Close

MAELEZO YA YOUTUBE: KRISMASI YA KUZIMU INAVYOSHEREKEWA

[ad_1]

NABII HEBRON: Karibu tena ndugu  mtazamaji na msikilizaji katika kipindi cha mahojiano kati ya Isaya na Nabii Hebron wa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE ambapo siku ya leo ndugu mtazamaji na msikilizaji kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2014 akiwa atashirikiana na wanadamu wenzie katika Krismas. Sasa leo tutahojiana kuhusu Krismas alivyoisherehekea miaka yote huko kuzimu na ilivyokuwa inafanywa na ilisherehekewaje; BWANA YESU asifiwe.
NABII HEBRON: BABA ninawakomboa fahamu zao na akili zao, naondoa kila aina ya upingamizi katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Asante baba yangu, kstiks jinsi la YESU amen. Karibu sana. Karibu Isaya.
NABII HEBRON: Supai…
ISAYA: Eeephva..
NABII HEBRON: Eeephva..
NABII HEBRON: Haya, nataka uwaeleze watazamaji na wasikilizaji na wana wa MUNGU, ukikumbuka Krismas, maana mara ya mwisho mwaka 2013 ulikula kuzimu si Ndio?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Haya, leo nataka uwaeleze wanadamu, mimi nayajua lakini nataka nikuhoji kwa faida ya watazamaji na wasikilizaji. BWANA YESU asifiwe.
ISAYA: Amen.
NABII HEBRON: Karibu
ISAYA: BWANA YESU asifiwe, kwa jina naitwa Isaya; kutoka kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, nimeokoka na ninampenda YESU, napenda kumshukuru MUNGU kwanza kwa sababu mwaka huu nasherehekea Krismasi nikiwa duniani na wanadamu wenzangu,  ninachopenda kuwaambia ni kwamba shetani hafai, na hata siku moja msije mkakubali hata kujaribiwa na shetani imani zenu, maana shetani hana akili wala adabu. Leo nitaeleza kwa upande wa Krismasi kuzimu huwa inafanywaje,  na inakuwaje na ni nani anasimamia  Krismasi kule kuzimu, ambayo inakuwa inafanyika tarehe ngapi muda gani. Krismasi ya kule kuzimu inakuwa ni kila mwaka tarehe 23 Desemba mpaka tarehe 27, katika hizo tarehe, Krismasi zao kwanza huwa wanaonana na tammuz mwenyewe.
NABII HEBRON: Mwelezee tammuz
ISAYA: Tammuz ni ule mti, ambao watu walikuwa wanauita ni “Chrismas tree”, lakini yeye ndiye mtu ambaye anaonekana kabisa kuzimu, wanamwona kabisa tammuzndiye ameenda, na pia, nitapenda kuelezea siku ya leo kwa sababu hata kule kuzimu siku za krismasi sherehe zao huwa wanatoa sadaka, huwa wakunywa damu za watu; sadaka zao ni damu na nyama za watu, na pia wapo washirika ambao wanashiriki kule kuzimu kila Krismasi, ambayo pia wanasherehekea kuzaliwa kwa yesu wao kule kuzimu,
NABII HEBRON: Yesu wao?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Labda Isaya tungeeleza kitu kimoja kimoja maana vitu ni vingi sana. Hiyo ni dondoo tu ndugu msikiliza ya yale yatakayokuwepo, lakini yapo mengi. Haya bwana, tueleze ilikuwaje mara ya mwisho.
ISAYA: BWANA YESU asifiwe; mara ya mwisho kula Krismasi kule kuzimu, walifanya sherehe, nakumbuka ilikuwa ni sherehe kubwa sana, sidhani hata huku duniani kama watu huwa wanafanya sherehe kubwa kama ile, waliitana viongozi wote wa kuzimu na kila mtu ambaye anahusika na kuzimu alikuwepo hiyo siku, walifanya mavurugu masherehe yao, wakatoa sadaka, wakaua watu, kwa sababu huwa wanapenda sana kuuwa watu na kutoa sadaka kila inapofika mwezi wa kumi na moja na mwezi wa kumi na mbili, wao inakuwa ni mwezi wao wa kutoa sadaka. Walifanya sherehe, tammuz alienda; walialikana walisherehekea vizuri, lakini ndio hivyo mwishoni na mimi nikaja kutoka.
NABII HEBRON: Ilikuwa ni mji gani huo mlikuwa mnasherehekea Krismasi?
ISAYA: Freeman village
NABII HEBRON: Kwa joka kuu kabisa
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Uliniambia kwamba tammuz katika krismasi iliyopita ulikuwa umekaa naye pamoja mnaongea. Mlikuwa mnaongea nini wakati wa krismasi?
ISAYA: Tulikuwa tunapanga mipango ya kuingiza vitu vingine tena ili watu waendelee kumwabudu tammuz, na pia tulikuwa tunaongea maongezi ya kule kuzimu, kucheka, kufurahi,.. basi.
NABII HEBRON: Mlikuwa mnacheka mnafurahi?!
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Na ubabe ubabe
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Haya, jambo lingine ambalo ningependa kuuliza uwaeleze watazamaji na wasikilizaji, mtu anapokuwa anaweka huu mti wa krismasi nyumbani kwake, ina madhara gani?
ISAYA: Kwanza anakuwa anafukuza baraka za MUNGU haziwezi kuingia nyumbani kwake hata mara moja, na pia anakuwa anamkaribisha mungu tammuz na anakuwa anamkaribisha kwa hiyo hata siku za krismasi anakuwa na uhalali na yeye, na hata akitaka kwenda kwake anaenda na anafanya chochote anachokiamua. Na pia unakuwa unakabidhi kuzimu maisha yako, na unakuwa unaingia maagano na shetani mwenyewe kwamba umekubali kila kitu chake, na upo tayari kufanya kila kitu ambacho tammuz atakuamuru. Sio kwamba atakuamuru kimwili, atakuwa anakuamuru kwenye ulimwengu wa roho, nafsi yako anaiamuru ifanye chochote pasipo wewe mwenyewe kuelewa. Unaweza kuwa unalalamika MUNGU hanioni lakini ni kwa sababu ya huo mti ambao umeuweka nyumbani kwako.
NABII HEBRON: Na jambo lingine kule kuzimu  mkiwa mnaangalia huku duniani mkiona nyumba zimewekwa miti mlikuwa mnajisikiaje?
ISAYA: Raha.
NABII HEBRON: Raha?
ISAYA: Ndio.
NABII HEBRON: Kabisa? Mnaona kwamba mmeshinda?
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe; nitakuja jambo lingine sasa kuhusu “father christmas” na yeye umuelezee. Maanake kuna “christmas tree” na “father christmas” huko kuzimu. si ndio?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Haya, hebu sasa tuelezee na “father christmas”
ISAYA: Father christmas, yeye kwa jina anajulikana kama saint Nicholas kule kuzimu, lakini yeye kule kuzimu ameshakufa na anatumikishwa na mapepo na majini pamoja na watu wengine ambao wanahusika na kuzimu. Na pia father christmas unapokuwa unaweka ule mdoli wake nyumbani kwako unakuwa kwanza tayari wewe umeshamtukuza yeye yamekuwa baba wa maisha yako siku zote.
