Close

JINSI KANISA LILIVYOPINDULIWA KUTOKA HUDUMA TANO NA KUTUMIKA NA SHETANI MAKANISANI (ALL OVER THE WORLD)!!!


YESU WA NAZARETI alipokuja hapa ulimwenguni alianzisha huduma hizi tano ndani ya kanisa lake ambalo alikuja kulijenga yeye peke yake. Huduma hizi ndizo silaha za kupeleka injili katika ulimwengu wote na kumshinda shetani; ukisoma katika kitabu cha Waefeso 4:11-12; “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.”

Ndugu msomaji mpaka sasa umepata picha kiasi fulani kuwa YESU ndiye aliyeamrisha huduma hizi tano ili kazi yake na mapenzi ya MUNGU yatendeke katika ulimwengu wote kama vile yeye alivyokuwepo na kwa kwanzia aliwateua wale wanafunzi wake kwanza. Sasa alichokifanya shetani baada ya wale wanafunzi wa YESU kumaliza muda wao wa kuishi katika ulimwengu huu, shetani akazivuruga hizi huduma tano na yeye akateua manabii, mitume, wachungaji, wainjilisti na waalimu hivyo hivyo, lakini kwa macho ya nyama hauwezi kuelewa kama ni mtumishi wa shetani labda kama unayo macho ya rohoni au unaye ROHO MTAKATIFU wa kweli ndio utamjua kuwa huyu siyo nabii, mtume, mchungaji, mwinjilisti, mwalimu ambaye asili yake ndio wale wa kanisa la kwanza.
Zaidi shetani alitumia mbinu kubwa sana ili kuwapiga wanadamu upofu uwaamini au uamini mtu yeyote anayeitwa mchungaji, nabii, mtume, mwalimu, mwinjilisti kuwa hawa wametoka kwa YESU na ndivyo ilivyo mpaka sasa, watumishi wengi kiasi cha kutisha ni watumishi wa uongo na matapeli na watu wengi wameshindwa kuwatofautisha sababu tu eti anaitwa mchungaji bazi anaaminika, ila leo utafunguka, yeye aliyeanzisha kanisa YESU wa Nazareti amenioa kazi ya kuukomboa uliwengu wote nikiwa na serikali yake ili kuwatoa watoto wake wanaoshikiliwa na mbwa mwitu, ambao wanajifanya wanamtumikia YESU WA NAZARETI kumbe ni mbwa mwitu. Wanaitwa mbwa mwitu sababu mbwa mwitu hana huruma hata akimkuta mnyama porini yeye humkimbiza mnyama na wakati anatembea yupo hai yeye hungata sehemu ya mwili na huendelea kula wakati mnyama akiwa hai, hivyo hivyo ndivyo hawa watumishi walioitwa na shetani na wale waliomsaliti YESU, huwaangamiza waumini na kuwaua roho zao ingali wapo nao hawana huruma. YESU aliposema watakuja makristo wa uongo yeye alishayajua, sasa cha kuelewa hapa, ni hivi jambo la kwanza, vile vyeo vya makanisa ya dini ambayo YESU na yeye aliyakuta ambayo mafarisayo na masadukayo ndiyo walikuwa wakiyaongoza, wao walikuwa na vyeo vyao mfano Askofu, na katika kanisa aliloliamrisha YESU yeye hakuweka Askofu, bali aliweka mitume, manabii, wachungaji, wainjilisti na waalimu ili waijenge mwili wake yaani kanisa lilo hai.
Cha ajabu sasa ufunguke uelewe zaidi na ufahamu wako na akili yako jiulize wewe peke yako je UASKOFU ndiyo huduma ya kuongoza hizi huduma tano? Jibu siyo, hapa tayari elewa kanisa limepinduliwa na shetani na kuvuruga huduma tano na kama zimevurugwa basi uelewe ni shetani, haijalishi hata kama wanalitaja jina la YESU, hapo tayari huduma tano zimeuwawa na shetani. Huduma inatakiwa iongozwe na mtume na nabii na siyo Askofu, tafuta katika biblia wapi YESU amesema maakofu ndio huduma tano alizozianzisha  ili kulijenga kanisa? Jibu hakuna, hata mimi namshukuru sana YESU, japo ni kiongozi mkuu katika huduma ya YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE ndani ya moyo wangu nilikuwa sipendi kabisa hili cheo cha mimi kuitwa Askofu kabisa, nilizidi kumtukuza MUNGU kwa ajili ya roho wake mtakatifu kunishuhudia haifai kabisa na kukinai hicho cheo na pia nilijiulizaga sasa mbona mimi aliponituma na hata siku zote hajaniita Askofu zaidi akaniita Nabii wangu, mtume wangu au Baba wa mataifa wa sasa (Ibrahimu) lakini siku zilivyozidi ndivyo alinifundisha sababu mwanzoni ilikuwa ni ngumu kumuelewa ila sasa namuelewa.
Katika siku chache zilizopita YESU akawa ananifundisha habari hizi za huduma tano na kunifunulia vizuri ili niwafungue macho na mataifa yote wamjue YESU vizuri ili wapone roho zao, akaniambia YESU hivyo ndivyo shetani alivyofanya na hata kuwatumia wale ambao kweli niliwaita ila sasa wamenisaliti sasa wanatumika upande wa adui badala ya kulijenga kanisa langu sasa wanatumika kulibomoa kanisa langu na kulijenga kanisa la mpinga kristo na watu hawajielewi yaani waumini, ila sasa uwaeleze na uwafundishe na watanirejea mimi.
1.     Jambo la kwanza huduma zote ambazo kiongozi anaitwa Askofu badala ya Mitume au Nabii hizo tayari zimeenda upande mwingine na pia wapo watumishi waliopo na mimi na wameiga, wakajipa jina la Askofu badala ya huduma niliyoweka ndani yake, hii ni makosa, unayetaka kupona tubu na uachane na cheo hicho kwa ajili ya kuongoza kanisa. Umeelewa asili ya cheo hicho siyo katika huduma tano alizozianzisha YESU, na kama siyo asili yake sasa hauoni tayari umebadili neno la MUNGU? Na je hauoni utakuwa na wewe ni mwenye dhambi? Amenituma niwaeleze ukweli ufunguke. Haiwezekani kabisa Askofu awe mkubwa kuliko zile huduma alizozianzisha YESU kwa kazi maalum ya kujenga kanisa lake, je kama hajazzianzisha (Askofu) je atautumia jibu hata utumia bali adui ndio atautumia na ndiyo sababu huduma hizi tano badala zikue zinazidi kufifia hii ni sababu zimetekwa na shetani na huduma hizi zikapewa zikapewa huduma tofauti ya sita ambayo YESU hajaitaja wala teua.
HUDUMA TANO ZA SHETANI JINSI ZILIVYO
·       Kwanza kabisa uelewe zinaitwa pia kwa majina haya yafuatayo: Manabii, Mitume, Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu. Sasa jinsi ya kuwaelewa kimwili nitaelezea zaidi sababu watu wengi hawana macho ya rohoni ila wenye macho ya rohoni wanaelewa vizuri.

