Close

KUZIKA BIBLIA NI KUMZIKA MUNGU

KUZIKA BIBLIA NI KUMZIKA MUNGU

[ad_1]
















KUZIKA BIBLIA NI KUMZIKA MUNGU

BIBLIA ni kitabu Kitakatifu ambacho  ndani yake upo ujumbe kwa njia ya  NENO ili aseme na wanadamu na awaongoze ili wamjue yeye  na awaongoze, Huyo MUNGU ni NENO  Yohana ( 1:1-4). Na ukisoma imeandikwa  hapo mwanzo kulikuwepo  NENO, naye NENO alikuwako kwa MUNGU, naye NENO alikuwa MUNGU, huyo mwanzo alikuwako kwa MUNGU, vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika, ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Ewe mwanadamu yeyote kwa jinsia yeyote na Taifa lolote na rangi yeyote wewe umeumbwa kwa mfano na sura yake yeye ambaye ni ALFA na OMEGA, aliyekuwepo na atakayekuwepo milele. Nimekuwa nikiongea na MUNGU mara nyingi na anahuzunika jinsi mwanadamu alivyomdharau kwa njia nyingi na wakitumia kanisa ili kuwapoteza wale wanaomtafuta  na kuangamia. Akaniambia endelea kusema ukweli  ili watoto wake wapone na waifuate njia yake halisi na wala  HEBRON  usiogope lolote anayekuchukia wewe hakuchukii wewe ananichukia mimi MUNGU, na hakuna atakayeweza  kukuzuia kusema kweli yangu mimi ndiye nipo ndani yako, na wanaoshindana nawewe mimi MUNGU nawashughulikia na shoka langu lipo juu ya shingo  zao na hukumu yao ipo tayari. Adui wakubwa wa MUNGU hao ni yuda tayari mkono wa MUNGU haupo juu yao tena, ndivyo alivyonieleza na mimi sibadili lolote wala kuongeza. Siku hizi  wameibuka watumishi na mafunuo ya shetani wanazika BIBLIA kanisani au hata katika nyumba .
Ewe mwanadamu hili ni jambo la kumuhuzunisha sanaMUNGU, wala siyo sahihi. Maana yake huku ni kumzika MUNGU au kumfukia asiwepo tena au lile NENO ambalo ni MUNGU linauliwa na huyo mtumishi na badala yake anatumia nguvu za giza japo anashika BIBLIA maana wakristo hufuata BIBLIA  akitumia kitabu kingine mtashtuka na kukimbia, ila ufunuo huu ulijificha  na leo nakufumbulia peupe waziwazi. Ni kuulize swali; Je, MUNGU anazikwa? Jibu ni hapana. Je! Ndani ya NENO nani hukaa?  Jibu ni MUNGU. Sasa kwa nini MUNGU azikwe na watumishi? Jibu  Hawa siyo watumishi wake tayari ni waasi, hawamtaki MUNGU wa kweli wanaongozwa na mungu mwingine ambaye ni wa uongo na kiongozi wao au baba yao aliyekuwa ndiye  joka kuu. Na huku ndiko kanisa kutekwa na shetani. Watumishi au mtu yeyote anayezika BIBLIA  huyo hamtaki MUNGU  wa kweli tena, ni nguvu nyingine ya adui hufanya kazi ya kuwaangamiza, ukiona mtu yeyote au madhabahu wanazika au kufukia katika kanisa ujue hilo haliongozwi  na MUNGU tena, haijalishi mnamtaja, hiyo ni siri ya mtumishi wa hapo na maagano yake ya nguvu za shetani ndani yake.
Madhara  yake kwa waumini hamuendi mbinguni wala hamutamuona  MUNGU, na zaidi hamtakua kiroho na badala yake hata kama ulishakua kiroho utaporomoka kabisa na mwisho wake ni jehanamu, sasa ufunguke ufahamu wako, na waulize swali je kwa nini mnazika BIBLIA? jibu  hawana la kuwaambia  badala yake ni aibu tupu maana umeujua ukweli na unapona. Na ili upone usishiriki hapo tena hiyo ni kambi ya shetani 100%, na kazi yake ni kuua NENO la MUNGU lisiende mbele kikweli ila liwe maandiko tuu.
Jambo lingine ufunguke zaidi, tunajua  tunapookoka majina yetu yanaandikwa mbinguni juu na hata siku moja hayafukiwi au kuzikwa ndiyo YESU atupokee, au kwa maana nyingine kufukiwa majina ardhini katika madhabahu tena inawekwa na sementi kabisa, maana yake ni wewe umeandikwa katika kitabu cha shetani  kuzimu na umeshafungiwa hapo na tayari upo kaburini japo unaishi, madhara yake maisha yako  yatakuwa ni shida tu na mateso na shetani anao uhalali na wewe sababu ya huyo kuhani wake anayekuongoza wewe na umekiri kwa kinywa chako unamuita baba wa kiroho. Nakuuliza swali, je upo kwa ajili ya jina lako  liadikwe kwenye kitabu cha uzima juu mbinguni?  Jibu ndiyo. Sasa mbona wengine majina yao yanaandikwa kuzimu? Je wakifa wataenda  wapi? Jibu ni kuzimu. Je kuhani au mtumishi wa jinsi  hii ni mtumishi wa MUNGU wa kweli? Jibu siyo. Na kama siyo huyu ni mtumishi wa nani?  Jibu ni mtumishi wa shetani 100%  (Kristo wa uongo na ni mpinzani wa MUNGU).
Na zaidi  baraka za vitu vyako vinatoka mbinguni na siyo kuzimu je ni kwa nini watumishi baadhi yao wanakuambia leta pesa zako, au dhahabu zako au vito vya thamani halafu wanakuambia uvilete vifukiwe kanisani eti ndiyo umemjengea MUNGU madhabahu? Wanapofukia hivyo vitu vya thamani  ni utajiri wako unachukuliwa na hiyo madhabahu na huyo mtumishi na kila utakachokipata utashangaa unampelekea vyote hata ufilisike wewe ukijua unampatia MUNGU. Hutumia njia hii kumuendesha  muumini uchumi wake amletee wote, sasa huu ni unyang’anyi na YESU siyo mnyang’anyi na usikubali funguka hapo, hakuna  YESU wa kweli.
Tabia nyingine ukikuta mtumishi ana au amekupa fedha akakuambia uihifadhi usiitumie siku yoyote ile, unapaswa ujiulize kwa nini aniambie hivyo kwanza? Pesa hiyo huwekwa majini ya chuma ulete na ukipata pesa utashangaa unamtafuta yeye tu umpe hufikirii kingine. Kama unayo ichome inayo mapepo ya wizi wa pesa zako, na tabia hizo ni za shetani za wizi wa kumuibia  muumini kwa kutoa mwenyewe na zaidi lazima akuibie nyota yako na akili yako ili usishtuke. Leo funguka na upone katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI na usiogope nakuombea.
NOTE:
Ujumbe kwa watu wote, ujumbe huu haujatoka kwangu mimi  HEBRON nimeambiwa na MUNGU aliye ndiye ALPHA na OMEGA, asiyefananishwa na chochote au kufanyiwa mabaya au asiyekufa kama viumbe alivyoviumba ambavyo vina muda wa kuishi na kufa. Mambo yote yatapita ila NENO lake litabakia palepale, ila hao wanaozika BIBLIA ameniambia ole wao shoka lake lipo kwenye shingo zao, na ndivyo ilivyo na haitabadilika, asema BWANA MUNGU WA MAJESHI.

NABII  HEBRONWILSON KISAMO.

[ad_2]