MAELEZO YA YOUTUBE: MTUME NA NABII HEBRON AMKAMATA MTOTO WA KIKE ANAYEIBA KWA UCHAWI BILA KUVUNJA MLANGO

MAELEZO YA YOUTUBE: MTUME NA NABII HEBRON AMKAMATA MTOTO WA KIKE ANAYEIBA KWA UCHAWI BILA KUVUNJA MLANGO

[ad_1]

Nabii Hebron: Unanichezea?
Nabii Hebron: Unanichezea?
Nabii Hebron: Hilo jiwe mkononi ni ya nini?
Annastazia: Nimeokota
Nabii Hebron: Umeokota wapi?
Nabii Hebron: Njoo hapa
Nabii Hebron: Utanieleza leo kila kitu
Nabii Hebron: Leta hapa
Nabii Hebron: Aisee unataka kupona?
Nabii Hebron: Niambie ukweli
Nabii Hebron: Au nikuache uchomwe na shetani?
Annastazia: Hapana
Nabii Hebron: Eeee?
Nabii Hebron: Niambie ukweli, maana nakujua.
Nabii Hebron: Si unanijua mimi?
Nabii Hebron: Jana si nimekuchapa?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Nilikuchapaje usiku?
Nabii Hebron: Usiogope, sisi tunakupenda. Sawasawa? hata huyo unayekaa kwake hatakufukuza, usiogope. Sisi tunakupenda. Sisi tunakupenda
Nabii Hebron: Si nilikuchapa jana usiku?
Nabii Hebron: Nilikuchapa saa ngapi?
Annastazia: Saa nane usiku
Nabii Hebron: Ulikuwa unafanyaje saa nane usiku?
Annastazia: Nilikuwa nimekaa mlangoni
Nabii Hebron: Kwa nani?
Annastazia: Kwa mama
Nabii Hebron: Ulikuwa unafanyaje mlangoni?
Annastazia: Sijui ni vitu gani vilikuwa mlangoni
Nabii Hebron: Hujasema ukweli, bado. Yale madini uliingia kwenye nyumba ya nani ukageuka tu mlango wa nani mlango ukafunguka ukayatoa?
Nabii Hebron: Eeeee?
Annastazia:  Sijui.
Nabii Hebron: Yaani tumemkamata na madini. Yale madini yako wapi?
Nabii Hebron: Aliyekuja na huyu mtoto yuko wapi? Yaani huyu mtoto akipita kwenye mlango akigeuka hivi, mlango unafunguka anakomba madini yote. Akigeuka tu hivi, anachukua na hela. lakini kwa watoto wangu “NO”. Hawa mimi nataka wapone bwana.
 Nabii Hebron: Mama, huyu amebatizwa?
Mama: Ndio amebatizwa.
Nabii Hebron: Huyu mtoto mmempata wapi?
Nabii Hebron: Sasa sema ukweli ili huyu mtoto hapa iwe ndio mwisho
Nabii Hebron: SItaki huo uchawi
Waumini: Ameeeeen
Nabii Hebron: Ndio maana watu wanafanya kazi benki, wanakuta wana shoti. Unafunga duka, unakuta shoti.
Nabii Hebron: Majamaa ndio hawa.
Nabii Hebron: Eeeeh….
Nabii Hebron: Aisee, bibi alikuambiaje rafiki yangu? Unajua YESU alinituma kwa watu kama hawa.
Nabii Hebron: Lakini mbona mnaogopa?
Nabii Hebron: Hilo jiwe lina maana gani?
Annastazia: Nimeliokuta mlangoni hata sijui maana yake.
Nabii Hebron: Hujui maana yake hili jie?
Nabii Hebron: Mmmmmh.
Nabii Hebron: Haya, litupe hapo chini haraka.
Nabii Hebron: Ile madini uliiba wapi?
Nabii Hebron: Na hajavunja hata solex; na watu wamelala, kawapita hapo hapo wanakoroma tirrrrrrrrrrrrrr… kabeba. Kavunja na geti. Lina solex na security guard (mlinzi) yuko hapo.
Nabii Hebron: Usiogope mama…. Hizi ndio dili bwana. Hizi ndio nini?
