Close

KWARESMA ZA SASA 99% ALL OVER THE WORLD NI FEKI.


NI BENDERA FUATA UPEPO WA MAPOKEO YA MPINGA KRISTO

Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron wa Kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY TANZANIA. YESU WA NAZARETI anawapenda watu wote wa ulimwengu huu na anataka mumrejee yeye ili awe BABA yenu na mwokozi wenu wa kweli ili katika ule mwisho muwepo mbinguni mahali alipo yeye. Ila ameniambia mwanangu Hebron endelea kuwaeleza watu ukweli ili wanijue mimi kiukweli 100% na siyo kidogo kidogo maana watu wengi wanafundishwa kunijua mimi kwa njia ya uongo japo wananipenda, sasa waeleze kweli yangu, maana shetani ameliteka kanisa kupitia njia ya Mpinga Kristo, ila sasa Hebron nimekupa mamlaka katika ulimwengu wote ubomoe ufalme wa shetani na kuwarejesha watu kwangu mimi. Muda wowote nitarudi kulichukua kanisa langu la kweli na silo kanisa lenye mafundisho ya uongo (maana ya kanisa atakalolichukua ni mtu aliyeokoka kikweli na ndani yake kweli ya neno lake lipo na liwe hai siyo neno mfu, maana watu wengi wamejaza maneno mfu yasiyo na uhai ya MUNGU).
Nitaelezea kwa ufupi kidogo kuhusu kwaresma. Hiki ni kipindi cha mfungo kabla ya Pasaka, ila shetani amemiliki hiki kitendo cha kwaresma kwa kuwapoteza watu na kuwashirikisha matendo ya kumpinga YESU (Mpinga Kristo) na kama watu wanafunga kwaresma na katika mifungo hiyo wanashiriki kuvunja amri za MUNGU, tayari mfungo huo ni wa yesu wa uongo (Kristo wa uongo). Kivipi? nitakuelezea utaelewa.
1.     Kwanza kabisa tarehe za kuanza mfungo watu wanawekewa alama ya majivu na msalaba kwenye paji la uso. Hii tayari ni kosa kwa YESU pia ni dhambi. Biblia inasea mfungapo hata mtu asikuelewe, pili alama ya msalaba na kupakwa majivu biblia haijaruhusu, tatu hayo majivu unayopakwa ni ya maagano ya Mpinga Kristo, na pia kabla ya YESU kusulubiwa na yeye alishiriki pasaka ila hakujichora alama ya msalaba. Yeye ndiye njia yapasa kumfuata yeye kwa kila kitu alichokifanya hata kufunga kwako, kuomba kwako na kumheshimu MUNGU. Ukienda kinyume tu na Neno La MUNGU tayari na wewe umemtukana MUNGU, yawezekana kwa kujua au bila kujua, sasa uelewe ukweli na upone. Misalaba na sanamu wala hakuna cha msalaba mtakatifu.
2.     Jambo lingine YESU hakutueleza tuwe tunafunga kipindi chake cha pasaka tu ndio tuache uovu, uovu uachwe milele na kila mtu na siyo watu kujitengea kipindi cha utakatifu na kipindi cha dhambi yaani kumtumikia shetani. Mifungo ya aina hii ya kwaresma ni feki na MUNGU haifurahii kabisa, ila shetani anaifurahia maana hata wanaofunga amewapa mafundisho ya kuzimu wayashiriki. Mfano kuabudu sanamu, kuwaabudu watakatifu watoto wa MUNGU waliopo mbinguni wakati MUNGU mwenyewe aliyewaumba amesema aabudiwe yeye peke yake.
Sasa utashangaa watu wanawataja na kushiriki kinyume na biblia na jina la YESU wanalitaja. Ninachokueleza uelewe wapo YESU wawili  yupo YESU WA NAZARETI aliye mwana wa MUNGU wa kweli aliyekufa na kufufuka na hata ule mwisho atakuja kuuhukumu ulimwengu huu. Na yesu wa pili ni yesu KRISTU, huyu ndiye kristo wa uongo ambaye asili yake ni kuzimu na hata YESU WA NAZARETI alipokuwepo hapa ulimwenguni alisema watakuja wakristo wa uongo na watatumia jina langu hili hili ila mtawatambua kwa matendo yao. Sasa chunguza ibada zao, wanamtaja YESU ila wanashiriki kuabudu watoto wa MUNGU, hii ni dalili tosha uelewe hao ni wa kuzimu. Japo hao wanaoshiriki wengine hawajijui ila usishiriki tena utoke huko. Ila viongozi wao wanajua kabisa anapewa maelekezo na shetani (Mpinga Kristo)
Ila mwisho umeshafika, sasa ndugu msomaji natumaini unazidi kuelewa sasa na hata ukiwauliza kwa nini wanaabudu sanamu au kuwataja watoto wa MUNGU wawaombee jibu hawana. Anayetuombea ni ROHO MTAKATIFU ndiye tuliyepewa na YESU zawadi. Sasa Mpinga Kristo amepindisha biblia na kuwa uongo badala ya kweli na watu wakiupokea uongo na hao tayari wamekuwa ni watoto au wana wa yesu KRISTU wa uongo na mbinguni hawaendi. Zaidi kinachofanyika kwenye ulimwengu wa roho wanapofunga ndipo wanapozidi kujiunganisha na ufalme wa shetani badala ya kujiunganisha na ufalme wa MUNGU aliye hai.
