NANI MUUAJI WA WAJANE?

[ad_1]

Umewahi kujiuliza ndugu msomaji wa makala hii kwa nini wajane wanahangaika mahakamani na kwenye mabaraza ya wazee wa ukoo kwa maswala ya haki zao? Na pengine hawazipati? Ni kwa sababu viongozi wa kanisa (watumishi wa pesa au matumbo); wenyewe wamekuwa wanyang’anyi wakubwa wa kudai pesa na kuchangisha pesa makanisani ndiyo maana hiyo roho ya kupenda pesa na vitu imeenea hata kwenye jamii na watu kukosa muelekeo, ndiyo kutumbukia kwenye roho hiyo hiyo ya kunyang’anya na kudhulumu wajane wa MUNGU.

Tukiangalia tangu enzi za wazee wetu wakina Ibrahimu mpaka Musa na Sulemani waliamua maswala ya wajane kwa haki kabisa, lakini sasa hivi viongozi wa kanisa wamesahau kuwa BWANA YESU mwenyewe ni MUME wa wajane, na kimbilio la wajane ni kwenye kanisa. Lakini sasa hivi sivyo ilivyo. Viongozi wa kanisa wametekwa na roho ya kupenda pesa na vitu. Jambo hili wanalifungia macho na kusahau wajibu wao kama kanisa na kwenda kinyume na neno.

Hebu tuone neno linasemaje kwanza kabisa. Kitabu cha Mwanzo 1: 26-29; MUNGU aliumba mwanaume na mwanamke akawabarikia Baraka za kiroho na kimwili, akawaagiza wakazae na kuongezeka na kumiliki vitu vyote (wote) wamiliki. Maana ya kutawala na kumiliki ni kuvitiisha pamoja na vile wanavyovizaa na kuongezeka. MUNGU hakuagiza kwa mwanamume tu ameagiza kwa mwanamume na mwanamke wote! Kisha akawapa wote kila kitu, hapa maana yake mwanamume na mwanawake wanapounganishwa kwa ndoa takatifu wanakua mwili mmoja na MUNGU anaachilia hivi vyote juu yao na kila wanapozaa na kuongezeka MUNGU anazidi kubariki zaidi kwa Baraka za mwilini na rohoni.

Kama ndivyo basi inakuwaje anapotangulia mwanamume kufa, wanadamu wanasema hizo Baraka ni za mwanamume kwa hiyo mwanamke aliyebaki hana haki? Ni mwanadamu anasema hivyo. Je? Kanisa nalo linasema hivyo? Jibu ni ndiyo. Hawa ni viongozi na watumishi vipofu, wamesahau wajibu wao, wamerudi duniani badala ya kuwaongoza hata hao wasioelewa na kuwatoa kwenye anguko la jehanamu.
Yeyote anayemuonea au kumdhulumu mjane jehanamu inamhusu. Hana njia ya uzima ndani yake, wa kwanza kabisa ni hao viongozi vipofu, wasaliti wa BWANA YESU. Mimi nawaita wasaliti! Kivipi NENO linasema katika kitabu cha Kumbukumbu La Torati 10:18 “Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.”
Kama ndivyo basi inakuaje wachungaji wamekuwa wa kwanza kunyang’anya pesa na mali ya wajane kichawi kuwafanya ATM mashine zao, bila huruma.

Wanazini na wajane na kuwapotosha kabisa badala ya kuziponya roho zao wanazielekeza kwenye moto kabisa. Wajane wakimbilie wapi? kila mahali panawaka moto wa uovu ndani ya kanisa hakufai, kwa jamii ndiyo balaa. Yuko wapi mtetezi wao? Yupo YESU WA NAZARETI ALIYE HAI. Lakini aonekane wapi?! Aliyewaachia kutetea wamemsaliti. YESU ni mwamuzi wa yatima na mtetezi wa wajane Zaburi 68:5.

Kama wachungaji wa kondoo wanafanya dhuluma kwa wajane unadhani jamii itafanyaje? Jibu, itafanya hivyo hivyo kuwanyanyasa na kuwagandamiza wajane kosa ni la nani? Kosa ni la wachungaji na viongozi wa kanisa siyo la jamii maana kanisa linatakiwa kuonyesha mfano mzuri kwa jamii lakini siyo hivyo, na shetani amepewa nafasi kubwa ndani ya kanisa akaweka makao.

