Close

MAHOJIANO KATI YA NABII HEBRON NA ALIYEWA CO-ORDINATOR WA SHETANI, PAMOJA NA ALIYEKUKUWA KIONGOZI NGAZI YA TATU KWENYE UFALME WA SHETANI

[ad_1]

Hebron:          BWANA YESU asifiwe, Karibu tena ndugu mtazamaji katika kipindi hiki cha mahojiano kati ya Nabii Hebron, Leo ninaye ambaye alikuwa co ordinator wa shetani ambaye sasa ni mwana wa MUNGU hapo mwanzoni alikuwa akiitwa Wariambora kwa sasa hivi anaitwa Debora, naye tutahojiana kwa utukufu wa MUNGU, ili mzidi kufunguliwa maana alinituma YESU na yeye nikamtoa.
Hebron:          Bwana YESU asifiwe! Haleluya!
Hebron:          Karibu Debora
Debora:          Asante: Bwana YESU asifiwe!
Bwana YESU asifiwe! Jina langu naitwa Debora kwa sasa hapo mwanzo nilikuwa ninaitwa Wariambora, Ninampenda YESU, YESU ameniokoa, YESU ana nguvu, YESU anaweza,
Debora:          Bwana YESU asifiwe!
Hebron:          Haleluya! Sasa huyu ndiye Debora, ambaye leo tutakuwa na mahojiano naye, kuhusu maisha ya Kuzimu alikaa huko muda mrefu.
Hebron:          Nafikiri miaka mingapi!  Thelathini na mbili eeee
Debora:          Thelathini na mbili na miezi minane
Hebron:          Na miezi minane!!! atatueleza yeye alivyofanya maana yeye alizaliwa lakini hakumbuki alivyopelekwa lakini, ila mimi MUNGU alinifungulia, jinsi alivyopelekwa akawa anatumikishwa mpaka alipofika kanisani nikamfungua,
Hebron:          Bwana YESU asifiwe!
Hebron:          Karibu Debora
Debora:          Asante,        
Debora:          Bwana YESU asifiwe, ni kweli kama mtumishi wa MUNGU alivyosema, mimi kuanzia nivyozaliwa, nilipelekwa kuzimu nilitumikishwa na shetani maana sikupenda mimi mwenyewe kwenda kule, na kama nilivyosema kuwa niliweza kukaa miaka thelathini na mbili na  miezi minane.Nilikiwa namtumikia shetani,
Bwana YESU asifiwe, na nilikuwa na vyeo vingi kule kuzimu, cheo cha kwanza nilikuwa co ordinator
Hebron:          Co ordinator!!
Debora:          Co ordinator ndio, na cheo cha pili nilikuwa mwalimu
Hebron:          Mwalimu!!! Mwalimu wa kufundisha lugha mbalimbali!
Hebron:            Kwa hiyo kule kuzimu wana lugha mbalimbali mh!!
Debora:          Ndio
Hebron:          Unaweza kukumbuka ni lugha ngapi ambazo ulikuwa unafundisha na za nchi ngapi?
Hebron:          Unaweza kutaja baadhi
Debora:          Ninakumbuka chache
Hebron:          Ehee! hebu zitaje
Debora:          Moja ya kwanza ambayo ninaikumbuka ni lugha ya kuzimu yenyewe
Hebron:          Kuzimu wana lugha yao wenyewe???
Debora:          Ndio
Hebron:          Unaweza kuiongea mpaka sasa hivi?
Debora:          Ninaweza ndio
Hebron:          Hebu ongea kidogo, alafu unitafsirie umesema nini kwa lugha ya kuzimu maana watu wangependa kuelewa maana yake
Hebron:          Maana pia mnajua watoto wa MUNGU kuwa mbinguni wana lugha yao na kuzimu pia wana lugha yao.
Hebron:          Hebu unaweza kuongea kidogo!
Debora:          Ndio
Hebron:          Alafu utatutafsirie
Debora:           Ndio
Hebron:          MUNGU akutie nguvu.
Debora:          BWANA YESU asifiwe! Lugha mmoja wapo ambayo ilikuwa inatumika kule kuzimu,  ambayo hata watumishi wa kipepo na wale ambao wamepewa nguvu na shetani ambao wanapenda sana kuitumia hiyo lugha , hapa dunia inaonekana,  wanaponena inaonekana  kwama wananena kwa lugha lakini sio wote wanaonena kwa lugha.
Lugha nyingine wamepewa na baba yao ambaye ni shetani, ambazo baadhi ya lugha hizo zipo ambazo pia wanapenda kuzitumia hapa duniani na wanapozitumia zile lugha watu wanafikiria kuwa wananena kwa lugha ambayo zinatoka mbinguni lakini sio hivyo.
Hebron:          Mimi kama Nabii Hebron hiyo lugha ya kuzimu siijui lakini yuko ambaye alikuwa naye kule kuzimu ambaye sasa ni mtoto wa Kanisa la YESU ni BWANA na Mwokozi wa Mataifa yote kwa jina Isaya, anaitwa Isaya, pia walikuwa naye kule kuzimu na wanaongea kwa mawasiliano kabisa:
Hebron:          Mda si mrefu nitamkaribisha Isaya na yeye, watakuwa wakiongea maana huyu pia (Debora) alimfundisha Isaya
Hebron:          Bwana YESU asifiwe wataongea hiyo lugha ya kuzimu na watu wapate kusikiliza
Hebron:          Usiogope lakini, Amen
Debora:          Bwana YESU asifiwe, baadhi ya lugha hizo nitaongea na mwenzangu ambaye na yeye pia alikuwa kuzimu lakini kwa neema ya MUNGU, ameweza kutoka,
Debora:          Bwana YESU asifiwe, Baadhi ya lugha hizi ni:
Debora:          shaboroseke shindorobosai?
Isaya:              Akaramaiska mafias
Debora:          Shiraboboko sendaraibaksi
Isaya:              Shanta marka makass
Debora:          Shuto senndere book sosi
Isaya:              Rika meuasi
Debora:          whichu bokosi ndasi
Isaya:              Kos mandesrsmis
Debora:          Roko shinda mandotos
Debora:          Bwana YESu asifiwe!
Debora:         Baadhi ya lugha hizo ambazo tumeongea nitazitafsi kidogo! Mwenzangu atakuwa anaongea na mimi nitazitafsi kwa Kiswahili
Isaya:              Taridosi
Debora:          Ndivyo ilivyo
Isaya:              Kar tarasi mat saba
Debora:          Wamwabudu MUNGU wetu
Isaya:              Ritmalakruksiii
Debora:          Walale chini
Isaya:              Kar taraa mat saba
Debora:          Wamwabudu MUNGU wao peke yao
Isaya:              Radhu madfass
Debora:          Wamwabudu shetani
Isaya:              Sikur mafitarsi
Debora:          Waabudu miungu
Isaya:              Sarmakka
Debora:          Waabudu misalaba
Isaya:              Deor madabass
Debora:          Waabudu mungu jiwe
Isaya:              Samsakar makass
Debora:          Waabudu mungu ambaye yuko kuzimu ambaye ni joka kuu
Isaya:              Sarkdur mamkasma
Debora:          Wamtolee sadaka ambazo ni nyama za watu
Isaya:              Deur mata makasi
Debora:          Wamwabudu yeye peke yake
Isaya:              Saur mau mata mau
Debora:          Wamwabudu roho mtakatifu
Isaya:              Ti aumar mamtaks
Debora:           Wamtolee sadaka peke yake
Isaya:              Au mar makamata
Debora:          Tuwafunge fahamu zao
Isaya:              Ribo tol maka mamtiss
Debora:           Ili wasimwelewe MUNGU wa kweli
Isaya:              M kairu mamtasasi
Debora:          Tuchukue na utayari wao
Isaya:              Ribo for Mauro mamtass
Debora:          Tufunge na fahamu zao
Isaya:              Ribo toll makkaqa mamtiss
Debora:          Tufunge na vinywa vyao
Isaya:            Sikar matassa  
Debora:          Tufunge nguvu ya maombi
Isaya:              Sikor malatassa
Deabora:        Tutengeneze mabomu kwenye ulimwengu war oho
Isaya:              Rediko fo mamtassess
Debora:          Tuwavuvie roho ya kuwalewesha usingizi
Isaya:              Ro of amamtakasssasss
Debora:          Tuwavuvie roho ya kumwabudu mungu jiwe
Isaya:            Re outor malamtakasasa
Debora:          Tuwapatanishe fahamu zao na bahari ya hindi
Isaya:              Kreopatriao
Deabora:        Kuna kijana mmoja ambaye yuko Tanzania anakiherehere sana tunataka tupange mbinu za kwenda kumwangamiza
Isaya:              Tormakasi Hebron
Debora:          Anaitwa Hebron
Isaya:              Teur mamtassi mam deur YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE
Debora:          Tukaangamize na huduma yake
Isaya:              Reu koll ma san mau massi Moses Kulola
Debora:          Na baba yake alikuwa anaitwa Moses Kulola
Isaya:              Teuorr mamkassi mamdersea Serengeti
Debora:          Ma huyu kijana alikuwa anafanya kazi Serengeti

Isaya:              Te markasi te assize ker mau hebron
Debora:          MUNGU alimwita alivyokuwa huko katika kazi yake ambayo alikuwa anaifanya
Isaya:              Te rranamau de mass YESSU
Debora:          YESU akamtoa akamwambia ukanitumikie
Isaya:              De teur markassii oo kore mattasisi
Deabora:        Akasema ndio Baba nitaenda
Isaya:              Creopratio
Debora:          Lakini vita vuliinuka
Isaya:              Treo marapratatissi
Debora:          Wakataka kumuua
Isaya:              Reokal matasasa  
Debora:          Lakini neno la MUNGU
Isaya:              Reo malakasa
Debora:          Lilitimia
Isaya:              Reobotasisisii
Debora:           Haikuwezekana
Isaya:              Reo kall matasisi max
Debora:          Na alitumwa kuzimu kwenda kumtoa Max
Isaya:              Treo makasisi waria boraa
Debora:          Na pia kabla ya max alitumwa kwenda kumtoa Wariambora
Isaya:              Creombota rmaraksii  
Debora:          MUNGU alimpa mtume na Nabii Hebroni huduma ambayo ni ya dunia nzima
Isaya:              Keo mapatiss marpatasao
Debora:          Ili akaziokoe roho za wana wa MUNGU ambazo zimepotea ili aweze kuwaokoa
Isaya:              Creomaba datapass
Debora:          Alitumwa kuwaokoa wale ambao hawamju MUNGU na waliotekwa na shetani
Isaya:              Tika bakosi
Debora:          Ili wamrudie MUNGU, kwa kuwa sasa hivi wako wengi wanadanganya wana wa MUNGU
Isaya:               Dreo mamtababsaa
Debora:          Hawasemi kweli, bali wanasema uongo
Isaya:              Reol mamkassi
Deabora:        Na wanatumia biblia za uongo
Isaya:              Reol makasi dreomapal sapa
Debora:          Na wanawapa watu neno la uongo
Isaya:              Rol makatatisso mapatsi
Debora:          Lakini yeye amenituma kuharibu ufalme wa shetani
Isaya:              Reo mapasisisisiii
Debora:          Wakati wa YESU umefika
Isaya:              Reokul mapatamsisi
Debora:           Wa yeye kurudi
Isaya:              Reomampatass
Debora:           Kuchukua kanisa
Isaya:              Reo mapatarada
Debora:          Na watu wataujua ukweli
Isaya:              Krisu masasa
Debora:          Na wakati umefika
Isaya:              Reo maksasisa
Debora:         Ijapo wengi wanampinga Hebron
Isaya:            Reo makala masisi masa
Debora:          Lakini MUNGU akiamua ameamua
Isaya:              Reol mall keo ormaadotobo martaba ai :
Debora:          Na shetani amewateka watu wengi wakiwemo wanawake, wametekwa kwa kuambiwa watoe fedha, waweke fedha kwenye miguu na wakanyage, biblia na sivyo neno la MUNGU linavyosema
Isaya:             Reol matasi
Debora:          Amentumwa ili kuangamiza ufalme wa shetani
Isaya:              Dreol mataka
Debora:          Waje kwa MUNGU
Debora:          Bwana YESU asifiwe!
