Close

KANISA LA SASA LIMEVUNJA KATIBA YA MUNGU ALIYE HAI 98% ALL OVER THE WORLD

[ad_1]


Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron karibu tena katika shule ya kukuelimisha kuhusu kumjua MUNGU wa kweli na kuponywa roho yako. Ujumbe huu ni kwa ajili ya mataifa yote na watu wote aliowaumba MUNGU na wale wanaotaka kupona roho zao wasichomwe moto katika ule mwisho atakapokuja kuhukumu ulimwengu YESU WA NAZARETI. Nitaeleza kwa kifupi na mifano ila zaidi uingie katika blog ya prophethebron.blogspot.com utajifunza zaidi na wala hautaishi maisha ya wasiwasi tena.
Nitaeleza nini maana ya katiba kidunia. Katiba ni mwongozo au sheria na kanuni zilizopitishwa na kuhakikishwa zifuatwe kwa ajili ya jambo fulani, inaweza kuwa ni katika mashirika, vyama vya siasa au vya biashara, au serikali yoyote lazima iwe na mwongozo wa kuiongoza nchi na katiba hiyo uhakikishwa au kupitishwa na bunge ya kuwa ndiyo ifuatwe kwa yale waliyoyapitisha. Na endapo wananchi au mtu yeyote atakayekwenda kinyume na katiba hiyo huyo huitwa amevunja katiba au amekataa kuifuata, hivyo anayevunja sheria hizo vipo vyombo vya kuwashughulikia au kuwahukumu wavunja sheria. Kidunia vyombo hivyo vinaitwa mahakama na ndani ya mahakama wapo majaji, mahakimu ambao wanateuliwa kwa ajili ya kutoa haki na kuhukumu wale wanaokutwa na makosa, huukumiwa kwenda gerezani (kifungoni).
Sasa ninakurudisha katika kanisa. Nimekupa mfano upate picha kuhusu katiba ya MUNGU (Biblia). Hiki ndicho kitabu alichokihakikisha MUNGU na ndicho akasema kifuatwe na asiwepo yeyote yule wa kupunguza neno lake au kuliongezea, atakayefanya hivyo hata uona uzima wa milele (Ufunuo 22: 18-19). Katiba hii ambacho ndicho kitabu kitakatifu mambo mengi sana yamevunjwa na watumishi au mafarisayo wasiyo na aibu wala heshima mbele za MUNGU, bali wamemtukuza shetani kama baba yao kwa jinsi matendo yao yalivyo na jinsi ya kuongoza waumini katika njia ya shetani au mwongozo wa shetani. Na kama wamevunja tayari hao wote ni wahalifu mbele za MUNGU na wao watahukumiwa kwa matendo yao na jaji mkuu siku hiyo ambaye ndiye YESU WA NAZARETI atawahukumu wote siku ile ya mwisho wa dunia akishirikiana na mahakimu wake ambao ni serikali ya mbinguni.
Katiba hii jinsi ilivyovunjwa ni kuweka mafundisho ya uongo ambayo hayapo katika katiba ya MUNGU, na hata hao wote wanao ongozwa na katiba isiyo ya MUNGU hao wote hukumu inawahusu maana wamevunja katiba ya MUNGU. Kibinadamu unavyokuwa umevunja katiba si unaitwa mhalifu na unahukumiwa na kupelekwa magereza? Jibu Ndiyo. Na kiroho ndivyo ilivyo, mfano ni huo huo, na kusudi la kanisa 98% kuvunja katiba ni shetani amewateka fahamu watumishi waliomuasi MUNGU na kuingiza sheria zao katika kanisa. Na kanisa kama linaongozwa na shetani hilo kanisa tayari ni kanisa halifu (limeasi) na kama limeasi linasubiri hukumu jehanamu, na siku ile ya mwisho kila sheria iliyovunjwa katika biblia utaonyeshwa kwenye screen ya computer ulichofanya, mtajiona live live, kumbukumbu zimehifadhiwa.
Nitaelezea baadhi ya vifungu vya sheria katika biblia vilivyo vunjwa:
a.      Ubatizo wa maji ya kikombe, ubatizo wa maji ya kisima.
b.     Ubarikio wa watu wazima badala wakiwa wachanga.