NABII HEBRON: Baba wa maisaha…..
ISAYA: Yako.
NABII HEBRON: Kwa hiyo watu wanaoweka midoli inafanya fanya hivi na madevu yake huyo ndio baba wa maisha yako kwenye ulimwengu wa roho. Unasikia ndugu msikilizaji na mtazamaji? Mambo yameharibika. Huyu niliyeko naye hapa alikuwa nafasi ya tatu katika ufalme wa shetani.Huyu ndie ngazi kubwa sana ya siri za shetani. BWANA YESU asifiwe; lakini sasa anatuelezea habari za huko kuzimu, ili wanadamu mzikatae. Zimeingizwa unaposhiriki tu, na wewe uko kuzimu. Sasa ndugu mtazamaji na msikilizaji, unapenda ule mdoli kuwa ndio baba yako? Jibu unalo. Karibu endelea.
ISAYA: Na pia unapokuwa na huyo mdoli nyumbani kwako, kwanza anakuwa na uhalali na wewe, kwa sababu ni baba yako, basi anaweza kukuamuru ufanye kitu chochote. Kwa hiyo pia anakuwa na uwezo wa kuchukua baraka zako, anabeba nyota yako, anabeba ufahamu wako, moyo wako anateka na nafsi, na anakuwa anakutumikisha kwenye ulimwengu wa roho na unakuwa umeshafunga naye ndoa pia.
NABII HEBRON: Na hawa wanaokuwa wameweka hii midoli makanisani, inakuwa inaashiria nini kwa kanisa?
Wanakuwa wanamkaribisha baba yao aje kuingia washiriki ibada.
NABII HEBRON: Wanamkaribisha nani?
ISAYA: Baba yao.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe. Ashukuriwe MUNGU wa Ibrahimu na Isaka; kama nilivyokwisha kuwaambia, ulimwengu ulikwisha tekwa na shetani. Na angalia Krismasi kwenye makanisa, hayo mamidoli ndio yamekaa. Je, ndiyo baba yenu hiyo? Ndiyo YESU huyo? BWANA YESU asifiwe. Ni wakati wa kufunguka. Ni wakati wa kuyakataa. Kama unataka kushiriki Krismasi nzuri, usiweke hiyo midoli wala huo mti. YESU sio mti, YESU sio mdoli. Hafanani na yeyote hapa duniani. BWANA YESU asifiwe. Haleluya..
NABII HEBRON: Jambo lingine ambalo ningependa kuulliza kazi aliyokuwa anaifanya father christmas kule kuzimu maana kule kuzimu ulikuwa una meli kubwa sana. Na hiyo meli ulikuwa unazunguka nayo dunia nzima. Hebu nataka ueleze, japo navijua; kwa faida ya wasikilizaji na watazamaji. Wewe ulikuwa na meli kubwa sana hapa duniani hakuna, na dreva wake alikuwa ni nani?
ISAYA: Father christmas.
NABII HEBRON: Ndio mdoli mnaoubeba huku. Alikuwa dreva wake huyu. BWANA YESU asifiwe. Haya, hebu tuelezee kwa ufupi kidogo kuhusu hiyo meli. Ulikuwa unafanya nini, lengo lake,  unazunguka, na umefanya nini?
ISAYA: Hiyo meli, nilikuwa nikitumia kufanya safari mbalimbali, kama labda nikihitaji kwenda kuangalia kitua au kwenda kutembelea manabii wa uwongo, kuangalia kazi zao; na pia hiyo meli ilikuwa na maana yake. Maana ya ile meli ni ule utatu mtakatifu wa kule kuzimu ambao ni joka kuu, lusifa na maxwel. Ukiwa umeitwa mtakatifu kule kuzimu, hata hawa ambao mnasikia wa madhehebu ya wenzetu, ukisikia mtakatifu ujue kwamba tayari yeye alishafanya kazi ya shetani kama inavyotakiwa kwa sababu amefanya kazi ya baba yake vizuri.
NABII HEBRON: Mmh,
ISAYA: Na anakuwa amefanya kile ambacho baba yake amemtuma.
NABII HEBRON: Mmh,
ISAYA: Kwa hiyo sasa, yule father christmas akawa ananiendesha mimi kwenye meli,
NABII HEBRON: Mh,
ISAYA: Na ile meli ilikuwa ina rangi saba.
NABII HEBRON: Rangi saba? Mmh..
ISAYA: Rangi ya kwanza ya ile meli ilikuwa ni blue, rangi ya pili ilikuwa ni njano, rangi ya tatu ni kijani, rangi ya nne ni zambarau, rangi ya tano ni nyeupe, rangi ya sita ni nyekundu, na rangi ya saba ni nyeusi.
NABII HEBRON: Unaweza kuelezea maana ya hizi rangi?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: MMh…
ISAYA: Rangi nyeusi maana yake ni giza ambalo wana wa MUNGU wanakuwa wanarushiwa kwenye ulimwengu wa roho, na ile rangi nyekundu ni agano ambalo shetani ameingia na wana wa MUNGU huku duniani pasipo wao wenyewe kuelewa, na manabii wa uwongo na watu wote wanaohusika kule kuzimu,
NABII HEBRON: Mmh…
ISAYA: Na maana ya ile rangi ya njano ndio vitu ambavyo wana wa MUNGU wanalishwa; yaani tuseme ni makufuru.
NABII HEBRON: Mmh…
ISAYA: Ambayo wana wa MUNGU wanakuwa wanalishwa usiku, na ile rangi ya blue ni rangi ya mto wa kule kuzimu ambao unakuwa umefanana na hiyo rangi ya blue,
NABII HEBRON: Ambao unaitwa timberland?
ISAYA: Ndiyo…
NABII HEBRON: Kwa hiyo hapa duniani watu wanasema navaa chata ya timberland, kiatu timberland, ndio mto wa nani? Kuzimu. Karibu endelea,
ISAYA: Kwa hiyo hiyo rangi ya blue inakuwa inatukuza mto wa kule kuzimu ambao watu wanakuwa wanabatiziwa bila wao wenyewe kujijua. Ukibatizwa ubatizo wa kikombe, au ubatizo wa kisima ujue wewe tayari umeshabatiwa katika ule mto bila wewe kujielewa, kwa sababu  unapobatizwa pale unakuwa na connection na kule kuzimu, na unapokuwa unabatizwa pale unaacha nyota, unaacha ufahamu, unaacha nafsi, unaacha kila kitu unatoka boksi wewe mwenyewe; Unatoka boksi!
NABII HEBRON: Mmh,
ISAYA: Na majini ndiyo yanakuwa yanakupelekesha na pia unakuwa umeshaingia maagano pasipo wewe mwenyewe kuelewa na shetani.
