MAFUVU YA VICHWA VYA WATU NDIO SAHANI ZA CHAKULA KUZIMU

[ad_1]


Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron wa Kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, napenda kukufunulia kuhusu kuzimu jinsi palivyo pabaya na jinsi hawa wanadamu wanaoendaga kuzimu ni watumishi wanaotumia nguvu za giza, kule lazima wale chakula cha kuzimu ambacho hukaribishwa kama vile mgeni anavyokuja kwa  mtu, ila tofauti ya mgeni wa kibinadamu anaweza akakataa kula kitu chochote kwa mtu ila kuzimu ni lazima na ni amri.

YESU aliponifunulia siri za kuzimu  pamoja na kunituma kufunga  malango yote ya kuzimu na kumuangamiza kiongozi wa kuzimu ambaye  alikuwa akiwapa watumishi nguvu za kipepo  za kuhubiri na kutenda miujiza ya kipepo na kuharibu maisha  ya wanadamu niliona mambo ya ajabu na yakusisimua. Ila nitaelezea hili la sahani za chakula cha kuzimu, sahani zao za chakula ni mafuvu ya vichwa vya watu waliokufaga , na chakula cha kuzimu ni nyama tu na damu  za wanadamu hao ambao wanaokufa bila YESU kuwa ndani yao na wale wanaotolewa makafara na baadhi ya wanadamu na pia kuzimu walikuwa na mpishi mkuu ila huyo tayari nimemteketeza. Sasa hivi  NO FOOD huko kuzimu ni njaa tupu, hata mapepo hayana kitu.
 Nitaelezea kwa ufupi ili uepuke na uakae mbali na asikuzoee mtu aliye mshirikina, freemason,watoa kafara, wanaotafuta vyeo kutoka kwa waganga wa kienyeji, iwe ni cheo chochote hata  uraisi, uwaziri, ubunge,umeneja, hata vyeo vya makanisani na vingine vyote tu, hao wote lazima wamekula nyama za watu na wametumia lile fuvu la kichwa la mtu kulia nyama ya binadamu.

Na watu hawa nitakuelezea ili uweze kuwajua kimwili katika ulimwengu huu kwa jinsi nitakavyokuelezea kimatendo kwa mifano.

  1. Jina la mtu yeyote ambaye ni freemason member angalia katika (google) 100%. Amekula nyama ya mtu na sahani ni fuvu la mwanadamu. Na watu ambao wanavaaga mapete makubwa ya ajabu tofauti na za ndoa au pambo, pete inakuwa mzigo.

  1. Watumishi wote wanaotumia nguvu za giza, mfano kufufua misukule, au kutoa vitu ndani ya miili ya wanadamu mfano eti jiwe, chuma, nywele na mengineyo.(mazingaumbwe).

  1. Watu wanaofanyaga mitambiko ya mila, na kuchinja wanyama na kumwaga damu makaburini.
  2. Ndoto yeyote unayoota pia unakula nyama,au unalishwa nyama, hiyo ni nyama ya binadamu na wanaokulisha ni mapepo na unapolishwa unanyang’anywa utajiri wako au baraka zako, hapo nimekueleza  uelewe, na nyama hizo pia wakati unalishwa zinakuwa katika fuvu la kichwa, ila hufichwa usione fuvu hilo ili usielewe na uzubae waendelee kutumia baraka zako. Na ili usiseme uombewe tatizo hilo lisikuachie.

       Hivi umeshawahi kufikiria kwa nini mara Meli zinazama na Magari yanapata  
             Ajali ovyo? Na watu wanakufa ovyo na mara nyingi watu wanabakia    
             kuwalaumu polisi hawasimami barabarani au hata dereva anaitwa mzembe?
             Haipaswi kuwalaumu inatakiwa waombewe ili MUNGU awalinde wasipigwe
             upofu wakati  wakiendesha magari.
             Mapepo ndiyo humteka fahamu au kumchanganya, ila katika meli  ukiona meli
             zinazama  katika nchi yeyote ile hiyo ni kafara kubwa na  hufanywa na
             viongozi wakubwa tu, katika nchi hiyo. Na tena hufanya siri peke yake, maana
             unakuta  huo uraisi au ufalme hakupewa na Mwenyezi MUNGU,  aliyempa ni     
             shetani na shetani anamdai  vingi vikubwa, na hata watu wote wanaofariki   
             katika meli hupelekwa kuzimu na hata kibinadamu mkizika mwili kaburini    
             lazima waje wamchukue wampeleke.
             Na inapotokea utashangaa wanazilaumu mamlaka hizo za usafirishaji ila   
             mmoja aliyefanya jambo hilo hunyamaza kimya na kujikausha. Natumaini  
             umeelewa kuhusu meli kuzama, hii ni katika nchi zote. Mwenye akili na     
             aelewe.

  1. Watu wengi maarufu duniani 90% wamekula nyama za watu kuzimu na wametumia fuvu la kichwa cha mtu. Na hii ni kwa waimbaji wa miziki ya kidunia, waimbaji wa miziki ya injili wanaotumia uchawi, wachezaji mpira wa aina zote na michezo yote ambao utayaona majina yao katika orodha ya freemason, wafanyabiashara, baadhi ya viongozi wa nchi nyingi zaidi wamekula ila wanajijua ni siri yao , ila hayo yote YESU WA NAZARETI  alinionyesha, na anahuzunika sana jinsi mwanadamu amegeuka kuwa kama shetani na kumkubali shetani ndie awe baba yake.

Watu hawa  hapa duniani hupendelea kutoa misaada sana kwa wanadamu, hata ya ujenzi wa makanisa, misaada hii mnapopewa hampewi bure ipo roho ya shetani inachukua baraka zenu, na nafsi zenu mnatekwa pasipo kujua. Shetani hatoi kitu bure. Ni YESU WA NAZARETI TU!  Chunguza sasa hiyo  misaada ili uwe salama usipende kupokea misaada ambayo ndani yake haujui asili yake, omba MUNGU  ukisikia amani pokea,  ukisikia hauna amani wacha!.

NOTE:
Hata hapa duniani usipende kupewa ofa zao za vinywaji hata kushirikiana  katika sherehe yeyote hizo ofa haupewi bure wanajua utazilipa. Hivyo ni njia nyingine ya kukuibia baraka zako, hii hufanywa na mtu mchawi. Ila asiye mchawi  hana shida yeyote roho yake ni upendo.  Ila na wachawi wanao upendo wao, ni kukupa ofa halafu baraka wanakuibia nyota yako. Utashangaa rafiki yako kila siku yeye haishiwi na matumizi ni makubwa sana, wewe unaishiwa ovyo ovyo tu. !  Akili kichwani.



NABII HEBRON.



[ad_2]