Close

JINSI MAKANISA YENYE MIMBA YANAVYONYONYESHA WAUMINI MAZIWA YA DHAMBI


 Enyi wanadamu wote wa mataifa yote, siku hii tena ya leo nitaendelea kuwafundisha kuhusu upendo wake YESU kwa watu wote watakaomrejea yeye. Amenituma mimi Hebron niwaeleze ukweli na niwaonyeshe njia ya kweli ya kwenda mbinguni, sababu idadi kubwa ya watu katika ulimwengu wote wanafikiri tayari wameshaishika njia ya mbinguni kumbe wapo katika njia ya shetani. Utaona katika kitabu cha Marko 13: 17-23
17Lakini ole wao wenye mimba; nao wanyonyeshao siku hizo! 18Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi, 19kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba MUNGU hata sasa, wala haitakuwa kamwe. 20Na kama BWANA asingalizikatiza siku hizo asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. 21Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki 22kwa maana wataondoka makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. 23Bali ninyi jihadharini, nimekwisha kuwaonya yote mbele.”
Hapa utaona YESU anasema ole wao ambao wenye mimba na ole wao ambao watakuwa wananyonyesha katika kipindi hiki cha manabii wa uongo, hapa siyo kwamba anamaanisha wanawake ambao watakuwa na mimba na kunyonyesha siyo hivyo, watu wengine wanakosea tafsiri yake hawataki kubeba mimba wanaogopa hata kunyonyesha. Nawasihi wanawake endeleeni kuzaa na kunyonyesha, sababu mwanamke kuzaa ni mpango wa MUNGU  mkaijaze dunia.
Nitaelezea YESU WA NAZARETI kwa nini alisema mithali hii na pia nitakufunulia maana ya mithali hii, mfano huu unahusu kanisa na watumishi pamoja na waumini ambao wapo katika kanisa hilo na jinsi lilivyo. Biblia inasema ole wao wenye mimba- hawa ni watumishi ambao wapo kinyume na neno la MUNGU au wamechanganya uongo katika neno la MUNGU na mafundisho wanayoyafundisha ya uongo huko ndiko kunyonyesha, sasa utajiuliza swali wanawanyonyesha nani? Jibu ni muumini ambaye aliyopo chini ya kuhani yule anayekufundisha mafundisho tofauti, mfano kuabudu sanamu, ubatizo wa uongo, au kukubatiza kwa jina lake, kuchangisha pesa katika nyumba ya MUNGU na mengineyo ya kifisadi hayo ndiyo maziwa yaliyo chachuka au kuharibika.
Sasa biblia inasema usile maziwa yaliyoghoshiwa. Hili ni neno ambalo halijabadilishwa lipo vile vile katika biblia, sasa ukipokea mafundisho potofu tayari umenyonya maziwa ya dhambi na matokeo yake afya yako ya kiroho itakuwa na msingi wa dhambi siku zote ila ni mpaka utakapoacha kuyanywa hayo maziwa yaani uyakatae hayo mafundisho na kupokea mafundisho yaliyo sahihi na hayajabadilishwa. Sasa ninaposema makanisa yanawanyonyesha waumini maziwa ya dhambi sasa umeelewa, na hata YESU aliliona hili sasa anasema ole omba asikukute ukiwa bado unanyonya hayo mafundisho ya mpinga kristo sababu ya neno hili yeye hatakuchukua sababu utakuwa unayo dhambi na mwenye dhambi haendi mbinguni, na hao wenye mimba ni watumishi ambao wapo kinyume na MUNGU, zaidi soma kitabu cha JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI cha Nabii Hebron katika blog au katika kanisa langu vipo utajua vizuri maziwa ya dhambi ni nini? Na nani mwenye mimba ambaye YESU WA NAZARETI aliokuwa anasema.
Amenituma niwatapishe watu wote maziwa ya dhambi ambayo umeyapokea kwa watumishi ambao ni wachawi, waliojiita, waliomuasi MUNGU, walio freemason, na waliompinga kristo, na walio wanafiki. Shetani anatumia njia hii ili kuvuna watoto wa MUNGU wasiende mbinguni pasipo wao kujua. Ila enyi mataifa yote unayosoma funguka na uwatumie na wengine ujumbe huu, na leo ukatae kunyonyeshwa maziwa ya dhambi (neno lilochanganywa na uongo na hata hayo madhabahu ili upone YOU MUST LEAVE ili afya yako ya kiroho itokwe na dhambi na uwe mtakatifu. Zaidi soma makala ya Nabii Hebron utaelewa zaidi na utajua jinsi gani ya kuepuka kunyonya dhambi na upone.
ILI UFUNGUKE:
1.     SEMA BWANA YESU WA NAZARETI NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NA UNIANDIKE KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE, NITAPISHE MAZIWA YA DHAMBI NILIYONYONYESHWA BILA  KUIJUA  AU KUJUA, NAJITENGA NA WATUMISHI WENYE MIMBA ZA SHETANI, NIONGOZE WEWE UNILINDE SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU UNIPE NA MSIMAMO IMARA.
2.     MATAIFA YOTE KARIBUNI KATIKA KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, WOTE WENYE MATESO YA AINA YOYOTE NJOO UTAFUNGULIWA BURE NA HUDUMA NI BURE, MUNGU YUPO KAZINI, NA SERIKALI YAKE. HAO WANAOTUMIA JINA LA YESU WA NAZARETI KUDAI PESA (HAO NI WANYANGANYI, WANA MAPEPO).

NABII HEBRON.