyo ni dalili ya kujua upo katika njia ya mbinguni, na kuishi maisha matakatifu usitende dhambi. Jambo la pili ni lazima uzaliwe mara ya pili (yaani ubatizwe ubatizo wa maji mengi yaani ni yanayotembea na siyo kisima, wala ubatizwe kwa jina la mchungaji, na pia anayekubatiza awe kweli ameitwa na MUNGU na siyo amejiita, au anatafuta pesa au ni mchawi. Nasema hivi sababu watu wengi wameokoka na wakabatizwa kwa maji mengi lakini ukiwaangalia rohoni hauoni kama wamebatizwa na ikiwa hivyo ina maana kuwa aliyembatiza na mtu ambaye ni msanii au anayeifanya hiyo kazi kama maigizo na siyo reality. Mambo haya aliponieleza YESU niliogopa sana akaniambia nenda uwabatize watu wote na mataifa yote sababu 98% ni ubatizo feki hawa waliobatizwa kwa ubatizo wa maji. Na wanaosema wamebatizwa kwa maji ya kikombe nawaeleza hakuna hata mtu mmoja aliyebatizwa, bado mwili wake ni mwili wa dhambi mpaka sasa na kama atakaa hivyo hivyo bila kubatizwa ubatizo wa kweli hakika mbinguni hataenda. Na kama mpaka sasa haujabatizwa ubatizo wa kweli uelewe haupo katika njia ya mbinguni, na zaidi ukisoma kitabu cha Yohana 3:1-10  inaelezea mtu asipozaliwa mara ya pili hataweza kuingia katika ufalme wa MUNGU (verse 5).
Sasa watu wanapigwa upofu katika eneo hili la ubatizo ambalo ni muhimu sana, ili uzaliwe mara ya pili ni lazima ubatizwe kwa maji mengi, YESU anaiita        kuzaliwa mara ya pili sababu ukisha zaliwa kimwili na ukisha kuwa mtu hauwezi tena kuingia katika tumbo la mama yako, hivyo kiroho kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya ubatizo wa maji mengi peke yake kama alivyobatizwa YESU WA NAZARETI, hivyo mpaka hapo utazidi kufunguka akili yako na utakuja ubatizwe ubatizo mtakatifu uzaliwe kiroho. Na adui mwingine wa kuwpofusha watu wasizaliwe mara ya pili ni DINI, tazama Nikodemo yeye alikuwa ni mmoja wa Mafarisayo  na yeye alikuwa anamjua YESU kuwa yeye ni mwalimu na ni ametoka kwa MUNGU. YESU akamfungua Nikodemo (mtumishi wa dini), haitoshi kujua mimi ni mwana wa MUNGU ikakusaidia uwe katika njia ya ufalme wa mbinguni, yakupasa uzaliwe mara ya pili, ki vipi? Ni ubatizwe ubatizo wa maji mengi peke yake, hivyo nataka uelewe umuhimu wa ubatizo au ubatizo ndio kuzaliwa kiroho na uishike njia ya mbinguni. Siku hizo makanisa mengi yanakuwa ni yale yale ya mafarisayo yanaamini YESU ametoka kwa MUNGU tu na hawabatizwi au kuzaliwa mara ya pili. Nasema hivi unapobatizwa kwa ubatizo wa maji ya kikombe au kisima au kwa jina la mchungaji, wewe mpaka sasa haujazaliwa kiroho bado unao utu wa kale wa dhambi na bila kubatizwa mbinguni hautaenda, hiyo ndiyo formula ya MUNGU. Leo hii kina Nikodemo (watumishi) wapo wengi wapo katika DINI wanaeneza injili ambayo ni MFU sababu bado hawajazaliwa kiroho, kama unabisha tafuta katika biblia kama utaona mahali imeruhusiwa watu wabatizwe ubatizo wa maji wa beseni, kikombe, kichwani tu, jibu haupo na kama haupo je hayo ni ya ufalme wa MUNGU? Au njia ya mbinguni? Jibu ni ya njia ya jehanamu, tokeni huko wewe unayependa kwenda mbinguni, uamuzi ni wako wewe.
Shetani ameliteka kanisa na kulivuruga kiasi ambacho nasema siyo kanisa la YESU WA NAZARETI bali ni kanisa la Mafarisayo, ni kanisa ambalo halijazaliwa kiroho bado lipo katika dhambi, huo ndio ukweli injili haifai kupapasa, injili ni kweli tupu na kweli ya MUNGU ndiyo iwawekayo watu HURU. Sasa unaposhiriki katika kanisa ambalo au mtumishi ambaye hana njia ya mbinguni na wewe anakupoteza kabisa, na nimekufundisha machache tu ambayo utayachunguza kimwili na zaidi soma makala ya Nabii Hebron Tanzania, utaijua njia ya kweli ya mbinguni na wewe uifuate kiimani, kimatendo, na kiutakatifu. Watu wengi wanajiita ni wakristo lakini hawajazaliwa mara ya pili, bado wana asili ya dhambi na wapo chini ya Mafarisayo wanaamini tu YESU ni mwana wa MUNGU, sawa je unajua hata mashetani wanaamini hivyo hivyo tu. Jitofautishe leo uokoke na ubatizwe ubatizo wa kweli, kinyume nakueleza jehanamu inakuhusu, na zaidi uelewe YESU hatakuja kuchukua wenye dhambi ni watakatifu peke yake. Sasa jichunguze je bado haujabatizwa na maji mengi? Je si unaona unayo dhambi bado? Ili dhambi hiyo ikutoke ukabatizwe, tazama Nikodemo alishtuka na wewe usktuke leo, mahali pasipo na ubatizo wa kweli au maji mengi yanayotembea mahali hapo uelewe ni gizani tu au pa kuwapotosha watu kama ilivyo katika ulimwengu wote. Watu hawasemi ukweli kuhusu YESU na neno lake, watu wanachanganya na uongo, hii ni dhambi na unayetenda hayo wewe ni mtenda dhambi na ni adui wa YESU. Bila kubatizwa ubatizo wa maji mengi mbinguni hauendi sababu bado unayo dhambi uliyorithi kwa Adam haijalishi unajiita mkristo, wewe ni mkristo hewa.
TUBU:
BWANA YESU naomba unisamehe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, na uniongoze wewe nikabatizwe ubatizo wa maji mengi na wa kweli na nibatizwe na mtumishi uliyemtuma afanye kazi yako ili ubatizo wangu uwe halali kwako niweze kuzaliwa mara ya pili ili nishike njia ya mbinguni na niishi maisha matakatifu na ROHO MTAKATIFU aniongoze.
NABII HEBRON.

[ad_2]