Close

NIMEIONA SURA YA YESU WA NAZARETI. IJUE ILIVYO!



Watu wengi ulimwengu huu hawaijui sura halisi ya YESU na hawajamuona YESU WA NAZARETI bali wamemuona mwigizaji wa sinema za YESU. Na watu wengi makanisani na nyumbani, kwenye biashara, kwenye misalaba hata mavazi, wamemfanya Mr Brian Decon kuwa ndiye BWANA YESU na wanaiabudu hiyo picha ya huyo mwigizaji anayeitwa Brian. Brian huyu ni mwigizaji na siyo YESU, bali yeye ni mwigizaji tu, ni vizuri alivyoigiza hii imesaidia kufundisha watu kuhusu YESU kama ilivyoandikwa katika kitabu cha injili ya Luka.
Mimi Hebron katika maisha yangu pia ufahamu ulitekwa ukaona ile picha ya Brian ndiyo YESU kutokana na jinsi nilivyofundishwagwa tokea utoto wangu katika madhehebu ya kikristo. Hata sasa itawezekana na wewe unayo picha ya Brian na unaiita picha ya YESU? Hii ni makosa, ile ni picha ya mwigizaji Brian. Na cha ajabu ingia katika makanisa utaona picha za Brian mwigizaji ndizo watu wanaziangalia na kuziita picha za YESU. Hapa watu wamepotea na ni mbaya kuiabudu picha ya mwanadamu, natumaini hata yeye Brian hapendi aitwe yeye ni YESU, maana YESU tunayemjua alikufa na kufufuka na sasa yupo mbinguni na ndiye mwana wa pekee wa MUNGU, hata kuzaliwa kwake ni kwa njia ya ROHO MTAKATIFU. Sasa tazama huyu Brian yeye ni mtu tu kama wewe aliyetumika kuifundisha jamii kwa njia ya sinema ili iwe rahisi watu wapate mfano ilivyokuwa.
Mara ya kwanza kumuona YESU sura sikuiona hii ambayo ipo hapa ulimwenguni na inauzwa madukani. YESU anang’aa, picha yake ipo kwenye macho yangu na haipo mahali popote katika ulimwengu huu. Na hata siwezi elezea kibinadamu mpaka picha itokee haifanani kabisa na  mtu yeyote na ndiyo maana anaitwa mwana wa pekee wa MUNGU. Brian na wenzake hata walio ACT ni wanafunzi wa YESU kama kina Petro, Mathayo na wengineo, hata Mama Maria picha zote hizo ni picha za wa act sinema tu.  Sasa watu wengi badala ya kumuangalia YESU katika roho sasa fahamu zao zimetekwa na shetani wanaziona picha za wa act sinema ndiyo YESU au ndiyo Mama Maria, Petro, Ibrahimu, Musa, Eliya. Na madhara ya kukaa na hizo picha ukutani na kuzibusu na makanisa na majengo yenye picha hizo yameunganishwa na malango ya kuzimu kwa sababu yule siyo YESU na watu wanamuita YESU.
Nawaeleza wala sura zao hazipo hivyo, hizo ni sura za wanadamu waliotegeneza sinema. Ni watu wengi wamepotezwa na imani zao kwenye hizi picha yamkini hata wewe usomae na hii ni katika ulimwengu wote, watu wanaziabudu picha za Brian na hata kuzitolea sadaka na kuzifanya ndiyo YESU, hiyo ni makosa, tayari umeabudu sanamu, hata kama ipo madhabahuni au kwenye madirisha ya kanisa. Ni makosa imeandikwa katika nyumba ya sala isikae sanamu yeyote. Sasa, hata hizo picha za waigizaji siyo sanamu? Na je kupitia picha hizo imani za watu wengi zimepotea na kufa, sababu ya kutokuwa na viongozi wa kiroho waliohai kiroho, wapo hai kimwili tu (viongozi vipofu).
Sasa elewa imetupasa kumuomba katika roho, alijua yeye yupo na sisi kiroho na siyo kimwili, ila atakuwa na sisi kimili katika ule mwisho na wale watakao ushinda uliwmengu. Usiweke tena imani yako katika picha za Brian (mwigizaji). Ndiyo maana YESU aliniambia watumishi hawasemi ukweli kuhusu yeye na kondoo wanapotea badala ya kuwa kondoo wake wanakuwa mbuzi pori, na yeye ni mchungaji wa kondoo na siyo mbuzi (YESU WA NAZARETI).
NOTE:
Picha zote za majina ya wana wa MUNGU waliopo mbinguni hakuna hata moja katika ulimwengu huu zote ni feki ni kwa jinsi ya mfano tu ila hata huo mfano siyo wa kweli, na ni machukizo kuziabudu picha hizo, na ukiziabudu au kuzisujudu tayari umeabudu sanamu.

NABII HEBRON.