Close

JE UNAJUA WATUMISHI (WAKUNGA) WANAZALISHA WATU MARA YA PILI (KIROHO) KWA NJIA ZA UONGO? JE UNAJUA MADHARA YAKE?


BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote ambao tayari ambao tayari mmezaliwa mara ya pili kiroho na hata wale ambao hawajazaliwa mara ya pili kiroho katika mpango aliouleta YESU. Lengo langu ni mfunguke sababu yamkini haujui au hauelewi kuwa bado haujazaliwa mara ya pili au unaona upo sawa na ni kiumbe kipya na kumbe bado wewe ni kiumbe kile kile cha mwili na bado asili ya dhambi ipo ndani yako. Zaidi soma katika makala ya Nabii Hebron, soma la KUZALIWA MARA YA PILI  nimeelezea vizuri na natumanini utaelewa na utafunguka zaidi na roho yako ipone.
Watumishi wanaozalisha watu kwa njia ya uongo au upotofu, au kwa njia za formula ya miungu au mungu asiyejulikana, na ambaye makao yake yeye ni jehanamu na ni mpinga kristo, watumishi hawa utawajua katika tendo lao la kubatiza, utaona ni ubatizo ambao haupo katika biblia (ubatizo wa mungu asiyejulikana na wa yesu wa uongo ili kukulaghai wewe uone umezaliwa tayari kiroho na umeondolewa dhambi kumbe umepigwa upofu. Hawa ni manesi wa shetani ambao ndani yao ipo roho ya mpinga kristo na kumpinga MUNGU na kuharibu neno la MUNGU na kulichanganya na uongo. Kibinadamu anayezalisha hospitalini anafuata kanuni za kuzalisha na endapo atakosea au kufuata kanuni tofauti mtoto atakufa, na pia kiroho mtu ili azaliwe kiroho zipo kanuni zake na amezileta MUNGU yeye zitumike ili aweze kuzaliwa mara ya pili kiroho, na ikiwa ni tofauti basi mtu huyo anapozalishwa kiroho kwa kanuni ambazo sizo za MUNGU mtu huyo anawaua kiroho na anakufa bali kimwili anaonekana anatembea. Ili uelewe amekufa kiroho, utaona anajiita ni mkristo wa kanisani anaenda lakini hajaokoka, anatenda dhambi, ni mlevi, ana wake wengi, waume wengi na yupo kwenye dini bado badala ya kuiga mfano wa Nikodemo katika dini akamfuate YESU sababu katika dini ni mahali pa dhambi na watu hawajijui na hawaendi mbinguni wamepigwa upofu sababu hawazaliwi mara ya pili kwa kufuata kanuni alizozianzisha MUNGU ili zifuatwe ndipo mtu ataweza kuzaliwa mara ya pili kiroho. Watu wengi wamezaliwa mara ya pili katika wrong formula na matokeo yake hawaendi mbinguni, ubatizo wao imekuwa ni kama vile mtu amejitupa katika maji kama vile bata au chura kasha akatoka akakauka.
JINSI YA KUELEWA MKUNGA FEKI WA KIROHO.
·        Kwanza anazalisha watu kwa mara ya pili watoto wadogo badala ya watu wazima, na anatumia maji ya kikombe na pia kumwekea msimamizi mwanamke au mwanume ndio mashahidi wako ukikua wanakuelezea badala ya kukubali ukiwa na akili yako uone kwa macho yako, peke yako na uokoke.
·        Atakubatiza kwa jina lake anachanganya na la YESU.
·        Anakubatizia katika kisima ndani ya kanisa au nje badala ya mtoni katika kijito cha utakaso maji yanayotembea kama vile Yordani.
·        Atakuchaji pesa za malipo ya ubatizo.
·        Yeye mwenyewe amebatizwa ubatizo wa maji ya kikombe (amekufa kiroho) hivyo na wewe anaiua roho yako.
·        Mtumishi ambaye amejiita, anatafuta pesa, kanisa linalofanya biashara na kuchangisha pesa, hapo ni mortuary ya kiroho.
·        Mtumishi ambaye hajaokoka na kuitwa na MUNGU na ni mchawi na ni freemason.
·        Watumishi wanaovaa kofia wakati wa kubatiza au kuhubiri (1 Wakorintho 11:7-8).
·        Watumishi wenye huduma tofauti na zile tano alizozianzisha YESU halafu wakazipa wengine majina yao na vyeo vyao.
·        Watumishi wanaozini na waumini, wanyang’anyi wa mali za waumini, wanaofanya mazingaumbwe, mfano misukule, kutoa watu vitu vinavyoonekana katika mwili wa binadamu mfano mawe, misumari, sigara na vinginevyo vyote hayo ni mapepo.
·        Watumishi wanaovaa misalaba, kuabudu misalaba (hawa ni waabudu sanamu na mtu uelewe kama haujui ukitenda hayo uelewe umetekwa nafsi yako badala ya kumuabudu MUNGU aliye hai unakuwa unaabudu miungu na wewe binadau pasipo kujua unakuwa na wewe umeabudu miungu wakati unampenda MUNGU, funguka sasa.
Yapo mengi zaidi, soma kitabu cha Nabii Hebron cha UBATIZO WA KWELI KWA WATU WOTE, utapata soma na utapona na wewe uendelee kusema kweli na watumie watu kila mahali ili watu waponywe na watoke katika mikono ya shetani. Na zaidi watumishi wa jinsi hii fuatilia mienendo yao na matendo yao ndio yatakupa picha ya uwazi haya nimekufunulia katika mwili ili uelewe kwa urahisi. Hawa siyo wazalishaji wa watu katika roho kwa mara ya pili bali ni waangamizaji wa roho za watu katika roho. Kama vile mkunga wa kibinadamu anapokuwa anazalisha bila kujua mtoto anatokea wapi badala ya sehemu yake yeye anatafuta mtoto azaliwe katika kisigino cha mguu, je mtoto atazaliwa kupitia katika kisigino? Jibu haiwezekani milele.
Basi ndivyo ilivyo wengi hawajazaliwa mara ya pili mpaka sasa sababu ya formula ya elimu ya wanadamu badala ya elimu ya MUNGU ambaye yeye peke yake ndiye anayemzaa mtu kiroho mara ya pili na yeye anao manesi wake aliowateua kufanya kazi hiyo yaani watumishi wa kweli na anaowajua yeye, siyo waliojiita, siyo wanaotafuta pesa, wachawi, waliomsaliti.
NOTE:
Uwe makini jichunguze, angalia usije ukawa unapoteza muda miaka yote ukifikiri utaenda mbinguni na umezaliwa mara ya pili, kumbe bado dakika hii haujazaliwa kiroho kikweli. Amua ubatizwe mara moja zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, uje ubatizwe uzaliwe mara ya pili na katika huko ulipo haijalishi utatengwa na dini wewe furahi sababu umekuwa nuru hauna giza (dhambi ya asili hivyo watakuona siyo mwenzao na wewe waeleze bye bye naenda mbinguni.
BWANA YESU naomba unisamehe, uniokoe, unifungue akili na roho yangu ili nizaliwe upya mara ya pili, uniongoze kwa mtumishi uliyemteua ili nizaliwe kikweli sawa sawa na mpango wako, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, niishike njia yako ya mbinguni na roho wako aniongoze siku zote. Amen.

NABII HEBRON.