MAJIRA YA TANZANIA, MUNGU AMEYAREJESHA SASA!!

[ad_1]

Tanzania ambayo ndiyo Edeni ya sasa katika ulimwengu wote, MUNGU amerejesha. Katika nchi yeyote unapoona kuna ukame basi uelewe kuwa majira yake ya hali ya hewa yamefungwa na shetani na wachawi, na sababu nyingine ni sababu ya laana katika nchi hiyo ambayo watu wanatenda dhambi au sababu ni kanisa kumsaliti YESU WA NAZARETI, na kanisa badala ya kuwa kanisa la kuchunga kondoo limebadilika kuwa mbwa mwitu. Mnamo June 2014 nilipokuwa katika maombi ya kuiombea nchi nilipambana na vita ambavyo hatimaye MUNGU aliniongoza na kunifunulia haya ni kwa nini mvua hazinyeshi kwa wakati au hakuna kabisa wakati mwingine au badala ya hali ya hewa watu walivyoizoea katika mji wao imebadilika kwa mfano miji yenye baridi unakuta inakuwa ni miji ya joto tofauti na MUNGU alivyoumba.
Hivyo kwanzia sasa mtegemee kupata mvua sawa sawa na majira yake na kiangazi kama ilivyopangwa na MUNGU aliyeiumba dunia hii, na mazao yetu kuwa  mengi sana na nchi haitakuwa na njaa tena, mazao yatastawi na kupatikana hivyo kila aliye na shamba alime kwa bidii na atapata faida.
Na jambo lingine katika hifadhi ya Serengeti muda siyo mrefu hifadhi hiyo mvua zitakuwa zinanyesha mara kwa mara katika kipindi cha mwaka mzima na kuifanya hifadhi hiyo kuwa na malisho kwa wingi wakati wote na maji katika sehemu mbali mbali na utafika wakati wanyama wanaohama kwenda mbali na Serengeti hawatahama katika hifadhi ya Serengeti sababu kutakuwa na chakula cha kutosha na maji hivyo watazunguka hapo hapo. Haya yote ni MUNGU atendaye ambaye ndiye mwana sayansi wa kweli kuliko wote katika ulimwengu wote. Mtakapo yaona hayo msishangae ni MUNGU peke yake ndiye afanyaye na tayari ameshafanya mtayaona mabadiliko.
NCHI
·        Hupata watalii wengi kupita makadirio waliyojipangia, mashirika ya ndege yapo njiani yanajiandaa kufanya route zao kuja Tanzania.
·        Mikataba mibovu itafutwa yote na pesa zilizowekwa nje ya Tanzania zitarejeshwa very soon.
·        Atakayetumia uchawi kutafuta Urais 2015 hatapata nafasi hiyo, MUNGU anataka mtu ambaye siyo mchawi na amweke yeye na siyo shetani, na hii itakuwa ni historia kwa mara ya kwanza katika nchi hii, sababu watu walizoea kujitamania tu kutaka kuwa rais na kutumia nguvu nyingine. Sasa hivi hiyo nafasi haipo tena. Nchi ameishika YESU WA NAZARETI, na yeye ndiye atakaye mweka RAIS kwa kusudi lake, na siyo waganga au mizimu, au chochote. Yeye YESU ndiye ajuaye peke yake.


NABII HEBRON.

[ad_2]