KANISA LA SASA LIMERUDI MISRI, BADALA YA KWENDA KAANANI NCHI YA AHADI 98%

[ad_1]

KANISA LA SASA LIMERUDI MISRI, BADALA YA KWENDA KAANANI NCHI YA AHADI. 98%
Ndugu msomaji na binadamu unayepata ujumbe huu usiogope unatakiwa ufurahi maana ndio utapona na kujua ukweli. Soma Isaya (31:1),-7). Ole wao watelemkao kwenda  misri wapate msaada, na kutegemea farasi,watumainio magari kwa kuwa ni mengi  na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana, lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli wala hawamtafuti, (Mstari wa saba) maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha na sanamu zake za dhahabu ambazo mikono yenu imeifanya, zikawa dhambi kwenu.
Ndugu, msomaji napenda kukufundisha kwa kifupi nini maana ya Misri kibiblia maana yamkini wengine watafikiria ni nchi ile ya Misri ambayo ipo katika bara la Africa Kaskazini. Misri imetumika katika Biblia kama ni mahali pa mateso katika kanisa, ikiwa ina maana  wana wa Israeli waliokuwa wakitumikishwa na Farao pamoja na mungu wa farao, na kuwatumikisha katika nchi hiyo hiyo ambayo inaitwa  Misri mpaka sasa. Ila MUNGU alimtuma MUSA kuwakomboa wana wa Israeli kama ilivyoandikwa pia katika kitabu cha neno la MUNGU cha Kutoka.
Ewe mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU ili umtegemee yeye peke yake na sio mungu wa Farao au shetani aliyewatumikisha wana wa Israeli kipindi kile mpaka akamtuma MUSA akawaokoe kutoka kwa farao na akafanya na wana waisraeli waachiwa wakawa huru kwenda kaanani. Kaanani ni nchi ya ahadi ambayo MUNGU aliwaahidia wanaisraeli  kuwa ndio nchi nzuri kwa nyakati hizo.
Ndugu msomaji,kaanani ya leo ni kwenda Mbinguni , na kwenda Mbinguni kuna sheria zake na maelekezo  ambayo yapo katika kitabu kitakatifu. Maana  waisraeli leo hii ndio kanisa na kanisa ni wewe mwanadamu ambaye unatakiwa kwenda mbinguni. Sasa enzi zile  MUSA aliwatoa kwa Farao na wakaonywa wasifanye mambo ya Farao au ya shetani. Mfano ni katika zile amri kumi  na mengineyo. Natumaini mpaka hapo umenielewa vizuri. Sasa utanielewa ninaposema kanisa limeacha kufuatia njia yake ya kuendea mbinguni na kufuatia kurudi misri penye mateso ya farao kama nyakati zile  nah ii ni kwa ulimwengu wote na mataifa yote. Na wanaofanya haya kulirudisha kanisa Misri ni viongozi 98% na siyo waumini, wao hufuata kiongozi tuu na kiongozi ambaye   anakupeleka misri huyo ndani yake anatumikishwa na shetani ( FARAO) kama Yule aliyewatesa wana wa Israeli kikatili. Na zaidi kanisa linalorudi misri inamaana lipo kuzimu  linaongozwa na shetani na siyo tena YESU.
Ndugu  msomaji sasa utambue na ufunguke ili upone na usikae katika kanis linalorudi misri. Haijalishi wanalitaja jina la YESU kanisani, kwani hata yeye muasisi wa kanisa yaani YESU KRISTO WA NAZARETI, alikwisha sema msiziamini kila roho, zichunguzeni je! Zinatokana na mimi  na pia hata katika NENO langu hayo wafanyayo nimeruhusu au nimeyakataa? kama nimeyakataa ina maana hayo siyo yangu ni ya shetani na kama ni ya shetani ndipo misri huko kwa Farao, mnabakia kuteseka kanisani.
NAMNA YA KUJUA KANISA LIMERUDU MISRI NA KAMA UNASHIRIKI IBADA HIZI UJUE NA WEWE UPO MISRI HAUENDI KAANANI NI KUPOTEZA MUDA HAPO USUBIRI KUFA UKACHOMWE MOTO SIKU YA MWISHO.