Waumini: Dili?
Nabii Hebron: YESU anataka atoke huko bwana.
Nabii Hebron: Amen
Nabii Hebron: (anauliza waumini)Hata wewe si ulikuwa huko bwana? Hata wewe si ulikuwa huko bwana?
Waumini: Ameeen
Nabii Hebron: Tumetolewa huko
Nabii Hebron: Tusijihehasabie haki. Si ndio?
Waumini: Ameen.
Nabii Hebron: Au sio jamani?
Nabii Hebron: Niambie, bibi anakufanyia bwana?
Annastazia: Ananiambia….
Nabii Hebron: Ongea basi. Usiogope basi.
Nabii Hebron: Hebu leta hata maji anywe bwana. Hapa kuna faraja. Sawa sawa?
Waumini: Amen.
Nabii Hebron: Mmesikia?
Nabii Hebron: Lakini nikikuonya usikie. Sawa sawa?
Nabii Hebron: Ameletwa kufanya kazi mjini lakini sio kufanya kazi mjini, ni kitega uchumi nakuambia anaiba pesa nyumba za watu malaki na hamjui zinakwenda wapi.
Nabii Hebron: Eeeh?! Kunywa maji rafiki yangu, kunywa usiogope.
Nabii Hebron: YESU alikaa na wachawi, sawa sawa? Na anawakumbatia, Mimi sijali hata kama amekwenda na kuzimu huyu.
Nabii Hebron: Eeeeh.. Lakini mpaka uwe na YESU, kumkumbatia tu na ile… shindwa, unashindiliwa!…
Nabii Hebron: Bibi alikufanyaje mpaka ukaingia kwenye hii mambo?
Nabii Hebron: Hapa tumeshamuombea jamani, hakuwa hivi.
Annastazia: Alinipa damu ya paka
Nabii Hebron: Alikupa damu ya paka?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Eeeh, Paka imechinjwa hapo akapewa.
Nabii Hebron: Ehe, damu ya paka vipi? ikoje ulivyokunywa? Sasa nieleze vizuri kila kitu halafu nikuombee. Si unataka kutoka?
Annastazia: Ndio
Nabii Hebron: Haya nieleze. Hamna mtu atakufuata akupeleke polisi bwana. sawa sawa? Hata polisi mimi nawapenda,  nawaombea. Na wao wanafurahi watu wanakuwa raia wema. Au siyo jamani?
Waumini: Ameeen.
Nabii Hebron: Hebu niambie sasa, bibi alikunywesha damu ya paka?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Nieleze kila kitu dakika mbili…
Annastazia: Alinikuta nimelala usiku,
Nabii Hebron: Enhe,
Annastazia: Mama alikuwa yuko chumbani kwake na baba.
Nabii Hebron: Enhe
Annastazia: Nilikuwa niko peke yangu. Siku hiyo wadogo zangu hawakuwepo.
Annastazia: Mimi nilikuwa sijui chochote. Akaingia, akaniita, nikagoma kutoka
Nabii Hebron: Usiogope, zungumza.
Annastazia: Nikasimama mlangoni nikajiuliza nani ananiita? Nikashindwa kuelewa. Nikarudi kwenda  kulala. Wakaja wapo wengi.
Nabii Hebron: Usiku?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Wamevaa nini?
Annastazia: Wamevaa nguo zao nyeusi na yeye amejifunga nguo nyeupe.
Nabii Hebron: Bibi huyo?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Ehe, wakakufanyaje? Zungumza kwa kifupi.
Annastazia: Nilikuwa nimelala siwaoni, lakini nikiwa kwenye ndoto nimelala nikamwona huyo hapo pembeni yangu. Wakaninywesha damu ya nyau lita mbili.
Nabii Hebron: Nyau?
Nabii Hebron: Ndio maana jamani na nyau zinakuwa kali kwa sababu ya wachawi.
