Close

NINI MAANA YA KANISA KUTEKWA NA SHETANI



Ndugu msomaji wa makala ya Mtume Hebron, nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliyeketi katika mkono wa kuume wa MUNGU BABA aliyeumba vitu vyote akiwemo na wewe  aliyekuumba kwa mfano na sura yake na kusudi kubwa umwabudu yeye tu na siyo miungu mingine mfano masanamu, matambiko au kuviabudu vitu alivyoviumba yeye.
Leo napenda kukufungua ufahamu wako zaidi uelewe maana ya kanisa kutekwa na shetani, ni jinsi gani? Kwanza uelewe kuwa kanisa ni nyumba ya ibada au ni mtu ambaye ndani yake lipo hekalu la MUNGU. Kama vile YESU alipomwambia Petro ndani yako nalijenga kanisa ambalo hata milango ya kuzimu halitaliweza.
Kanisa lililotekwa na shetani ni makanisa yanayojiita kwa jina la YESU lakini yamekuwa kama boksi yapo (empty). YESU WA NAZARETI hayupo na kama hayupo lazima zipo sababu zilizomfanya YESU aondoke hapo na sababu hizo lazima ni mbaya na ni machukizo mbele za MUNGU na kwake pia, kwa sababu silo kanisa alilolijenga yeye na tunajua ya kuwa YESU alilijenga kanisa ndani ya Petro ambalo hata kuzimu na shetani hakukiweza.
Sasa lijue kanisa lililotekwa na utalijuaje? Maana haliandikwi kuwa limetekwa na shetani na pia utashangaa bado YESU anatajwa katika ibada zao lakini ni shetani ndiye mnayemuabudu. Njia kubwa ya kujua na pia ujue kama upo salama au na wewe upo kwenye kanisa lililotekwa na haujijui unafikiri unaenda mbinguni, kumbe hauendi;
a)    Kanisa linalofundisha kinyume na neno lilivyoandikwa katika biblia ambalo ndicho kitabu kitakatifu alichokichagua MUNGU ujue hilo limeshatekwa na shetani hata wanaosali hapo wameshatekwa ni mali ya shetani, sababu kuhani yale anayoyafundisha hayatoki kwa MUNGU ila yanatokea huko pasipojulikana yaani mungu asiyejulikana.
Biblia (Neno lililoandikwa ndani halijaandikwa na shetani, na ndiyo maana inaitwa kitabu kitakatifu, ina maana yaliyoandikwa ni maneno safi na salama aliyoyahakiki MUNGU aliyekuumba uyafuate na kanisa alilolijenga yeye kupitia mwanae wa pekee YESU WA NAZARETI). Nitaelezea kwa kifupi tu ila zaidi usome kitabu changu mimi Hebron (JINSI KANISA LILIVYOMKUFURU ROHO MTAKATIFU na MJUE YESU WA UONGO) zipo katika blog ya Prophet Hebron utaelewa zaidi.
Kanisa lenye YESU wa kweli hilo shetani haliwezi kuliteka au kuingia ndani yake na kuweka mafundisho yake na kuyachanganya na ya YESU WA NAZARETI, sawa sawa na kuchanganya mchanga na sukari= hiyo siyo sukari tena, au kuchanganya chakula na kinyesi= siyo chakula tena au uchanganye coke na pombe= haitakuwa coke tena. Hivi ndivyo kanisa 98% all of the world lilivyo, limeacha Neno asili kutoka kwa MUNGU aliyokileta na kuruhusu litumike. Wanadamu wenye kiburi na kumdharau MUNGU wakaingiza yao halafu wanayahubiri pamoja katika mapango ( naita mapango sababu) kama ni kanisa la YESU WA NAZARETI alilolijenga yeye lipo Neno lake 100% halichanganywi. Na mapango ni yanayojiita makanisa ambayo yanachanganya Neno la MUNGU na uongo, huu uongo ndiyo kinyesi wanacholishwa wana wa MUNGU pasipokujua wao na matokeo yake roho zao zinaangamia maana wameumbwa ili walishwe Neno takatifu na ndipo watapata afya ya kiroho.
Sasa shetani amewaingia na kukamata masikio yao na akawafundisha hayo ya tofauti na wao wakamsikiliza na kama wewe unamsikiliza yeye basi unaongozwa na shetani. Tazama hata YESU alipojaribiwa pale jangwani akakataa kumsikiliza shetani, yaani YESU angemsikiliza shetani na kutii yale aliyomueleza na yeye angetekwa na shetani ila yeye alikataa. Na hii ni mfano uliotakiwa uigwe na wakristo wote ila imekuwa kinyume. YESU alikataa kula kinyesi yaani maneno ya shetani na akawa salama mpaka leo. Hii ni technic ya hali ya juu iliyojificha na siyo rahisi ujue ila nimewafunulia siri hii watu wote wa ulimwengu huu. Mmrudie YESU na mkatae kulishwa vinyesi vya shetani, tena ukinai kabisa.