Hauwezi kujiunganisha na ufalme wa MUNGU katika mfungo wakati unachokitenda japo umefunga unamkufuru MUNGU na sheria zake ambazo amesema zisitoke katika kinywa chako yaani uzishike na uzitende siyo uzijue halafu uzitupilie mbali, zisitoke moyoni mwako.
3.     Jambo lingine mfungo unafunga wakati wewe mwenyewe siyo mwanafunzi wa YESU WA NAZARETI, haujabatizwa ubatizo wa maji mengi (Mathayo 28: 16-20). Sasa kama hawajawa au kuwa wanafunzi wa YESU wanafunga nini? Je ni mfungo wa YESU WA NAZARETI, jibu siyo, ni kwaresma ya Mpinga Kristo. Jambo la kwanza point ya kuelewa kuwa tayari siyo wanafunzi wa YESU tazama wanabatizwa ubatizo gani? Je biblia imeagiza watu wamwagiwe maji kichwani ndio uitwe ubatizo? Jibu siyo. Na je nikuulize swali, je MUNGU aliagiza watu wabatizwe ubatizo gani? Jibu, ubatizo wa Yohana ndio umetoka mbinguni na ili uwe mwanafunzi wa YESU WA NAZARETI fuata ubatizo wake. Ila mabilioni ya watu katika ulimwengu wote siyo wanafunzi wa YESU WA NAZARETI ni wanafunzi wa yesu wa uongo wa kuzimu.
Najua mabilioni ya watu hawaelewi ni sababu shetani aliliteka kanisa na Mpinga Kristo. Ni wakati wa wewe kupona sasa uje upande wa YESU wa kweli maana haukujua ukweli hata wakabadilisha tendo la ubatizo kimatendo wakachukua kibakuli. Nakueleza wazi ili upone Jehanamu moto ni mkali. Rejea kwa YESU utakumbuka ujumbe huu usipobatizwa ubatizo wa YESU wa kweli. Ona sasa na wewe unafanywa kuwa mwanafunzi wa yesu KRISTU wa kuzimu au Mpinga Kristo tena waeleze na wengine watumie ujumbe huu na utapona. Tazama sasa uone jinsi kwaresma 99.9% watu wote wanaofunga wamepigwa upofu kumbe wapo kambi ya yesu wa uongo na hii ni sababu ya kufuata mapokeo ya elimu ya wanadamu na siyo ya MUNGU wa kweli. Na pia MUNGU ametuelekeza tuwe watakatifu siku zote na tusitende dhambi.
Sasa cha ajabu Mpinga Kristo amewapiga watu upofu wasijielewe wakatengewa kipindi cha utakatifu tena feki kwaresma na baada ya pasaka utakatifu bye bye see you next year the same Lent time, muda mwingine ni uovu tu. Nikuulize swali, je MUNGU wa kweli aliye BABA wa YESU WA NAZARETI alituagiza tuwe na kipindi cha dhambi na utakatifu? Jibu, MUNGU hana michangano ni utakatifu peke yake. Sasa elewa ya kuwa kwaresma hizi ni feki hazina ushirika na YESU WA NAZARETI bali zinaushirika na yesu KRISTU wa uongo (Mpinga Kristo). Na watu muelewe ili mpone, haya yote aliyenieleza YESU WA NAZARETI aliyekufa pale msalabani na kufufuka ili wewe uokolewe. Ila amenieleza niwaeleze ulimwengu wote mjue ukweli na mumrejee, aliwatuma watumishi siku nyingi waseme ukweli nao wakamsaliti sasa ni yeye  mwenyewe na serikali yake ndio wanaukomboa ulimwengu na wewe nakusihi umrejee, mambo yameharibika katika ulimwengu wote, ibada ni za mpinga kristo only 2% ndio ina YESU wa kweli. Na mimi Hebron nautoa ujumbe kama alivyonieleza na hakuna atakayeweza milele kunizuia kusema kweli yake, maana siyo mwanadamu bali ni MUNGU yupo ndani yangu, sasa kuna atakayeweza kumzuia MUNGU akijaribu majibu yake ni kuangamia na ndivyo ilivyo wala haitabadilika. Ufalme wa shetani unachomwa moto kila siku kwanzia 2010 na wachawi wanajua, hata freemason wanajua, hata miungu yote inajua sasa hivi ni kipigo tu. Hivyo msiogope shetani na mpinga kristo aliwatesa sana wanadamu ila sasa ni mwisho sikilizeni haya niwaelezayo mtapona roho zenu na zaidi soma makala ya Nabii Hebron na vitabu utakuwa salama.
SALA YA TOBA
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE UANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA UZIMA, UNILINDE, UNIONGOZE MILELE, NITENGE NA MPINGA KRISTO NA YESU WA UONGO.
AMEN.
SOMA:
Mathayo 7: 13-27
Mathayo 15: 7-9
Ufunuo wa Yohana 22:15
Kumbukumbu La Torati 32:39
Kutoka 20: 1- 20

NABII HEBRON.