JE UNAJUA SURA YA SHETANI?! SURA YAKE IPO HIVI…..

[ad_1]

BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye BWANA WA MABWANA na MFALME WA WAFALME na pia aliye BABA YANGU NA MWOKOZI WANGU, yeye aliyeniokoa nay eye aliyeniita nikamtumikie sawa sawa atakavyo ili kuwarejesha ulimwengu wote kwake, sababu aliwatuma watumishi wachache nao wakamsaliti YESU na wengine wakajiunga na freemason na wengine kuzimu nay eye YESU akawaacha. Kazi aliyonipa ni kubwa ila nitaelezea leo kuhusu shetani alivyo, mimi nimempata bahati ya kumuona shetani alivyo na nilimuona wakati nilikuwa na malaika wa serikali ya mbinguni.
Nimeamua kuwaelezea alivyo sababu kabla ya hapo hata mimi nilikuwa sinjui alivyo, nikionyeshwa picha za ajabu na za aina aina, ila ukweli hakuna kata picha moja ambaye ni ya kweli ambaye niliyoiona katika ulimwengu huu. Hii ni neema ya YESU alipenda nimuone na nimshughulikie kuharibu ufalme wake na bado naendelea mpaka atakaporudi YESU kuja kulinyakua kanisa lake. Shetani ambaye anaitwa lusifa yeye sura yake alivyo nitaelezea at least upate picha. Yeye yupo kama mwanadamu yupo uchi anayo mabawa mawili mgongoni kama vile ya malaika, pia anaomkia mrefu katika sehemu zake za nyuma, pia mkono wa kushoto katika kidole kidogo anaoukucha mrefu sana na pia katika macho yake, katika jicho lake la kulia amepaka wanja kama vile unavyoona watu hapa ulimwenguni wanavyopaka wanja katika macho ila shetani yeye anapaka katika jicho moja la kulia.
Ni jitu la kutisha kama hauna YESU wa kweli. Natumaini mnapata ukweli halisi, mimi Hebron namfahamu vizuri ndio sababu haniwezi na hatakaa aniweze, nitaendelea kuangamiza majeshi yake na kazi zake zote, sawa sawa na nilivyotumwa na YESU WA NAZARETI pamoja na MUNGU aliyeniumba. Shetani huyu lengo lake akuteke wewe na wengine wasiende mbinguni ili wakachomwe nae. Na wewe okoka sasa, usije ukakutana naye huko alipo akakuteka.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizosababishiwa na shetani adui yako. Namkataa sasa hivi, naja kwako YESU uniokoe, nitoe katika mikono yake, niwepo katika mikono yako, na katika kitabu cha ufalme wako. Shetani sikutaki kuanzia sasa YESU WA NAZARETI niongoze, mimi ni mali yako sasa. Amen.
NOTE:
Kama haujaokoka mpaka sasa uelewe wewe ni mali ya shetani. Ili uwe mwana wa YESU kiri hiyo sala ya toba hapo juu.
Nakufunika kwa damu ya YESU WA NAZARETI aliye hai.

NABII HEBRON.

[ad_2]