NABII HEBRON: Ahaaaa… Na kwa nini ulikuwa una-survey na hiyo meli unazunguka? Umeniambia ulikuwa unaenda kuangalia mipango mbalimbali; sasa ukiwa kama mshiriki namba tatu wa shetani kwa hiyo ukapewa na mamlaka ya kuzunguka?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Na dereva wako alikuwa huyu ambaye wanamwita father christmas?
ISAYA: Mmhh,
NABII HEBRON: Ambaye wanadamu ndiye wanamuweka ndani?
ISAYA: Mmmh.
NABII HEBRON: Kwa nini sasa walikupa mtu mkubwa hivyo kule kuzimu akuendeshe wewe?
ISAYA: Ni kwa sababu mimi nilikuwa mkubwa wake, nilikuwa juu yake kwa hiyo alikuwa akifanya chcochote nilichokuwa nakitaka mimi.
NABII HEBRON: Huyo ni wewe ulimwajiri, au ulipewa na joka kuu akuendeshe?
ISAYA: Ni mimi mwenyewe nilimwajiri.
NABII HEBRON: Sasas ulimwajiri mtu ambaye leo hii watu wanamueka ndani wanamuita father christmas?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: ALikuwa ni mfanyakazi wako tuseme?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Sasa wanadamu wanamuweka na madole, wanamuweka ananyoosha nyoosha na vidole na madevu. Najua anafanana hivyo hivyo. Sasa watoto wa MUNGU na wasikilizaji, shetani alikwishawateka wana wa MUNGU na hawajielewi, na anawatengenezea mashtaka kila wakati. Lakini amenituma kuleta habari njema, kueleza siri za shetani na kuzifichua na kuzibomoa.  Sasa utakapoacha tu, utakuwa umepona.
Tukija kwenye habari ya utatu mtakatifu, huyu ni mmoja wa utatu mtakatifu. Utatu mtakatifu namba moja ni joka kuu, namba mbili ni lusifa, namba tatu ni huyu ambaye ni maxwel. BWANA YESU asifiwe. Haleluya; Na hapa nitakuonyesha picha kidogo ya huyo max ambaye watu wanasema utatu mtakatifu. BWANA YESU asifiwe. Kwa ufupi ili ukaweze kujua. utaona ni mambo ya ajabu na ya kutisha. BWANA YESU asifiwe. Sasa hawa hapa wako watatu, wa kwanza ni joka kuu, ambaye picha yake sina hapa, wa pili ni lusifa, ambaye pia sina picha yake hapa, na wa tatu ni max ambaye ni mwanadamu saa hizi ni mwana wa MUNGU. Haya ni manyoka yalikuwa yanamzunguka. Huyu ni mtoto wa nyoka, huyu ni mtoto wa yezebeli, BWANA YESU asifiwe. Ndio wanamzunguka. Alikuwa ni mwanadamu mwenye ma vyeo vyeo yake. Alikuwa ni mwanadamu mwenye mikono minne, na huku minne, ina maana ni nane. BWANA YESU ASIFIWE. Alikuwa na jicho hili hapa ndilo alikuwa anaangalia nalo dunia nzima, alikuwa ana pembe, BWANA YESU asifiwe. Maxwel alikuwaje? Alikuwa ana pembe hapa lakini nimekwisha kuzikata. Hapa allikuwa na jicho la kuangalia dunia nzima. BWANA YESU asifiwe. Hayo mengine endelea kufuatilia katika vipindi, na karibu katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE utafundishwa. BWANA YESU asifiwe. Huyu ndiye mwanadamu mnayemwona sasa hapa, lakini ameshakuwa mtoto wa MUNGU ametulia. BWANA YESU asifiwe; Hebu tuendelee. Kama wanadamu wanamuweka huyu mdoli wanamuita father christmas alikuwa ni mfanyakazi wako, je, hamuoni wanadamu mnapotea kumwabudu mwanadamu? Hamuoni mnamuudhi MUNGU? Yako wapi makanisa ya kusema ukweli? Makanisa yenyewe ndio yamejaza midoli, hata sasa hivi wanaiandaa kwa ajili ya kuiweka. Ninawaambia, itoeni katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Kama mnampenda YESU itoeni, kama mnamchukia YESU iacheni. Huo ndio ukweli, na muitupe. Kama unampenda YESU achana na kuweka mti wa krsimasi.Kama unamchukia, weka. Zaidi nimekwishafundisha, fuatilia katika makala na katika wesite ya www.prophethebron.org ingia katika blog na vitabu, uyatafute haya masomo. nimeyaelezea vizuri sana. Amenituma YESU kuupindua ufalme wa shetani. Nilichofanya, nilimchomoa kwanza huyu. BWANA YESU asifiwe. Ilikuwa ni vita kubwa sana kumchomoa huyu, sasa shetani hana chake tena. Lakini usiogope. Karibu tena tuendelee msikilizaji. Enhe, hebu tuelezee, hiyo meli wakati mkiwa mnazunguka, mlikuwa mnavua samaki?
ISAYA: Hapana
NABII HEBRON: Ndani ya meli kulikuwa kuna nini na nini?
ISAYA: Kulikuwa kuna mapepo, kulikuwa kuna majini na kulikuwa na nguvu za kuwapa manabii wa uwongo.
NABII HEBRON: Nguvu za nini?
ISAYA: Nguvu za giza na nguvu za kufanya miujiza huku ulimwenguni ili kuchukua pesa za wana wa MUNGU, na mali zao, na pia kulikuwa na mapepo mbalimbali ambayo yangeweza kuwasaidia hao manabii wa uwongo.
NABII HEBRON: Ahaaa… Sasa baada ya wewe kuondoka, ile meli ilibaki inafanya nini?
ISAYA: Haikuwepo tena.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe. Unakumbuka katika watumishi, (lakini usitaje jina) ambaye alikuwa mwenyekiti wa manabii wa uwongo dunia nzima ambaye ulimpa hicho cheo? Na utataja mmoja ambaye alikuwa ni rais wa nchi, utuitaja hiyo nchi ambaye alikuwa msaidizi wake wanashirikiana?
ISAYA: Huyo rais aliyestaafu katika hiyo nchi alikuwa ni rais wa America, yeyendiye alikuwa amesimama pia kama kwenye uongozi wa namba mbili kwenye hicho chama, cha kuwasimamia manabii wa uwongo, na pia alikuwepo huyo ambaye ni mwenyekiti wa manabii wa uwongo, naye pia alikuwa anahusika kuwapa nguvu manabii wenzake, ili kufanya maajabu mengi, ndio maana mnasikia watumishi wengi wanakwenda Nigeria, wanakwenda wapi, lakini wanachokwenda kukifanya huko wanakwenda kuchukua nguvu za giza, kama vile ambavyo Mtume na Nabii Hebron amekwisha kueleza kwamba ziko nchi ambazo kuzimu inapatikana chini ya hizo nchi.
