Close

MAELEZO YA YOUTUBE: JINSI YA KUTOFAUTISHA MITUME WA MUNGU NA WA SHETANI


NABII HEBRON:  Mtakatifu, Mtakatifu, BABA MUNGU wa majeshi uketiye mahali pa juu, asante kwa ajili ya muda huu na vipindi vyote vilivyopita, nazidi kualika upako wako na neema yako na ukuu wako na nguvu zako ziendelee kutamalaki mahali hapa katika kuwafungua watoto wako; sema nao ukiwafundisha; ninawavua mavazi ya uchovu, ninawaondolea giza, ninawapiga wakuu wa anga, malango yote, ninavunja kwa jina la YESU, roho za upinzani, majini, mapepo, maajenti, ninaachilia moto, moto kwenye viti, kwa jina la YESU; ninawachoma ninawachoma, ninawateketeza kwa jina la YESU, kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti, kwa jina la YESU, kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti, ninachoma, ninachoma, kwa jina la YESU, kwa damu ya YESU,ninaondoa, ninaondoa kwa jina la YESU, roho za upinzani, waliovalishwa uchawi, ninaamuru moto upite kwenye viti kUwa jina la YESU, ninaamuru kwa jina la YESU,  iOndoke kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti, kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, moto upite, moto upite kwenye anga, upite kila mahali, kwa damu ya YESU, kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Masikio yenye mapepo yatoke haraka haraka, Toka haraka kwa jina la YESU, kwa damu ya YESU. Ninakomboa Biblia, ninakomboa viti, ninakomboa anga kwa nalibadilisha kuwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti. Roho za kuchoka naziondoa kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, Amen.
NABII HEBRON:  BWANA YESU asifiwe; napenda kufundisha kidogo kwanza halafu tuingie kwenye kazi huko huko, maana siku zote maombi bila kuwa na kitu kichwani ni kazi bure. Penda sana kumjua huyu YESU. Haleluya; nimependa nikamja, na wewe nataka umjue. Na siku moja katika kumjua utafika pale alipo yeye. Lakini kama humjui, hautafika. Nataka nikufundishe, Haleluya; Utafungua katika kitabu cha Neno la MUNGU, 1YOHANA 2:18 – 19. BWANA YESU asifiwe, BWANA YESU asifiwe,
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Leo tunakwenda kujifunza habari za Mitume. Habari za nani?
WAUMINI:  Habari za mitume.
NABII HEBRON:  BWANA YESU asifiwe;
NABII HEBRON:  1YOHANA 2:18-19. Naomba usome.
MTUMISHIBWANA YESU asifiwe; “Watoto ni wakati wa mwisho, na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja,…
NABII HEBRON:  Haleluya, MUNGU anasema hivi, watoto huu ni wakati wa mwisho, na kama mmekwisha kusikia kabla, mpinga Kristo yupo, na tayari amekuja, nataka uelewe, ni wewe MUNGU anakuambia ukae tayari. Mpinga Kristo ameshakuja, sasa unapomjua yeye, ninavyokwenda kukufundisha, hakika hatakupata. Tuendelee..
MTUMISHI:  Hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo, kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho, walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu.
NABII HEBRON:  Haleluya; Biblia inasema hivi, walitoka kwetu lakini hawakuwa wa kwetu. Ni hivi, habari za mittume nakuja kuwafundisha hapa, maana sasa hivi kumekuwa kuna mitume wa uwonngo. Kama kulivyokuwa na mitume wa kweli, ujue kuna mitume wa uwongo. BWANA YESU asifiwe. Sasa kuna watu wengine wanasema ni Wakristo, wametoka kwetu sisi tukijiita Wakristo, au huko tulikopita, lakini ni mitume wa uwongo. Nitakufundisha, hawaitwi wa uwongo. Utawajuaje? Nitakwenda kuwafundisha, maana YESU anarudi, na shetani na yeye ameandaa mitume wake, akawatuma habari za uwongo, kuhakikisha kwamba anakupoteza wewe. Wewe unaweza kuona uko nao pamoja, ila hauko nao pamoja. Haleluya; BWANA YESU asifiwe
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Unapenda kuelewa?
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Angalia usitoe machozi lakini. BWANA YESU asifiwe. Maana unakwenda kufunguka vizuri. Tutasoma pia Mathayo 16:18-19.
MTUMISHIBWANA YESU asifiwe, nitasoma. “Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu, nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda, nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni.
NABII HEBRON:  Haleluya; hayo ni maneno YESU aliyoniambia pia aliponituma. Na leo yanakwenda kufanya kitu kwako.
WAUMINI:  Amen..
NABII HEBRON:  Lakini nikufundishe kidogo, YESU aliposema kwa Petro nalijenga kanisa langu, sasa Petro yuko mbinguni. Kulikuwa kuna mitume wengine pia ambao YESU alikuwa nao. Wote walienda vile vile. Lakini kwa viwango tofauti. BWANA YESU asifiwe. Lakini pia nataka uelewe, shetani na yeye, ana mitume wake kuhakikisha anawafungia watu wasiende wapi?
WAUMINI:  Mbinguni.
