NABII WA KWELI NA WA MWISHO MATENDO YA MITUME 7:37 -38

[ad_1]

Musa ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana MUNGU wenu atawainulia nabii katika ndugu zenu, kama mimi , msikieni yeye. Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zenu ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. Nabii huyu ndiye masihi au YESU KRISTO WA NAZARETI au Mataifa wanamuita Nabii Issa, na ndiye ambaye ile siku ya mwisho atakuja kuwachukua wale walio wake, yaani waliookoka ki kweli na kuwa watakatifu wala siyo kujiita Mkristo jina tu, Mkristo wa kweli lazima aokoke, kama hajaokoka huyo ni mkristo feki na ndani yake asiwe anaongozwa na watumishi freemason, au wachawi, au wanamazingaumbwe. 

Nabii huyu YESU KRISTO wa Nazareti huyu ndiye mwana wa pekee hata katika Biblia yaani kitabu cha MUNGU aliye hai hautakuta jina la mtu yeyote akiitwa na MUNGU mwana wake wa pekee. Tafuta mwanzo mpaka mwisho hautaona. Ni mwana wa pekee sababu ni tofauti na mitume wote, na manabii wote waliopita, ni wa pekee sababu ametofautishwa, ni wa pekee kwa sababu alikufa msalabani, akazikwa na siku ya tatu akafufuka kwenda mbinguni. Na hakuna nabii aliyepitia yote ya YESU, alitabiriwa na ikatokea na kifo chake hivyo hivyo na mwisho alipaa kwenda mbinguni. Sasa nikuulize swali je, kuna Nabii na mwana pekee zaidi ya YESU? Jibu hakuna, na alisema wote watakao kuja nyuma yake ni wezi? 

Na Nabii huyu ninaye kuelezea mimi Hebron, mimi nimebahatika kumwona kwa macho yangu akiwa na alama zake za misumari katika mikono yake. Na maneno haya ni yake yeye ninavyokueleza, “Hebron mtumishi wangu waambie ukweli watu wote wa mataifa yote wanirudie mimi, maana wamepotea na kupotezwa na watumishi walioniasi na kuwa wanachama wa freemason, wachawi na kujiita wenyewe ili kuwaibia wanadamu pesa zao na mali zao wakitumia jina langu.” Mimi siyo mnyangi wa mali zenu bali mimi huwapatia nyie. Pasipo mimi hakuna mtu yeyote atakayemwona MUNGU ambaye ndiye Baba yangu waokoke kiimani, kimatendo, kuacha uovu, wasishiriki katika makanisa yanayoabudu sanamu, hilo silo kanisa langu 100% (ILI UELEWE SOMA KITABU CHA NABII HEBRON KANISA ALILOLIJENGA YESU WA NAZARETI ALIVYOKUWEPO HAPA ULIMWENGUNI). 

Nabii huyu ndiye uzima wa wanadamu na ndiye mkombozi wa mataifa yote kwa wale ambao watakao muhubiri yeye kikweli na katika madhabau iliyo hai. Ukiongozwa sala ya toba katika madhabahu mfu hiyo toba yako haifiki. Nabii huyu ndiye atakaye uhukumu ulimwengu wote siku ile ya mwisho! Je Ni kuulize swali kama huyu YESU ndiye atakaye kuja kuhukumu ulimwengu huu ile siku ya KIAMA. Je, kuna zaidi ya YESU WA NAZARETI KUABUDIWA TENA KATIKA ULIMWENGU HUU? JIBU NO!!! 

NABII HEBRON .

[ad_2]