1.    Kanisa linaloabudu sanamu, hilo lipo misri na halina mpango wa kuwapeleka kondoo katika nchi ya ahadi. Maana misri ndio walioabudu sanamu , wana wa Israeli na sanamu zilipobomolewa na MUSA wana wa Israeli wakakataa wakamfuata MUSA wakaendelea na safari.( IKorinto 10:5-22 soma mstari wa 20) hata kutoa sadaka yako mahali kama hapo imeandikwa unaitoa kwa mashetani na zaidi kama MUNGU amekataa je inawezekana , MUNGU kuwa na ushirika  au kukaa meza moja na masanamu? Jibu ni hapana. ( zaidi soma kutoka 20: (1-24)
2.    Kanisa lolote ulimwengu wote  ambalo halibatizi kwa maji mengi tena ni maji yanayotembea na siyo ya kisima au ubatizo wa kikombe , kanisa hilo lipo misri ikiwa inamaana linabatiza ambao haupo hata kwenye BIBLIA  wala Mbinguni na siyo ubatizo wa YOHANA.
3.    Kanisa la kuchangisha pesa na harambee hilo limerudi misri , na mkono wa MUNGU haupo juu yake, MUNGU siyo ombaomba, na hata YESU alivyokuwa hapa ulimwenguni alikataa nyumba ya BABA yake kuitwa au kufanywa soko, Huko ndiko misri. Na  mwisho wake ni jehanamu.
4.    Kuzika Biblia, kuzika majina ya waumini kanisani kubatiza kwa jina la mchungaji ,halafu baba mwana na roho mtakatifu, kukufanya eti partiners kwa ajili ya pesa yako huo ni utapeli unaotumiwa na watumishi kumfanya YESU aitwe mnyanganyi, hao wanaofanya hayo wanaitwa wanyang’anyi na sio YESU anawanyang’anya. Hao wapo misri katika safari ya mbinguni hayo hayapo. Kumbuka MUSA  aliwatoa wana wa Israeli kwenda nchi ya ahaadi bila kuchaji gharama yeyote.
5.    Makanisa baadhi katika ulimwengu huu, hao wanayoyaongoza wakidai ni ya YESU wameenda kinyume na amri ya MUNGU. Mojawapo ya amri ya MUNGU (Kutoka 20:5-6) Usivisujudie wala kuvitumikia, kwa kuwa mimi BWANA MUNGU wako ni MUNGU mwenye wivu,nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao. Name nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.
Nitakuelezea kifupi na utajua ukweli maana NENO la MUNGU ni kweli na lipo wazi na sio giza linaeleweka vizuri na ndiyo katiba yetu hii. Na kama katiba ya MUNGU haifuatwi aliyoichagua yeye yeye kuongozea kanisa basi hayo yaliyo nje ya BIBLIA  ni ya uongo na ni ya shetani hata kama mtumishi huyo alianza na MUNGU wa kweli , atakuwa anaongozwa na MUNGU wa uongo au mungu wa Farao aliyepo misri. Kumezuka miongozo ya ajabu ambayo waumini badala ya kuja kumwabudu MUNGU tu, watumishi wanataka waabudiwe wao kwa majina yao japo  wanamtaja YESU wakati katika kitabu cha kutoka (20:5-6) Inaelezea MUNGU ana wivu juu yake , anataka aabudiwe yeye tu ila baadhi ya watumishi wamekuwa Mungu mtu! Je nikuulize swali, je? Anayo mbingu ya kukupeleka? Jibu ni hapana na kama hana mbingu yake inamaana mapigo ya MUNGU yanakuhusu.