 Kwa hiyo utaona kuwa baadhi ya lugha wapo ambao wamejiita na wanasema wametumwa na MUNGU kwamba ni za uongo, lakini kama haujafunguliwa ufahamu na kumwelewa MUNGU hutaweza kuelewa na watu wengi sana wamedanganyika sana kupitia  hizi lugha na kupitia hizi lugha wengi wametekwa na shetani
Debora:          Bwana YESU asifiwe!
Wametekwa na shetani kivipi, unapoenda kwa mtumishi ambaye anatumia nguvu za giza na ambaye  amepewa hizi lugha na ambaye amefundishwa hizo lugha aje kuwadanganyia wana wa MUNGU unapoenda tu pale,  na kuwekewa mkono ama  unaposikiliza hizo lugha ni pepo ni nguvu ya roho mchafu, ambaye roho mchafu  tayari tunamshukuru MUNGU kwamba alishatolewa unaposikiliza hizi lugha na  zinakuvuvia na ile nguvu inakuingia, kwa hivyo na wewe tayari unakuwa umeshaingiwa na ile lugha ya kunena kwa lugha bila wewe mwenyewe kujua na hiyo lugha yenyewe sio ya mpango wa MUNGU bali ni mpango wa shetani kuharibu wana wa MUNGU ili waende kuzimu ambapo ni kwa shetani mwenyewe.
Bwana YESU asifiwe!
Kwa hiyo  ninawasihi na ninawashauri muwe makini na mahali mnapoenda, watu wananena , watu wanaongea, wengine wana tafsiri, lakini wengi wao sio lugha  ya Mbiguni,  sababu lugha ya Mbinguni inakuja automatic na inakuja mahali ambapo yupo mtumishi  wa kweli na ambaye amesimamia kweli, lakini wengi wamechukua huko kuzimu na aliyekuwa anafundisha hizo lugha  ni mimi ambaye nilikuwa ninafundisha. Nilikuwa nafundisha hizo lugha kwa aina tofautitofauti kwa kiwango ambacho mtumishi mwenyewe labda anataka akazitumie, hizo lugha ndio maana na unaweza kukuta huyu anaongea lugha hii na huyu hii, na mwingine lugha hii, lakini zote zinajumuisha kitu kimoja.
Kama vile kwa MUNGU, tunavyoombewa,  tunapokea nguvu za Roho Mtakatifu utasikia kila mmoja ananena kwa maneno yake mengine lakini kinamaanisha kitu kile kile.
Isaya:              Bwana YESU asifiwe! 
Debora:          Amen
Kwa jina naitwa Isaya ni mtoto wa madhabahu ya YESU ni  Bwana na Mwokozi wa Mataifa yote, ndimi ambaye nilikuwa kiongozi wa ngazi ya tatu kwenye ufalme wa shetani, ndimi  nilikuwa roho mchafu wa kuzimu,  ndiye ambaye nilikuwa kiongozi wa vikosi vya vita vya shetani,
Nilikuwa nikiongoza watu mbalimbali lakini siku ya leo pia nipo na ambaye alikuwa ni Mwalimu wangu kwa upande wa silaha, alikuwa akinifundisha, ndiye aliyenifundisha kutumia silaha zilikuwa silaha za aina nyingi ambazo alinifundisha kuzitumia na kama ni kwa upande wa vita, kwa kutumia silaha yeye ndiye aliyekuwa zaidi kiukweli mimi nilikuwa ni bado mdogo sana kwake kwa upande wa silaha za kupigania vita.
Na pia yeye neema ya MUNGU ilikuja kumwokoa akawahi kutoka kabla yangu, lakini pia MUNGU alikuwa na kusudi lake akaamua kumtoa yeye kwanza, yeye ambaye alikuwa akinifundisha mbinu za vita ili kwanza kasi iweze kupungua,  ili nisiweze kupigana kisawasawa.
 Pia namshukuru MUNGU kwa siku ya leo kwa maana tumeweza kueleza upande wa Lugha ambazo watu huwa wanaziongea; kwa kweli kabisa ziko lugha ambazo watu wanaziongea,  pasipo nyie wenyewe kuzielewa mnakuwa mnasema, MUNGU wewe ni mjinga , kwanza hujibu maombi yetu,  tunakudharau hatukitaki, ndio maana yunatoa machozi yetu, ndio unaona mtu anakuwa anaomba au naongea anatoa machozi mengi pasipo kupigwa au amefanyiwa kitu chochote au unaweza ukawaona hata waumini katika makanisa ambayo ni la mtumishi, labda mtumishi wa kipepo,  wanakuwa wanaongea kwa lugha ambayo labda wanajisifia na kujisifu kuwa wanaongea kwa lugha  pasipo wao kujielewa.  Mda mwingine wanakuwa wanatukana watumishi wao, mda mwingine wanakuwa wanasema maisha yetu na yawe mabovu, hatutaki maisha mazuri siku zote.
Namshukuru MUNGU pia kwa kuwa siku  leo yapo mengi ambayo pia tutayaeleza nikiwa na aliyekuwa mwalimu wangu zamani kama teacher, lakini siku ya leo wote tuko katika mikono ya MUNGU na mikononi mwa Mtume na Nabii Hebron, namshukuru sana MUNGU kwa ajili ya hilo.
Debora:          Bwana YESU asifiwe!
Debora:          Ah! Kama alivyosema mdogo wangu Isaya ni kweli lakini tunamshukuru MUNGU kwa kuwa kwa sasa tumetoka na tunamtukuza MUNGU
Bwana YESU asifiwe!
Ah nitapenda kuelezea kazi ambazo nilikuwa nikizifanya kule kuzimu,
Bwana YESU asifiwe!
Mimi nilikuwa kama mwalimu nilikuwa ninafundisha kama nilivyosema, lugha mbalimbali lakini katika ulimwengu ulimwengu waroho, nilikuwa nafundisha vyuo mbalimbali vikiwepo vya hapa duniani kabisa.
Bwana YESU asifiwe!
Kwenye ulimwengu waroho nilikuwa ninafundisha, nilishaingia vyuo vingi, vingine viko Dar vingine viko mikoani, vingine Arusha lakini pia vipo vingine nchi mbalimbali nilikuwa ninaenda kule inaweza kuwafundisha kwenye ulimwengu wa roho.
Bwana Yesu asifiwe!
Nilikuwa ninafundisha walimu ambao na wao pia wanafundisha wanafunzi, Lakini neema ya MUNGU imeweza kunitoa huko na lingine nilikuwa kama nilivyosema nilikuwa mwalimu wa lugha kule kuzimu mfano wa lugha hizi za kunena kwa lugha, nilikuwa nawafundisha wale ambao walikuja kuzimu na walikuwa  wanahitaji kufundishwa zile lugha nilikuwa nawafundisha ila sikupenda mimi bali nilitekwa na shetani.
Bwana YESU asifiwe!
Niliweza kuwafundisha nyingi sana, na nilikuwa na uwezo wa kuwafundisha lugha nyingi sana, na kupitia hizo lugha wana wa MUNGU wengi walitekwa kupitia hizo lugha.