NABII HEBRON: Ahaaa…. BWANA YESU asifiwe, sasa baada ya yale majini kuuawa, na wewe kutoka, watapata wapi tena?
ISAYA: Hakuna
NABII HEBRON: Kwa nini hakuna?
ISAYA: Kwanza kabisa, yele aliyekuwa anawapa nguvu aameshatoka, na pia kile chombo ambacho kilikuwa kikitumika kimeshalipuliwa.
NABII HEBRON: Nani kalipua?
ISAYA: Ni Mtume na Nabii Hebron
NABII HEBRON: Mambo yalikwisha kuharibika watoto wa MUNGU, kanisa ikawa ni mazingaombwe, ni kutafuta pesa, na bado tu inaendelea, makelele tu yanapigwa kwenye ma tv, kwenye maredio. Ingekuwa kweli ni MUNGU, ninawaeleza kuzingekuwa kuna shida katika dunia hii. Wengine wamejiita mungu wa majeshi, mnatakiwa muelewe wana wa MUNGU. Hivi toka lini mwanadamu akajiita MUNGU wa majeshi? MUNGU wa majeshi ni huyu mmoja. Lakini wengine walikuwa wanafikiri wanazo nguvu za shetani, hizo nguvu za shetani walipewa na joka kuu, ila nimekwisha ziondoa. Sasa huyu ni mwanadamu kama wewe. Anajifunza sasa kula kama watu, anajifunza sasa kukaa na wanadamu, anajifunza sasa kucheza na watoto, vitu vingi alikuwa havielewe, maana alikuw aanaelewa vitu vya huko chini. BWANA YESU asifiwe. Lakini MUNGU anamtengeneza. Haleluya; Hebu elezea kuhusu miziki ya injili ambayo inaimbwa na wanadamu ambao hawajaokoka. Maana sasa hivi unakuta yaani mtu hajaokoka kabisa, lakini anaimba nyimbo za injili, watu wanakuwa wanasikiliza, lakini anakuwa ni mlevi, ni mzinzi, zinakuwa zina maana gani? maana wewe ulikuwa unatoa hicho kitengo. Amen?
ISAYA: Amen.
NABII HEBRON: Sawa ero? BWANA YESU asifiwe,
ISAYA: Amen. Hawa wanaoimba hizi nyimbo, kwanza wanakuwa wanamwimbia baba yao ambaye ndiye joka kuu, na wanakuwa wanatukuza umoja wa freemason, na wanakuwa wananitukuza mimi ambaye ndiye niliyekuwa nafasi ya tatu kwenye ufalme wa shetani,
NABII HEBRON: Ngazi ya tatu?
ISAYA: Ndiyo.
ISAYA: Na pia unaposikiliza hizo nyimbo zao, kwanza wanakunajisi kiroho na kimwili, na pia unakuwa unachukuliwa vitu vyako pale pale pasipo wewe mwenyewe kujielewa unapokuwa unasikiliza hizo nyimbo zao tu. Ndio maana unakuta hata wengine wanaimba wanakatika, wengine wanaimba wanafanya vurugu,
NABII HEBRON: Wanakatika?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Kukatika kupo kwa aina nyingi, mikono, kiuno au miguu?
ISAYA: Kiuno.
NABII HEBRON: Wanakatikaje? unaweza kuonyesha kwa ishara ya mikono? BWANA YESU asifiwe.Utakuta mtu anakatika kiuno hivi (akionyesha kwa mikono), ile ni kama matusi. BWANA YESU asifiwe, hivi wewe utafanya mbele ya baba yako mzazi umkatikie hivi? Lakini kwa shetani ndio hivyo. Sasa watu wanaona waimbaji duniani wanakatika viuno kama vile sangoma, au sangoma dance wanasema ni za YESU, aaaaa, zina mambo mengine. Hebu elezea madhara yake.
ISAYA: Na pia unapokuwa unaendelea kusikiliza hizo nyimbo zao, wanakuwa wanakuvuta wanakuingiza kwenye kitabu cha uzima wa shetani, na wanakuwa wanakuingiza kwenye mafaili ya kule kuzimu ambayo kwa sasa hayapo tena, na pia wanakuwa wanakuteka wewe mwenyewe ufahamu wako, moyo wako na nafsi yako na kumkabidhi baba yao na wanakuwa na uhalali kwa sababu tayari wewe ulishawafuata tayari. Na pia waoimba zile nyimbo wanakuwa hawaimbi wanadamu, yanakuwa yanaimba mapepo ndani yao ambayo ni mapepo muziki, ndio wanakuwa wanaimba miziki yao, wanaitoa kule kuzimu, huku duniani nyie mnakuwa mmepigwa upofu, mnakuwa mnaona mtu ana kipaji, lakini ndani yake ni mapepo ambayo yanakuwa yakimtukuza mungu wao kwa furaha.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe, wana wa MUNGU na wasikilizaji, madhara ya kusikiliza nyimbo za mtu ambaye hajaokoka anayeimba nyimbo za Injili,  anakunajisi wewe anakuunganisha na kuzimu. Na katika dunia hii, waimbaji wengi hawajaokoka, na hata wale wachache waliookoka, wengi wao ni wachawi, ni freemason, ndio maana ukiimbiwa ujumbe wa MUNGU hausikii chochote inakuwa ni matakataka. BWANA YESU asifiwe. Ndio maana hata leo hii utasikia nyimbo za injili zinachezewa disco. Mnajua, ziko nyimbo za kiingereza zinachezewa disco, zimefanywa kama blues lakini si blues, BWANA YESU asifiwe. Wanamtaja MUNGU, lakini yakupasa uelewe shetani naye pia ni aina ya MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Lakini msiogope, unakwenda kufunguka.  Amen.
ISAYA: BWANA YESU asifiwe, zipo hata product makanisani ambazo hata tulikwisha kuelezewa na Mtume na Nabii Hebron, na hizo product zipo chache zake ambazo tumeshaelezea kwa upande wa vitenge, kwa upande wa mavazi, kwa hiyo zile product unapozivaa zinakuunganisha wewe na shetani na pia na umoja wa kule kuzimu ambao ndio joka kuu, lusifa na maxwel, na unakuwa na ukaribu nao vile vile, na pia nitaelezea wachawi, mapepo na majini wana ushirika gani na wanakuwa wanafanya kazi gani, na kazi zao zinafanyika saa ngapi na kila lini, na muda gani na wanakuwa wanapata kitu gani.
NABII HEBRON: Enhe, hebu  tudili na hiyo kwanza, maana ma,bo ni mengi sana. Hata tukirekodi masaa mia sita haviishi. Twende hatua kwa hatua.
ISAYA: Wachawi na mapepo na majini wana ushirika wao ambao unaitwa MPW, na wao wanakuwa wanafanya vikao vyao lakini wao hawapatani na shetani. Na kisa cha kutopatana na shetani ambaye ni lusifa ni kwamba yupo mmoja ambaye alitumwa hapa ulimwenguni aje kuchukua nyota za watu, lakini akaja huku akashindwa akaanza kuloga, kwa hiyo akawa amepindua amri za shetani akaamua kumuua kabisa.
