Close

MADHABAHU YENYE USHIRIKA NA MUNGU ALIYE HAI IPO HIVI! MADHABAHU ISIYO NA USHIRIKA NA MUNGU IPO HIVI!

MADHABAHU YENYE USHIRIKA NA MUNGU ALIYE HAI IPO HIVI! MADHABAHU ISIYO NA USHIRIKA NA MUNGU IPO HIVI!













2 Wafalme 23:15
Katika ulimwengu huu kuna aina mbili ya madhabahu ipo madhabahu ya MUNGU aliye hai na ipo madhabahu ya miungu au ya shetani na madhabahu hizi huwa katika ulimwengu wa roho na katika mwili madhabahu hizo hukaa ndani ya mwanadamu na mwanadamu huyo huwa ni kuhani. Madhabahu hizi ili ziingie ndani ya kuhani huyo kwa mfano madhabahu ya MUNGU aliye hai ili iingie ndani ya kuhani ni mpaka MUNGU peke yake aamue na hivyo hivyo na madhabahu ya shetani, mpaka shetani aamue kuingia kwa kuhani katika kanisa, na kwa shetani katika madhabahu yake ipo njia nyingine, ni pale mtumishi anapojiita, kujifanya au kuwa freemason, mchawi au kuwa mtumishi wa mshahara au atakapomsaliti YESU, hapo ndipo shetani huipanda madhabahu yake na ndipo wengi mnaona watumishi wengi ni wachawi hii ni sababu ndani yao ipo madhabahu za shetani (miungu) na hata wewe muumini kama unaongozwa au kusali katika kanisa la jinsi hiyo au mtumishi wa jinsi hiyo uelewe na wewe ndani yako unapandikiziwa pasipo kujijua maana jinsi alivyo kuhani ndivyo na picha ya kanisa lilivyo.
A.    MADHABAHU YENYE USHIRIKA NA MUNGU ALIYE HAI
§  Hii ni madhabahu ya MUNGU mwenyewe inayotenda kazi ndani ya mtumishi, nitaelezea  kwa kifupi upate picha. Kwanza haionekani kwa macho ya nyama na damu ila kitakachokujulisha ni madhabahu ya MUNGU aliye hai inatenda kazi, chunguza tabia za kuhani, kanisa liwe lina wokovu wa kweli siyo wokovu halafu kanisa linachangisha.
§  Lazima kuhani awe ameitwa na MUNGU na pia asiwe msaliti atende yaliyo ya MUNGU tu.
§  Neno la MUNGU halibadilishwi, watu wanafunguliwa pasipo kutoa pesa au kuchajiwa malipo yeyote kama vile katika hospitali za kibinadamu.
§  Lazima ubatizo wa maji mengi na yanayotembea ndiyo yanayotumika kubatiza, hakuna ubaguzi kwa watu wote ni sawa. Majibu ya waumini wanayapata kila waombapo katika madhabahu ya kuhani huyo. Kanisa hilo halichangishi pesa au harambee, bali hujitegemea peke yake maana madhabahu ya MUNGU aliye hai inajibu kwa moto, na madhabahu ya MUNGU milango ya kuzimu hailiwezi milele. Madhabahu ya MUNGU ina nguvu kuliko madhabahu zote za aina yeyote ile.
2 Wafalme 23:15 Neno linasema “tena zaidi ya hayo, ile madhabahu iliyokuwako Betheli, na mahali pa juu alipopafanya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli,madhabahu hiyo aliibomoa; na mahali mahali pa juu alipateketeza, akapaponda-ponda hata pakawa mavumbi, akaiteketeza ile Ashera.”
Katika neno hili utaona kuwa zilikuwepo madhabahu za kuwakosesha watu wa Israeli ili wapotee na hata leo zimejaa na madhabahu hizi zinaongozwa na mungu mke na ndizo zilizopo kwa idadi kubwa katika ulimwengu huu ili kuwaangamiza watu roho zao ili ule mwisho wasimuone MUNGU, maana kazi ya madhabahu ya MUNGU ni kuhakikisha watu wanavunwa na MUNGU na madhabahu ya shetani ni kuhakikisha inawavua watu wapelekwe jehanamu, na jinsi ifanyavyo kazi haitaitwa madhabahu ya shetani, ili msifunguke ila siri anakuwa anaijua kuhani peke yake, ila nakufundisha uelewe vizuri maana watu wanashindwa kutofautisha madhabahu ya kweli na mfu.