NABII HEBRON:  Amenituma nifungue muende mbinguni bwana. Haleluya,
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Nataka uelewe, shetani amebadilisha Biblia kila kitu, Haleluya; MUNGU alivyonipa habari hii nilishangaa sana na kushtuka. Maana tumezoea kusikia wachungaji wa uwongo. Si ndio, Lakini leo ninawaambia hivi, wapo mitume wa uwongo. Watume wa uwongo, watasema wanafanya kazi ya YESU; tumesoma katika kitabu cha kwanza, mtaona mpo nao, kumbe hamp njia moja. BWANA YESU asifiwe, Kazi ya mitume wa MUNGU wa kweli ni kupeleka kweli, na kazi ya mitume wa uwongo wa shetani ni kupeleka uwongo, ambapo pasipo hao mitume wa uwongo, leo hii kungekuwa hakuna elimu ya uwongo. Nakwambia, unataka kuwajua? YESU katika watume wake, BWANA YESU asifiwe, YESU alikuja akaonyesha njia, enendeni kwa mataifa yote mkawabatize kwa jina la BABA na la MWANA, wakazamishwa, Haleluya, wakafuata kama ilivyo; wakatokea sasa na mitume wa uwongo, wakakusubiri na wewe wakaja kwa mataifa, wakasubiri vitoto vidogo wakawamwagia maji vichwani pwa, pwa,… Hao ndio mitume wa uwongo hao. Hao wanapeleka watu jehanamu. Ninakuambia hata mimi nilikutana na mitume wa uwongo, wakawawahi wazazi wangu, BWANA YESU asifiwe, mimi sikuitwa na baba yangu, ameniita mwenyewe. Sasa kuna mitume wanaitwa na ma-dini, wanaitwa na makampuni, wanaitwa na mashirika kwa ajili ya kuendeleza uwongo, wewe unaona uko njia ya kwenda mbinguni, lakini mtume anakuja kuanzisha kazi ya uwongo. Mafundisho ya uwongo. Tafuta kwenye Biblia, anasema mtawajuaje? Kwa matendo yao. Tafuta kwenye Biblia, hakuna ubarikio wa watu wazima, hakuna.! Sasa hao ni mitume wa uwongo kuanzisha kazi hiyo. Amenituma YESU niwaambie mataifa yote. Usije ukajiona uko nao unaenda nao mbinguni kumbe hawaendi. Na wako wengine wanampenda MUNGU, wakaona wamtumikia MUNGU, kumbe wamevutwa na ile roho wameingia kwenye mitume wa uwongo. BWANA YESU asifiwe. Lakini hawataijiita mitume wa uwongo utawajuaje? MUNGU anasema watoto wangu, wakati ni wa mwisho, wamekuja kuvuna watoto wa MUNGU. Wewe kinachokupeleka mbinguni ni ukweli tu. Lakini uwongo ndio njia umekamata ya kwenda wapi?
WAUMINI:  Jehanamu.
NABII HEBRON:  Sasa angalia dunia nzima. Tuendelee mtumishi wa MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Sasa mmeambiwa kwamba YESU kaleta mitume wake kuhakikisha maisha yako yananyooka uende wapi?
WAUMINI:  Mbinguni.
NABII HEBRON:  Na shetani akaweka wake, kuhakikisha anakufungia kwenda mbinguni na kukufungulia kwenda jehanamu. Lakini hawakuambii jehanamu, si umepokea mafundisho ya uwongo? Unakwenda wapi? Umefungiwa wapi?
WAUMINI:  Mbinguni.
NABII HEBRON:  Unakwenda wapi?
WAUMINI:  Jehanamu.
NABII HEBRON:  Leo chomoka bwana tuende pamoja, haleluya…
WAUMINI:  Ameen.
NABII HEBRON:  BWANA YESU asifiwe. Tutafungua Waefeso 2:20-22
MTUMISHIBWANA YESU asifiwe, Waefeso 2: 20-22; Nitasoma: “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii”
NABII HEBRON:  Mmejengwa juu ya misingi ya mitume na….
WAUMINI:  Manabii.
NABII HEBRON:  Ahaaa.. Nataka nikuambie, wewe umejengwa kwenye misingi ya manabii wa kweli na mitume wa kweli au wa uwongo? Kabla ya hapa ulikuwa umejengwa wapi?
WAUMINI:  Wa uwongo.
NABII HEBRON:  Eeee?
WAUMINI:  Wa uwongo..
NABII HEBRON:  Sasa nataka nikufundishe uelewe. Utashindana habari ya kwenda mbinguni, utakuwa wewe umefaidika kwenda kuzimu. Lakini wewe unataka kwenda wapi?
WAUMINI:  Mbinguni.
NABII HEBRON:  Amenituma habari njema nikueleze. Endelea mtumishi..
MTUMISHINae Kristo mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
NABII HEBRON:  BWANA YESU asifiwe, na YESU KRISTO ndio jiwe la…
WAUMINI:  Pembeni.
NABII HEBRON:  Yaani YESU amekaa, YESU yuko zake mbinguni kimwili, ameandaa mitume. Sasa mitume wa kueneza kazi ya kweli YESU anaangalia kama anavyokuangalia hapa kwamba utafika mbinguni. Lakini shetani naye ana yesu wake wa uwongo ambaye amekaa huko chini, anangalia mitume wake wa uwongo wakibatiza watu mambo ya uwongo, wakifundisha watu vitu vya shida,  wakikataza watu kuokoka, BWANA YESU asifiwe.. Wakisema wao ni Wakristo,  wakiruhusu watu kuabudu sanamu. Hawajiiti mitume wa shetani, lakini utawajuaje? Kwa matendo yao. Watu wanaona wanaenda wapi?
WAUMINI:  Mbinguni.
NABII HEBRON:  Na idadi kubwa sana ni mitume wa uwongo, na wewe ukikaa huko unyashika, unakuwa wa mitume wa uwongo. BWANA YESU asifiwe.