NABII HEBRON: Kwa hiyo historia ya kuanza kuloga ni kwamba shetani mjumbe wake mmoja alimuasi.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Alimtuma kuiba nyota za watu.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Apeleke kuzimu, yeye akaanzisha kuloga wakakosana na shetani.
ISAYA: Ndiyo
NABII HEBRON: Kwa hiyo na wachawi wameasiana na shetani.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Sasa kama wameasiana kuna uhusiano gani, wanasaidiwa bado na shetani? Au ni nini kinaendelea?
ISAYA: Wachawi hawasaidiwi na shetani, ila nguvu ambazo majini na mapepo wanazo wanakuwa wanawakabidhi wachawi, mapepo na majini wanaunda umoja wao na wana nguvu ndio maana wanakuwa wanarukaruka usiku, ndio maana wanafanya vitu vya ajabu ajabu, lakini hutakiwi kuogopa mwana wa MUNGU, kwa sababu kwa sasa ule uchawi haufanyi tena kazi katika nchi ya Tanzania, na hata hakuna nguvu yoyote kutoka kuzimu inayoweza kusimama juu ya mwana wa MUNGU yeyote.
NABII HEBRON: Haya, tunakuja, kwenye swali lingine, umesema kwamba, chanzo cha uchawi ni mjumbe aliyetumwa huku duniani, akaibe nyota.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Yeye akaamua kuloga, hakurudi. Sasa alikuwa anaitwa nani? Unaweza kumkumbuka?
ISAYA: Ndiyo, alikuwa anaitwa Matiku.
NABII HEBRON: Anaitwa Matiku?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Mjumbe wa shetani anaitwa matiku.
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Ndiye alitumwa huku duniani kuiba nyota akabadilika akaanza kuloga.
ISAYA: Mmmh.
NABII HEBRON: Sasa huyu Matiku yupo bado hai au ameshakufa?
ISAYA: Ameshakufa tayari.
NABII HEBRON: Na huko kuzimu alikuwepo alipokufa?
ISAYA: Ndiyo. Ndio mzimu wake ulikuwa unasaidia wachawi wengine.
NABII HEBRON: Kwa hiyo ndio kazi anayofanya huko?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Haya sasa Isaya, nataka unieleze maana ya zile rangi saba na kadi za krismasi na vitu vyenu vyote mnavyoweka, na wanadamu wanaponunua kadi za krismasi bado wanakuwa wameshiriki tena. Hamkuchoka, mkaendelea kuwabana.
ISAYA: Bwana yesu asifiwe, nitaelezea kuhusu hizo rangi saba zinazokaa kwenye kadi za krismsi, au kadi za bethidei (bithday), na kwenye kadi za vitu vingine vingine, hizo rangi kwanza tayari zinakuwa zinatukuza zile rangi ambazo tayari nilikuwa nimeshawaeleza
NABII HEBRON: Rangi saba hizo?
ISAYA: Ndiyo, na pia hiyo kadi unapoitumia ina maana wewe tayari umeshashiriki katika utatu wa kule kuzimu, na unapompelekea mwingine ina maana unamsajili kwenye chama cha kule kuzimu bila yeye mwenyewe kujijua.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe. Ndugu mtazamaji na msikilizaji, kadi ile  yenye rangi rangi, unapompelekea mtu au kuletewa ina maana mnasajiliana wenyewe kwa wenyewewe kwenye vile vyama pasipo kujua. BWANA YESU asifiwe. Kwa hiyo kadi ya Krismasi inatakiwa iweje?
ISAYA: Kwa kweli hakuna kitu kinaitwa kadi ya krismasi, kwa sababu hata hicho ni shetani alianzisha.
NABII HEBRON: Hahahahaaaa… Dunia imepinduliwa. Hakuna kadi ya nini?
ISAYA: Krismasi.
NABII HEBRON: Ila zipo salamu za krismasi na baraka za krismasi. BWANA YESU asifiwe. Hebu elezea tena kuhusu kadi ya krismasi. Shetani hakuchoka tena. BWANA YESU asifiwe. Kinachotakiwa wakati wa krismasi, ni unampa mwenzako zawadi kamili. Au sio?
Kama vile YESU alivyozaliwa, watu walimletea zawadi. Watu wapeane zawadi. Lakini shetani akaanzisha nini? Kadi. Kadi ina zawadi? Ina hizo rangi saba, au mbili au tatu. BWANA YESU asifiwe. Na wewe unaletewa! Unakuwa umeshiriki vilevile. Makanisani zimejaa, Kwa watu zimejaa, hata mimi nilikuwa sijui, mpaka nilipopelekwa huko na BWANA YESU nikaonyeshwa? Krismasi inatakiwa watu wanapeana zawadi, wanakula, wanashiriki, wanafurahi. Sasa utasikia nitakutumia kadi ya krismasi. Kwenye internet ndio zimejaa, BWANA YESU asifiwe. Ni heri umtumie mwenzako kwenye meseji heri ya krismasi. Inatosha. Amen, MUNGU akubariki. Sasa hebu elezea bwana Max wa zamani, sasa wewe ni Isaya wa Hebron kuhusu hizi kadi.
ISAYA: Na pia hizo kadi zinakuwa na ushirika na mzimu wa mtu anayeitwa maxwel kule kuzimu ambaye tayari baba yetu wa kiroho ameshatuonyesha, kwa hiyo unapoituma hiyo kadi kwa mtu yeyote, ina maana kwamba tayari wewe umeshamtumia max kadi yako, kwa hiyo inaonyesha kwamba unampenda sana. Unapomtumia kule labda umeandika MUNGU akubariki, na yeye anasema safi. Kumbe kazi ya tammuz inafanya kazi vizuri, unakuwa unamkaribisha sasa tayari.
NABII HEBRON: Hebu ngoja ndugu watazamaji na wasikilizaji, napenda kuwaonyesha huyu sasa, ukishamtumia mtu yeyote kadi ya krismasi, huyu ndio maxwel, ana mikono nane, ana jicho kubwa hapa, ana mapembe na kuna linyoka linazunguka pembeni yake. Na ndivyo ilivyoandikwa lakini hapa tumechora rafu rafu BWANA YESU asifiwe. Ana manyonyo kama mwanadamu, lakini nyonyo lake moja ni kubwa sana.  BWANA YESU asifiwe. Ni vitu vinatisha sana. BWANA YESU asifiwe. Haleluya. Sasa unapomuandikia mtu kadi ya krismasi, huyu na yeye umemuandikia, anafurahi, umejiconnect. Je, unapenda kujiconnect na jitu kama hili, hawa ndio wameanzisha kadi ya krismasi. YESU hajaanzisha kadi ya krismasi. MUNGU alichokianzisha, mtoto wake alipozaliwa nyota iling’aa na watu wakampelekea zawadi na watu wanatakiwa wapelekeane zawadi.BWANA YESU asifiwe, lakini zawadi sasa ikaongezwa na nini? na kadi ya krismasi. No kadi ya krismasi katika jina la YESU. Amen.? Karibu endelea.