Lakini namshukuru MUNGU kwa kuwa amenitoa kule na “Aliyekuwa anafundisha hizo lugha sasa ameokoka na anampenda YESU”  Na kingine nilichokuwa nafundisha nilikuwa mwalimu, mwalimu wa kwaya, unaweza ukaona kwaya mbalimbali zinaimba unasema kweli hizi kwaya zinaimba ama ukaona kwamba wanamuziki wa nyimbo za injili mfano,  akiwepo mmojammoja unaweza na ukaona wanaimba unashangaa labda wanaimba vizuri sana, au mtu anasauti nzuri , mimi ndio nilikuwa ninawafundisha, nawafundisha na kuwaelekeza sauti nikiwepo nashirikiana na roho mchafu ambaye na sasa ametoka ambaye sasa ni mwana wa MUNGU sasa ni Isaya
Lakini ninamshukuru MUNGU sana kwa kuwa hakuna tena, kule kuzimu mtu anayefundisha hizo lugha. Na pia nilikuwa ninafundisha kiswahili nilikuwa nina uwezo mkubwa sana wa kufundisha lugha ya kiswahili kwenye ulimwengu wa roho lakini kimwili mtu hawezi akafahamu.
Lakini pia  namshukuru MUNGU kwa kuwa hiyo roho ya shetani imeondoka na nimekuwa mtoto mzuri  wa YESU, nitaelezea vitu ambavyo pia nilikuwa ninavyo kule kuzimu,  kama nilivyosema kuwa mimi nilikuwa co ordinator. Cordinator ni mtu ambaye  nilikuwa na cheo  kikubwa  sana pia nilikuwa nikiheshimika sana nilikuwa na ofisi zangu lakini zimeshachomwa moto na mtu ambaye aliyetumwa kule kuzimu kwenda kunichomoa huko na pia nilikuwa nina nyumba na pia nilikuwa nina hospital, hospital zilikuwa hospital za kutibu mapepo na malaika wa shetani ambao walikuwa wamejeruhiwa ambapo malaika wa MUNGU walipokuwa wanakuja kupigana kule kuzimu ili kuharibu ufalme wa shetani,  walivyokuwa wakiumia walikuwa wale wanakuja kwenye hospital yangu naweza kuwatibu, na huo uwezo nilikuwa nimepewa na shetani na sio kwamba ni uwezo ambao nilikuwa nao mimi mwenyewe, Namshukuru MUNGU kwa kuwa kwa kuwa uwezo huo pia  MUNGU ameuondoa huo, uwezo wa shetani.
Bwana YESU asifiwe!
Na pia nilikuwa na ofisi nyingi lakini tu zimeshachomwa moto, pia nilikuwa nina wafanyakazi, madereva pia nilikuwa na ndege.Namshukuru MUNGU kwa kuwa ni MUNGU.
Bwana YESU asifiwe,
Licha ya kuwa na ndege pia nilikuwa na ninauwezo mkubwa sana wa kuweza kupaa, nilikuwa naweza kupaa sekunde moja nikaweza kuizinguka Tanzania, naweza nikazunguka pia nchi kadhaa na pia nilikuwa na nguvu, hiyo nguvu ilikuwa kwenye mkanda.
Bwana YESU asifiwe!
 Nilikuwa na nguvu kwenye mkanda na nilikuwa na nguvu kwenye saa, ambayo hiyo saa ndiyo ilikuwa inanielekeza na ule mkanda nilikuwa ninauvaa kama mwanajeshi unafungwa kama mwanajeshi anavyovaa( kuanzia begani na kuzungukia kiunoni) na nilikuwa na kofia lakini hiyo kofia ilikuwa ina upanga pia ile ilikuwa ni nguvu kubwa sana kwenye ulimwengu waroho.
Bwana YESU asifiwe!
Lakini namshukuru MUNGU kwa kuwa ameweza kuniokoa na ameweza kunibadilisha
Pia nilikuwa na nguvu ya kuweza kuua nimeangusha magari,
Bwana YESU asifiwe!
Lakini MUNGU ameniokoa na MUNGU amenisaidia na nilipokuwa nipo Co ordinator nilikuwa nahakikisha kwamba kazi zote za kuzimu zinaenda salama,kama ambavyo zinatakiwa na kama hazijaenda salama nilikuwa ninaenda kwa aliyekuwa namba tatu ambaye alikuwa roho mchafu, anieleze kwa nini kazi hazijaenda sawa na nikisha enda kwake, na yeye pia anaenda kwa wale ambao waliokuwa wanahusika na kile kitengo, na nilikuwa pia na nguvu nyingine ya kuzuia wana wa MUNGU wasiwezekuomba nilikuwa naweka giza nilikuwa ninachafua anga, nilikuwa nikitaka tu kuzuia maombi, mimi mwenyewe nilikuwa na uwezo wa kupaa na nilikuwa ninaweza kujitanda kwenye anga ili maombi ya wana wa MUNGU yasiweze kupenya na nikijitanda angani makanisani hawataweza kuomba, inakuwa ni vurugu inakuwa ni faraka, kwa mtu mmoja mmoja na pia hata kwa familiawanakuwa hawaelewani,  hata kama ni wanandoa walikuwa wanaomba au kikundi cha maombi wanakuwa hawawezi kuendelea sababu ya kile ambacho nimekiachilia kule, na pia nilikuwa na wafanyakazi kama nilivyosema, pia nilikuwa na mtumishi mmoja ambaye sitamtaja jina, yeye ndiye alikuwa kama mfanyakazi wangu ni mtumishi wa kike anajulikana yupo Arusha, lakini sitamtaja jina lake, maeneo ya Ngaramtoni. Yule pia alikuwa ni kama mfanyakazi wangu wa kunipokea mabegi na kuhakikisha kama nimekula vizuri na kufagia nyumba na kufanya vitu vingine ambavyo vinahitajika kufanywa kwenye  nyumba, na ninamshukuru MUNGU kwa sababu hayo yote nilikuwa nikiyafanya ni kwa sababu nilikuwa nimetekwa na shetani kama vile wakati mwingine mtu yeyote na yeye anaweza akatekwa, lakini namshukuru MUNGu kwa kuwa nimeweza kutoka.
Kule nilikuwa nina magari lakini  ninamshukuru MUNGU alivyoshuka mtumishi wa MUNGU kule aliteketeza na yale magari kule, niliyokuwa ninayatumia kule kuzimu pia nilikuwa  nina ndege,  pia namshukuru MUNGU kwa kuwa zile ndege na vitu vyote vya shetani niliviacha kule na nikatoka kama nilivyokuwa
Bwana YESU asifiwe
Nitaelezea kuanzia nilivyozaliwa na mpaka ilipokuwakuwaje nikapelekwa huko kuzimu mpaka nilivyotoka.
Bwana YESU asifiwe
Nakumbuka kwamba nilivyozaliwa,ijapokuwa  nilikuwa mdogo, lakini ukishatekwa na shetani hata kama ni mdogo unakuwa na ule uwezo wa kuelewa kwa sababu unakuwa sio wewe tena bali umebadilishwa ufahamu
Bwana YESU asifiwe!
Ninakumbuka nilivyozaliwa tu mimi nilikuchukuliwa nikiwa bado mdogo na mimi kivuli changu kikafanywa mfano wangu mimi, Bwana YESU asifiwe!  
Bwana YESU asifiwe!
 Kwa hivyo, nilivyozaliwa nikachukuliwa  na pepo ambaye huyo pepo alikuwa kama baba yangu, na alikuwa anaitwa Tikiko,  na nilipokuwa kule kuzimu nilijua kuwa ndiye baba yangu
Bwana YESU asifiwe!
Na nilipokuwa kule kuzimu kivuli changu kilikuwa kama vile ndio mimi kikawa na sura yangu Kamili na mama yangu aliendelea kunilea akifikiri kwamba analea mtoto,
Bwana YESU asifiwe,
Lakini kwa kweli sikuwa ni mimi kilikuwa ni kivuli tu kile na kile kivuli hakikuwa ni kivuli tu cha kawaida bali kiliambatanishwa na pepo
Bwana YESU asifiwe!
Na nilivyokuwa huku duniani kile kivuli kilikuwa kinateseka na magonjwa ya mbalimbali,
Bwana YESU asifiwe!
Magonjwa yasiotibika, ugonjwa wa moyo, ukitibiwa huu, unakuja huu, ukitibiwa huu unakuja huu
Bwana YESU asifiwe!
Na nilikaa kama nilivyosema nilikaa kule kuzimu, nilikaa miaka thelathini na mbili na miezi nane, kama nilivyosema hapo awali, wakati huo wote nilimtumikia shetani
Bwana YESU asifiwe!
 na nilimtumikia shetani bila kupenda na nilitekwa na shetani, na nikaweza kumtumikia shetani nikawa naishi kule kama vile mtu anavyoishi huku duniani lakini maisha ya kule kuzimu naya huku ni maisha ya hapa duniani, kwa sababu ni maisha ambayo kila  saa upo hatarini
Bwana YESU asifiwe!
 kwa sababu kila saa ni kupigana, Chakula kikuu kule ni nyama za watu na damu za watu ndio vitu ambavyo nilikuwa nakula, pamoja pia na wengine ambao ndio wako kule, niliweza kuishi na mapepo bila kujua maana unajua unapokuwa mdogo, hauelewi kwa hiyo niliishi nao , niliishi nao kule kama vile ambavyo sasa ninaishi na wanadamu huku duniani tofauti ya maisha ya kule ni maisha ambayo ya taabu, kwa sababu ni maisha ya ubabe kila saa kupigana
Bwana YESU asifiwe!
Na mda wote ambao nilikuwa nikiishi kule nilivyokuwa nasema kwamba huku duniani nilikuwa dhaifu , naonekana kama asiyefaa, nilikuwa sipendi sana kukaa na watu, na nilikuwa sipendi kuongea kila mara nilikuwa napenda kujitenga nikae peke yangu , peke yangu, lakini ni kwamba sikuwa bali mimi kile kilikuwa ni kuvuli na mimi mwenyewe sikuwepo.
Na nitaeleze jinsi ambavyo niliweza kutoka kule kuzimu ambapo nilikuwa na nilivyokuwa aah ilifika wakati ambapo MUNGU mwenyewe alipenda nitolewe kule
Bwana YESU asifiwe!