Wewe tayari umeingizwa kwenye mkumbo wa shetani au unarudishwa misri na ndiyo maana mateso hayakuachilii. Pia unakuta waumini wanadanganywa ili wapotee. Mfano mtumishi au nabii anaitwa Fulani na katika kanisa waumini wanamtaja kama yeye ni MUNGU, awalinde awajibu. Jamani embu fungukeni mnaangamia  na mimi YESU kaniambia niwaambie ukweli, kumbuka wana wa Israeli nyakati zile waliika anaye mlilia MUNGU  kwa sababu hawakumjua MUNGU, walimjua MUSA ambaye aliongozwa na MUNGU na sasa ni nyakati tofauti. Tumemjua YESU ambaye ndiye njia ya uzima na ya ukweli na ndiye tunaye mlilia na pasipo yeye hakuna atakayemfikia MUNGU, na sisi sote tunajua hivyo. Je ni halali ulitaje jina la mtumishi kama yeye ni MUNGU? Huko mmepotea na wivu wa MUNGU utamtandika anayechukua utukufu wa MUNGU na zaidi MUNGU mahali hapo ni machukizo. Wewe tafuta kwenye BIBLIA kwenye kitabu cha kwanza mpaka cha mwisho, hakuna mahali watu wanaelekezwa wamuabudu mwanadamu katika ibada, jibu hakuna sasa huko ni kurudishwa misri kumwabudu Farao, ukubali ukatae ukweli ndio huo, hapo ni misri.
Ndugu msomaji  usikubali kuabudu wanadamu, hamna tofauti na kuabudu sanamu kwa maana hilo jina halijaruhusiwa liabudiwe, ni kujiamulia peke yake ndipo kujitengenezea huko.
Nitatoa mfano, eti watu katika kanisa langu wakija kanisani waanze kufanya maombi eti Hebron nisaidie, nisamehe, nibariki, niponye na mengineyo. Nakuambia hivyo haifai ni mpango wa shetani na zaidi ni kuchukua utukufu wa MUNGU, na kurudishwa misri. Mahali kama hapo ibada zote ni feki hamna ukweli wa MUNGU ni roho ya kuasi au kumdharau na wote mnashiriki hivyo mnaangamizwa na dhambi hiyo vizazi na vizazi.
6.    Jambo lingine ili ujue kanisa limerudi misri ni watumishi kujia au kujiita majina ya ajabu katika kazi yake. Jamani huku ni kukosa nidhamu na kumjaribu MUNGU (soma Luka 4:12) Tunajua kanisa alilolijenga YESU lina huduma tano na aliziacha YESU, MITUME, MANABII, WACHUNGAJI, WAINJILISTI na WAALIMU. Siku hizi watumishi baadhi yao wanamjaribu MUNGU wanajiongezea majina kwenye kazi ya kanisa wameamua kufuata mafundisho ya wanadamu na kuyaacha ya MUNGU.(Marko 7:7) wengine wanajiita wachungaji ila anaongeza mbele mjukuu wa YESU, mwingine babu wa upako, mama wa upako, mwingine jina kubwa na siyo la YESU ndio kubwa , haya yote ni mafundisho ya kibinadamu, ili kuvuruga huduma za majina ya huduma zake TANO, huduma ya MUNGU na haya majina ya huduma TANO yamehakikishwa Mbinguni haya mengine ni mafunuo kutoka kuzimu ili kuzinajisi huduma  TANO za MUNGU na wengi wao walioongezea majina ya ajabu 99% wanatumia nguvu za giza, huko ni kurudi misri.
7.     Ukikuta mtumishi anafanya mazingaumbwe, mfano maji anaayabadilisha kuwa mafuta ya taa na ameyaleta kwa kusudi la kuwaonyesha muone, huyo ni mchawi, kama ule uchawi wa farao wakati ule alivyofanya, ila miujiza ya MUNGU haifanyiki kama mazingaumbwe, huyo hana MUNGU ndani yake ni roho ya kuangamiza wanadamu wasiende mbinguni awarudishe misri, na tabia zao wanakuwa ni wazinzi sana. Hao ni matapeli wanatumia jina la YESU kuwaibia pesa kama unavyoibiwa.           
8.    Kanisa linalopinga wokovu hakuna ujue kweli kanisa hilo lipo misri kama wale wanaisraeli walivyokuwa hawajakombolewa wakati ule, ujue na hilo halina wokovu lipo kwa farao bado, lingekuwa lipo huru lingekubali wokovu kama wale wana waisraeli walipomsikiliza wakatii wakaokoka.
9.    Watumishi wote ambao wapo kwenye listi ya wanachama wa freemasoni dunia nzima hao wote ni watumishi wa shetani,wala hawapeleki mtu yeyote mbinguni wanawapeleka misri, au kwa lugha nyingine kwa shetani na ni watenda kazi wa shetani, haijalishi wanajiita  mitume,manabii,wainjilisti, waalimu, wachungaji. Huo ni ujanja wa kukupofusha, funguka ufahamu wako.
