JINSI KONDOO WA YESU WANAVYOBADILISHWA NA KUWA WANA WA MBWA MWITU PASIPOKUELEWA.

[ad_1]

YOHANA 10: 1-6
“YESU aliwaambia, amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwe penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni. Mithali hiyo YESU aliwaambia; lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia.”
Leo watoto wa MUNGU nitawafundisha jinsi ya kuelewa kuwa wewe  ni mwana kondoo wa YESU au ni mwana wa mbwa mwitu, nasema hivi sababu idadi kubwa ya wanadamu aliowaumba MUNGU na akamtuma mwanae wa pekee ili awe mchungaji wao kwa wale watakaoisikia sauti yake watakuwa kondoo wake na yeye atawachunga, ila wale ambao hawataisikia sauti yake hao hawataingia katika zizi lake ili awalinde yeye. Sasa katika ulimwengu wote shetani amewapiga upofu wakristo wengi wakaona wao tayari mchungaji wao ni YESU WA NAZARETI na kumbe bado wapo katika zizi la mbwa mwitu na wafanyika kuitwa mbwa mwitu pasipo kupenda katika ulimwengu wa roho kwa sababu baba zao wa kiroho hawaongozwi na YESU bali wanaitumia jina lake kunyanganyia watu mali na kuiba pesa za waumini kwa kuwalaghai; YESU kawatuma hizo pesa na kumbe YESU hajatuma wachungaji pesa ili mtoe kama hospitali ndio mponywe.
Sauti ya YESU ni neno lake la kweli ambalo halijabadilishwa au kuchanganywa na uongo. Mfano  wewe mkristo unajua neno linasema usiabudu sanamu, halafu unakuta kanisa linajiita kwa jina la Kristo na linaabudu sanamu, na watu wote waumini wanatii hilo neno, ujue sasa hiyo siyo sauti ya YESU na kama siyo sauti ya YESU tayari YESU siyo mchungaji wako sababu umeisikia sauti ya mbwa mwitu na ukakaa katika zizi hilo. Au kanisa linabatiza ubatizo wa maji ya kikombe, kubatizwa kwa jina la mchungaji, kwenye kisima ubatizwe, michango makanisani, harambee, kuandika sadaka majina, kudaiwa pesa  ndio umuone mtumishi, kanisa kutumia sala ya nikea na mitume, au salamu za sala, kuwa na partiners, kanisa kutoruhusu watu waokoke, kubusu misalaba, ibada za wafu, kanisa lenye huduma 6, lenye benki, kufanya biashara, na mengine ROHO MTAKATIFU akufunulie, mahali kama hapo YESU siyo mchungaji bali iko roho ya mbwa mwitu ndani ya kiongozi huyo inatenda kazi na kuwateka watu fikra zao waone wapo sawa sawa.
Sasa nakuuliza swali, je hayo yote yanatoka kwa YESU? Jibu siyo, sasa kama unashiriki au upo huko ujielewe wewe haupo katika zizi la YESU bali upo katika zizi la mwzi, na kazi ya mwizi kuiba, mnyanganyi na hata kuua na ndio sababu watu mnawachoka watumishi ni sababu yeye ni mbwa mwitu yupo kukunyang’anya tu na hata mbinguni hakupeleki bali anakupeleka kuzimu. Leo funguka akili kusikia sauti ya YESU iliyopo ndani yangu mimi Hebron na ukiri wokovu ikutoe huko na uondoke katika zizi hilo, sababu hayo yote siyo ya YESU (sauti yake) na wewe ukafanywa kiziwi katika uliwmengu wa roho ukaisikia sauti ya mbwa mwitu ukafikiria ndio sauti ya YESU, kumbe umeifuata sauti ya shetani na mbwa mwitu wake. YESU anasema kondoo wake wanaijua sauti yake! Sasa nikuulize swali je wewe uliijua sauti yake? Na kama haukuijua sasa ninakufungua masikio na ufahamu, sasa uelewe na utoke huko uokoke leo, ujitenge kabisa na zizi hilo, sababu lipo kwa ajili ya kuangamiza roho tu. Amenituma YESU niwarejeshe kondoo wake na hata wale ambao mpo katika zizi la mbwa mwitu mkitubu nanyi mtakuwa kondoo na mchungaji atakuwa ni YESU WA NAZARETI wala siyo MBWA MWITU.