Kivuli hichi ambacho kilikuwa duniani kilikuwakihangaika hangaika, unajua shetani , unajua ili shetani aweze kupumbaza watu akikuteka ni lazima akuwekee kitu ambacho kitakufanya wewe uonekane kuwa ndio udhaifu wako kwa hiyo mimi kitu ambacho kilikuwa kimewekwa kenye kile kivuli ni magonjwa kwa hiyo wazazi walikuwa wanahangaika huku na kule kwa hiyo hata ilifika kipindi ambacho nikatoka kwa wazazi wangu nikaenda kukaa na ndugu mkoa Fulani lakini hali ilizidi kuwa mbaya kadri ambavyo miaka inaenda ndivyo ambavyo magonjwa yalikuwa yanaendelea ndani ya mwili wangu na mimi mwenyewe bila kujielewa na niliendelea pia kwenda kutibiwa maeneo mbalimbali nikiwa nasumbuliwa na ugonjwa wa moyo ndio ulinitesa sana lakini bila mafanikio yeyote
Bwana YESU asifiwe!
Lakini huku duniani nilionekana ni mimi, nilionekana  ni mgonjwa Na  niliweza pia kwa sababu nilisoma, nilisoma nilivyokuwa mdogo kwa sababu kile kivuli kilipelekwa shule nilisoma mpaka darasa la sita, darasa la saba kile kivuli kilisoma lakini kilisoma kidogo sana kwa sababu ilikuwa inafika wakati kile kivuli chenyewe kilikuwa  kinachukuliwa linabakia pepo moja kwa moja kuna wakati ilikuwa inafika  kile kivuli kinashushwa kuzimu, kinaunganishwa na mwili wangu kwa hiyo darasa la saba, nilisoma kidogo. Nilipoingia darasa la saba kidogo nilishikwa na ugonjwa , ukaonekana kama ni ugonjwa wa Malaria nikaanguka kwa hivyo nikaanguka nilivyoanguka pale kile kivuli kilichukuliwa moja kwa moja  napepo likawa ndilo limebakia pale kwa hiyo kivuli changu nikawa nacho kama kawaida
Bwana YESU asifiwe
Kuanzia hapo kile kivuli sasa kilipodondoka kikapelekwa kule kuzimu pale nyumbani likawa limebaki pepo
Bwana YESU asifiwe!
 na lile pepo  liliendelea kuishi na wazazi wangu bila kujua lakini kulikuwa na tofauti moja kati ya lile pepo na mama walikuwa hawaelewani kwa sababu niliingia maagano mengi, mimi mwenyewe niliingia maagano mengi,Kwanza niliingia maagano ya kuuwa na agano lingine lilikuwa agano la kutanda kwenye anga, nafsi yangu ilikuwa inaganyika sana kwa hiyo kuna wakati mwingine nafsi yangu ilikuwa inagawanyika inaenda inakaa kwenye anga, ili kuzuia maombi na hilo ni agano langu la kwanza, kabisa ambalo niliingia kwamba hakuna ambaye atamwelewa MUNGU na hata kuzuia watu wasiokoke na hata wakiokoka watu wasiweze kuelewa
Bwana YESU asifiwe!
Agano la pili lilikuwa ni agano la kupandishwa cheo,
Bwana YESU asifiwe
Ni agano la kupandishwa cheo cha coordinator pamoja na kuwa cheo cha ukoordinator kiendelee kupanda zaidi, na  pia agano la tatu ni agano lingine la kuwa malkia, lakini nilikuwa Malkia, lakini litakiwa niweze kuwa malkia mkubwa zaidi wa kuzimu nzima kama vile tuseme katika nchi ya Tanzania awepo Malkia mmoja tu au kama vile mfano mkuu wa Nchi mmoja tu anayesikika hivyo nilikuwa ndio niingie agano hilo la kuwa malkia mkuu ilifika wakati sasa niliambiwa nikamtoe mama yangu mzazi hapo ndipo ilipokuwa shida.
Bwana YESU asifiwe!
Ndio maana kuna mahali nilisema kuwa lile pepo baada ya kivuli kuondoka lilikuwa mara kwa mara halielewani na mama, sababu lile pepo lilikuwa limevaa sura yangu kwa hiyo lilitakiwa kumuua mama yangu ili niweze kupandishwa cheo, zaidi lakini pale haikuwezekana.
Bwana YESU asifiwe!
Na ndipo ilipotokea vita kule kuzimu,  kati yangu na baba yangu ambaye alikuwa ni Tikito, lakini pia alikuwepo na lusifa, roho mchafu na alikuwepo na joka kuu, lakini mimi nilikuwa, unajua  wale walikuwa, sana sana Joka kuu na Lusifa walikuwa kama mabosi wangu tulikuwa tunatembeleana, tulikuwa tunakaa tunapanga mipango,
Bwana YESU asifiwe!
na ninamshukuru MUNGU kwa kuwa haya yote MUNGU alinipitisha ili niweze kuja kusimama kuweza kumtumikia.
Ilipofika sasa wakati wa kumtoa mama yangu, (Kafara) nilikataa nikaanza kupewa kibano(adhabu)
Bwana YESU asifiwe!
Nilikuwa napewa adhabu, (kibano) ikawa mara nyingine nafungiwa kwenye sanduku nakunjwa kunjwa, unajua kule kwenye ufalme  wa shetani wanaweza kukufanya mkubwa sana na wanaweza kukufanya kama mlima na pia wanaweza kukufanya  mdogo kama karatasi hivyo mara nyingine nilikuwa nakunjwa nawekwa kwenye sanduku kwa sababu nilikataa kumtoa mama yangu.
 Unapokuwa Ukiwa umeenda kule kuzimu kuna maagano mengi sana unaweza kuingia unaweza ukawa umeua watu wengi sana, lakini itafika mahali utaambiwa kwamba umtoe mama yako au ndugu yako  au mdogo wako kwa hivyo wakati hayo sasa yalipokuwa yakiendelea ninatakiwa nimtoe mama yangu ndipo ulipofika wakati sasa alikuja ghafla mtumishi wa MUNGU Mtume na Nabii Hebron, akiwa na kikosi cha malaika nilikuwa sijawahi kuwaona Malaika lakini siku hiyo niliwaona walivyo, walikuja na vikosi vya farasi, walikuja na vikosi mbalimbali vya kupigana walikuwa pamoja na Malaika akiwepo na Bwana YESU na akiwepo na Mtume na Nabii Hebron, ndipo walikuja kunichukua  kule ilikuwa ni vita na ndipo ambapo mimi nilikuja kuchukuliwa, nilipokuja kuchukuliwa nikajikuta niko kanisani kwake, kwa sababu jinsi ambavyo nilikuwa nateseka na magonjwa, ni lile pepo sasa ambalo lilifanywa ndio mimi baada ya hospital  kushindikana.
Nilianza kupelekwa maeneo mbalimbali ya maombi nikapelekwa, lakini kwa kweli nilikuwa naenda tu kwa ajili ya kuwatii wazazi lakini mimi mwenyewe nilikuwa naelewa ni nini ambacho kilikuwa kinaendelea ila niliwewa agano la kutokusema na lile agano lilikuwa ni la damu kwa hiyo ukishatekwa Unapokuwa na ile roho ya shetani imeingia unaweza kufanya kitu chochote bila kujipenda.
Bwana YESU asifiwe!
Na baada ya kutoka kwa  wazazi , baadhi ya ndugu  ambao  pia nilikuwa naishi nao waliweza kunipeleka  kwenye maombi sehemu mbalimbali na katika kipindi hicho hicho lile pepo pia lilikuwa linafanya kazi katika shirika fulani na alikuwa alikuwepo baba mmoja ambaye alikuwa akinishuhudia habari za YESU,  Na nilikuwa namkubalia naenda, lakini  mimi mwenyewe nilikuwa najua ni nini kinaendelea ila sasa kusema ili niweze kufunguliwa nilikuwa siwezi kusema sasa  baada ya yule baba kuendelea kunishudia, ilikuwa ni vigumu na alinishuhudia maeneo mbalimbali nikaenda lakini aliponishuhudia kwa habari ya kwenda kwa Mtume na Nabii Hebron  Kanisani kwake ilikuwa vigumu.
 Alinishuhudia kama miezi nane, mwezi wa nane, lakini nikakubali nikamwambia nitaenda,  Lakini kwa kweli ilikuwa sio mimi bali ni lile pepo ndio lilikuwa anaongea nae na bada ya kufika pale lile pepo lilikutana za nguvu ya MUNGU, mahali pale, kwanza lile pepo lilipofika pale, mahali pale walikuwa na malaika wako pale, wengine walikuwa wamekaa kwenye viti kwenye anga, yeye mwenyewe (Mtume na Nabii Hebron) nilikuwa nikimwangalia nilikuwa namwogopa kwa sababu alikuwa anawaka, alikuwa na mng’ao ambao sio wa  mwanadamu kwenye ulimwengu wa roho.
Na nilipofika kwa mara ya kwanza sikujielewa kwa kweli, nilikamatwa maana hata pia lengo la kwenda pale ilikuwa niende nikapime nguvu aliyonayo, lakini mambo yalibadilika, nilikwenda mara ya kwanza, nikashindwa lengo lililonipeleka pale nikashindwa maana nilikutana na nguvu za MUNGU, hivyo nilienda mara ya pili.
