Close

MNYAMA MWENYE PEMBE KUMI NA VICHWA SABA AKAMATWA 17TH JANUARY 2013. UFUNUO WA YOHANA 13: 1-10

MNYAMA MWENYE PEMBE KUMI NA VICHWA SABA   AKAMATWA  17TH  JANUARY 2013. UFUNUO WA YOHANA 13:  1-10

[ad_1]


  MNYAMA MWENYE PEMBE KUMI NA VICHWA SABA
 AKAMATWA  17TH  JANUARY 2013. UFUNUO WA YOHANA 13:  1-10
Ndugu msomaji nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, Mfalme wa wafalme;
Nitakuelezea  kwa ufupi tu; umjue huyu mnyama ni nani, na asili yake, na kazi yake, na aliyofanya hapa ulimwenguni na jinsi alivyotumika kuwaongoza manabii wa uongo, mpaka hatima  yake 17.1.2013 , Nilipoongozwa na YESU kumkamata nikiwa na malaika Mikaeli.
Kama wewe ni msomaji wa makala / unabii ambao mimi HEBRON nimekuwa nikiutoa katika ulimwengu huu sawasawa  na anavyoniamuru YESU wa Nazareti, utakuwa unaelewa hicho ninacho kuelezea. Soma katika makala ya Joka kuu kukamatwa ambayo kazi hiyo niliifanya alivyoniamuru YESU na kwa uweza wake  yeye mwenyewe.
Huyu mnyama mwenye mapembe na vichwa saba,ni mmoja wa wale  malaika waliofukuzwa Mbinguni wakatupwa humu ulimwenguni na baba yao Joka kuu, au kwa lugha nyingine ndiye baba yake shetani, mnyama huyu alipewa uwezo mkubwa  sana na nguvu za kuwadanganya wanadamu na hata kulichezea kanisa  na kulipoteza  na kwenda kinyume  98% . Mnyama huyu ndiye aliyewawezesha  wachawi kusafiri kwa ungo au kupaa, ndiye aliyekuwa anawapa mabawa, mnyama huyu ndiye aliyekuwa anawekeza nguvu zake kwenye pete ( zenye vito vya rangi) wanapozivaa hasa kwa  watumishi zinakuwa na miujiza ya kipepo na mtumishi anapokuwekea mkono lazima uanguke chini na wakristo wanapoanguka wanaona ni nguvu za  MUNGU hizo.
Ninachokuambia kitendo cha wewe kuanguka chini,  maana yake umepelekwa kuzimu. Nikuulize swali, Je! Nguvu za MUNGU  zinakaa kwenye pete? Jibu  ni Hapana. Na wachawi , waganga wa kienyeji au mtu yeyote anayevaa hayo mapete ya ajabu, tambua mtu huyo ni mshirikina na maisha yake, au utajiri wake, cheo, huduma aliyonayo haongozwi na MUNGU aliye hai, na njia nyingine ili kuwapumbaza wanaweka hiyo nguvu ya mnyama huyo kwenye cheni za shingoni. Kwa wanaume  wanaoongozwa na mnyama huyu huvaa cheni shingoni wanapo hubiri na pia hutoboa masikio na kuvaa hereni, haijalishi anatenda miujiza, ujue asili yake ni huyu mnyama mwenye  vichwa saba; Ila  sasa  hivi hawana  pa kupatia msaada tena, maana huyu ndiye mungu wao, na sasa ufalme wake YESU  ameubomoa.
Mnyama huyu ndiye kiongozi wa miungu yote  isiyo ya kweli, mfano nitakutajia tu, baadhi ya miungu . Kuna mungu pembe, mungu jicho, mungu baali, mungu wa kutoa vyeo vya kipepo, mungu dagon, freemason, mizimu na wengine wengi tu.., nikisema kuwaandika itachukua siku nzima. Hawa wote wanaongozwa  na mnyama huyu. Na mnyama huyu katika ufunuo wa Yohana 13: 4-10, wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake ; na wakamsujudu  yule mnyama wakisema  ni nani afananaye  na mnyama huyu ? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Tena akapewa kinywa cha kunena maneno. Maneno  makuu ya makufuru, akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi ( 42). Akafunua kinywa chake amtukane MUNGU  na kulitukana  jina lake, na maskani yake, nao wakaao Mbinguni. Tena  akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda,  akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa za lugha na  Taifa, na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina  lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima  cha mwana kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya Dunia.
Mtu akiwa na sikio na asikie , mtu akichukua mateka. Atachukuliwa mateka. Mtu akiuwa kwa upanga,, atauwawa kwa upanga.  Hapa ndipo penye subira na Imani ya watakatifu.
Nimekuelezea kidogo kama kitabu Kitakatifu  kinavyoelezea ( BIBLIA ). Hivyo ndugu msomaji,  wa nchi yoyote na rangi yeyote wewe umeumbwa na MUNGU  aliye Hai, MUNGU  wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Hawa miungu mingine yote unayosikia au kuiona tofauti na MUNGU  wa Ibrahimu , Isaka na Yakobo miungu hiyo yote ni ya shetani, mfano waganga wote wanaongozwa na  huyu mnyama mwenye vichwa saba, na ndiyo maana  mnao au mlio endaga kwa wanajimu, waganga wa kienyeji, wapiga ramli, utaambiwa lete sadaka ya mungu wetu ndie atende, au ajibu, nakufungua ufahamu wako,wacha  maana unakuwa connected ( kuunganishwa) na huyu mnyama aliyefukuzwa pamoja na joka kuu nyakati zile, wewe mwenyewe unajua kabisa shetani hana ushirika na MUNGU aliye hai, Je kwa nini wewe unajilinganisha na joka?
Madhara yake hautaurithi ufalme wa  MUNGU na mauti na kiama inakusubiri, Tubu wachana  na hayo.
Mnyama huyu alikuwa amejificha  baharini chini kilindini kwenye bahari ya  Atlantiki mahali ambapo  ni vigumu kumuona, na ndiye aliye wazaa waganga, watumishi wa dini zote wanaotumia nguvu za uchawi na ndiye aliyekuwa anawapandisha viwango ( Ngazi), baada ya kufanya kazi nzuri ya shetani , mfano kutoa makafara, kuharibu maisha ya wanadamu na kufunga ndoa nao.
Nitakueleza kwa upande wa kanisa zaidi, watumishi wanavaa mapete tofauti na pete tofauti na pete za ndoa, na vidole  tofauti na wengine  wanatoboa masikio halafu wanahubiri , ujue huyo ni anaongozwa na huyu mnyama wa vichwa saba na macheni ya shingoni, na wengine hutumia uchawi.
VYEO VYA KUZIMU KWA KANISA.
Vyeo hivi vyote vimeteketezwa tarehe 17. 1. 2013. Kazi hii ilifanywa na wazee 24 , akiwepo MUSA na fimbo yake; Ngazi hizi zilikuwa zinawawezesha kufanya  kazi ya Kanisa kwa njia za uongo na kuwafanya  wathaminike na kusikilizwa, na watu huamini na kule kuamini kwao ndio kuangamizwa, mfano imeandikwa, usiabudu sanamu, ila kanisa linaabudu sanamu au kuomba watakatifu, au kuleta ubatizo  usio wa YESU , ubatizo wa kikombe, japo waumini wanajua ila hukiri tu. Huko ndiko kupotea .