ISAYA: BWANA YESU asifiwe, na pia katika kadi hizo hizo unakuwa unatii utatu mtakatifu wa kule kuzimu pia, na unakuwa unanyweshwa damu, unanyweshwa kila aina ya makufuru kwenye ulimwengu waroho bila wewe mwenyewe kujijua, na kazi ya makufuri ni kukuvuta uli uingie kwa shetani bila wewe mwenyewe kuelewa. Na kazi ya yale makufuru ambayo unapewa, ni ili uweze kuvutwa vizuri kwenye serikali ya shetani, ili aweze kuharibu vizuri maisha yako, abebe nafsi, abebe na maisha yako, zipelekwe kwa baba yao ambaye ni joka kuu pamoja na shetani na juo mzimu ambao umebaki kule ambao ni max. Na pia unaweza kukuta ile kadi ya krismasi ina alama crown imekaa, ile taji, ndio hiyo ambayo imeshaonyeshwa hapo na Mtume na Nabii Hebron, ambayo max ameiweka kichwani kwake.
NABII HEBRON: Hii hapa. Haya mapembe ambayo mnayaona hapa ndugu watazamaji na wasikilizaji, crown ndio hizo pembe, kwa hiyo na wewe unakuwa umejivisha limwili lake. Enhe.
ISAYA: Na pia unakuwa tayari umesahaunganishwa ule ufalme wake ambao yeye mwenyewe anao kule kuzimu, na hiyo ndio serikali yake kule kuzimu kama ilivyochorwa, na yeye ameonyeshwa  amekalia kitu cha duara, bna hicho kitu cha duara ni kwamba amekalia dunia ya kule kuzimu yaani ulimwengu wa kuzimu, upo chini yake yeye yupo juu yake, na hivyo vidude viwili vimekaa chini yake ni kishikizo cha dunia ya kule kuzimu, na hao nyoka ndio nyoika ambao alikuwa akilala nao na kutembea nao kila muda. Kwa hiyo unapokuwa unamtumia mwenzako kadi ambayo ina mojawapo kati ya vitu hivyo hapo, ni kwamba unakuwa umemconnect mwenzako na maxwel na wewe mwenyewe umejiconnect na maxwel pasipo kujijiua, na unapojiconnect naye maxwel anajiconnect na familia yako yote mkaingia kwake mpaka na ukoo mzima, akajiunganisha na mizimu ya kwenu, akajiunganisha na watu wote ambao wameshakufa, ndio wanaanza kuchafua maisha yako bila kuelewa.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe, zaidi ingia katika blog ya prophethebron.blogspot.com, YESU aliyonituma ni kufichua uovu. Angempata nani? angemshika nani? watoto wa MUNGU mnampenda sana YESU, lakini kila mahali wameshikwa. Ni maamuzi yako, heri ya krismasi tu inatosha. Heri ya Krismasi kwa mdomo, hiyo hela anayotaka kukunulia kadi akupe zawadi basi. YESU hakuletewa kadi. Nikuulize, kadi ina chochote, si karatasi? Kwenye ulimwengu wa roho unakuwa umeunganishwa huko. BWANA YESU asifiwe. Na kadi ya pasaka vivyo hivyo. Hebu elezea kuhusu kadi ya pasaka. Happy Eater…!!
ISAYA: Hiyo kadi ya pasaka unapokuwa umemtumia mwenzako au unapokuwa umeitumia wewe mwenyewe, unakuwa umejiconnect na pepo linaitwa lukman, anakupeleka kwenda kuhiji, anakuuwa kulekule, unaporudi unakuwa umerudi boksi.
 NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe. Labda jambo lingine nikuulize kuhusu hizi kadi watu wanatumiana, darling, my wife, congratulations, na hizi zina maana gani?
ISAYA: Unapomtumia mtu yeyote kadi za namna hii unakuwa tayari umeshamtumia mtoto wa yezebeli kule kuzimu, na pia unakuwa umemtumia maxwel, na pia unakuwa umemtumia pepo ambalo linaitwa abubakari, maimuna na sharifu, ndio wanakuwa na uhalali na wewe, kwa hiyo unapowatumia wanaona kumbe unatupenda, wanakuwa na uhalali na kukufuatilia, na ukituma tu hiyo barua, wanahakikisha usiku lazima wakufuatilie wakuzinishe wao wote na umoja wao.
NABII HEBRON: BWANA YESU asifiwe, Haleluya. Sasas ninapenda kukukuliza, wewe hizi kadi ulikuwa unazifaidi vipi ukiwa kule? Maana hata mimi nilishatuma hizi kadi kwa watu wengi sana, kwa hiyo nikituma ulikuwa unaipokea?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Hebu waelezee tena watu kuhusu hizi kadi, maana wengi wanatumiana hizi kadi, my love, my lover, my honey, my dady, my mum, my best friend, zina maana gani? Lakini kwanza kumbuka sio kumwambia mwenzako my best friend au my honey, my love, my dad, my mum. Sio mbaya kwa kinywa. Lakini ile kadi iliyotengenezwa, wafaidikaji ni hawa.
ISAYA: BWANA YESU asifiwe, Hizo kadi kama nilivyokwisha kuwaeleza, kwamba unakuwa unamtumia mtoto wa yezebeli, maimuna, makata, sharifu, abubakari wa kule kuzimu, wanaona wanapendwa na wengi, na katika wewe mtu mmoja kutuma hiyo kadi kumtumia mtu mwingine, wao wanaweza wakaharibu familia yako nzima au ukoo wako mzima kwa sababu wanakuwa wanajua wote wanatupenda. Kwa sababu chimbuko la ukoo ni bibi na babu, kwa hiyo bibi na babu wanapokuwa wanachimbuliwa, ile mizimu yao inakufuatilia wewe na maisha yako na wanakuwa wanakuzinisha kila usiku. Kila mmoja wa majini anakuwa anakuzinisha kwa sababu anakuwa ana uhalali na wameshakupenda na wanajua tayari huyu anatupenda. Kwa hiyo kila wakikufuata wanajua nafsi yako haitalalamika kwa kuwa unawapenda, na pia ile kadi unapoituma kule kuzimu wanachokuwa wanakifaidi wanaona ulimwengu wao unapendwa na watu wengi, na pia wanakuwa wanaona watu wamemkubali shetani kuwa mwokozi wa maisha yao, na wao wanakuwa wanajipongeza kana kwamba kama mtu mmoja akituma kwa siku moja, wanafanya sherehe, na shetani anajua kwamba tunapendwa, anawaongezea vyeo kwa sababu anajua kazi yao wamefanya vizuri na imeenda sawasawa kama alivyokuwa anataka.
