JINSI KANISA LILIVYOJIINGIZA KWENYE FREEMASON KWA KIASI KIKUBWA

JINSI KANISA LILIVYOJIINGIZA KWENYE FREEMASON KWA KIASI KIKUBWA

[ad_1]
















FREEMASON NI NINI?

Ndugu msomaji wa blog hii, huu ni wakati wa yale yote maovu yaliyofanyika na yanayondelea kufanyika kinyume na maagizo ya MUNGU kufichuliwa sasa (Mathayo 10:26-28).
Mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU, YESU anakupenda sana, haijalishi upo nchi gani, bara gani, una rangi gani, au cheo gani, iwe ni wafalme, marais, viongozi na hata wasio na chochote, siku ya leo nakuletea agizo nililoambiwa na YESU niueleze ulimwengu wote kuhusu freemason ndani ya kanisa ili upone na usiangamie! Maana kwa sasa, asilimia kubwa kanisa linaongozwa na freemason, ulimwenguni mwote imebaki asilimia kidogo sana. Ila sasa ndio mwisho wao. Wengi watajiua, kuwa vichaa, kazi hii anaifanya YESU mwenyewe na wazee 24 waliopo mbinguni. Haya yote ninayokueleza ndivyo ilivyo.
FREEMASON KATIKA KANISA:
Huu ni mtandao wa shetani 100%. Shetani anashirikiana na watumishi waliomwasi MUNGU na ndani yao ipo ile roho ya Yuda Iskariot aliyemsaliti YESU, na yaliyompata Yuda Iskariot yatawapata wote walio wanachama wa freemason. Watu wote walio kwenye mtandao huu ni watoto wa shetani na siyo wa YESU.
Mtandao huu unapojiunga lazima uingie kwenye mtandao wao kupitia (google) kuna kadi ya usajili na unapojaza taarifa zako (majina), kuna mahali mtandao unakuambia toa damu yako ya kidole, unaweka kwa computer screen halafu ndipo jina lako linasajiliwa, na ndani ya huo mtandao ipo roho ya shetani inakuvaa papo hapo. Baada ya kutoa damu yako, analamba shetani au kwa lugha nyingine unampa shetani uhai wako na maisha yako!
Baada ya kuwa mwanachama,  sasa ndiye anakaa ndani yako, utu wa MUNGU unaondoka, shetani anakaa ndani yako, na anaanza kukutumia kuharibu na kuwaua wana wa MUNGU kiroho na kimwili. Ukisoma katika injili ya Mathayo 7:2-24 hawa ndiyo manabii wa uongo; utawatambuaje? Kwa matendo yao. Ingia katika internet, utawaona na hayo matendo yao, na ule mwisho utakapofika, YESU atawaambia “sikujui”. Watu hawa hutumiwa na shetani ndani ya kanisa kuwapeleka kuzimu na watu pasipo kujua wanapelekwa wapi. Watu wote wanaoongozwa na mtumishi wa freemason, hamna hata mmoja anaenda mbinguni. Ufunguke ufahamu wako YESU hana ushirika na shetani, hata wewe unalijua hili. Usiangalie miujiza, kwani hata shetani anayo miujiza, kumbuka hata Farao alifanya miujiza kupitia waganga akishindana na MUNGU na Musa, tofauti ni kwamba miujiza ya MUNGU inaangamiza hata miujiza ya shetani, kama vile nyoka wa Musa alivyowameza nyoka wote wa Farao. Ukikuta jina la mtu kwenye mtandao, amini kabisa ni ukweli, maana ili jina lisajiliwe kwenye mtandao wa shetani ni lazima utoe damu yako kwa hiari yako mwenyewe, kinyume na hapo, hata mtu aingize jina lako haliingii. Mkimbie mtumishi wa namna hiyo. Ni kwa mabara yote wamejaa, America, Europe, Asia, Africa, na mengineyo! Na hawa ambao majina yao yapo, hawa ndio wale wasaliti wa YESU 100%. Usikubali kuongozwa na mtumishi aliyemsaliti YESU, anakuunganisha na wewe kwenye ulimwengu wa kiroho wa kipepo bila wewe kujua! Tabia zao 100% lazima huua wanadamu, kutoa makafara, na wengi hufanywa misukule, ila hao huishi maisha ya kuwaibia nyota zenu na mnashangaa wanakuwa matajiri ghafla, na ni wazinzi. Wote huu ndio ukweli YESU alioniambia na mimi nakueleza. 