     JAMBO LINGINE.
1.    Nitaelezea kuhusu biashara ya majeneza kushamiri
2.    Kuhusu vyama vya kufa na kuzikana.
1.    BIASHARA YA MAJENEZA KUSHAMIRI
Nilipokuwa naongea na YESU katika baadhi ya mafundisho kwa ajili ya kazi yake ya kujenga na kumuandalia kanisa lake. YESU akaniambia kwa kuniuliza swali, je! Ni kwa nini siku hizi ukipita mahali unakuta vijana wapo bize na oda nyingi za majeneza na hata kuonekana ni biashara kubwa ya kutengeneza majeneza? Sikuwa na jibu , akaniambia siyo vibaya watu kutengeneza majeneza, ila kwa nini imeshamiri kiasi hichi tofauti nakipindi kile mimi YESU nilivyokuwa hapa ulimwenguni. YESU akaniambia , maovu yamezidi . MUNGU alituma watumishi ili kuwaombea waumini wasiuliwe na adui, maana 96% ya vifo vya watu wanavyokufa wanauliwa na shetani na maajenti wake. Wala hawaendi mbinguni ndio maana biashara ya majeneza imeshamiri , mimi niliwaweka watumishi ili kuwaombea na kuwaponya waumini watu wengi wanatolewa kafara,kulogwana watumishi hawana nguvu za MUNGU wengi wao wananguvu za adui, hivyo Belzebul hawezi kumtoa belzebul mwenzake. Niliogopa sana na wengi sipo nao nao wanajua ila ole wao upanga wa MUNGU upo juu yao, aliongea kwa sauti ya uchungu wamenisaliti watoto wangu wanateseka kazi imebaki ni kulitumia jina langu, kunyang’anya mali na kukusanya pesa kupitia jina langu, kazi niliyowatuma nikuwaponya watu wasiteswe na shetani na wasiuwawe ila wako wapi Hebron, angalia pesa tuu na mafanikio na wengine wamekuwa wachawi maarufu. Akaniambia unafikiri wataondoka na kitu hapa duniani, niliogopa sana, ole wao hukumu ipo tayari akaniambia hiyo ndiyo sababu ya biashara hiyo kukua japo mwanadamu wakati wake alioupanga afe , atakufa tuu ila vifo hivyo 96% siyo vifo  vya mpango wa MUNGU, na kama siyo vya mpango wa MUNGU , ole wao watumishi.
Akaniambia kazi yao imebaki kuwaambia waumini ukitoka hapa tuangalie nani atakuzika? Nikajua kazi imezidi kuharibika na waumini wamerudishwa misri kwa farao, ndiyo maana vifo vimezidi  ni sababu ya uovu wa dunia hii na hao walioitwa wauondoe huo uovu wa dunia 98% wamekuwa rafiki wa dunia 98% wamekuwa rafiki wa dunia au misri hawataki kwenda nchi ya ahadi kwa kuamua kutoka moyoni ni kwa kiujanjaujanja tuu. Akaniambia ukiwa mtakatifu ina maana ni kuanzia moyoni mwako, kinywa, ufahamu wako na kumwamini bwana YESU huo ndio utakatifu, sasa kama mkono unashika pombe, unachangisha
2.    KUHUSU VYAMA VYA KUFA NA KUZIKANA
Ndugu msomaji jambo lingine ni la aibu sana na ni la hatari sana linalozidi kuangamiza maisha ya watu. Hizi elimu za wanadamu , kama elimu hii haijatoka kwa MUNGU imetoka kwa shetani, ili azidi kuuwa miili ya watu apate chakula huko kuzimu au kwa lugha nyingine  aunapojiingiza kwenye chama hicho tayari unajiweka oda kwa shetani kwa kujisajili na kulipa pesa. Ndugu msomaji embu tafuta kwenye Biblia ni wapi kuna chama cha kuzikana? Jibu ni hakuna, akaniambia kanisa limerudi misri ndio maana halifundishi  ukweli watu na watumishi wapo kwenye vyama vya kuzikana. Mwanadamu ameumbwa ili aishi na akifa ataendelea kuishi , huu ndio mpango wa MUNGU ila kwa hao waliojiandikisha kwenye chama cha kufa na kuzikana wanapokufa shetani huwashikilia milele maanatokea hapa duniani walishasaini na kujisajili kwake, na wote  waliokufa na wapo katika hicho chama, hakuna hata mmoja atakayeishi akifa wala nkwenda mbinguni, huu ni mchomeko wa shetani ili kuwavuna wanadamu. Ndugu natumaini umeelewa , jitoe huko hata na pesa hizo usilipe na hata waliopo katika vyama hivyo wote wanayo roho ya mauti na vitu vyako vyote vinakuwa haviendi, kama ni biashara inayumba hata maendeleo ya familia yanayumba. Haijalishi hata kama umeokoka, tayari umerudi misri kwa farao na huendi kwenye nchi ya ahadi. Nikuulize swali je? Nchi ya ahadi au mbinguni kuna maandalizi ya namna hii? Embu angalieni YESU alipokufa alijijengea kaburi? Jibu ni hapana, na wewe usijijengee kaburi. Kuwa mwanachama wa chama cha kufa na kuzikana hilo ndilo kaburi lako, linakuita Fulani njoo!!