NABII HEBRON: Ndugu watazamaji, ni wangapi mmetuma? Ni wangapi mnazo kumbukumbu? Ashukuriwe YESU. Alikosa mtumishi wa kumtuma miaka yote wala msimlaumu. Ndio maana watu wakazidi kuangamia. Na yeye kwa uchungu wake na hasira, akiwa na BABA yake (MUNGU) akaamua atumie njia nyingine alikomboe kanisa lake. Utukufu wa kanisa la mwisho ni mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza. Na ndio huu sasa alionituma unatenda kazi. Yale yasiyojulikana yanafichuliwa, na utakapoelewa utapona. Yamkini hutendi dhambi, unayakimbia lakini umekamatwa. BWANA YESU asifiwe. Na zaidi, karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE utaupata ukweli. Na jambo lingine ambalo napenda kukuelezea, shtani akawa bize “(busy)” kuhusu kadi; ukiingia kwenye internet, kadi ni nyingi sana. Eee namba tatu ya ufalme wa shetani wakati huo, maana ulitoka tarehe 02.06.2014. Hizi kadi kwenye internet mnazifaidi kivipi na mbona mmeweka nyingi sana?
ISAYA: Kwanza tunatakiwa tuzisambaze ili watu mzione, muendelee kzitumia ili muendelee kuwatukuza zaidi na ili wao wapate vyeo bila nyie wenyewe kujijua, na pia hata manabii wa uwongo wanatumia zile kadi kuvuta nyota za watu ili watu waende kwenye makanisa yaoili mmkaibiwe huko vitu  vyenu pamoja na nafsi zenu.
NABII HEBRON: Kivipi wanaibaibaje kupitia hizi kadi?
ISAYA: Kwa sababu kwanza wanakuwa wameweka pepo la tamaa na pepo la kivutio katika zile kadi.
NABII HEBRON: Pepo kivutio, pepo tamaa….
ISAYA: Ndiyo. Kwa hiyo unavyoangalia zile kadi mapepo yanavuta macho yako unaona hizi ni nzuri.
NABII HEBRON: Mmh..
ISAYA: Unaposema hii ni nzuri, ujue kabisa wewe umeshavutwa na upo katika ufalme wa shetani. kwa hiyo shtani mwenyewe ndio anakuwa anakumiliki bila wewe mwenyewe kujijua kwenye ulimwengu wa roho.
NABII HEBRON: Sasa unaelezeaje kuhusu makanisani maana ndio unakuta zimejazwa kwenye miti tena, na waumini, au kwenye nyumba za waumini kadi zimejaa mpaka chini. Hii ina maana gani?
ISAYA: Kwanza unapokuta nyumba ya mtumishi ina hizi kadi, ina maana kwamba kwanza yeye anatukuza ule ufalme uliopo kule kuzimu, sio watumishi wote, ni wachache ambao unakuta wanatukuza huo ufalme wa shetani ambao unakuta wanamshangilia mungu wao, kwanza wamefanya kazi vizuri, na wamekaribia kuumalizia mwaka bila matatizo, na wanajua kabisa krismai ikiisha wanaenda kupata vyeo kule kuzimu.
NABII HEBRON: Isaya, unaweza kuelezea hizi zawadi za krismasi, maana nyingine unakukuta zina viboksi, vi-ball na taa zinawakawaka. Hizi taa zinawakawaka ndio zile rangi saba, kwa hiyo kila mahali unakuta tu zinafanya hivi… Ukiingia kwenye madisco, kweye miti unazikuta, zina maana yake; si mpango wa MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Lakini hebu eleza isaya maana wewe ulikuwa navyo huko bwana mimi sikusaidii kazi. Japo mimi nilishaagaliaga huko nikaviona kila kitu, na YESU akanionyesha jinsi ulimwengu ulivyopinduliwa.
ISAYA: Kwanza zile taa zinavyokuwa zinabadilika zinakuwa ndivyo shetani anapindua maisha yako, kwa hiyo maisha yako yanakuwa yanacheza cheza, unaenda mbele unarudi nyuma, na vile vidude vimekaa kama vibomu (viduara) ndio dunia ya kuzimu ambayo wewe unakuwa umetekwa umekaa ndani yake, ndani ya kile kibomu.
NABII HEBRON: Unapokuwa navyo tu nyumbani kwako?!
ISAYA: Ndiyo. Na kile kidude ambacho kinakuwa kimekaa juu kwa ajili ya kuchomekea kamba, ndio bomu ambalo linakuwa limetoka kule kuzimu linakuja kukutungua wewe ambaye umekaa kwenye dunia ya shetani, kwa hiyo hata shetani akitaka kuwaua watoto wake, akkishachoka akiona kazi imeenda vibaya, kwa hiyo shetani akiona kazi yake imeenda vibaya anakuwa na hasira kiasi kwamba anaweza hata akaua watu wote wanaohusika na kuzimu.
NABII HEBRON: Hana upendo yeye?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Watoto wa MUNGU mnazidi kuelewa. Ni wangapi wana hizo taa? Maisha yanakuja, yanarudi.. Hiyo siyo nuru. Jua likumulike. BWANA YESU asifiwe, pia katika hizi taa unakuta za rangi rangi, labda brown, nyekundu, watu wanasema “night light”, wakati wa kulala wanawasha taa labda ya rangi ya zambarau, labda ya kijani, zote hizo ni mbaya. labda hebu elezea. Lakini wana wa MUNGU hawajui. Na hata katika mambo haya ya kadi, watumishi wengi hawajui kwa sababu kanisa limetekwa na shetani. Wangejulia wapi? Hawapendi lakini watoto wa kiroho ndio wanawaletea. Mimi sitaki katika jina la YESU. BWANA YESU asifiwe. Hata nikiletewa mimi napiga kiberiti tu.. Nilishazichoma, miezi mitatu iliyopita. nilishazichoma. Maana nilikuwa nazo nyingi sana, lakini hata walioniletea hawakuniletea kwa nia mbaya lakini walikuwa hawaelewi.. Na mimi nilikuwa nawatumia watu. BWANA YESU asifiwe.
NABII HEBRON: Ni wakati umefika wa kusema ukweli, anayetaka kupona apone. BWANA YESU asifiwe. Hata makanisa hayataiwi kupambwa na yale mamiti, mataa, makadi, yote yamekwisha kuelezwa hapa. BWANA YESU asifiwe. Haleluya. Labda Isaya endelea kidogo kuelezea vingine.
ISAYA: BWANA YESU asifiwe, nitaelezea kuhusu zile nyota ambazo zinawekwa kwenye ile miti ya  krismas tree, ile nyota ndiyo nyota yakowe inakuwa imekamatwa na tammuz ndio anakuwa ameishika mwenyewe, lakini bila kuelewa kwenye ulimwengu wa roho nafsi yako ndio unaona ni nyota yake ni ile pale. Tammuz ndio anakuwa anakufanyia nyota yako hii hapa, kwani utanifanya nini. Lakini wewe mwenyewe unaona ni kama kipambo bila kuelewa wewe mwenyewe kuwa nyota yako imeshikiliwa na tammuz. Mpaka uje upate mtu wa kuirudisha nyota yako, na zaidi labda ufike Moshono katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE ndio nyota yako inaweza ikarudishwa.