Nabii Hebron: Aha. Sasa kwenye nyumba unawezaje kuingia ukachukua hela?
Annastazia: Mimi hata sijui, nikifika hapo mlangoni wenyewe wanaugusa mlango unafunguka wenyewe.
Ndipo nikiingia hawanionyeshi sehemu yoyote. Napita tu pale walipokuwa wanapoweka hela nachukua. Lakini hii juzi nimepotea na hata sijui nimepotea poteaje. Japo nilisema nimeshafuta nikasema sitarudia tena.
Annastazia: Nikaenda kubatizwa,
Nabii Hebron: Usijali
Annastazia: nikarudi.
Nabii Hebron: Anavyozungumza hivi ndiio anafuta maagano
Nabii Hebron: Na yale madini uliibaje?
Annastazia: Nilitoka nayo nyumbani.
Nabii Hebron: Enhe,
Annastazia: wakati nakuja mjini nikapitia kwa bibi. Nilivyopitia kwa bibi
Nabii Hebron: enhe
Annastazia: Akanipa hirizi, pete tatu na maji yaliyochanganywa na damu ya paka lita mbili, nikawa
nakunywa njiani.
Nabii Hebron: Enhe.
Annastazia: Nakunywa tu lakini sijielewi elewi
Nabii Hebron: Enhe
Annastazia: Nilipokuwa kwenye gari, gari ilitaka kupinduka.
Nabii Hebron: Enhe
Annastazia: Yule bibi akanisogelea, akaniambia sitaki ufe, wewe ndio ninayekutegemea, hautatoboa siri yangu.
Nabii Hebron: Hutatoboa siri?
Annastazia: Ndio.
Nabii Hebron: Siri gani hizo?
Annastazia: Alizokuwa anazifanya kwa watu.
Nabii Hebron: Kama nini?
Annastazia: Wanaenda wanaua watu
Nabii Hebron: Wewe ulishaua?
Annastazia: Hapana.
Nabii Hebron: Sasa kwenye nyumba ya watu unaingiaje mpaka unachukua hela bila kuvunja hata mlango?
Annastazia: Nilikuwa naingia kwa njia ya kwenye kona
Nabii Hebron: Hebu onyesha kwa mfano ulikuwa unaingiaje mfano, onyesha tu. Usiogope wewe rafiki yangu bwana. (Ananyanyua na kukuja mguu kwenye goti kuelekea nyuma)
Nabii Hebron: Ukishafanya hivyo halafu inakuwaje?
Annastazia: Ninapotea
Nabii Hebron: Mlango unafunguka?
Annastazia: Haufunguki. Unaingia kwenye njia ya ukutani
Nabii Hebron: Enhe…
Annastazia: Niliingia nyumbani kwa mama yangu kabisa alifunga mlango, akaenda kwenye msiba. Aliporudi akakuta laki tatu hazipo.
Nabii Hebron: Laki tatu hazipo!!!
Annastazia: Akaniuliza hela nikamwambia mama sijui wewe si ulifunga mlango wako ukaondoka na ufunguo?
Nabii Hebron: Hata anayekaa naye asimchukie, aliwekewa robot. Sawasawa?.
Nabii Hebron: Mmesikia jamani? Unatumikishwa…
Nabii Hebron: Lakini sasa umesema, hii kuongea ndio anafuta maagano.
Waumini: Ameen
Nabii Hebron: Damu ya paka! watu mnaua? Watu mnaibiwa mapesa. ndio maana unakuta kuna watu wanacheza bao tu, hawataki kufanya kazi. Kumbe wana hizi eee? (anakunja mguu)
Nabii Hebron: Eeee?!
Nabii Hebron: Si unaona kuna watu wanacheza bao tu hawataki kulima wala kufanya kazi?
Waumini: Ndio.
Nabii Hebron: Kazi yao ni …(anakunja mguu)
Nabii Hebron: Nyumba zenu haziingiliwi kwa damu ya YESU.

Waumini: Ameen.

[ad_2]