Nakusubiri umejifunga mwenyewe! toka huko madhara yake siku zote hapa ulimwenguni utaishi kwa shida tuu, na jambo  lingene kuzimu pakipungua chakula, maana chakula chao ni nyama za watu wanakuchukua kirahisi bila shida kwa muda wowote unakuwa chakula chao. Na zaidi mtu yeyote aliyepo katika chama hicho kwa jinsi YESU alivyonifunulia haya yote mimi Hebron tayari anayotiketi ya kifo mkononi! Usishiriki tena ili usiishi kwa matumaini ya shetani. Ukifa utazikwa tuu mbona YESU alizikwa tuu bila chama cha kufa na kuzikana? Utubu ili upone huko ni misri na kanisa halina macho mpaka waumini wametekwa na watumishi hawajui. Huu ni wakati wa ukweli tuu kila mtu apone ila wapo wale wa jehanamu inawasubiri.
MAJIBU YA NCHI ZOTE NA VIUMBE VYOTE ALIVYOVIUMBA MUNGU, KWA ULIMWENGU WOTE.
YESU amenipa majibu yao kwa wanadamu wa Taifa lolote na kwa rangi yeyote na kwa bara lolote, kitu chochote kilichokusumbua na umefika mahali umekwama njoo nitakupa majibu yako,hata kwenye nchi zote zenye vita visivyoisha na imeshindikana kuisha, majibu ya vita hivyo kuisha kabisa na mamlaka hiyo YESU kanipa, hata kwa wanyama aliowaumba yeye wanateseka sana nao wanamlilia muumba wao ambaye  ni MUNGU. Sasa ni mwisho wanyama kuteseka wanyama aliowaumba MUNGU nah ii yote hufanywa na wanadamu, ole wako wewe, mfano mnyama fisi wachawi , manabii wa uongo huwatumia kama gari  katika kazi zao za uchawi na kuwatesa badala ya wanyama kufurahia maisha yao, wanadamu wanawapanda kama gari usiku. Ndege bundi ni aina ya ndege aliyemuumba kama ndege wake ila leo hii ndege huyo unakuta huyu mwanadamu aliyekuwa taahira anaishi ndani ya bundi na kumtumia kiuchawi na kuteseka, ole wao hukumu inawangoja.