MTUMISHIKatika yeye jengo lote linaungamanishwa hata kuwa hekalu takatifu la BWANA. Katika yeye ninyi nanyi mmejengwa kuwa maskani ya MUNGU katika roho.
NABII HEBRON:  Tunarudi, Haleluya… Tukiwa katika misingi ya mitume wa uwongo na mafundisho ya uwongo tumejenga na hekalu la shetani. Wewe sio wa…..
WAUMINI:  MUNGU.
NABII HEBRON:  Na mstari wa mwisho unasemaje? Katika nyumba ya MUNGU, ndio kumetoka kulipa pesa ndipo uombewe. Hii haijatoka kwenye misingi ya mitume na manabii wa MUNGU. Haleluya
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  BWANA YESU asifiwe.
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Haleluya.
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Mnanielewa watoto wa MUNGU? Nataka leo ukajiondolee kabisa vitu vya mitume wa uwongo. Kwa sababu mitume wametumwa kupeleka ukweli na shetani ametuma kupeleka uwongo watu wanaupokea. Ukiupokea uwongo umepotea! Ukipokea ukweli umepona! Sasa watu wanaomba na kutoa machozi miaka na miaka, hawamwoni MUNGU,  kumbe wamejengwa katika misingi ya mitume na manabii wa uwongo. Lakini hawawezi kujiita wa uwongo. Utawajuaje? Kwa matendo yao.
MTUMISHINaye alitoa wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu. Kwa kusudi la kuwa kamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe.
NABII HEBRON:  Haleluya.. Alitoa Manabii na Mitume, wainjilisti, wachungaji na nani?
WAUMINI:  Na waalimu.
NABII HEBRON:  Ili kuhakikisha kwamba mwili wa Kristo ukajengwe. Yaani wewe. Lakini nataka nikuambie, na shetani na yeye akatoa mitume wake, wainjilisti wake, manabii wake, waalimu wake, ili kuhakikisha kuujenga ule mwili wa mpinga kristo, ili siku moja wasiende mbinguni, wakaende jehanamu. Haleluya..
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Mnanielewa lakini? Nitaanza kwanza kukueleza kwa nabii moja kwa moja, kwa mfano upate kuelewa. Anakuja watu wanasema yeye ni nabii, anatoa nabii na hazitokei. Hao MUNGU hajawatuma kwa sababu MUNGU anasema ukweli. Ankuja nabii anawanyang’anya watu mali, hao ni wa uwongo. Anakuja nabii, annyang’anya vitu vya watu; anachangisha, anasema MUNGU anasema njoo hapa, leta milioni, hao ni wa shetani.
WAUMINI:  Amen..
NABII HEBRON:  Utawajuaje? kwa matunda yao. Na kama unasali hapo, uelewe kwamba umejengwa kwenye msingi wa manabii wa uwongo. Amenituma kubomoa na kuteketeza; tuende mbinguni. Tunapenda kwenda mbinguni watoto wa MUNGU. Au siyo?
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Lakini upo ujanja shetani alioingia nao, akaona BWANA YESU ametoa mitume na manabii na yeye akaenda kuweka wa kwake. Mtu anajuaje? Hawa  wanakuwa ni tofauti na wale wa BWANA YESU. Leo amenituma habari njema, niwaeleze mataifa yote, anakayesikia atapona, ujumbe alionituma wa kukutoa na wewe. Haleluya?!
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Ngoja kidogo kidogo, atakuja kwa mitume, BWANA YESU asifiwe. Mimi MUNGU aliponituma, nilikutana naye Serengeti. BWANA YESU asifiwe. Lakini nilikuwa sielewi kwa muda mrefu. Ilikuwa ni kama vile kwa Paulo; ukisoma kwake ilitokea. BWANA YESU asifiwe. Haleluya! Na hata nataka nikuambie ni ushuhuda sikuwa nimekuambia. Pamoja na kuongozwa sala ya toba hapa duniani, lakini nilirudi nikaongozwa sala ya toba na YESU mwenyewe nikiwa Serengeti, nikapokea ya kwake upya. Maana katika kupokea sala ya toba nilipita kwa mitume wa uwongo, wakaja wakanichafua na sala yangu ikaharibika toba yangu. Lakini neema ya YESU ikanipenyesha. Na wewe nakueleza sasa, BWANA YESU asifiwe.
WAUMINI:  Amen..
NABII HEBRON:  Akaniambia na wewe nakutuma kwa mataifa kama nilivyotuma wale mitume kipindi kile, useme kweli kama ninavyokueleza. Mimi sijali kama nachukiwa, nasema “no sweat” YESU ananipenda. Nasema hakuna shida, wanichukie, hata kina Petro walichukiwa. Kwa nini walichukiwa? Kwa nini walikuwa wananyongwa, kwa nini walikuwa wanauawa? Kwa sababu walikuwa wanapeleka ile habari ya kweli. Sasa hawaitaki, lakini hauawi mtu hapa! Amenituma habari njema. Muwe makini sana na mitume wa uwongo. Maana mmezoea kusikia wachungaji na manabii. Mitume wa uwongo nakwambia habari hiyo. ulikuwa unaelewa? Haya, unajua YESU alianzisha huduma tano, lakini sasa zimekuwa sita. Utume si ndio unasimamia pale? Wakatengeneza askofu ndio inasimamia pale. eeeeee??!funguka sasa. hayupo YESU, hakuanza hiyo. Unayechukia chukia, lakini upone. siko kwa ajili ya kukufurahisha wewe, bali Baba yangu wa mbinguni.
WAUMINI:  Ameeen.
NABII HEBRON:  Na wewe ninakuona utakuwa mbinguni.