 Sasa vita vikawa vinaendelea kule kuzimu ndio kwenye ulimwengu wa roho akashuka, Mtume na Nabii Hebron  pamoja na vikosi vile ambayo nilivitaja na mafarasi, wakawa wamebeba silaha mbalimbali ndipo ambapo vita vilianza kule kuzimu magari yangu, yakachomwa moto, lakini ofisi zangu zikachomwa moto, magari, ndege  wasaidizi wangu pia waliuawa  na wengine wakakatwa vichwa, mapepo yakaktwa vichwa, yakauwawa na ndipo ambapo mimi niliweza kutolewa na nilivyotolewa, nilijishangaa nilijikuta nimerudi duniani, bila mwenyewe kujielewa nini, kilitokewa lakini vita vilikuwa vinaendelea kule Malaika walikuja wakanichukua alafu kwenye ulimwengu wa  roho Mtume na Nabii  akaniambia njoo! Basi ndipo ilipofika wakati nakatolewa nikajikuta niko kanisani, nikajikuta niko na watu, ijapokuwa mimi kipindi hicho kabla sijatolewa nilikuwa siwezi kuonana na watu; hilo pia ndio agano ambalo nilipewa, hata mfano kama nilikuwa nimekuja duniani kufanya vitu vibaya, nilikuwa kabisa sionani na watu nilikuwa napita anga kwa anga, hata nikitoka chini napita anga kwa aga na nilikuwa sionani na mtu ana kwa ana.
 Kwa hiyo nilishangaa sana kutolewa kule kuzimu ilikuwa ni kitu cha ajabu sana kwa sababu kitu cha kwanza mimi nilipitolewa nilishangaa wanadamu kwa sababu nilizoea kukaa na mapepo, nilizoea kukaa na Joka kuu nilizoea kukaa na watu wa ajabu ajabu sana lakini ninamshukuru MUNGU kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni ya ajabu sana na sitakaa niisahau maishani mwangu kote kwa kuwa MUNGU ni MUNGU tu, Mtu anayesema MUNGU hayuko kwa kweli hajui anachokisema.
Kwa sababu kwanza nilishangaa hii dunia, nikashangaa sana, nikashangaa watu wanavyoongea, mimi nilikuwa nimekaa kimya naangalia lakini nawashangaa na nilipokuwa nimetoka hapo sasa napelekwa nyumbani, maana bado ufahamu ulikuwa bado haujarudi, nilikuwa nawashangaa watu, siongei lakini nilikuwa nawashangaa watu wanaongeaj ! nikaanza kupenda kukaa na watu nitaanza kuwa marafiki sasa na watu, ninapenda nikae nao kwa hiyo ninamshukuru MUNGU  aliyenitoa kule ilikuwa ni jambo la ajabu sana, kumwelezea mtu hivihivi  ni vigumu lakini ndivyo ilivyokuwa lakini YESU anaweza, na wakati huu ni wakati wa Mwisho na ninashukuru MUNGU yale yote niliyokuwa namtumikia shetani kipawa ambacho MUNGU aliyaweka ndani yangu na shetani akakiwahi sasa kabla sijaanza kumtumikia MUNGU sasa kimerudi na ninatumikia MUNGU na nimekuwa mtoto wa MUNGU na ninawasihi watu wamrudie MUNGU na ninawasihi hata wale ambao wametumikishwa na shetani kwa kujijua au  kutokujijua nawaambuiia waache wamrejee YESU, sababu YESU ni mzuri, na anaweza, sababu wakiendelea kukaa huko watachomwa moto lakini wakimrejea YESU siku ya mwisho wataenda mbinguni na pia nilikuwa nawafundisha baadhi ya watumishi ambao wako huku duniani ambao wamtumikia shetani wengine wajijua na wengine hawajijui, lakini nilikuwa hasa nawafundisha  wale waliokuwa wanajijua, jinsi ya kuhubiri, jinsi ya kunena kwa lugha, na pia jinsi ya kufanya ishara na miujiza  mingi nilikuwa pia nahusika
Na kuna mtumishi mmoja ambaye kule kuzimu  ni rais mpaka sasa na mimi mwenyewe nilikuwa ninashirikiana naye  na mimi mwenyewe nilikuwa raisi, na nilikuwa na hicho cheo kuanzia nilivyoenda huko mpaka ile siku ambayo nilivyokuja kutolea lakini mpaka sasa mtumishi huyo ambaye anajiita …. Hapo mwanzo aliitwa na MUNGU na baadae aliamwacha MUNGU. Na kumtumikia shetani mpaka mimi nimeondoka kule yeye bado ni rais wa wa kule lakini huku duniani anaonekana kwamba, ni mtumishi wa MUNGU na anaonekana kwamba anafanya kazi ya MUNGU lakini kwenye ulimwengu wa roho ni kinyume bali anatumikia shetani na anamtumikia shetani moja kwa moja anajitambua lakini ndio hivyo tena ameamua kumtumikia shetani, na lakini  hapa duniani anaonekana kwamba anamtumikia MUNGU, watu wengi wanamkimbilia bila hata kujua lakini wakati  MUNGU umefika
ISAYA:           Huyo mtumishi nakumbuka alikuwa ni pia alikuwa akikusafisha vyoo vyako, pia tulipokuwa kule chini, pia nakumbuka alikuwa unampa adhabu mda mwingine alikuwa akienda kinyume na wewe, ulikuwa unampa adhabu ya kudeki nyumba na kudeki vyoo na kusafisha viatu vyake kwa mate yake
Debora:          Ndio
 na pia alikuwa anakusaidia pia kubeba mabegi mda mwingine alisimama badala ya yule mfanyakazi wako ambaye alikuwa akikusaidia kubeba vitu zamani, ulipokuwa ukienda sehemu mbalimbali. Na huyo mtumishi pia alikuwa ni mtumishi wa MUNGU kweli, alikuwa kweli anafanya kazi ya MUNGU lakini ninaelewa historia ambayo ilimfanya mpaka akaacha kuifanya kazi ya MUNGU
Kilichomfanya aache kazi ya MUNGU …!!!!
Ndio maana hata kanisani kwetu Mtume na Nabii Hebron huwa anasema  “Usipende sana kudadisidadisi sana vitu” sasa huyo mtumishi alikuwa anadadisi dadisi mambo ya Mbinguni,  na kutaka kujua kuwa Mbinguni kukoje, kulikuwa kuna nini Mbinguni, wanaishi vipi, kwa sababu unajua YESU akiwa amekuita anajua mwisho wako, kwamba utafanya kazi yake, anajua kwamba utamsalitikwa wakati fulani anajua kama utaifanya kazi yake mpaka mwisho akiwa kama anarudi.
 Tazama wengi ambao walikuwa wameitwa na YESU walikamatwa na shetani kwa sababu ya vitabia tabia Fulani Fulani tu, lakini ni neema ya MUNGU siku ya leo tena ametuletea Mtume na Nabii ambae ni kwa ajili ya kuturudisha Mbinguni tena, watoto wa MUNGu wote ambao tulikuwa tumepotea, hata mimi na wewe.
 Huyu mtumishi nakumbuka hiyo siku alikuwa amekaa nyumbani kwake anajiuliza ni namna gani mbinguni kulivyo akawa anajipa aidia (tathmini) yeye mwenyewe pasipo kuelezwa na Roho Matakatifu, na shetani akamfuata hapo hapo kwa sura yake lakini shetani hakuwa na sura  yake   kabisa kabisa, alimfuata kwa njia kama ya Malaika, akamwambia ee mtumishi wa MUNGU nataka mimi nikuonyeshe jinsi kulivyo Mbinguni, asema bwana, unifuate mimi nami nitakuonyesha  jinsi njia ya Mbinguni ilivyo, Yule Mtumishi kwa kuwa tayari alikuwa amekwishatekwa na shetani ufahamu wake,  mda ule ule na kwa kuwa shetani alikuwa amekwisha mtumia, akakubali shetani akamshika mkono akapotea akaondoka nae pasipo kuelewa kimiujiza miujiza tu na hiyo siku familia yake ilikuwa inamtafuta lakini kikainuka kigezo kwamba sipo nipo hoo! Akapiga simu niko mjini nimekuja (akajutetea) kutafuta vitu gani kwa ajili ya kazi ya Bwana, alivyo kuwa amefikishwa kwenye lango la kuzimu shetani akamwacha hapo juu yeye akapotea (shetani) kisha akatokea Malaika mmoja kule kuzimu akamweka muhuri wa moto ambao huo muhuri ukipigwa wewe hata ufanye nini hata iwe vipi ni kwamba tayari MUNGU hatakujua.
Shetani ndio atakaye kutumia sasasawa na vile atakavyotaka yeye mwenyewe baada ya hapo, MUNGU Hakuongea maneno mengi ila alisema kwamba mia sita sitini na sita (666) maana yake ni kwamba  mimi tayari nimeshamchukua huyu mtumishi sio wako tena ni mwanangu wa pekee ninayependezwa naye,  YESU akamwacha kwanzia hiyo siku akenda na baada ya hapo kitu kilichofuata  juu yake kilikuwa ni kipigo
Isaya:              Sijui kama unakumbuaka??
Debora:          Ndio, Nakumbuka
Kilikuwa ni kichapo maana alipewa kipigo hicho na shetani mwenyewe, na unaambiwa kipigo cha shetani mwenyewe, na unaambiawa kipigo cha shetani ehhh kama unampiga kwa jiwe, siku ambayo shetani atakupiga na jiwe lake rafiki yangu, utasuuzika na roho yako.
 Alivyokuwa anapigwa na shetani ndivyo hivyo, shetani akampa majukumu  yake pamoja alikuwa na jukumu mmoja wapo la kuwa mfanyakazi wa Debora ambaye zamani alikuwa anaitwa Wariambora, kazi ali zokuwa akizifanya ndizo hizo alikuwa ni makamu wa Rais wa ambaye nilikuwa naye kuzimu hapa lakini kwa sasa tunamshukuru MUNGU kwa kuwa hatupo tena.