Sababu wapo watumishi ambao kweli baadhi yao waliitwa na MUNGU na watu mnayajua hayo ila mbeleni walimgeuka MUNGU wakawa mbwa mwitu (ninamaanisha madhabahu ya MUNGU ikaondoka na shetani ndiyo akaingia na kuendeleza hilo kanisa pasipo watu kuelewa, ila wengi mtaona sasa tofauti. Kwanza nguvu za MUNGU zinaondoka, shida zitaanza kujaa kwa waumini, hakuna uponyaji, inabakia ni story tu na kupoteza muda. Ukiona hivyo ondoka maana uelewe tayari MUNGU ameondoka na MUNGU akiondoka ni nani anayebakia? Jibu ni shetani.
B.    MADHABAHU ISIYO NA USHIRIKA NA MUNGU ALIYE HAI
Madhabahu hii kwanza zipo za aina mbili lazima uelewe. Madhabahu ya kwanza uelewe kimwili ni ya waganga wote wa kienyeji hawa wanazo madhabahu za shetani, pili katika kanisa na inakuwa ipo ndani ya mtumishi. Kiongozi na yeye anawaambukiza wote wanakuwa katika ushirika na shetani, jinsi alivyo kuhani ndivyo na kanisa lake lilivyo!!!
§  Kwanza wanabatiza ubatizo wa maji ya kikombe, na wengine wanabatiza ubatizo wa maji mengi ila kuhani anakubatiza kwa jina lake halafu anachanganya kwa jina la BABA na MWANA na ROHO MTAKATIFU. Hii ni madhabahu ya miungu na inaongozwa na mungu aina ya mungu mke.
§  Kanisa linaloabudu sanamu, kufanya ibada za wafu, kubatiza watoto wadogo, kubariki watu wazima kinyume na biblia, haijalishi wanaimba nyimbo za kumsifu YESU, uelewe yupo yesu wa kuzimu na wanapotenda hayo uelewe ni kristo wa uongo ndio anainuliwa na miungu. Madhabahu hiyo haina ushirika na MUNGU aliye hai ni ya miungu (mke).
§  Lazima iwe na mapartiners na lazima ili ufunguliwe lazima utoe pesa kama vile kwa mganga, wapo walioambiwa MUNGU anataka damu ya kuku au pesa kwanza, na wewe unao akili ukisoma neno la MUNGU linasema nimewapa bure, toa bure, sasa uelewe hiyo ndiyo formula ya madhabahu ya MUNGU aliye hai hachaji pesa sababu damu ya YESU ilishalipa kila kitu. Ila ya shetani hakuna bure na zaidi hauponi unawekewa pepo lingine la kupona tu kwa muda fulani shida inakurudia pale pale, belzebuli hawezi kumfitini belzebuli mwenzake.
§  Katika kanisa hilo waumini humuabudu kuhani kama yeye ndiye MUNGU na hata kuimba nyimbo za kumsifu kuhani ndani ya kanisa. Ukiona hayo elewa ni shetani ndiye atendaye kazi.
§  Hakuna majibu, uponyaji, ni shida tupu. Waumini wanafunga na kuomba hakuna majibu, hiyo ni dalili hiyo madhabahu ni ya baali. Tazama kipindi cha Eliya na baali, madhabahu ya Eliya ikajibu lakini ya baali haikujibu na ndivyo ilivyo leo hii makanisa mengi yanaabudu baali.
§  Inafanya biashara, kuhani ni mchawi au anaongozwa na mizimu, kuhani ni mzinzi ni mlevi, anavunja ndoa za waumini na matendo ya ufisadi, uonapo hayo uelewe ni madhabahu ya shetani.
§  Ukiona unatoa sadaka na unafilisika elewa hiyo madhabahu imekufa na kazi ya madhabahu mfu ni kuua maendeleo ya watu na kuharibu na kufilisi, wewe utabakia kutiwa moyo tu, siku ukishtuka umeishiwa hata pesa ya chakula hauna tena. Na hata kuhani na yeye akiishiwa ataanza kukopa benki, au kukopa pesa waumini na wala harudishi anakuwa na yeye ni mzimaji na ukisha ishiwa utaona kuhani hana muda na wewe hata kama alikuwa anakuja nyumbani kwako au kukupigia simu mara nyingi utaona simu zake zimekatika hakuna mawasiliano na wewe. Ameshajua hauna kitu tena, amejipanga kuwatafuta wengine, tena anawanyanganya akitumia jina la yesu aliye naye wa uongo.