c.      Kuabudu sanamu na kuabudu majina ya watoto wa MUNGU tofauti na jina la YESU tu aliloruhusu MUNGU.
d.     Kubatizwa kwa majina ya watumishi.
e.      Kuchangisha pesa za harambee kwa ajili eti ya kanisa.
f.       Kanisa kufanya biashara ya kuwa na bar, mabenki.
g.      Kufungia watu ndoa kwa agano la shida.
h.     Kufanya ibada za wafu.
i.        Kuzika watu ndani ya kanisa (watumishi kutumia uchawi na kuloga)
j.        Waumini kumuabudu mtumishi na kumfanya yeye ndiye MUNGU, FREEMASON kuongoza kanisa (hawa ni wachawi tupu).
k.     Kufanya maombi kwa kudai pesa kama hospitali za duniani. Kuomba pesa kwenye TV, REDIO kwa kutumia jina la YESU yeye siyo maskini (hajawaita hao), ni waizi wa pesa za wanadamu MUNGU SIYO MASKINI.
NOTE:
Ndugu msomaji mpaka hapa umepata picha japo kidogo na umeelewa sasa biblia ilivyovurugwa na watumishi na makanisa yao katika ulimwengu huu. Najua watu wengi wanayohofu ya MUNGU ila hawakujua katiba ya MUNGU na sheria zake na madhara ya kutokujua katiba utafanya au kushirikishwa yale yasiyokupasa kushiriki na ukija kujua ukweli jinsi katiba ilivyo kwako inakuwa ni majuto na kuangamia.
Hayo ni machache tu nimeyataja kukupa picha halisi uelewe maana biblia haijaruhusu na MUNGU amekataza kabisa, sasa kama amekataza halafu watumishi na makanisa yanayatenda yale aliyoyakataza, hapo nini kinaendelea? Ni kumsaliti MUNGU, na yeye amewakataa hao waliomsaliti. Usione MUNGU amelala, yupo macho na halali. Ole wenu, mimi nasema kama alivyonieleza hayo yatakayowapata watajua na jehanamu.
JAMBO LILILOWAZI KABISA KUJUA KANISA LIMEVUNJA KATIBA YA MUNGU NA HALINA MUNGU TENA NI;
Kanisa linalobatiza ubatizo wa maji ya kikombe, ubatizo huu tafuta katika biblia haupo na ni machukizo mbele za MUNGU, makanisa hayo tayari yameshaachwa na MUNGU na ndivyo alivyo nieleza na mimi sibadilishi lolote. Nawaeleza mnaotaka kupona tokeni huko mkatengwe nao ili mapigo ya MUNGU ya sikukute maana hao wote ni wahalifu kwa MUNGU, msibabaishwe na ibada zao na nyimbo za kanisani, mnapoteza muda, okokeni na mwache. Hao ni adui wa MUNGU na majumba yao ya ibada ni mahali pa kuua roho za wana wa MUNGU. (SOMA KITABU CHA NABII HEBRON, UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE) utaelewa vizuri.
Watu wote ambao wanabatizwa ubatizo wa maji ya kikombe na hao wanaowabatiza wote hawatauona ufalme wa MUNGU milele, na siyo wanafunzi wa YESU WA NAZARETI. Yeye alionyesha njia ya ubatizo na MUNGU alimtuma Yohana akabatize, sasa, muone jinsi katiba ya MUNGU ilivyovunjwa na watumishi na makanisa? Na kama wamevunja hao wote ni wahalifu na mhalifu mahali pake ni gerezani.
Hivyo ndivyo ilivyo watumishi na makanisa yalivyojijengea uadui na MUNGU, na hapa hakuna ujanja, wewe uliyevunja katiba (Soma Ufunuo 22: 18-19) ni mmemkufuru ROHO MTAKATIFU. Kwa waumini mnaompenda YESU nawaeleza ukweli na hata mkiwauliza hawana majibu hao watumishi waliomkufuru MUNGU. Na kama wamemkufuru MUNGU basi hata waumini mnaongozwa na roho ya kumkufuru MUNGU mmejengewa uadui na watumishi kupitia mafundisho ya uongo ili muwe adui wa MUNGU. Ni bora ukae nyumbani tu na MUNGU anakusikiliza kuliko kwenda kwenye makanisa yanayomkufuru MUNGU. (SOMA KITABU CHA NABII HEBRON JINSI KANISA LILIVYOMKUFURU ROHO MTAKATIFU).

NABII HEBRON.

[ad_2]