JINSI MAKANISA YALIVYO MUACHA MUNGU NA KUIFUATA MIUNGU!!!

[ad_1]

Kila mtu anajua yupo MUNGU mmoja peke yake aliyeumba mbingu na dunia na ndiye peke yake anayestahili kuabudiwa na kuheshimiwa peke yake hao wengine wote ni wa kukataliwa na kudharauliwa maana hao ni miungu na asili yake ni shetani. Ukisoma katika kitabu cha kutoka 20: 1-3, MUNGU akanena maneno haya yote akasema, mimi ni BWANA MUNGU wako niliyekutoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa, usiwe na miungu mingine ila mimi. MUNGU alijua shetani na yeye atataka ampotoshe mwanadamu na ajitengenezee vitu na aviite miungu. Sasa vitu vyote vilivyopo katika ulimwengu huu ni MUNGU ndiye kaviumba, na haistahili uvione vitu hivyo kuwa ndiyo MUNGU. Ila MUNGU hajaumbwa na mtu yeyote yeye hana mwanzo wala mwisho (ALPHA NA OMEGA).
Naelezea katika kanisa ni jinsi gani kanisa na watumishi wamewapotosha watu na kuwaingiza kwa miungu badala ya kanisa au watumishi kuwapeleka kwa MUNGU aliye hai. Na hii ni katika ulimwengu wote kiasi kikubwa makanisa yapo chini ya miungu na siyo MUNGU aliye hai. Kivipi? Nitawaeleza sasa. Miungu imejiingiza katika kanisa kwa kulishirikisha kanisa na mafundisho tofauti na biblia ambayo mafundisho hayo siyo ya MUNGU wa kweli bali ni ya shetani na shetani ndiye baba wa uongo na YESU WA NAZARETI ndiye BABA wa ukweli. Kanisa kuabudu miungu ni pale kanisa linapotenda mambo ambayo MUNGU aliyakataa na akasema usiabudu miungu mingine ila mimi peke yake tu. Unaposhiriki ubatizo ambao haupo katika biblia, tayari umeabudu miungu na kanisa hilo asili yake linaongozwa na roho ya shetani, mfano kanisa linasanamu na kuiabudu kanisani au kuziweka sanamu kanisani tayari hizo sanamu ni miungu na huko ndipo kuabudu miungu.
Najua wengi hamuelewi mnaona mpo salama katika kanisa, kumbe tayari shetani kwa kutumia ujanja wake ameleta maneno yake katika kanisa na yakakubaliwa yatendeke pasipo watu kujua na watumishi wamepigwa upofu wa kupokea mapokeo ya shetani yasiyojulikana yalipotoka. Japo kuna watumishi maarufu na wasio maarufu katika ulimwengu huu wamepewa umaarufu huo na huduma hizo na nguvu kutoka kwa miungu na wanafanya maagano kabisa ya shetani na wanajivalisha mavazi ya kipepo wasitambulikane na wanadamu. Sasa ukikuta  mtumishi yeyote ambaye anabatiza ubatizo tofauti na wa kwenye Neno la MUNGU, ujue ubatizo  wake ni ubatizo kutoka kwa miungu na hao anaowabatiza anawakabidhi kwa miungu na siyo MUNGU aliye hai. Ukikuta mtumishi anabatiza watu kwa jina lake ujue huyo asili ya nguvu zake ni miungu na mizimu siyo roho ya MUNGU wa kweli itendayo kazi ndani yake.
Kanisa lenye ibada ya wafu ujue na hilo lipo chini ya miungu na siyo MUNGU aliye hai maana MUNGU wa kweli ni MUNGU wa wenye uhai ila miungu ni mungu wa wafu.
Ukikuta kanisa katika ibada badala ya sala na kumuabudu MUNGU peke yake  wakaanza harambee, michango ndani ya kanisa, hilo silo hekalu la MUNGU aliye hai, linageuka na kuwa hekalu la miungu na watu waliopo katika kanisa hilo nao wameunganishwa na ibada ya miungu pasipo kujua, japo viongozi wanaelewa wanachokifanya ni uovu mbele za MUNGU.
Makanisa yanayoruhusu pombe na hata kuzibariki (Neno linasema usimpe mwenzako kileo). Makanisa ya jinsi hii ujue yanaongozwa na miungu ya shetani.
Watumishi wote waliojenga makaburi na kuyaita majina ya watoto wa MUNGU mfano: kaburi la Daudi, au YESU au yeyote yule. Huyo mtumishi yeye anaongozwa na miungu ya shetani na kanisa lake hakuna roho wa MUNGU ni roho za mapepo ya miungu ndizo zifanyazo kazi hapo.
Makanisa yenye benki, au bar club, yote yanaongozwa na miungu maana miungu ndiyo hufanya mazingaumbwe, bali MUNGU aliye hai anatenda wazi wazi, yeye hafanyi kazi za kiini macho.
Mpaka hapo natumaini sasa umepata picha japo kidogo utapona roho yako, usije ukaingizwa katika janga hili la kuabudu miungu badala ya wewe kumuabudu MUNGU aliye hai.
NOTE:
Mpaka hapo umepata picha na ROHO MTAKATIFU azidi kukufunulia ili ujue wewe upo katika sehemu gani, je katika miungu au MUNGU aliye hai, na ili upone roho, toka ukatengwe huko maana huko ni kwa miungu na siyo kwa MUNGU aliye kuumba wewe. Amenituma niwaeleze watu wote na mataifa yote msiabudu miungu, ikataeni leo ili yeye awe MUNGU wenu na muokoke na kubatizwa ubatizo wa maji mengi peke yake na muishi maisha matakatifu maana yeye ni MUNGU mtakatifu ila miungu siyo mitakatifu ni michafu na mahali pao ni pachafu yaani kuzimu ila leo utakapomkiri YESU WA NAZARETI jina lako linatolewa kwa miungu na utakuwa mwana wa MUNGU aliye hai. Msishiriki katika makanisa yanayoongozwa na miungu, utayajua kwa matendo yake tofauti na biblia, hata tabia za watumishi ukiona ni tabia chafu ujue yupo chini ya miungu na mizimu sasa mahubiri yake ujue mnapokea elimu ya miungu ili mfe roho zenu.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU KWANZIA LEO WEWE NDIYE BABA YANGU, NAJITENGA NA MIUNGU YOTE KIZAZI CHA KWANZA HADI CHA NNE. NISHIKE MKONO MUNGU ALIYE HAI, UNILINDE MILELE. AMEN.

NABII HEBRON.

[ad_2]