§  Kuhani anakuwa na tamaa ya pesa sana, na hata huwachagua wenye pesa ndiyo huwapa vyeo vya kanisani ili asiye na pesa hampi cheo chochote.
§  Hufungisha ndoa kwa agano la shida, hubariki pombe, hushiriki matambiko.
§  Hubusu misalaba na sanamu (Daniel 3:18, 28-30[soma]) utaona jinsi watu wanavyotengenezewa na makanisa baadhi katika ulimengu huu waabudu miungu na maashera. Wewe kataa kama Shadraka, Meshaki na Abednego, kimatendo na kiimani.
§  Huzika majina ya waumini na vitu vyao vya thamani katika altare na wengine huchimbia pesa au kufukia mnyama au biblia na kuzika madhabahuni.
§  Huomba omba michango kwa njia ya TV au Redio na harambee, na pia zina mabenki, kuuza madawa ya kulevya, hufufua misukule kimazingaumbwe, wanatumia elimu ya hekima ya wazee kuongoza makanisa hayo badala ya ROHO MTAKATIFU.
§  Hufundisha mafundisho potofu, soma makala ya Nabii Hebron ufunguke zaidi pamoja na vitabu vyangu.
§  Huuza vitambaa vya leso, stika zenye alama za vidole vyao na stika zenye saini zao kwa majina yao. Wakikueleza ipo nguvu katika hivyo vitu, hawaelezi hizo ni hirizi amekufunga wewe Baraka zako zinaenda kwake na ndani ya stika hizo yapo majini yanakuangalia Baraka zako katika ulimwengu wa roho yanaiba na wewe utabakia kuteseka siku zote.
§  Ilikumuona mtumishi kwa private lazima utoe pesa na uandikwe jina au upewe coupon mfanyiwe arrangement ya siku yako. Huyo siyo MUNGU aliye hai ni mungu wake unaenda kuonana naye uelewe.
§  Mtumishi kujiita yeye ni YESU au ni MUNGU, huyo ni pepo liko ndani yake.
§  Watumishi wanaotoa makafara na wengine wanazika mafuvu ya vichwa kanisani au mtu.
§  Jambo lingine ni ashera katika makanisa ambayo asili yake ni miungu ili yawapoteze wanadamu lazima yanakuwa na maashera, mfano masanamu ndani ya kanisa, kuvaa kofia kuhani, kubeba mkuki na majoho yenye msalaba au picha ya njiwa, hayo ndiyo maashera, na mahali pa jinsi hiyo uelewe ni mungu mke ndiye aabudiwayo hayo madhabahu mfu.
§  Ukisoma 2 Wafalme 23:15 utaona zinabomolewa na sasa unapoabudu mahali hapo madhabahu hiyo inajengeka ndani ya moyo wako, na wewe unakua ni pepo sasa, mfunguke, maashera ni misalaba makanisani. Hizo zote ni dalili ya kuwa ni madhabahu mfu.
NOTE:
Enyi watu wote wa mataifa amenituma YESU niwaeleze na mfunguke msishiriki, shetani ameliteka kanisa, jiangalie wewe kama haujatekwa na shetani unayobahati usimame imara, uwatumie na watu wengine ujumbe huu wasome na wewe utakuwa unatenda vyema mbele za MUNGU, roho za watu zitapona nyingi.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA, UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE, NAKUREJEA WEWE, NISHIKE MKONO, TAWALA NAFSI YANGU NA AKILI YANGU, NAJITENGA NA MIUNGU NA MAASHERA YAO, NITOE HUKO YESU, NISISHIRIKI HATA KUINGIA HUKO KIMWILI NA KIROHO, NISHIKE YESU. AMEN.
Endelea kusoma makala na vitabu, pia karibu sana katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, nawakaribisha watu wote wa nchi zote, karibuni, na mimi nitafurahi sana kuwaona na pia YESU WA NAZARETI anayeishi ndani yangu.
NABII HEBRON.