Close

MAKANISA YENYE YESU WA KWELI KATIKA ULIMWENGU WOTE MARUFUKU KUFANYA KAMPENI ZA KISIASA!!!

[ad_1]

Watu wote wa mataifa yote nawaandikia ujumbe huu, shetani amejiingiza katika makanisa mbali mbali na kuyafanya ndio sehemu ya kufanyia kampeni za kisiasa badala ya kanisa kufanya kampeni za kuwaleta watu waje kwa YESU waokoke imekuwa ni kinyume. Nawaeleza kama mlikuwa hamjui sasa muelewe yale yenye YESU wa kweli yataacha ila yale yenye yesu wa uongo yataendelea kufanya kampeni za kisiasa siku zote na pia madhabahu ni sehemu ya kumuabudia MUNGU tu na kuomba na kusujudu.
Nyie wana siasa ambao hamjui jambo hili sasa fungukeni mkifanya hivyo mnamkufuru MUNGU. Imeandikwa nyumba yake ni sehemu ya sala tu. Sasa kama ni nyumba ya sala tu haya mambo ya kampeni za siasa yametoka wapi? Au viongozi wa siasa kwenda kusutana na kuongelea mipango yao katika madhabahu je huu ni mpango wa MUNGU? Jibu, huu ni mpango wa shetani kulichafua kanisa na hata sasa baadhi ya nchi nyingi zinanuka hii dhambi ya kulichafua kanisa. Watu badala waende kusali na kusikiliza neno la MUNGU nafasi ya MUNGU ikachukuliwa na wanasiasa kusikiliza sera zao za kibinadamu.
NOTE:
Wanasiasa ili mpone msijemkahukumiwa ile siku ya mwisho usijaribu kwenda madhabahuni ufanye kampeni zako za siasa, tafuta hall au uwanja waite watu itakuwa ni vema na unamheshimu MUNGU. Ila pia siwalaumu wanasiasa sababu wangeambiwa ukweli wasingeichezea nyumba ya MUNGU baadhi yao. Hili ni kosa la watumishi hawasemi ukweli na wengine tayari ni wanasiasa wa vyama fulani wakati mtumishi ile kuwa ni mwanachama wa chama fulani tayari anayo dhambi. Sababu imeandikwa usiwatumikie mabwana wawili ni mmoja peke yake, ukiwa unao wawili hautaweza kuwatumikia wote utakuwa unao ubaguzi. Kama ni mtumishi umeamua kufuata siasa, wacha kazi ya utumishi katika kanisa maana unakuwa haufai tena mbele za MUNGU. Chagua leo ni yupi utakayemtumikia. Ila wengi wa watumishi wa jinsi hii hawa ni watafuta pesa kwa ajili ya matumbo yao.
Jamani muwe makini na watu wanaoruhusu makanisa yao kama chombo cha kufanyia kampeni za siasa badala ya sala tu. Kanisa likiruhusu kampeni za siasa katika nyumba ya sala ujue kanisa lina pepo siyo ROHO MTAKATIFU tena.
Makanisa yatakayosikia yasikie.
Makanisa yatakayokaza shingo shauri lao.
Wanasiasa mnaotaka mpone roho zenu sikilizeni neno la MUNGU leo na mtapona, siasa ni siasa na MUNGU ni MUNGU, ya Kaisari mpe Kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU.
Marko 11: 15-19.

NABII HEBRON.

[ad_2]