WAUMINI:  Ameeen…
NABII HEBRON:  Ndivyo watu walivyopetezwa na kupotezwa. Haya, wakaja mitume wengine, wakaanzisha; watu wanaabudu sanamu sasa Wakristo. Hivi ndio wametumwa hayo?
WAUMINI:  Hapana.
NABII HEBRON:  Leo hii wako watu wengi wanawafuata hao mitume. Wamepotea! Warudi wabadilike na watubu. Maana bado ni mchana. Usiku unakuja. Wakati unafika, haiwezekani haiwezekani pa kupita. Haiwezekani kurejea tena, wakati wa kurejea ndio huu. BWANA YESU asifiwe. Haleluya! Haohao mitume ninaoelezea, BWANA YESU asifiwe;  Hao mitume wa uwongo ndio walitumwa wakaja kubadilisha ubatizo wa kikombe. YESU hakutuma hivyo, nawaambia wako mitume wa shetani. Mnasikia? Wakaja tena kufundisha kufungia watu ndoa kwa shida. Soma katika Biblia, hajatumwa kulaani watoto wa MUNGU. Amesema kama ni mtumishi wangu nimekutuma nitakufungulia njia. Lakini waliotumwa na shetatani wana roho ya kuombaomba, hawana kitu. Ni michango michango  kataa katika jina la YESU. Ni mara ngapi umeshiriki kwa mitume wa uwongo? Utawajuaje? kwa matendo yao. Ni wakati wa kuja kupindua mafundisho ya mitume wa uwongo. Nitafanya na nitaendelea kufanya, huo ndio ukweli MUNGU anyanyuliwe!
WAUMINI:  Amen..
NABII HEBRON:  Yeye anayesema iwe usiku na inakuwa usiku ndiye aliyenituma kwako wewe. Yeye anayesema uishi na unaishi ndiye aliyenituma. Na yule anayekusumbua na kukufungia mambo yako mimi leo naenda kushughulika na yeye.
WAUMINI:  Amen.
 NABII HEBRON:  Mitume wa uwongo ni lazima wataporomoka. Nakuambia mitume wa kichawi wataporomoka. Nakuambia na ndivyo ilivyo. Na Tanzania mitume wa uwonngo wataporomoka. Ni wakati wa kuwaachia watoto wa MUNGU. Wengi utasikia wanaitwa Apostle utafikiri ni Apostle wa YESU. Wengi sana, wanabatiza watu kwa majina yao. Hao ndio YESU alituma hivyo? Wengine wanachimbavisima ndani ya kanisa, wanabatiza watu, ukisoma kwenye kitabu cha ufunuo, ole wake aongezaye au kupunguza maneno ya kitabu cha unabii. Haya sio ya uwongo haya? Watu wakapokea. Watu wakadanganywa. Haya, wakaleta wokovu wao sasa; wa kuombaomba, ndio maana watu wengi katika wokovu wanakata tamaa. Mimi nakuambia hapa hakuna kukata tamaa, ni mbele kwa mbele.
WAUMINI:  Ameeen..
NABII HEBRON:  Umesikia? Hivi YESU amechoka? lakini watu waliookoka ndio wengi wamechoka. Kama wamechoka, wamekutana na mitume waliopanda mbegu kwa wainjilisti, wachungaji, waalimu wa uwongo, kwa hiyo ile mbegu inaenda inaangamiza. Unajua nikikuambia uinuliwe ni lazima uinuliwe. Nikikuambia ufanikiwe ni lazima ufanikiwe. Lakini kama nakuambia na haitokei ina maana ni uwongo. Maana kinywa cha nabii ni cha MUNGU. Na pia uelewe kinywa cha nabii wa uwongo ni kinywa cha shetani. Kama ni cha MUNGU hakiwezi kunyang’anya watu pesa, lakini kama ni cha shetani, ule mkono unakamatwa na shetani rikababababababa… wapi? Hii kunena wanakopi na ku-paste. sema sitaki kukopi na ku-paste nataka wewe YESU. Anaweza akaja akawa amenyanyua suruali akaanza,.. ririririririri… nini? Uwongo mtupu.  Hivi mtu atasemaje BWANA amesema halafu anachangisha pesa? Huo mdomo ni wa MUNGU au ni wa shetani? Ni wa shetani.
WAUMINI:  Ni wa shetani.
NABII HEBRON:  Wanakaaga kwenye TV, tuma pesa hapa ya kusapoti. MUNGU jamani ni omba omba?
WAUMINI:  Hapana.
NABII HEBRON:  Hivi nikuulize hapaduniani tunachajiwa bili yamaji, lakini mvua yeye ni free.. Hivi unalika heka 100 au heka 50, mazao yako anayanyeshea bure, hapa duniani ukinyeshea na maji ya kampuni unadaiwa bili mwisho wa mwezi. Kwa nini tunadanganyika hivi jamani? Huyu ndiye  MUNGU. Hewa anatupulizia bure. Hiyo nakuambia wameshindwa tu maana wangedai. Sasa watu tunatengenezewa mafundisho ya uwongo; nampokea Yesu kumbe ni mitume wa uwongo. Wangefundishwa ukweli ungekuwa maisha yako ya ajabu sana. Yeye alisema damu yangu ilishamwagika ili tusiteseke tena. Lakini sasa ni mateso mpaka kwenye mto (pillow). BWANA YESU asifiwe. unapenda nikueleze tena?
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Haya, wakaja wengine tena; BWANA YESU asifiwe. Hivi, kuna mtakatifu zaidi ya MUNGU?
WAUMINI:  Hapana.
NABII HEBRON:  Kuna mwanadamu ni mtakatifu?
