Close

NINI MAANA YA MKRISTO JINA? NINI MAANA YA MKRISTO HEWA? NINI MAANA YA MKRISTO FEKI?

[ad_1]

BWANA YESU ASIFIWE, YESU anawapenda watu wote na anataka mumrejee hata sasa anasema mumrejee yeye sababu yeye ndiye njia ya kweli nay eye ndiye njia ya uzima, na pasipo yeye hakuna atakayemuona MUNGU. Nawaandikia waraka huu nikitamani niweze kuongea na wewe kimwili au ufike katika kanisa  langu nikueleze yale aliyonieleza YESU nikueleze na wewe, YESU ni mzuri sana anao upendo amabo hakuna aliye nao katika ulimwengu huu, pamoja na uwezo. Leo nitaelezea hayo machache sababu watu wengi ndivyo walivyo sasa ni bora kabisa ujielewe kama wewe upo katika hayo matatu wewe hauna tofauti na mtu anayeabudu miungu, mila au mpagani au asiyemjua YESU kabisa.
ILI UWEZE KUJIJUA AMA NI MKRISTO JINA, MKRISTO HEWA AU MKRISTO FEKI.
·        Kwanza unakua unajiita mkristo lakina haujaokoka wala kuzaliwa mara ya pili.
·        Unabatizwa ubatizo ambao YESU hajabatizwa mfano moja ya kikombe, maji ya kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji.
·        Unatenda maovu na unaenda kanisani mfano mlevi, mzinzi, mchawi na mengineyo.
·        Ni mtumishi ambaye ni freemason, ni mchawi, ni mfufua misukule, ni anayezini na kondoo, ni mtumishi anayechangisha pesa kanisani au mahali popote analazimisha watu wa pledge, ni mtumishi wa mshahara, ni mtumishi anayevaa kofia akihubiri, ni mtumishi anayeongoza kanisa na hajaokoka wala hajazaliwa mara ya pili, ni mtumishi aliyejiita, ni mtumishi anayetoa huduma za kiroho kwa kudai mpaka sadaka au malipo fulani. Ni mtumishi anayefanya ibada za wafu kinyume na biblia imekataa, MUNGU siyo wa wafu, kuabudu sanamu, busu misalaba, watumishi wanaotumia nguvu za giza na waliojiita, watumishi wote wanaoomba pesa kwa njia ya television, radio, internet hao ni wezi wanamfanya YESU yeye ni omba omba, hiyo ni dalili YESU mwenye utajiri hayupo nadni yao yupo yesu mnyang’anyi wa uongo. Afanyaye biashara haramu, mtumishi afanyaye biashara ya benki chaji riba, na mengineyo soma katika makala ya Nabii Hebron Tanzania utafunguka zaidi na utakaa vizuri ili uwe mkristo wa kweli na mwana wa YESU wa kweli.
Ni faida itakuwa yeye atakaporudi kulinyakua kanisa atakukuta na wewe ni mkristo wa kweli hivyo ile kweli yake ndani yako ataiona, ila akiona hayo matatu yapo juu yako hatakuwa na muda na wewe sababuumefanyika kuwa ni adui yake. Ufunuo wa Yohana 21:27, Ufunuo wa Yohana 22: 18-19.
BWANA YESU naomba unisamehe uniokoe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, namkataa shetani na mpinga kristo. Karibu ndani yangu weka kweli yako na mimi niwe mkristo wa kweli Roho wako mtakatifu aniongoze mpaka ule mwisho wangu nifike ulipo wewe na ukija kwa unyakuo usiniache. Amen.

NABII HEBRON.

[ad_2]