Na pia huyo mtumishi anajulikana sana hapa Tanzania, kwa cheo chake alichonacho anajulikana kama mwalimu, mpaka leo, hii watu wanajua kuwa bado ni mtumishi,  lakini sio Mtumishiwa MUNGU akisema kuna mkutano watu huenda kujazana hapo kibao lakini pasipo wao kuelewa ni kwamba wanaenda kuhudhuria kwenye mkutano wa mapepo na wana  vyohudhuria kwenye ule mkutano, wa mapepo, shetani anakuwa anawa nyanyulia bango lake, sababu bango moja la shetani ni likubwa na akiliweka mbele za MUNGU ni kwamba wewe tayari MUNGU anakuhesabia kuwa tayari ni muovu na umeshamwacha MUNGU umeshamfuata shetani na kwa hiyo unapokuwa umeenda kwenye hiyo mikutano wake shetani ananyanyua bango kwa MUNGU anasema Tazama MUNGU hawa wamekuja kwangu kwa hiyo hawa sio wako tena , labda iwepo neema  ya MUNGU akikuhitaji anakuja kukuchukua tu yeye mwenyewe, Utakuta tayari umeshafuata njia yake ya kwenda Mbinguni  na kwenda kwa mtumishi aliye sahihi kama alivyo Mtume na Nabii Hebron.
Na pia yapo maisha ambayo tulikuwa tukiyaishi, yako baadhi yake ambayo tumeyaelezea pia lakini tulikuwa tunatembeleana, tulikuwa na sehemu nyingi za kwenda kutembelea tukiwa tunakula , tukiwa tunapiga story za kupanga kazi za shetani.
Bwana YESU asifiwe!
Sasa nitakwenda kuwaelezea ni jinsi gani tulikuwa tunatembeleana kwa ajili ya kupanga  mipango ya kuendeleza kazi za shetani na pia huku duniani tulisha wahi kwenda sehemu fulani, iko Dar es salaam
ISAYA:           Sijui kama inakumbuka
DEBORA:      Ndio nakumbuka
Tulienda tukiwa peke yetu tulikuwa tunatokea nchi ya Uganda, tulivyotoka tulikuwa tunadrive mpaka tulipofika Dar es salaam, kwa sababu mda mwingine pia tulikuwa tunakuwa tuko kimwili, mda mwingine tunakuwa tunaingia kiroho, sasa hiyo siku tulivyokuwa tumeenda kwenye hiyo hotel tulikuwa tumekaa, tulikaa kama nusu saa kwa sababu tulikuwa hatukai sehemu moja kwa kipindi cha mda mrefu, tukivyotoka katika hiyo sehemu,Nakumbuka  tunasikia watu wakawa wanasema sema Moses Kulola, Moses Kulola, Moses Kulola, mimi nikamuliza mwenzangu hapa (Debora) unaelewa habari za huyu mtu anayeitwa Moses Kulola? Akaniambia namfahamu ndio tulivyotoka hapo tukawa tunaendelea kuwasikiliza watu waliokuwa wanataja jina la Moses Kulola, mimi nikashuka kwenye gari, ndio nikauliza kuwa Moses Kulola anapatikana wapi? Pia nilikuwa natafuta anapokaa ili niweze kufika kiwili pia wakanielekeza kanisa lake, mimi nikaenda nilivyoenda pia nikatumia mbinu Fulani nikatumia mtumishi wa Moses Kulola  nikamwuliza huyo mzee anapatikana sehemu gani,  Maana nina shida kubwa nataka nionane naye, kumbe kweli yule mtumishi akafikiri kweli nina shida kubwa na kiu ya MUNGU kumbe walaa!!!!! Haikuwa hivyo, Akanionyesha sehemu ambayo Moses Kulola anapatikana na pia nakumbuka siku ambayo nilienda kwa Moses Kulola nilibahatika kuonana naye, ilikuwa ni Mwanza, nilivyoenda kukutana na Moses Kulola Mwanza yupo mtoto wake ambaye pia nilimtumia kama kunipa kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea kwa mda huo mahali ambapo Moses Kulola alikuwepo. Mtumishi huyo wa Moses Kulola ndio ambaye pia alimwelekeza  Mtume na Nabii Hebron kwa mara ya kwanza, mahali ambapo  Moses Kulola alikuwa anapatikana.
Nilipofika mahali pale mimi sikuingia ndani, yaani Moses Kulola alikuwa amekaa sebuleni  kwake lakini mimi sikuingia sebleni kwake mahali alipokuwa amakaa, nilikaa sehemu moja nikawa namwangali, tulivyotoka nikatoka nje nikaanza  kuongea na mwenzangu nikamwambia je huyu mtumishi unaonaje tukianza kumfuatilia kuanzia sasa hivi …
Isaya: Unakumbuka jibu ulilonipa? Akanimbia tupo tayari tuanza kazi sasa hivi,
Akaniambia tupo yayari tuanze kazi sasa hivi!!  Basi, tutakapotea tu pale tukatokea kuzimu tulivyorudi, tukavaa nguo zetu za kijeshi tukavaa silaha mbalimbali tukatokea tena duniani tukamfuata tena Moses Kulola, Kwa mda huo tulipokuwa tunamfuata hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa anaona wala aliyekuwa anaelewa kitu chochote kilichokuwa kinaendelea, kauli moja ambayo Moses Kulola alisema, MUNGU mimi siongei lakini MUNGU shughulika na hao matakataka, Nikamuuliza wewe mzee umetuita sisi matakataka, kwa kitu gani ulichonacho? ….. Kidogo ikashuka nguvu ya MUNGU na alishuka Malaika Mkuu Mikael siku ile
Isaya: Debora unakumbuka??
Debora: Ndio
MikaEli alivyoshuka kwa sababu tulikuwa na tabia moja kama tumeanzisha vita labda na serikali ya mbinguni, tukiona labla wamekuja wengi wengi tunaanza kuwavuta kwa kukimbia, tunakuwa tumejifanya kama vile tumeshindwa vita, tunakimbia tunawavuta tunawavuta tukiona kuwa tunaona kuwa  tumefikia sehemu ambayo tunaweza kupigana nao kisawasawa tunasimama, Wakifika  na wao kwa sababu ni serikali ya mbinguni wana akili  ya Kiungu, wanaanza noa  kupigana vita hapo hapo pasipo kuuliza kitu chochote,  hiyo siku nakumbuka tukapigana mimi nikaotea kupigwa na rungu la mguu mmoja  nilivyopingwa na rungu la mguu mmoja, huyu mwenzangu alikuwa na mishale  yake aliyochukua ile mishale yake akaipiga chini kwenye ardhi, ardhi ile ikalipuka ikatoa kitu kama moshi sisi tukapotea
Na baada ya hapo Moses Kuloka akasema bahati yenu naye akaanza kutufuatilia nyendo zetu, lakini tukamtumia mtu mmoja ambaye alienda kumloga Moses Kulola Akamloga mguu, akawa anaumwa mguu baada ya hapo, haikupita mda mrefu ndipo MUNGU akamwinua Mtume na Nabii Hebron.
 Baada ya hapo, ndipo na sisi tukaanza kutangaza vita na Mtume na kumbuka siku ile ambayo YESU alikuwa anamwita Mtume, mimi nilikuwa nazunguka zunguka tu onyo, Nilikuwa zangu peke yangu, nilipokuwa natembea tembea Nikawa nasikia hali Fulani ambayo YESU akiwa mahali popote hiyo hali unakuwa unaisikia, nikasema mahali hapa patakuwa na jambo mimi nikasogea nikakuta mtume na Nabii anaongea  na YESU nilichokifanya nilichukua kamera yangu, nilikuwa na kamera Fulani, nikapiga picha lile tukio halafu nitarudi zangu kule kuzimu.
 Kwanza nilisikia yale Maongezi halafu nilivyomaliza nakashuka zangu kuzimu nikawaambia jamaa kuna mtumishi mmoja ambaye anaitwa naona  kama kweli atakubali wito huu shughuli itakayotukuta sio ya kawaida, wakakubali wote.
Hiyo siku tukaitana kikao, huyu mwenzangu alikuwa amesafiri baada ya hapo akawa amepigiwa simu, akaambiwa aachana na huko sehemu unayooenda, itakubidi ugeuze. Alivyogeuza akawa anarudia, tukakaa chini sehemu tunayokaa hiyo meza moja ni mfano wa Mkoa wa Arusha wote ndio meza moja ya makutano makuu tukiwa tunafanyia kuzimu, tukakaa hapo ile picha nikaiweka kati nikaikuza, nilivyoikuza ikawa ni kubwa hivyo nikaiweka kati, kila mtu akawa anaiona, na kila mtu alitoa neno lake mwingine anasema huyu tumpake mavi, mwingine anasema tumfanye hiki, mwingine anasema tumrudishe nyuma, mwingine tumpige misumari, mwingine anasema hivi, Mimi nikanyanyuka nikasema kwa kuwa tupo sisi wawili ambaye ni mimi pamoja na Wariambora ambaye kwa sasa anaitwa Debora kazi hii tunawezakuifanya sisi  wenyewe, lakini mwenzangu akasema hapana katika hilo mimi naomba usinishirikishe kabisa kama wewe utakwenda nenda mwenyewe mimi naomba uniache kinyangu nikamwambia basi kama wewe hutahitaji kupewa cheo kingine na shetani au kupewa pesa na shetani basi acha mimi niende nikajaribu bahati nilivyotoka hapo nikaanza kumfuatilia Mtume na Nabii lakini kila nikijaribu kwenda nikirusha  vitu vyangu ili vijaribu kumpata , kipindi kile bado alikuwa bado anafanya kazi Serengeti, alikuwa bado hajaanza kuifanya kazi ya MUNGU sawasawa, vingine vilikuwa vinaingia lakini YESU alikuwa anachomoa, na vingine vilikuwa haviingii wakati mwingine nilikuwa naambulia makofi vile vile  na ni kitu cha  kushangaza sana  na pia mda mwingine nilipokuwa nataka kusogea nilisikia Malaika wakiniambia wewe uliyekuwa unamfuataga Moses Kulola, tunaomba usisogee mahali hapa utakufa lakini kwa sababu nilikuwa na ujasiri na nilikuwa ni kiongozi wa ngazi ya tatu na nilikuwa mtu wa Karibu sana na shetani nilikuwa sioni hasara yeyote nikawa nawaambia mna kitu gani nyie kama mnaweza kuniua njooni, lakini wakisogea wakitaka kuanza kupigana na mimi nakimbia.