WAUMINI:  Hapana.
NABII HEBRON:  Eeeh, mmeona sasa mitume hao? Hakuna mwanadamu mtakatifu hapa, ni MUNGU peke yake. Sasa watu wanapigwa upofu, BWANA YESU asifiwe; na hii ilifanyika baada ya kumuua Petro. BWANA YESU asifiwe, nataka uelewe. Ikabadilishwa. Petro mwenyewe alikuwa anasema ukweli, wakasema tumpige huyu! Yesu akasema ndani yake nimejenga Kanisa na ni jiwe, jiwe ni kweli. Nakuambia kweli ikakusaidie wewe. Ukweli wa neno la MUNGU usibadilishwe. Ukweli wa MUNGU ufuatwe. Hakuna kupunguza ndivyo inatakiwa. Ikichanganywa kweli na uwongo baasi. Watu wanaabudu sanamu wanaona kwamba ni utakatifu. YESU mwenyewe alikataa. Wakashika Biblia kama nilivyowaambia, BWANA YESU asifiwe, mtaingia Neno la MUNGU lakini mnaabudu sanamu, na kuifuta futa ndevu. Lakini huyu MUNGU aliyenituma amesema msiabudu sanamu wala kitu chcochote. Ndivyo ilivyo, lakini watu wamepotezwa.Haitoshi, wako wengine wakaanza kuchemsha maji ya kubatizia ya moto. Yanawekwa kwenye kisima, yanapashwa kiasi fulani; unaingia unatoka. Mambo yameharibika nawaeleza hii dunia jamani. Sasa ndicho walichotumwa na MUNGU.
WAUMINI:  Hapana.
NABII HEBRON:  Mitume wa uwongo. Utawajuaje? Kuna kelele nyingi sana. Wewe unamtolea MUNGU ni siri yako lakini kwa kuwa hakuna uaminifu, anakuja kwa sababu ni jangili na amakaa na majangili anajiita yeye ni mkurugenzi. Hivi YESU ana wakurugenzi madhabahuni?
WAUMINI:  Hapana.
NABII HEBRON:  Chukua namba yangu hii unipigie mimi utanikuta mkurugenzi mwenyewe. Mnasema eeee… Mmeibiwa! Wewe unatoaga pesa kwa mkurugenzi au kwa BWANA YESU?
WAUMINI:  Kwa BWANA YESU.
NABII HEBRON:  BWANA YESU asifiwe, mnaona utume wa uwongo ulivyotapakaa? Mnaona utume ulivyojaa kila mahali? Utapona? Sasa utapona katika jina la YESU.
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Mnasikia watoto wa MUNGU? Yaani maubarikio haya yote ya watoto wakubwa yaliletwa na mitume wa uwongo. YESU alivyokuwa mdogo, hata Biblia inaonyesha alibarikiwa akiwa mtoto ndogo. Akasema mimi ni njia ya ukweli na uzima nifuate. Hata mimi baba yangu alikamatwa huko nikapelekwa kwa mitume wa uwongo nikiwa mdogo mdogo nikapewa (ubatizo wa watoto), lakini nimetoka. Na wewe unayesubiri wewe njoo. Usije ukasema una ubatizo wa baba yako na mama yako,. haujatoka kwa mitume wa kweli, umetoka kwa mitume wa uwongo. BWANA YESU asifiwe; imeandikwa katika kitabu cha Warumi BWANA YESU asifiwe Warumi 10:9-10 naomba utusomee.
MTUMISHIBWANA YESU asifiwe; Kwa sababu ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu utaokoka.
NABII HEBRON:  Kwa kuwa ukimkiri YESU kwa kinywa chako, sasa kuna watu wengi wamejifunga hapo, umeelewa? kama umeongozwa sala ya toba mahali kuna mitume wa uwongo, ukisema umeokoka umekata shauri kuna kukata shauri? Kuna kuta shauri jamani? Unaambiwa kwa kumkiri YESU. Nataka nikuambie vile vile iko kumkiri yesu wa kuzimu vile vile. Kwa sababu yeye mahali ulipo ni mahali ambapo wanaongozwa na mitume wa uwongo kwa hiyo adhabu inakuchukua vile vile. BWANA YESU asifiwe. Sasa madhara yake, watu wengi wameokoka, wamekata tamaa wanampenda sana YESU mpaka wamegombana na YESU; mimi nakuambia usigombane na YESU bwana. Leo nitakufungua katika jina la YESU. Haleluya. Maana yake ni kila mtu aliyeokoka hakuna shetani kukusogelea unampiga teke teke. Lakini leo anatupandia mpaka kichwani, uwongo?
WAUMINI:  Kweli.
NABII HEBRON:  Unasema nimeokoka; nimeokoka majaribu yakija; sio kwamba hayatakuja, yatakuja lakini yatakuwa na mlango wa kutokea. Katika mlango wa kutokea, ndio unazidi kumjua MUNGU na kushinda. Mimi nilipita nikashinda. YESU alipita akashinda, mitume wa YESU walipita wakashinda. Ukishinda unafurahi. Au siyo? BWANA YESU asifiwe. Hebu uendelee kusoma. Ukimkiri YESU kwa kinywa chako mwenyewe utaokoa; sawa imeandikwa! Lakini, upo kwenye msingi wa MUNGU wa kweli au wa uwongo?