·        Kwanza injili wanayoihubiri ni injili isiyo nyooka, ipo ina michanganyo ya kweli na uongo humo humo. Mfano watahubiri lakini matendo yao ni uovu mtupu au amefanya kazi hiyo kwa ajili ya kupata mshahara tu, au wanafanya biashara katika nyumba ya MUNGU na kuchangisha pesa na harambee makanisani. Wanahubiri halafu hapo hapo wanabusu sanamu, au wanapinga wokovu au wanabariki pombe au ukiona katika makanisa wengine wanajipa vyeo ambavyo havihusiani na huduma tano alizozianzisha YESU, ili kulijenga kanisa lake, ukiona wanamjua tofauti uelewe hao wanaujenga ufalme wa mpinga kristo. Na hata hao wote wanaowaongoza hawawapeleki mbinguni bali wanawapeleka kuzimu wanabomoa maisha yao katika ulimwengu wa roho.
·        Wachungaji walio wachawi au freemason, wafufua misukule hao wote wameitwa na shetani, hivyo watu msiwaamini tena, hawa ni mbwa mwitu lengo lao ni kuziua roho za wana wa MUNGU kama ilivyo sasa.
·        Anayekubatiza kwa jina lake, (ameitwa na shetani au ameachwa kwa YESU).
·        Anayebatiza ubatizo wa maji ya kikombe (ameitwa na shetani).
·        Anayetoa huduma ya kiroho kwa kuchaji pesa (ameitwa na shetani).
·       Anayekopa benki wakati YESU alisema msisumbuke mtakula nini mtavaa nini (anayesumbukia hayo hayupo katika msingi wa YESU wa huduma tano zake bali yupo katika msingi wa huduma tano za shetani na mpinga Kristo.
·        Kufanya ibada za wafu.
·       Na wengine watajiita wachungaji, manabii,mitume, wainjilisti, waalimu peke yake, na wanaongoza huduma zao ila vyeo hivyo siyo kutoka kwa YESU, wamejiita, wanajifanya au walishamsaliti YESU au wameteuliwa na shetani kwa kusudi la kuziuwa roho za wana wa MUNGU tu ila siri hii wao wanaijua na kazi yao wanawapiga waumini upofu kila siku ili wasiwaelewe uovu wao na njia zao.
·        Na huduma zote ambazo watumishi wanategemea michango ndio zifanye kazi hizi asili yake siyo huduma tano za YESU bali asili yake ni shetani.
NOTE:
Na tabia au matendo ya uongo yanayotendeka katika makanisa yao kinyume na biblia uelewe sasa ulikuwa unaongozwa na huduma tano za shetani na siyo za YESU, mamilioni ya watu wanampenda YESU WA NAZARETI, ila kwa sababu ya hawa wenye huduma tano za shetani na wanayaongoza makanisa 98% na hata kuongoza sala za toba watu hawajampokea YESU mpaka sasa bali walimpokea yesu wa uongo kupitia vinywa vyao, utubu leo tena kwa usalama uhakikishe jina lako lipo mbinguni utakapo hivi tena sasa.
SALA YA TOBA:
BABA YANGU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU, NAMKATAA SHETANI NA HAO WOTE WENYE HUDUMA TANO ZA SHETANI WALIONINAJISI NA KUNITENGA NA WEWE PASIPOKUJUA. NAKUPENDA YESU WA NAZARETI, NIOKOE LEO HII. UNIANIDKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE. UNIONGOZE WEWE MAHALI AMBAPO WEWE ULIWEKA MISINGI KAMILI YA HUDUMA TANO ILI KANISA LIJENGWE NDANI YA WATU NA WAPONE NA KUURITHI UFALME WA MUNGU. NAJITENGA NA MAFUNDISHO YA MPINGA KRISTO. AMEN.
Karibu sana katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

NABII HEBRON.