Close

JINSI MAMA MCHUNGAJI NA BABA MCHUNGAJI WANAVYOWAIBIA PESA WATU MAKANISANI


Ø KUPITIA KAPU LA SADAKA LA MAMA MCHUNGAJI
Ø KUPITIA KAPU LA SADAKA LA BABA MCHUNGAJI
Nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye mwana wa pekee wa MUNGU na ni mtakatifu wala siyo mnyang’anyi. Siku ya leo nawafungua watu ufahamu sababu uwizi na unyang’anyi umekithiri katika makanisa mengi ulimwenguni na ni uwizi wa kisayansi unaibiwa pesa zako ukijua ni sadaka kumbe umenyang’anywa na watumishi walafi na walioibadilisha biblia.
Kwanza kabisa mchungaji hatakiwi kujitengea chombo maalum cha sadaka yake, sababu yeye siyo MUNGU, ila anayetakiwa kutolewa sadaka ni MUNGU peke yake. Na zaidi ukiona kanisa lina kikapu cha sadaka ya mchungaji au mama mchungaji uelewe hao wanampinga YESU neno lake bali kwa midomo wanakiri wanampenda YESU ila ndani ya mioyo ni wanafiki. Ni wanafiki sababu biblia inasema mtu hutenda lile lililomjaa moyoni mwake, sasa hilo kapu la sadaka ndilo lililomjaa moyoni mwake. YESU alisema msisumbukie mtakula nini mtavaa nini? Ndugu msomaji akili yako ielewe kauli ya YESU. Sasa kama katika kanisa si kuna sadaka ambayo watu humtolea MUNGU? Jibu ndiyo, sasa na hii sadaka ya kikapu cha mama mchungaji kimetoka wapi wakati neno limekataa asisumbukie chochote?  Sasa anaposumbukia hilo kapu la sadaka tayari amebuni mbinu kuwanyang’anya watu pesa akitumia jina la YESU.
Na zaidi watu wengi wanalia sababu waumini wanalazimishwa kutoa pesa ya kapu la sadaka ya mama pastor na usipotoa unachukiwa.  Sasa nawaeleza ukweli kama unatoa ujue unaibiwa na wala MUNGU hatakubariki kamwe sababu biblia haijaeleza pawe na kapu la sadaka la mchungaji. Hivi jiulize unatakiwa umtolee MUNGU sadaka au mchungaji au mke wake? Jibu ni MUNGU tu. Sasa madhara ya kutoa pesa na ikaitwa sadaka ya kapu la mchungaji ina maana huyu pastor na yeye amejiinua kama miungu na shetani na yeye  anatolewa sadaka kama vile MUNGU. Muulize pastor wapi imeruhusiwa katika katiba ya MUNGU yaani biblia kumtolea sadaka mtumishi badala ya MUNGU au wapi biblia imeruhusu sadaka iitwe au mchungaji atolewe sadaka? Jibu hana. Haya ni machukizo makubwa sana ukitoa sadaka hizo unakuwa umetoa kwa mashetani na zaidi sadaka hii ya kapu la pastor au mke wake hii ni kutoza ushuru. Sadaka haipaswi mtu adaiwe wala aandikwe jina, amelipa ngapi na hiyo nyingine ataleta lini. Ukiona kanisa lipo hivyo ujue hilo ni kanisa la watoza ushuru na siyo YESU WA NAZARETI. Hapo ni makao ya pepo mfilisi.
Kataa kushiriki katika sadaka hizo za unyang’anyi na ni machukizo mbele za MUNGU. YESU amechukia sana watoto wake wanafikiri wanamtolea yeye kumbe wananyang’anywa kwa njia hiyo sasa elewa ili upone. Ni marufuku kutoa sadaka ya mchungaji wala mke wake. Kanisani ni mahali pa kutoa sadaka ya fungu la kumi na shukurani tu na iwe ni siri yako. Hizo sadaka za kapu ni za unyang’anyi na kuwafilisi na mtaendelea kufilisika mpaka utakapo acha. Zaidi soma vitabu vya mafundisho ya Nabii Hebron na makala utaujua ukweli.
·        Maswali ya muhimu muulize huyo anayetenga kapu la sadaka ya pastor na mkewe je yeye ni MUNGU? Jibu hana.
·        Je unakwenda kanisani kupeleka sadaka yako kwa pastor au MUNGU? Jibu MUNGU.
·        Je kama haujatoa sadaka ya kapu ni dhambi? Jibu ukitoa ndiyo dhambi.
NOTE:
Kila mtumishi anayefanya hivi ujue yeye ni mwizi, mnyang’anyi na amemkufuru MUNGU na zaidi amegeuka badala ya kutenda atakavyo MUNGU amekuwa mtoza ushuru.

NABII HEBRON.