Ndugu msomaji uliyetangulia kusoma makala za Mtume na Nabii Hebron umejua kuwa kanisa limetekwa 98% ndiyo maana hakuna haki ndani ya jamii. Itoke wapi ikiwa hakuna haki ndani ya kanisa? Kivipi?! Kwa ukweli huu:
Viongozi wa kanisa wanashiriki sherehe za mila na matambiko na kufanya (misa) za wafuu, kubariki mbesi, sendoff, matanga na mengine mengi yanayofanana na hayo. Hii yote ni ibada ya sanamu na katika kufanya hayo yote ni kumtukuza shetani na kuzidi kuwapiga upofu hata wasijue kuwa MUNGU aliye hai ndiye MUME wa wajane. Lakini shetani anajua hayo toka mwanzo kuwa MUNGU ndiye mtetezi wa wajane akaliteka kanisa na kulipiga upofu.


ANGUKO
Mwanzo 3: 1-19; uharibifu ulitokea hapa mahali ambapo Adam na Eva walimuasi MUNGU, shetani akakamata ndoa toka mwanzo mpaka mwisho utaona kwamba hata baada ya mwanamume kufariki kikao cha kwanza kabisa cha kufanya maamuzi ya maisha ya mjane inaanza kwa usimamizi wa wazee wa ukoo, badala ya viongozi wa kanisa, wachungaji. Kama ndoa hiyo ilifungwa kanisani, umejiuliza kwa nini maamuzi ya ndoa hiyo iliyofungwa ndani ya kanisa linaloitwa kanisa la YESU, maamuzi na mashauri yafanyike ndani ya ukoo? Jibu ni kwamba toka mwanzo watu hao wawili walianzia kwa wazee kabla ya kupelekwa madhabahuni.

Inavyokuwa ni hivi; kijana akimpata binti anampeleka kwao na wazee humpokea kwa sherehe za kimila. Je nikuulize ndugu msomaji, hapo aliyepewa kipao mbele ni nani? Kama siyo shetani (mizimu) na siku ile ya kikao baada ya mazishi unadhani ni nani atakayetawala hicho kikao? Jibu, ni shetani, ndiyo maana kunakuwa na mvutano mkubwa sana baina ya ukoo na mjane. Kwa hiyo ndugu msomaji wa makala hii ninavyo kwambia kwamba kanisa limeacha kutetea wajane ni viongozi na wachungaji wametekwa na shetani 98% hata hawajui wajibu wao kwa kuwa wamemsaliti YESU na YESU amewaacha wabaki na upumbavu wao.

UKWELI
Ukweli ni kwamba mwanzilishi wa ndoa ni MUNGU mwenyewe, na ikitokea mmoja wa wanandoa hawa ametangulia kufa anayebaki pamoja na familia hiyo wakabidhiwe ndani ya uongozi wa kanisa ili kuzungumzia swala hilo, kwa kuwa neno linasema, YESU KRISTO WA NAZARETI ndiyo mwamuzi wa yatima na wajane. Na mtumishi ambaye anatumiwa na YESU wa kweli, hufuata taratibu na uongozi wa neno la MUNGU na kuangalia hizo roho zisipotee bali zipone. Je? Nikuulize ndivyo inavyofanyika ndani ya kanisa? Jibu ni hapana.

Kitu cha kwanza kabisa viongozi wa kanisa huwashauri wafiwa; mjane na watoto ni kuwakazania kufanya ibada ya wafu, misa ya kumbukumbu. Je? Nikuulize ndugu msomaji, mtu aliyekufa kumbukumbu lake halijasahaulika? Jibu, limesahaulika Soma Mhubiri 9: 3-5; hana ijara maana yake ni asikumbukwe kabisa siyo wakuzungumziwa tena wala kutajwa haisaidii lolote.

Kinachotakiwa ni kuwashikilia waliohai roho zao zisipotee kwa kuwaongoza vizuri wavuke washinde, wasonge mbele kuangalia mahali YESU aliyefufuka alipo siyo mahali wafu walipo. Shtuka mwana wa MUNGU unazidi kuunganishwa na huo ufalme katika kila hatua ya maisha yako ili usione NURU. Hii ni janja ya shetani na himaya yake kubwa sana kwa sasa ni kanisa!

Kwa wewe mjane na yatima, tafuta kanisa ambalo YESU wa kweli yupo akutetee.

UBARIKIWE SANA. AMEN.

MCHUNGAJI DORCAS SAMUEL MDEE.

[ad_2]