MTUMISHIBWANA YESU asifiwe, nasoma mstari ule wa kumi (10). Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
NABII HEBRON:  Haleluya! Kwa moyo na kinywa mtu huamini. Ukovu wa kuzimu, uko wa mbinguni. Utaupataje? Wa mbinguni umeandaliwa na wale mitume MUNGU aliowatuma; lakini shetani naye akatuma wa kwake, lakini watu hawaelewi. Ndio maana kanisa limekuwa kama biashara. People are looking for money. Semina kubwa wanatafuta pesa tu watumishi. Nilipita huko mimi nikakutana na hao, wakaniambia mwanzoni unajua wewe Hebron twende tukafanye mkutano mahali fulani wewe utakuwa ndio msemaji mkuu; tutapiga hela nyingi sana pale. Hee… MUNGU wangu. Nikarudi nyumbani; nikasikia sauti, ulikiona hicho nilikuwa nakuambia? Nimeacha uone. Nilikuwa mchanga mchanga bado simuelewi MUNGU vizuri. Haikutosha, Hebron changamka; tafuta wamama 60 wa nguvu. Mimi nikafikiri ni waombaji, kila mwezi akupe laki moja uwaambie nyie ni marafiki wangu wa karibu BWANA ameniambia!!!! umeshawahi jiuliza, wanafunzi wa YESU walipigwa vita sana, Kwa nini? walisema kweli. Lakini wa uwongo leo hii hawaguswi. Wanapendwa, wanakumbatiwa kwa sababu ule uwongo umeshika mizizi, umwshika kila mahali na yule aliyeshika hawajui kama ni uwongo walio nayo; sasa kiboko cha YESU kinakuja  wale watu watajua. Wengine wanasema mimi ni mtume, mimi nakuuliza YESU alimtuma mtume gani akawe na benki? Eeee? nawauliza. Amekuwa na benki; ndio ametumwa kuwa na benki? Hao ni mitume wa uwongo. Wamekuja wengine wanauza bhangi, madawa ya kulevya na vitu mbalimbali. BWANA YESU asifiwe, wanakaa madhabahuni unasikia upako unashuka; hao ni mitume wa shetani hao. Umesikia? Muwe wajanja, sasa ni kusimama. Haleluya! Na wao yesu wao (yesu wa uwongo) amewapa vya kuwawezesha kufanya kazi yao. Na mimi MUNGU amenipa uwezo wake wa kufanya kazi yake.Haleluya! Uishi salama, ufanikiwe na kumwinua yeye. BWANA YESU asifiwe. Watu wanasema tutamiliki, lakini leo hii Wakristo ndio wamechoka hatari. Uwongo?
WAUMINI:  Kweli.
NABII HEBRON:  Wanaotumia uchawi ndio wako juu. Waporomoke katika jina la YESU. Mnaweza mkakaa katika ndoa, mnachukiana. Shida ni msingi wa mitume wa uwongo uliyopokea inakaa ndani yako kama mbegu. Maisha yanaweza yakaharibika kabisa. Haujalogwa. Umechukua mafundisho ya uwongo. Natoa mfano, unapanda mche wako wa nyaya, mmoja umepanda kwenye udongo mbaya, mwingine kwenye mbolea. Ni upi utazaa?
WAUMINI:  Wenye mbolea.
NABII HEBRON:  Na wewe ni hivyo hivyo. Ukijengwa kwenye msingi wa kweli kama YESU alivyotaka utafanikiwa sana. Lakini wewe ambaye umekulia kwenye msingi wa mitume wa uwongo utasinyaa. Utaanza kuona YESU ameniacha, YESU anabagua, hapana, njoo twende mbele. Uchumi wako umeshikiliwa huko. Ulifikiri unamtolea YESU sadaka, Ulitoa kwa yesu wa uwongo.  Na yeye anazilaani. Mitume wa uwongo; kuna watu wanasali kanisani unasikia hakuna wokovu hapa, ujue kwamba umethengwa.YESU alituma watu wakaokoke au wazubae tu?
WAUMINI:  Waokoke.
NABII HEBRON:  Sasa kwa nini wanakataa watu wasiokoke? Hao ni mitume wa uwongo.Hata mimi nilikuwa kuokoka kwa sababu niliona ni ujinga nikiokoka. Lakini nakuambia wokovu ni wa maana sana mbele za MUNGU. Na wewe ambaye ulikuwa hutaki kuokoka, okoka uwe wa thamani sana mbele za MUNGU. Yamkini ulikuwa umekata tamaa kabisa, mimi nakuahidi MUNGU atakutendea jambo. Atabadilisha maisha yenu. Uliyeitwa kichaa utaitwa una akili sasa. Wewe uliyekuwa unaitwa masikini utaitwa tajiri. Uliyefungwa mnyororo wa kwenda jehanam sasa wewe ni wa kwenda mbinguni. Kuna watu walishaambiwa hawatakaa wafanikiwe; mimi nakuambia kwa jina la YESU nafungua maisha yako. Wagonjwa watafunguliwa hapahapa. MUNGU mwenyewe jina lake ni amani. Kama kuna amani maisha yanakuwa mazuri. Kama kuna amani baraka zinakuja. Kama kuna amani kuna njia ya kupita na kusonga mbele. Lakini njia zimefungwa na shetani. Ole wake shetani, jini, mchawi au mtume wa uwongo aliyekufingia. Mkono wa MUNGU utakutana naye.
WAUMINI:  Ameeen…
NABII HEBRON:  Kabisa! Hata mimi nilifungiwa umesikia? Lakini neema yake alijua kuwa nikifika wakati fulani Hebron nitamtoa. Akanificha maana mimi walinichukia sana. Wewe unafikiri ni kwa sababu gani wananichukia? Nafanya   dhambi? sema nafanya dhambi gani! Sema nimefanya dhambi gani? Si ukweli tu?