 Naanza kuwapa mawasiliano wenzangu kuwa jamani eeeh hali mbaya, tayari huku nawavuta ikifika mahali ambapo naona hapa naweza ninajaribu kuwacontol, au kupiga nao, nasimama, hivyo hivyo naendelea kupigana nao ikifika mahali nashindwa . mwenzangu anakuja ananisaidia ndivyo yaliilikuwa hivyo  maisha yetu.
 Mda mwingine tulikuwa tunatoka tunaweza kwenda kwenye nchi yoyote, tunaweza kutoka kuzimu tunaenda kwenye nchi yoyote tunakaa kama wiki hivi, wiki mbili, ikiisha tunarudi zetu kuzimu kawaida.
Mwenzangu alikuwa na nyumba yake,alikuwa na magari yake, alikuwa na ofisi yake, mimi pia nilikuwa na magari yangu, nilikuwa na ofisi zangu na nilikuwa nina vitu vingi sana ambavyo, kama tukitaka kuonana kule kuzimu labda kama kuna mtu anataka kwenda ofisini kwa mwenzake, kwa shida Fulani au kwa ajili ya kufanya kitu fulani au shida fulani ndio tulikuwa tunaenda na pia kupo mahali Fulani ambapo tulienda, ni hapa duniani, nakumbuka ilikuwa ni nchi ya China:
Isaya:              sijui unakumbuka
Debora:          Nakumbuka
Isaya:              ilikuwaje? Sijui mwenzangu labda anaweza akaelezea  safari yetu ilivyokuwa, mpaka tulivyofika, kwa sababu China ndiko sehemu ambayo lango kuu la kuzimu lipo hapo,  katika sehemu fulani katika mlima mkubwa sana katika nchi ya China tulikuwa tumetoka na tulikuwa na ndege yetu moja. (Kwa sababu tulikuwa tuna ndege zetu kila mmoja alikuwa na ya kwake.) tulivyotoka hapo tukafika katika hilo eneo pasipo watu kuelewa lakini tulienda na tukaonekana kimwili lakini ndege haikuonekana kimwili labda kwa mtu mwenye macho ya rohoni ambayo amepewa na MUNGU basi tukafika katika hiyo nchi hatukukaa mda mda mrefu tulikaa kwa nusu saa tukazunguka zunguka tuliacha vitu vyetu, na  silaha zetu hapo, lakini katika hiyo nchi kipindi hicho kulikuwa kuna mtumishi mmoja wa MUNGU ambaye alikuwa anaitwa Kindaee
Isaya: Sijui nakumbuka!!!!
Debora: Namkumbuka
Tulipofika mahali hapo, tukakutana nae, yule jamaa akaanza kutulipua sababu alishtuka tyari sisi ni kina nani!  Alivyoanza kutulipua sisi tukawa tunamwamwalia, nikamgeukia na mwenzangu, nikamwambia huyu jamaa anaanza kutafuta vita na sisi na sisi tuende nae kimwili, tukaanza kumfuatilia gari lake alilokuwa anaendesha nae, jamaa na akapata wasiwasi nae akaanza kukimbia ndio ile unakuwa mtumishi wa MUNGU bado huweki imani yako kwa MUNGU, kwamba MUNGU anaweza kila kitu, sasa akaanza nay eye kutumia akili zake kimwili akawa anakimbia na alivyokuwa anazidi kukimbia na sisi tukaanza kuongeza speed ya gari ambayo tulikuwa tunaitumia ilikuwa aina ya  Range Sport, gari zetu nyingi ambazo tulikuwa tunapenda kuzitumia sana sana zilikuwa ni range sport, sana sana ndizo tulikuwa tunapenda kuzitumia,hata huku duniani ukiwa na Range anaonekana sana mtu mwenye hela,  mtu tajiri.
 Tulivyokuwa tunaendelea kungeza spidi ya gari, tulivyokuwa tunamfuata jamaa tukamuotea sehemu, tukaenda tukaovateki gari yake, akapata kihoro akaangukia sehemu nyingine kwenye mlima, huyo jamaa, sisi tulivyomfuata tukampiga visu, tukamuua hapo hapo kimwili,
Isaya:              sijui kama unakumbuka
Debora:          Ndio nakumbuka
Baada ya hapo wale watu wengine wakaenda kumfuata wakaenda kusema kifo chake kimetokana na ajali, na baada ya hapo tukakamata roho yake, tukaichukua, tukaenda kuifanyisha kazi sisi wenyewe, mpaka siku ya leo kazi ambayo anaifanya kule kuzimu ni kutawazisha majini, wakiwa wametoka kujisaidia katika haja yoyote ile, kule chini.
Na pia, katika safari moja ambayo ndio ilikuwa safari ya mwisho, ndio mwenzangu akapewa kazi ya kumuua mama yake, kuna safari moja ambayo tulienda katika nchi ya Israel, tulikuwa tumeenda katika kaburi ambalo watu walikuwa wanasema kuwa ni kaburi  la YESU, hiyo siku ambayo tulikuwa tumeenda katika hiyo sehemu, tulivyofika tukaacha pale vitu vitu vyetu kwa sababu hapakuwa na kitu chochote kile ambacho YESU alikuacha pale, YESU alikuwa ameshatoka, baada ya kupaa kipindi kile alipokuwa na wanafunzi wake.
Tukaacha vitu vyetu pia, tukakutana na mtumishi mmoja wa MUNGU, tulipokuwa kule Israel, hatukumbuki jina lake, mimi simkumbuki kisawasawa
Isaya:              Labda!  Mwenzangu sijui kama unamlikumbuka
Debora:           kwa sura ninamkumbuka lakini kwa jina silikumbuki,
Isaya:              Na pia baada ya hapo sasa tulivyokutana na huyo mtumishi, kwa sababu huyo mtumishi alikuwa na NGUVU za ajabu , kiasi kwamba tusingeweza kupigana nae, ikabidi nimtafutie mwenzangu njia namna ya yeye kurudi kule kuzimu, alafu mimi nione kama naweza kufanya kitu chochote.
Na pia nataelezea kuwa ni namna gani tulikuwa tunaweza kuwakamata watumishi, kuwafanyia kitu chochote, kuwaangusha, au la kuwamaliza kabisa kutoa uhai wao. Ilikuwa inawezekana sisi kufanya hicho kitu kwa sababu ya , unaweza ukute mtumishi mwingine bado imani yake haijakaa sana kwa MUNGU, au anahofu au anajiuliza nitafanya  kazi ya MUNGU, lakini kitu gani kitakachoinuka kwa sababu kila ambaye ataitwa na MUNGU, kabisa kabisa kwanza ataonyeshwa sura ya shetani, sasa hapo wengine, ile sura ya shetani, inakuwa tayari amekwishapata hofu, akisikua sauti ya shetani yaani imani yao inaanza kushuka, wapo watumishi wengine ambapo tulikuwa tunawaweza kwa tamaa, unaweza kukuta mtumishi labda ameitwa na MUNGU lakini bado anakuwa na tamaa fulani, za dunia dunia, ndipo na sisi tulikuwa tukipata mlango hapo hapo, tunafanya kitu chochote ambacho tulikuwa  tunakitaka.
Kama huyo mtumishi ambaye nilikuwa nilimwuelezea kuwa tulimuua kwa ajali, huyo mtumishi kilichokuwa kinamsumbua ni hofu,  alikuwa anafanya kazi ya MUNGU vizuri lakini akawa bado haamini kwamba MUNGU, yeye alichokuwa anakijua ni kwamba MUNGU atasaidia kupigana na maadui zangu katika vita vya kiroho na lakini vita vya kimwili lazima nitumie akili yangu, hapo ndipo tulipopata mlango, ndipo shetani akamnyanyulia shitaka mbele za MUNGU, na MUNGU akakaa pembeni, ndipo na sisi tukafanikiwa kufanya kile ambacho tulikuwa tumekidhamiria. Na unapokuta kuwa mtumishi anaanguka, sio  mtumishi anaanguka na kuacha kufanya kazi ya MUNGU kama vile amependa, kipo kitu, ambacho kitakuwa kimesababisha mpaka anaacha kufanya kazi ya MUNGU, kama hivyo nilivyosema ni imani, utakuta mtu mwingine bado anayo hofu, hajiamini yaani, na hajamwamini sawasawa MUNGU ambaye anakuwa amemwita.
Na pia wapo watumishi wa MUNGU ambao wanafanya kazi ya MUNGU kweli lakini, kulingana na hao wengine ambao yanafanya kazi za shetani, hawafanyi kama vile ambavyo MUNGU anataka nao wakaiga, wakafanya mkumbo, wengine wakapotea na wengine, wanajijua na wengine hawajijui.
Na pia nitaendelea pale ambapo nilikutana na mtumishi huko Israel, ndipo ambapo nikaona kuwa huyu mtumishi anakuwa na nguvu za MUNGU nyingi kuliko hata sisi ambao tunakuwa tunafanya hizo kazi ya shetani, ndipo nikamtafutia mwenzangu mlango wa yeye kutoka, kwa sababu mimi mda mwingine nilikuwa sitegemei sana silaha, nilikuwa nategemea maneno, nilikuwa naweza kumjaribu mtumishi yeyote na kumpoteza kwa maneno tu, basi huyo mtumishi nikaongea nae,
Isaya:              Nikamuuliza je wewe kweli ni mtumishi wa MUNGU akawa ananijibu!
Mtumishi:       Ndio
Isaya:              Nikamuuliza sasa umefuata nini kwenye hili kaburi?
Mtumishi:       Nimekuja hapa nimekuja kuomba
Isaya: Basi hapo ndipo nilipokuwa nimepata mlango, kwa sababu kwenye kaburi lile la YESU hakuna kitu, YESU alikwisha kuzikwa tayari, na tayari yuko zake kwa Baba yake Mbinguni, na tayari ameshapaa,  pale inamaana hakuna kitu chochote.