Vinyesi hivi ni kubatizwa tofauti na ubatizo aliouagiza MUNGU, na hata katika kitabu cha biblia haupo ubatizo wa maji ya kikombe, hivyo unapakwa kinyesi cha shetani na unanuka katika ulimwengu wa roho na hautamuona MUNGU sababu umeacha Neno lake ukalikubali la shetani, sasa utajiteteaje hapo mbele za MUNGU hauna ujanja. Tubu uokoke upya na ubatizwe kwenye kijito cha utakaso; maji yanayotembea. Hata kama ulibatizwa kwenye kisima kwa maji mengi hiyo ni kinyesi cha shetani, Neno linasema maji yanayotembea. Na yeye aliye njia ya uzima na kweli alibatizwa mto Yordani (njia aliionyesha) sasa hiyo njia nyingine imetoka wapi? Shetani. Sasa huko ndiko maana ya kanisa kutekwa na shetani.
Imeandikwa msiabudu sanamu, na MUNGU ameonya ila leo hii katika ulimengu huu ametajwa YESU na pia sanamu zipo= hii siyo YESU wa asili tena ni kinyesi.
Kubatiza wanadamu kwa jina la mchungaji badala ya YESU na ROHO MTAKATIFU na MUNGU BABA ni kinyesi wana wa MUNGU wanapewa au kwa maana nyingine ni sumu ya kuua hizo roho na wakishiriki mafunzo hayo tu tayari wamekufa roho zao na roho iliyokufa haiendi mbinguni ni jehanamu. Kama unashiriki mafundisho ya jinsi tofauti na biblia yakachanganywa na uongo tayari jijue umeshakufa kiroho hiyo ni sumu umelishwa.
Nilipokuwa naelezwa na YESU WA NAZARETI habari hizi nilishtuka sana nilipojua kumbe wote wanaoshiriki mafundisho yanayochanganywa na uongo kuwa tayari wamekufa kiroho, maana alinionyesha ulimwengu wote nikaona wengi mno wamekufa ni maboksi tu yanatembea ila ndani ni mauti imekaa badala ya uzima wake. Akaniambia usiogope, endelea kuifanya kazi yangu, nimekuonyesha uelewe zaidi, kumbuka nilipokuita ulikuwa wewe peke yako na mimi tu, haya ni baadhi ya yale niliyokueleza nimekufunulia uyaone. Akasema kwa sauti ya ukali; Hivi Hebron mwanadamu ni nani hata abadilishe Neno la MUNGU? Sikuwa na jibu, akasema Ole wao wamekuwa na kiburi cha shetani, jehanamu ndipo mahali pao. Akasema tena hawa watumishi wameujua ukweli kuhusu Neno lilivyoandikwa lakini hawasemi ukweli wanasema uongo wa shetani. Neno la MUNGU halibadiliki, halichanganywi, halibuniki na chochote, ameshalihakikisha. Ole wao, hayo mengine hajaniruhusu niyaseme. Hivyo zaidi ROHO MTAKATIFU akufunulie utayajua mengi kuhusu YESU na jinsi kanisa lilivyotekwa. Soma kitabu cha Nabii Hebron (JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI) na pia ingia katika YouTube ya Prophet Hebron usikilize jumbe alizonieleza YESU WA NAZARETI, nimetoa baadhi na hakika utapona.
NOTE:
Ili usife kiroho usiyapokee hayo maneno tofauti na biblia na ujitenge kabisa na madhabahu za jinsi hizo, maana ni makanisa ya kuua roho za wana wa MUNGU ili wasiende mbinguni na hata hao wanaofundisha uongo ni watoto wa shetani wanafanya kazi yake kumsaidia shetani awapate watu wengi na MUNGU awakose. Ila amesema haitawezekana, mwanadamu atashindana na MUNGU? Kumbuka Yona alishindana na MUNGU ila alifikia mwisho mbaya. Na wanaowapoteza wana wa MUNGU, kusema kweli mwisho ni mbaya. Uyakatae hayo mafundisho potofu ni kinyesi unapewa. Tena uone kichefu chefu uyatapike yakutoke na usiende katika ibada hizo. YESU amenieleza nikueleze ili upone.
HAPPY NEW YEAR 2014

NABII HEBRON.