JE UNAJUA SURA YA JOKA KUU?! JOKA KUU SURA YAKE IPO HIVI….

[ad_1]

Ufunuo wa Yohana 20:1-3
1kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na shetani, akamfunga miaka elfu. 3Akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.”
BWANA YESU ASIFIWE, nitawaeleza kwa ufupi jinsi sura ya joka kuu ilivyo, maana nilimuona kwa macho yangu tarehe 5.11.2012 muda saa sita ya usiku. Nilichukuliwa na serikali ya mbinguni pamoja na Malaika Mikaeli ambaye ndiye malaika mkuu wa vita, nilichukuliwa katika uliwengu wa roho nilivyokuwa naomba japo nilipewa taarifa kutoka mbinguni taarifa ambaye Malaika Gabriel alikuja kunijulisha akaniambia leo saa sita ya usiku itakapogonga saa sita kamili uwe katika maombi na baadhi ya watumishi wangu, akaniambia atakamatwa joka kuu leo, basi ilipofika muda huo katika maombi, alishuka malaika mkuu na funguo (Mikaeli) ukakamatwa na mamilioni na nililiona kwa macho yangu, ilikuwa ni vita ambavyo sijawahi kuona tokea kuzaliwa kwangu au kuisikia jinsi malaika wa MUNGU walivyopigana mpaka akashikwa, na kuamuriwa aiteme dunia aliyoimeza katika ulimwengu wa roho  na vingine ambavyo sijaruhusiwa kutaja bado. Na kuanzia tarehe 5.11.2012 ndipo ilianza ile miaka elfu moja. Sasa watu wengi wanafikiria atakuja malaika kimwili watamuona amkamate joka kuu, hapana. Vita vyetu ni katika ulimwengu wa roho na tayari sasa tupo katika miaka 1000, na mtaona ufalme wa mpinga kristo ukibomoka kila siku, na watumishi waliokuwa wanatumia nguvu za giza wataporomoka sababu hawana pa kupatia msaada tena.
Mnapoyaona msishangae, mengine mtasikia ni manabii na watu waliwaamini, lakini watapatwa na aibu nanyi myaonapo muelewe haya niwaelezayo mimi Nabii Hebron. Joka kuu sura yake ipo hivi, ni joka likubwa na sura ya uso wake inafanana na mtu bali katika kichwa chake kuna magamba na anavichwa saba, na katika mkia anayo kucha kubwa. Mpendwa msomaji inatisha sipendi kuendelea zaidi, ila mpaka hapo umeijua sura yake. Naifahamu sababu nilimuona na nilishuhudia akifungwa na mimi nilitumika kwa neema ya MUNGU na nilimpiga. Huyu ndie kiongozi au baba wa miungu yote, wachawi, wapinga kristo, lusifa, amjini, mapepo na lengo lake ni kuhakikisha hakuna mtu ataenda kwa YESU. Amewawekea watu mioyo migumu wasiokoke, kama haujaokoka uelewe ni joka kuu anakushikilia hadi sasa, na YESU akija utabakia kwake. Karibu uokoke sasa, sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, nitoe katika mikono ya joka kuu, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, uniongoze wewe, najikabidhi kwako YESU WA NAZARETI. Amen.
NOTE:
Nakufunika kwa damu ya YESU WA NAZARETI.
NABII HEBRON.

[ad_2]