NABII HEBRON: Kwa hiyo, watu wengi mnakuwa mmeibiwa nyota, na maisha yenu. Wengine si wachawi wamewaloga, wengine si mizimu, ni kwa sababu umeweka lile pambo lenye nyota, na crown – krismasi. Sasa toka watu wamezaliwa, toka watu wakiwa wadogo, wana mambo hayo. BWANA YESU asifiwe. Na hebu elezea kuhusu mwezi.
ISAYA: Ule mwezi ndio kuwa maisha yako yanatandikwa kila baada ya miezi ambayo wewe mwenyewe umeingia maagano na kuzimu bila kuelewa mimi kila mwezi fulani, kila siku fulani maisha yangu nimeyafanya hivi lakini kwenye ulimwengu wa roho bila wewe mwenyewe kujielewa. Kwa hiyo kila ule mwezi ina maana maisha yako yanakuwa yanamulikwa, mwezi ule ukiondoka maisha yako yanakuwa tena giza bila wewe mwenyewe kujijua. Kwa hiyo ule mwezi unakuwa na muunganiko na malango ya kuzimu, na pia unakuwa unakata maisha yako, kwa hiyo shetani anakuwa amekaa huku, huku amekaa joka kuu na maxwel yupo katikati, na pembeni umezungukwa na majeshi ya kuzimu kwa hiyo hakuna pa kutokea wewe mwenyewe.
NABII HEBRON: Sasa nikuulize, wewe uliwakata watu wangapi kipindi hicho?
ISAYA: Wengi sana.
NABII HEBRON: Unaweza kujua hesabu yake?
ISAYA: Au kwa hesabu tu ya rafu rafu?
ISAYA: Kama milioni mia nane (800,000,000).
NABII HEBRON: Umeua?
ISAYA: Ndiyo.
NABII HEBRON: Ambao ni binadamu.
ISAYA: Ndio.
NABII HEBRON: Na shetani akaingia ndani yako kukutumikisha, lakini leo umetoka.
ISAYA: Ndio.
NABII HEBRON: Sasa ni wakati wa wewe kuwaeleza wana wa MUNGU wapone, maana wengi hawatendi dhambi, ila hivyo vitu vimewashikilia. Na mbinguni hawaendi kwa sababu ya vitu vya shetani pasipo kujua. Haya, unawaelezaje sasa watu wanaoandikiana kadi za uchumba, za harusi, unawaambia nini? Maana hapo zamani nilichokuwa nakijua mimi, watu walikuwa wanaadikiana barua. Barua ni salama. BWANA YESU asifiwe, ooh sikuoni, ooh nakupenda sana, na wanaweka vitu vingi  na nyie wenyewe mnajua. Lakini shetani akaingia kati katika mahusiano ya uchumba, akaleta kadi ili ashiriki uchumba wako wewe. Unapotoa kadi. Unakuta mabalaa balaa, mikosi mikosi. Shida ni nini? Ukiangalia wazazi wetu zamani walikuwa wanatumiana barua wamedumu na wako katika ndoa imara mpaka leo. BWANA YESU asifiwe, lakini hawa wa siku hizi wamekuja na kadi I love you so much; I love you wapi? Ni pepo linakuambia linakupenda so much. BWANA YESU asifiwe. Kuna wengine wanakuambia me & you; unajua me & you? Hebu elezea maana ya me & you kuzimu ni nini? Mkaileta duniani.
ISAYA: Maana ya me & you, kwanza kabisa wewe unayetumia ndio maana ya me, ambayo ni mimi. You inakuwa ni ulimwengu mzima wa kule kuzimu, sasa anaweza kuwa mmojawapo, jini, pepo, mchawi, nabii wa uwongo, shetani, joka kuu, maxwel, au watoto wao ndio unaweza ukawa umewaambia you.

NABII HEBRON: Sio mwanadamu mwenzako. BWANA YESU asifiwe, lakini msiogope, iko habari njema. Ninawatakia Krismasi njema. Lakini sasa, sio Krismasi ya ma-father christmas, miti hiyo, na makadi. Inatakiwa Krismasi uwe mtakatifu. Uokoke, umtukuze MUNGU. Umwabudu na kumsujudu yeye. Kama ni mambo ya kutoa kadi, usimpe mtu kadi, mpe zawadi. BWANA YESU asifiwe. YESU alipozaliwa hakupelekewa kadi, alipelekewa zawadi. Sasa kadi nikuulize ndugu mtazamaji na msikilizaji, ina chochote? Si inakaa tu hapo unaweka hapo. BWANA YESU asifiwe. Mpe mtu zawadi. Unapotoa kadi, unashirikisha na kule kuzimu krismasi ya kwao ambayo ni ya mpinga kristo. BWANA YESU asifiwe. Huyu hapa alikuwa anakaa nao, anatufichulia siri zote leo, mpate kuzielewa. BWANA YESU asifiwe, Haleluya… Una jambo lingine la kuwaeleza kuhusu krismasi? Maana Krismasi hii sasa unaenda kula na wanadamu. BWANA YESU asifiwe.  Na wewe mwenyewe usingependa kula na makadi, hataki kurudi huko! Asingependa kushiriki na ma-miti, asingependa kushiriki na ma-midoli, BWANA YESU asifiwe. Hata wafanya biashara wote ambao wanauza hizo kadi, ni kwamba wanatumikishwa kuendeleza kazi za shetani, pasipo wao kujua. Haleluya; Zaidi shetani akaona YESU karibu anarudi, akabuni mtandao wa internet kusambaza faster. BWANA YESU asifiwe. Hata wauzaji wa kadi siku hizi hawapati, ni internet. Unakuta mtu mmoja anaweza akatuma kadi hata mia tano (500) si bure? Lakini uelewe, ni madhara tupu, na ninabomoa katika ulimwengu wa roho katika jina la YESU. Nawafarakanisha na hizo rangi zote saba katika jina la YESU. Wanadamu wote. Ninaomba MUNGU Neno lako lisonge mbele. Na watoto wako wabadilike, wakujue wewe. Na ufalme wa wachawi ninaubomoa, na manabii wa uwongo ninawaharibu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti, ninasimamisha ufalme wako. MUNGU awabariki. Heri ya Krismasi. Tutaonana muda mwingine na wakati mwingine tena. Zaidi, karibu katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, ewe mtu wa nchi yoyote, taifa lolote, njoo ukutane na YESU. Huduma aliyonipa ni ya mataifa yote, ina maana ni mataifa yote, kwa watu wote, niwaonyeshe njia kama MUSA alivyotumiwa kuwapeleka wana wa Israel Kaanani. BWANA YESU asifiwe. Mambo yamebadilika, MUNGU awabariki, Amen.

[ad_2]