WAUMINI:  Ameen..
NABII HEBRON:  Asimame aseme ambaye nimefundisha mafundisho ya uwongo. Lakini ningesema uwongo ningukuwa nimeongezeka kwenye ile kampuni ya uwongo. Leo hii tungekuwa ma-best. Sina u-best na mashetani mimi. Haleluya! Baba yangu yeye ni mkwli. Wewe ukifundisha uwongo, baba yako anakuwa mwongo. Na uwongo baba yake ni nani? Ni shetani. Mahali pake ni wapi? Jehanam. Unataka kwenda mbinguni?
WAUMINI:  Amen..
NABII HEBRON:  BWANA YESU asifiwe. mmenielewa watoto wa MUNGU? Kazi ya mitume ni kuweka mambo ya MUNGU anavyotaka kama ilivyo na kuanzisha kweli. Hapa tumeanzisha kweli, na sehemu nyingine kweli na nyingine kweli watazaliwa hapa hapa mitume, watazaliwa wachungaji, BWANA YESU asifiwe; kwa sababu mtume yeye aliyetumwa sio mhuni. Lakini unaweza ukazaa wengine wakaenda wakabadilika. Watakutana na mkono wa MUNGU. Mimi nakuambia ukweli, iga ya YESU yeye ndiye baba yako. Haiwezekani mimi nikuambie wewe usichangishe halafu mimi nachangisha. Hivi utanielewa? Kama anachangisha tumaini la MUNGU limeondoka kwake. Hao mitume hao; juzi juzi Tanzania kwenye uchaguzi wakawaambia watu wasisali siku ya Jumapili baadhi yao. Uwongo?
WAUMINI:  Kweli.
NABII HEBRON:  Ndio mitume wa MUNGU amewatuma hivyo? Sasa Biblia inasema ikumbuke siku ya BWANA MUNGU wako ukaitakasr uende madhabahuni. Au siyo? Ni ajabu! YESU alifufua kitu kinachoonekana. Na mitume wa YESU walifufua kitu kinachoonekana. Lakini wanakuja wengine wanasema dondoka! Halafu wanakuja majitu wenye midundiko. Mara wamepakwa majivu. Wanayaandaaga! Mnapigwa upofu hamuoni mnaambiwa haoooo… Wapi; kumbe walikuwa kwenye gari! Haleluya. Nampenda sana MUNGU kwa sababu yaani akikupenda neema yake akuonyeshe utasema hii dunia imechafuka hii. Umesikia? Ujanjua miujiza inapeleka watu. Wengine wanasema wanafuata miujiza; wewe hutaki miujiza? . Kanisa pasipo wokovu miujiza ni bure. Lakini shetani naye ana miujiza yake. Na haikuanza leo, kumbuka Musa na Farao hakufanya na waganga wake?  Kama kweli hao mitume wana uwezo wa kufufua, waende kwenye hospitali Marekani wamekufa watu wengi huoni. Haooo… Muhimbili si wamejaa? Watu wengi hapa watu wamekufa wanalia lia si ndio? Lakini YESU anafufua. Waambie waende mahospitali, huwaoni! Wanaandaa watu, wanawapiga watu upofu, Wewe ulishawahi kuona wanatoa mtu msukule amekaa vizuri? Si anakuja anatisha tisha? Saa nyingine kama li-nyani, kumbe wajamaa wameweka kwenye ofisi zao tu. Nakuambia ukweli maana ni kweli. Kama kweli wanafufua, twende hospitalini; twende kwenye nyumba zenye misiba kama utamwona!  Anakuambia yuko kwenye maombi anamsihi BWANA. Haleluya!
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Ikishindikana atamwambia sekretari wake hapatikani sasa hivi! Unajua ilitakiwa watu sasa waone kama wanajua wana imani, kama watu wanafufua; watu waliofiwa wagome kuzika wapeleke makanisani wasitoke hapo! Mimi nakuambia watapasua ukuta!! BWANA YESU asifiwe; Haleluya! Sitaki udanganyike tena BWANA.. Yamkini uliongozwa sala ya toba na watu hao; nakuambia jina lako litashikiliwa. Kuna maeneo unatafuta upenyo unashindwa; lakini iko mahali ahadi ulikiri. Maana kinywa cha mtume kama ni cha MUNGU amemtuma kina connection na shetani. Kama ni cha shetani amemtuma, kina connection na shetani. BWANA YESU asifiwe. Zamani kina Barthalomayo walipata mateso sana pamoja na mke wake. Maana unajua hata mitume wengine walikuwa na wake!  Unajua hilo? Petro mwenyewe alikuwa na mke kabla hajaitwa na YESU. unajua? Mitume hawakuzuiliwa kuoa, wanaruhusiwa! Sasa wengine wanasema hakuna kuoa. Madhara yake ni uzinzi; macho macho tu. Mitume hawa wa siku hizi baadhi yao. Sasa wamemuiga Paulo. Paulo ni Paulo; aliamua yeye mwenyewe. Ni mpango wa MUNGU watu wakaoe na kuolewa. Au siyo?
WAUMINI:  Amen!
NABII HEBRON:  Haya, wengine wanasema mimi ni mwanamke siolewi. Mbona yeye ndiyo anahangaika huko? sasa wanatengenezeana spea zao kwa spea zao!!!Unataka nikuambie?
WAUMINI:  Ameen..
NABII HEBRON:  Unataka nipasue pasue?
WAUMINI:  Ameen…
NABII HEBRON:  Kwani uwongo?
WAUMINI:  Kweli.