Nitakueleza kwa ufupi tu kuhusu hizi ngazi, Aliyekuwa ana ngazi  hizi idadi kubwa kuliko watumishi wote , alikuwa ana ngazi elfu moja  (1,000)  ni kiongozi  wa dini  kubwa kuliko zote ulimwengu wote, pia alikuwa anao ukucha wa joka kuu, ambaye ameshakamatwa; na wapili ni muhubiri maarufu kutoka  Amerika yeye ndiye wa pili alikuwa ana ngazi hamsini (50) inamaana aliyakamata majimbo yote hamsini (50) ya Amerika na watu wake,  ili awaangamize awapeleke  kuzimu na mke wake aliyajua  akamkimbia. Mwingine yupo Afrika  Magharibi yeye alikuwa na ngazi kumi (10) za shetani, Afrika ya Kusini  walikuwa ni wengi sana,, na Tanzania walikuwa wengi, Kenya,UK, Asia na  Afrika wengi walikuwa na ngazi  mbili, tatu, moja na tano.
Ujumbe huu ninaokufikishia  mimi HEBRON  nimeambiwa niutume Ulimwengu mzima, na itafika wakati nitaamriwa niwataje na nitawataja  wala hakuna wa kunizuia na mimi siogopi lolote na kila atakayefikiria  tu jambo baya huyo hataishi tena; Ndivyo nilivyoambiwa  na MUNGU na Neno lake halirudi bure lazima litimie.
Mtashangaa sasa watumishi waliokuwa na miujiza na kujulikana sana Ulimwenguni wanaporomoka na  kuacha kazi ,  Sababu  hawana tena hizo nguvu na mambo hayaendi, na hayataenda milele, na watumishi wa YESU  wa Nazareti ndio mtawaona sasa, wakiukomboa ulimwengu , na hao sasa mtawaona wanafariki vifo vya ajabu na kwa mfululizo , hii ni kwa ulimwengu wote, na dini zilizokuwa zinatumiwa  na huyu mnyama mwenye vichwa saba, zitasambaratika zote, mtakapo yaona hayo yametokea msiogope mjue serikali ya mbinguni ipo kazini kufanya  maandalizi ya ujio wa YESU ili awapate wengi. Yawezekana  na wewe ni mmojawapo wa kuokolewa.
Na kwa wale watumishi wa pesa  ( Warumi 16 : 17 -18) . Ndugu zangu, nawasihi waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kufuata kinyume cha mafundisho mliyojifunza mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu KRISTO bali matumbo yao wenyewe  na kwa maneno ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.
Mlizoea kuwanyang’anya kondoo mali zao mkitumia jina la YESU na YESU amekataa, Ole wenu upanga wa MUNGU upo juu ya kichwa chako. Mimi sipunguzi neno nasema kama ilivyo.
Ewe mwanadamu usitumie stika ukipewa na mtumishi, na anakuambia inayo nguvu za mungu, ndugu msomaji nguvu za MUNGU anakaa nazo yeye na hukupa kiroho, na nguvu za MUNGU hakuna anayeweza  kununua. Ila za shetani zinanunuliwa, kama hirizi. MUNGU amechukia watoto wake wanapotezwa, hiyo ni sanamu, tena mlio na hivyo vitu, stika, kalenda, picha vitambaa, ndio maisha yenu yanazidi kuwa mabaya, inamaana  unapopewa na kuweka kwako baraka zako zinaibiwa na hizo stika zina mapepo mfilisi na mbinguni hauendi, na hapa ulimwenguni ni shida tuu.. Mtafute  YESU wa kweli, omba atakuongoza.
NOTE: Baada ya ngazi hizi za kipepo, watumishi waliokuwa na nguvu hizo wameporomoka na mwisho ni kifo, na hukumu . Haijawahi kutokea  tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Mnapo yaona msishangae ni YESU anafanya kazi hiyo peke yake.
Na Freemason wote (Watumishi ) – Watakufa , kuumwa magonjwa yasiyotibika na vifo vya ajabu.

MUNGU AMEKASIRIKA NA AMESHAAPA HATAGHAIRI TENA. YATATIMIA , ASEMA BWANA WA MAJESHI.
NABII HEBRON

[ad_2]