Kwa msaada ili utolewe huko, fika kanisani kwangu; YESU amenipa mamlaka ya kumtoa mtu atakayetubu hadharani, ni kitu cha dakika chache, nakutoa kwa jina la YESU. Kwa wale mliokuwa hamjui madhara yake na ukikataa masharti yao, lazima na wewe wakuuwe! Nilipelekwa kuzimu na kuonyeshwa wanavyoteseka. Ewe mwanadamu, usijaribu. Wanajuta sana. Wapo marais wengi waliokufa, wanamuziki, viongozi wa dini, matajiri wanalia na wanateswa na shetani. Niliogopa kuona sura za viongozi maarufu duniani huko kuzimu wanatumikishwa kuliko hapa duniani, au hata mateka wa vita, haielezeki.
JINSI YA KUWAPATA NA KUWAJUA WATUMISHI WA KI-FREEMASON
Ingia kwenye internet, andika mji au nchi halafu “search”. Kama yupo, jina lake utaliona na kama hayupo, jina lake hautaliona. Pia, wapo watumishi ambao wanapatikana kupitia mitandao ya kijamii ambao ni wanachama wa mtandao wa freemason.
Mfano, waweza kuingia mtandao wa google, halafu ukaingiza neno wachungaji freemason. Hii itakuletea habari za wachungaji na viongozi freemason, na unaweza kusoma zaidi na ukajua mengi, na jinsi ya kujihadhari nao.
KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, litakusaidia kuvunja agano ulilounganishwa nalo kwa freemason. Fika kanisani Moshono – Arusha, na utasaidiwa bure kutolewa kwenye mtandao huo, kupitia Mtume na Nabii Hebron, aliyepewa na YESU mamlaka ya kuwatoa walioingia au kuingizwa katika mtandao wa freemason na kubatilisha agano walilojiunganisha nalo kwenye mtandao huo.
Pichani chini, Mtume na Nabii Hebron akifawafungua watu kutoka katika vifungo mbalimbali katika ibada iliyofanyika katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, kama inavyoonekana wakiwa wameshikilia vazi lake, na nguvu ya YESU iliyopo ndani yake iliwaponya wote (Mathayo 9:20-22).
Wagonjwa na wenye vifungo mbalimbali wakishikilia vazi la Mtume na Nabii Hebron wakati wa maombi ya kuwafungua. Kila aliyeshikilia Vazi la Mtume na Nabii Hebron, alipata uponyaji siku hiyo kama NENO la MUNGU linavyosema (Mathayo 9:20-22).
MATUKIO YA IBADA YA LEO TAREHE 16 DESEMBA 2012 KATIKA KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

Waumini walipata fursa ya kumshika Mtume na Nabii Hebron, ambapo walipokea nguvu na baraka kutoka kwa YESU mwenyewe aliyeshuka kupitia mwili wa Mtume.

Waumini wakiendelea kumshika Mtume na Nabii Hebron kupokea baraka za YESU zilizoshuka ndani yake wakati wa ibada ya leo.

Mtume na Nabii Hebron akimshukuru MUNGU kwa baraka alizoziachilia kwa kanisa na kwa matendo makuu na makubwa yaliyotendeka kanisani hapa katika ibada ya siku ya leo.

Ndugu msomaji wa blog hii, ili kupata msaada zaidi, wasiliana nasi kupitia namba za simu zilizoonyeshwa hapo chini, au fika kanisani Moshono – Arusha.

Pia kwa mafundisho zaidi, tembelea website hii www.prophethebron.org
 Kwa mawasiliano;

+ 255 759 610 820
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149


Email:
[email protected]

Imeandaliwa na Priscus & Dorcas Macrine,

KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

[ad_2]