Sasa yeye alipoenda inamaa pale alienda kuabudu mizimu na kwenda kuabudu vitu vingine. Kwa sababu sehemu ambayo shetani anakuwa amepakanyaga ina maana, ni mahali ambapo tayari shetani ana uhalali napo, sasa sisi tulipoikanyaga hiyo sehemu nay eye akasema anaenda kuomba ndipo mahali na mimi nilipomkamata,   
Isaya:              Nikamuuliza yuko wapi Bwana MUNGU wako ambaye alikuita uje kuifanya kazi yake?
Mtumishi:       Akasema yuko mbinguni
Isaya:              Nikamwambia kwa nini unakuja kuomba katika kaburi?
Mtumishi:       Akasema nimekuja kuomba kwa sababu alishalala mtoto wake wa pekee!
Isaya:              Nikamwambia basi tayari nina uhalali wa kukufanyia kitu chochote ninachotaka   kuanzia sasa muite MUNGU wako.
Akaita jina la YESU haikuwa, akaita mara ya pili haikuwa, akaita mara ya tatu, haikuwa!!!
Isaya:              Nikamuuliza? Nikufanyie kitu gani? Akaanzaa aa, yaani hapo tu kwa kumjaribu kwa hilo neno, akaniambia nisamehe.  Basi ndipo  na mimi nilipopata mlango, na mimi nikamuua nikamchukua kabisa, nae pia nikashuka nae  kuzimu kimwili, sikumfanyia kitu chochote, tuliposhuka kuzimu, shetani akaanza, kumtandika, kwa sababu  na yeye pia alikuwa anafanya kazi ya kumpunguza nguvu shetani.
                        Alivyomaliza kumtandika akamuua, mpaka na roho yake tayari ipo kule kuzimu.
Ninapenda kuwaambia kitu kwa upande wa watu wale ambao mnapenda kwenda kuabudu na kusujudu katika lile kaburi la YESU, ni kwamba pale hakuna kitu chochote, kama ni YESU ulikuwa ni mwili wake tu ulikwisha kuwekwa pale, na tayari mwili wake umeshatoka kwanza yeye yuko mbinguni, kwa hiyo kama wewe kweli una imani ya kumwabudu MUNGU, ina maana unatakiwa umwabudu kwa imani kwa sababu yeye yuko mbinguni,  na maombi yako yatakwenda  mbinguni.
Unapokuwa unaenda pale ina maana kwanza unaenda kuabudu mizimu kwanza, kwa sababu moja kati ya imani za mizimu, ni mtu aende akaabudu kweny kaburi lao, unapoabudu kwenye kaburi lao ina maana na tayari wewe umekwisha kufa, inamaana kwenye ulimwengu wa roho umekwisha kufa pasipo wewe kujielewa na Imani yako inakuwa imekwisha kufa, sasa mtu yeyote anayesema kuwa anaenda kuabudu, labla kwenda kuabudu katika kaburi la mtu Fulani, au kaburi la mtumishi Fulani, huyo tayari anakuwa amekwisha kupotea.
Lakini kwenda tu kutembelea kama historia, kwenda kuangalia hilo kabuiri la YESU, sio mbaya ni vizuri kwa sababu unakwenda kujifunza pia, vitu ambavyo, vilitokea hapo zamani, chanzo cha kifo chake.
Lakini pia tukirudi kwenye neno la MUNGU limesema kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU wako usiabudu miungu mingine, wewe tayari ukishaenda kwenye hili kaburi, kualibudu, kulisujudu, ukisema unashika mlango ambao  Bwana YESU alipopitishiwa, kushika mavazi ambayo YESU alifunikiwa,  kwanza yale mavazi ya YESU yalishaondolewa, yakawekwa mavazi ya mtu mmoja kule kuzimu,  ambaye alikuwa anaitwa Brian. Huyo Brian alikuwa mkuu wa uzinzi kwa hiyo unavyooenda kushika lile vazi unaenda kushika uzinzi vilevile, ndipo unapotoka pale unatoka na nuksi, balaa, lakini kama unaenda kuangalia kwa historia sio mbaya, haikatazwi lakini ukienda pale kwa nia ya kwenda kuabudu, au kufanya kitu kingine, kwa kweli unakuwa pia umeshaasi moja kati ya amri kumi za MUNGU,
Hebron:          Bwana YESU asifiwe
Hebron:          Hawa makomandoo ya shetani ya zamani, bwana sasa ni watoto wa YESU, sasa ni watoto wa YESU wanamtumikia YESU. Haleluya
Hebron:          akamuuliza Isaya.Vipi Bwana unamwambiaje shetani sasa?
Hebron:          Mwageni kwa lugha yake ya kuzimu, maana wako ambao wanasikiliza na wengine ni maajeti wake,
Hebron, Isaya na Debora:              haaaaaaaaa wamecheka
Isaya:              Crcomatau makasi reotaimasctac reo matumarasctac marbata matao
Debora:          Shetani sikutaki na vitu vyako vyote mimi ni wa YESU, nimetoka kwako, sina kitu chako chochote, mimi sasa hivi ninamilikiwa na YESU
Isaya:              Cicomasts trrcbccao maobata       
Debora:          Unikome mimi sio wa kwako tena
Isaya:              Kcomastastams mastcbaco
Debora:          Mimi ni wa YESU peke yake
Hebron na Debora:             Amen, haleluya
Debora:          Bwana YESU asifiwe,  ninamshukuru MUNGU kwa kuwa sasa hivi nimeokoka na ninampenda YESU, na pia nina wasihi wale ambao wamebakia kule,  wako ambao wanajifahamu kabisa, ninawasihi wamrudie MUNGU waache hayo ambayo wanayafanya maana yanamfaidisha shetani na wala sio MUNGU,mimi nimeokoka na nampenda YESU na ninafurahia maisha ya wokovu.
Isaya:              Napenda kuwasihi watu wote ulimwengu mzima, mataifa yote, makabila yote, rangi zote, mumrejee Bwana YESU, mumrejee MUNGU, kwa maana kwake kuna kila kitu, kwake kuna raha, maisha ambayo niliishi kuzimu na maisha ninayoishi nikiwa kwake kwa kipindi hiki, ni maisha tofauti na sikuwahi kufikiri kuwa nitawahi kuishi maisha kama haya, kwa hiyo na mimi nawasihi mmrudie MUNGU kwa sababu duniani hakuna kitu na nitawashangaa sana wale ambao, wanaing’ang’ania dunia, kwa sababu sijui ni kitu gani ambacho kitawafanya waing’ang’anie dunia, ninawasihi mrejee kwa YESU ndugu zangu wote, ili siku ya mwisho tuende zetu Mbinguni tukamfurahie Bwana YESU.
Hebron:          Na mimi nakusihi ndugu mtazamaji na msikilizaji, nchi yeyote mahali popote, nilipokuwa nikiongea na YESU, siku moja alikuwa anatoa machozi, kwa ajili yako wewe na kwa ajili ya wengine hata kwa ajili ya hawa ambao nimewatoa kuzimu, maana alikwisha kunipa habari zao,leo hii wanamfurahia  na wewe pia YESU anakutaka, lakini tatizo haliko kwako, tatizo liko kwa watumishi ambao, wengi wao wanawaongoza sala za toba kumbe ni waongo, wamewapumbaza watu, kuna watu wanalia, wanamtafuta MUNGU lakini hawampati MUNGU wa kweli, hawapati injili ya kweli, injili imekuwa ni biashara ambayo ni namna ambayo hata hawa walihusika kuharibu injili hiyo na kwa wale waliokubali, wako watumishi wanaompenda mwenyezi MUNGU, mumrejee mwenyezi MUNGU, nyie ambao mmeamua kumfuata shetani ninawaeleza  mateso yanawasubiri sio ya kawaida. YESU anarudi, Amerca najua mnateseka, Europe mnateseka, Africa mnateseka, India mnateseka, Asia Mnateseka, mabara yote mnateseka, na nchi zote, lakini nina jambo la kukwambia, nitakuja huko  wakati wake MUNGU ameshanituma.
Hbebron:       Halelluya
Jiandae wakati tutakapo onana utukufu wa MUNGU utakuwa kwako, na siku moja tutakwenda mbinguni, hawa nimewatoa kuzimu mimi nawafahamu na mbinguni, wewe unasubiri nini ni Mkristo lakini hutaki kuokaka unasubiri nini? Ili uwe Mkristo ni lazima uokoe, usidanganyike na hizi injili eti hakuna kuokoka hao ni waongo nakuambia, cha kwanza YESU ni mwokovu.
 Bwana YESU asifiwe!
Hebu jiulize!  Wewe unakuwa Mkristo lakini hujaokoka!
Simameni imara watoto wa MUNGU, ninapokwenda kukuongoza sala ya toba rudi usigombane na MUNGU, kama mpaka sasa hivi hujaokoka wewe umegombana na MUNGU, nachoona wengine mmeshakwazwa katika maombi mnachajiwa pesa, haaaa hao ni waongo ni majangili, nawaambia huyo sio YESU wa kweli.
 Bwana YESU asifiwe!
 Na wengine mmetoa mali mpaka mmefilisika, mjiulize ni kwa nini mumtolee MUNGU mfilisike?  Ninakuambia dalili ya mvua ni mawingu, hayuko YESU hapo, ninakuambia pokea injili ya YESU, zaidi ingia katika website ya www.prophethebron.orgingia katika link ya blog utajifunza mengi, na MUNGU atakutengeneza, nakukaribisha nikuongoze sala ya toba na siku moja tukae mbinguni tukae katika meza na Bwana YESU,
Haleluya!
NA KUANZIA SASA SEMA:          Bwana YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua, uniandike jina langu katika ufalme wako, siku moja YESU nitapata kuwepo na wewe,  ee YESU unilinde nisipotee. Amen.
Mbarikiwe na MUNGU na MUNGU awatenge na maisha ya kuzimu siku zote za maisha yenu—Amen

[ad_2]