NABII HEBRON:  Atakuwekea mikono… mtumishi mume wangu hajatulia nyumbani, lakini akienda anawekewa mikono na mtume gani yeye mwenyewe ana vitamaa. Mume halali nyumbani huyooo… unabaki kusema baba nanii baba nanii… Acheni kulaumiana nyie kwa nyie. Shida ni nini? Mitume wa uwongo. Haya, anaitwa ofisini; umetenda dhambi ngapi? Ndio tumetumwa hayo?
WAUMINI:  Hapana.
NABII HEBRON:  Wewe tubu dhambi zako hapo bwana MUNGU anakuona.
WAUMINI:  Ameen…
NABII HEBRON:  MMesikia?
WAUMINI:  Ameen.
NABII HEBRON:  Umezini mara ngapi? Mara nne. Tarehe ngapi na tarehe ngapi? Ndio mitume wametumwa hayo?
WAUMINI:  Hapana..
NABII HEBRON:  Sasa ni wakati wa kusamehewa, taja dhambi zako zote. Unataja kwa mwanadau au unataja kwa MUNGU wewe? Ni nani awezaye kusamehe dhambi?
WAUMINI:  MUNGU mwenyewe.
NABII HEBRON:  Anakuja muda fulani anakuambia basi njoo BWANA atakutia nguvu. ee ukikaa na mimi tukizini pamoja bwana atatenda jambo. haleluya.. Usidanganyike wewe! Wangapi wamepona? Akili imepona?
WAUMINI:  Ameeen…
NABII HEBRON:  Sasa naachia vitu sasa naachia baraka, naachia uponyaji. Ninakuachia furaha. Haleluya! Na milango kufunguka. Naona MUNGU akinionyesha mambo yenu mengi sana.
WAUMINI:  Amen..
NABII HEBRON:  Wengine wana shida kwenye meno, mpaka ulimi. Mtakuwa safi leo. Na wengine shida zimekwisha na wengine wanazidi kutengenezwa..
WAUMINI:  Ameen..
NABII HEBRON:  Maana MUNGU anasema kila unapozidi kusogea karibu na mimi ninazidi kukupatia, kukupatia. Unajua kila siku unapokula chakula bora unazidi kubadilika. Haleluya! Huwezi ukawa sawa na mtu anayekunywa uji wa chumvi bwana. Eeeh! Haleluya! Sura zinapendeza!! BWANA YESU asifiwe.
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Haya, wanakuja mitume wanakuambia wewe huji kanisani wewe, imeandikwa afanyaye kazi ya MUNGU kwa ulegevu atapigwa,. hiiii…. kumbe umefanya kwa uwongo. Asubuhi mpaka jioni – kanisani! Kafanye kazi wewe..
WAUMINI:  Amen…
NABII HEBRON:  Labda kama unapenda. Asiyefanya kazi na asile. Au siyo?
WAUMINI:  Amen..
NABII HEBRON:  Mimi mwenyewe kwa ubishi wangu aliponiambia MUNGU, nakuwa naenda Serengeti faster, Jumapili napiga kazi; wewe mtume nimekutuma ufanye jambo hili moja. Achana na hili!  Nilikuwa sijui. Nikaelewa, na sijaona shida yoyote. Haleluya!
WAUMINI:  Amen.
NABII HEBRON:  Waliopigana na mimi walifikiri wanpigana na mimi, kumbe wanapigana na MUNGU. Wewe pigana na MUNGU sasa; utatolewa meno yote! Apigane na watoto wangu atakutana na MUNGU. Ndio maana wengine wanashangaa gari inawakanyaga hakuna mchubuko huyo ndiye MUNGU. Ninasikia roho mtakatifu ananiambia, kuna baadhi ya nyumba wachawi wanaingia sasa utachukua mafuta ya annointing, paka kwenye mlango wako. Kila wiki unakuwa unapaka. ole wake aingie, utamkuta amedondoka.
WAUMINI:  Ameen…
NABII HEBRON:  Yaliyoombewa na Mtume Hebron, aliyetumwa na MUNGU. Ile nguvu iko pale. haleluya!
WAUMINI:  Ameen..
NABII HEBRON:  Haya wakaja wengine mitume wa uwongo, mafuta haya tunayauza kama bei ya dukani. Lakini unasikia anauza mara mia tano, laki… hao ndio mitume wa uwongo. BWANA YESU asifiwe. Wanauza sijui kanda za upako. Kanda inauzwa shilingi elfu tatu, unasikia elfu ishirini. usipeleke unaibiwa wewe. Mbona mnacheka? Ukaumia, ukakwazika wewe huna shida, ulipewa mambo ya uwongo. Sasa mimi ninakusihi hebu samehe bwana. YESU anakupenda, tuingie mbinguni, tuchote baraka, tusonge mbele. Naomba msimame; Haleluya!
WAUMINI:  Ameen…
NABII HEBRON:  Sema BWANA YESU, naomba unisamehe, dhambi zangu zote, nilizozifanya kwa kujua au kutokujua. Nilipofuata maneno ya mitume wa uwongo.  Nikapotezwa.  Nimejua ukweli.  Nimerejea BABA, na kukataa mafundisho ya mitume wa uwongo, nikateswa na misingi ya uwongo, na wachungaji wa uwongo, wainjilisti wa uwongo, waalimu wa uwongo, wenye huduma za uwongo, nimerejea kwako BABA. Nishike na wokovu. Nifufue, nipe uzima, kwa jina la YESU, na jina langu liandike mbinguni. Nimejengwa kwenye msingi wa mitume na manabii wa mbinguni. Haleluya….

WAUMINI:  Amen.