Jambo lingine aliloniambia MUNGU ole wao waharibuo uhasili wa uumbaji wake ni dhambi kuharibu mazingira, ni kuharibu kazi aliyoifanya yeye kasha akampa mwanadamu aishi, Nikuulize swali ndugu msomaji? Je MUNGU alimuumba mwanadamu ili aje aiharibu dunia? Jibu ni hapana. Jambo hili pia MUNGU halipendi tubu na uache kuharibu uasili wa MUNGU, Roho ya uharibifu ni ya shetani ikatae usije kuangamia. Ndugu msomaji hii yote ulimwengu kukosa majibu ni sababu kanisa 98% limemuacha MUNGU mwenye majibu ya kila kitu na kumfuata mungu baali asiye na majibu na majibu ya baali ni kuangamia na kuteseka milele kama ilivyoandikwa katika kitabu cha ( IFalme 18:21-40)
TANZANIA
Taifa kubwa kiutajiri kuliko yote duniani, ila utajiri umefichwa na MUNGU; na utatolewa kwa watanzania wakisha jielewa na kujua, maana kuna nchi zinasubiria kuwalaghai viongozi wa nchi hii ili wauziwe ila haitawezekana tena ni MUNGU  mwenyewe kaishikilia nchi hii ili aiinue kiuchumi na maisha ya mtanzania, ila atawatumia viongozi hawa hawa viongozi na watafanya vizuri tuu. Ndege za nchi zinakuja nyingi sana kama nilivyokwisha kuwaambia mwaka 2012 June, nchi hii Reli zimerudishwa na MUNGU sasa si mnaona, Bandari ya Tanzania imeinuliwa si mmeona sasa. Nikawaambia baadhi ya mawaziri wataondolewa na YESU si mmeyaona? Na kuhusu Gesi si mmeyaona? Mfano, nilivyotabiri Papa kuacha kazi, si mmeyaona? Na mengineyo mengi ambayo nimeyataja katika makala hii.
Nilipowaambia nchi imeinuliwa juu na MUNGU si mmeona na sasa hata Serengeti, Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro zimeingia kwenye maajabu  ya dunia? Ndugu msomaji nchi yetu ya Tanzania ilikuwa imezikwa kipepo na baadhi ya nchi za Ulaya, wakachukua udhamani wetu na vitu vyetu, hata na udhamani wa maisha ya mtanzania na sisi tulibakia kuteseka na kuwa ombaomba ila hao waliotuibia muda sio mrefu walichokifanya kwa watanzania kitakuwa kwao hao, ndio watakaokuwa masikini na utajiri wao utaporomoka kila siku, na watanzania mtashangaa maisha yatakavyobadilika na nchi yetu.
Kuhusu vita nchi yetu haita kaa iwe na vita wala haitavamiwa na Taifa lolote , ila humu ndani ya nchi hii kwa wale ambao hawafuati sheria za MUNGU, kama atakavyo yeye na hata katika kitabu kitakatifu kimeandikwa amri zake na hazifuatwi na sehemu nyingine katika dunia hii hawatakuwa na amani, hivyo ndivyo alivyoniambia MUNGU. Huu ni wakati wa kumjua MUNGU wa kweli na mungu wa uongo. (Baali)
Muda sio mrefu elimu kwa nchi hii itakuwa ni bure na ni serikali italipia kuanzia elimu ya chini mpaka ya juu. Na matibabu yatakuwa bure isipokuwa kwa hospitali za binafsi. Hii yote ni YESU ndiye anayefanya na anajua itakuwaje ili yatimie na yawezekane na itakuwa hakuna wa kupinga.
Mafisadi atawafichua peke yake MUNGU kwa njia anayoijua yeye peke yake ila atatumia watu  na ukweli utajulikana, uchawi haufanyi kazi tena katika nchi hii kwa wale baadhi ya viongozi wanaotoa makafara kuuwa watu kichawi ili wapate vyeo, mtaporomoka na kukataliwa na watanzania ni MUNGU mwenyewe atawabadilisha na wawakatae na utafichuliwa uovu wenu na wengine watafungwa na kufilisiwa kila kitu, maana mumeiibia nchi, nah ii ni kwa viongozi wote na wafanyakazi wote katika idara zote katika nchi hii hata secta binafsi, na wengine watasemana na kugeukana wao kwa wao.
Jeshi la Tanzania litaanza kugundua silaha ambazo hazipo katika nchi yeyote duniani, na limeinuliwa na MUNGU mwenyewe. Hayo mengine sijaruhusiwa kuyasema ni siri ya nchi. Usalama wa taifa watakamata na kufichua uovu ambao ulikuwa haujulikanaji hii ni katika nchi nawatenda haki, MUNGU awabariki sana.
Kuhusu uchaguzi katika serikali kuanzia Uraisi, udiwani, wenyeviti wa vijiji – atakayetumia uchawi na kuhonga hatashinda, MUNGU atawabadilisha watu wampigie kura yule anayemtegemea yeye tu.

– Mtume na Nabii Hebron W. Kisamo

[ad_2]