Njia nyingine inyotumika ili kuhakikisha watu wanakuwa mbwa mwitu na watoto wa mbwa mwitu YOHANA 12: 42 neno linasema hivi “walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.”
Zidi kufunguka masikio yako na uwatumie na wenzako ujumbe huu ili nao wapone sababu hawapendi waangamie ila shetani ndivyo alivyowateka watu na akawaandaa jeshi lake ambalo ni watenda kazi kimwili ili waendeleze kazi ya kuharibu roho za wana wa MUNGU, na kuwafundisha wao waamini tu kuwa YESU ni mwana wa MUNGU lakini wasimkiri. Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron usikubali roho yako iangamie tena, leo ndio siku yako ya kupona na utoke katika zizi la mbwa mwitu ambalo ni kanisa linaloenda kinyume na biblia. Utaona katika mstari niliokuandikia hapo juu na uchunguze katika ulimwengu wote watu wanaomwamini YESU ni wengi sana ila hawajamkiri yeye kama BWANA NA MWOKOZI WAO, ila watabakia katika makanisa tu wakifikiri wataenda mbinguni na kumbe hawaendi bila kutoka katika zizi hilo.
Sasa hii haina tofauti na mashetani pia wanaamini YESU ni mwana wa MUNGU ila hawamkiri. Hivyo kila asiyemkiri YESU na kuokoka huyo yeye yupo katika zizi la mwizi na YESU SIYO pastor wake, asitegemee kwenda mbinguni. Ni mpaka atakapomkiri leo hii, na zaidi pia uwe mjanja kama YESU, ukiwa mjanja ukiijua sauti yake vizuri, hakika hautakaa mahali ambapo sipo. Pia gia ingine ambao watumishi wanatenda matendo ya kimbwa mwitu katika makanisa ya wokovu pia uchunguze sababu shetani anawatumia hao hao tena idadi kubwa sana na waumini wakiamini wapo na pastor kumbe wapo na mbwa mwitu, kazi yake ni michango, biashara, kuzini na waumini, uchawi, freemason, anatumia nguvu za giza, elewa umepotea hata hapo tena. Ujue upon na mbwa mwitu tena. YESU alipotoa mfano wa mbwa mwitu akielewa jinsi hata mnyama mbwa mwitu alivyo yeye hula mnyama angali bado anatembea ananyofoa kipisi cha nyama wakati mnyama anakimbia, alimeze anaendelea tena kunyofoa sehemu nyingine hivyo hivyo mpaka  mnyama anakata roho akitembea na kuishiwa nguvu. Hivyo hivyo na watumishi wa mishahara hao siyo wachungaji na YESU hawajui bali ndani yao ipo roho ya mbwa mwitu na kazi ya hiyo roho inaiua roho ya mtu taratibu na mwishowe ukishtuka tayari miaka imeenda na umefilisika umechoka maisha, na umepoteza muda kumbe siku zote haukumfanyia MUNGU bali ulikuwa unanyang’anywa tu mali zako na shetani pasipokujua. Ni kazi kwako jichunguze wewe upo wapi, ipo nafasi sasa, tubu kwa sala hii ili YESU awe mchungaji wako.
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NA LEO UNIANDIKE KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE, NATOKA KATIKA ZIZI LA MBWA MWITU KIROHO NA KIMWILI, NIONGOZE SASA WEWE MAHALI ULIPO WEWE NA KWA MTUMISHI WAKO WA KWELI NA SIYO MBWA MWITU.
Karibu sana Arusha katika kanisa langu, watu wote na mataifa yote. Ukija pigia simu zetu utapokelewa na kupewa maelekezo, utafika ukutane na YESU. Wengi wamekuja na wanakuja kila siku; MBARIKIWE.

NABII HEBRON.

[ad_2]