NINI MAANA YA UBATIZO WA KISIMA (SWIMMING POOL)??

[ad_1]

Ubatizo huu unaofanya watu wengi waone wamebatizwa yaani kuzamishwa kama vile YESU alivyoamuru lakini matokeo yake ni feki bado mtu anakuwa hajabatizwa kabisa, sababu ya kwanza maji hayatembei (siyo kijito cha utakaso) na pili hairuhusiwi kabisa kujenga kisima, halafu ubatizwe hapo tayari umelibadilisha neno la MUNGU na shetani anamwekea MUNGU bango la mashtaka hawa siyo wakristo ni mwili mmoja na mimi shetani kivipi endelea kufuatilia mafundisho ya Nabii Hebron yanayosema ukweli na uwazi mtupu ili kuwaongoza mataifa yote wamjue MUNGU wa kweli na siku moja wafike mbinguni ambapo mwanae alienda kuandaa makao na hata sasa makao yapo tayari ila hayana watu watakaoenda ni kidogo sana mpaka ni aibu hata kutaji idadi hiyo kwa siku ya leo, na ndio ninaogeza bidii kuwafundisha ili anayekubali na kubadilika apate makao mbinguni.
YESU alibatizwa katika mto unaotembea maji kijito cha utakaso na katika tendo la ubatizo ni la asili kutoka kwa MUNGU kwa kupitia umbaji wake wa asili mfano Jordan river, mto ulikuwa na asili ya MUNGU peke yake. Hivyo swimming pool, kisima, hivi  havina uhalisi wa MUNGU bali vina uhalisi wa        kazi za binadamu,mpaka hapa uelewe, kama ulibatizwa ubatizo wa jinsi hii ujijue bado mpaka sasa unayo dhambi ya asili na siyo mkristo, haijalishi unajiita mkristo na umeokoka, wokovu wako ni bure sababu kinachokuunganisha wewe uwe mwili mmoja na YESU ni ubatizo wa maji mengi yanayotembea. Na ujanja huu aliutumia joka kuu ili kuwapiga upofu watu waliokoka wakiri sala ya toba na katika kumalizia swala la kuunganishwa kuwa mwili mmoja akawatega na mafunuo tofauti ya kujijengea visima.
Ila katika kufundisha yeye aliyonituma YESU WA NAZARETI alinipeleka kuzimu akanionyesha kila kitu ambacho shetani anawategea watu ili wasiende mbinguni. Maana ya kila kisima kwanza kinachimbwa kinaenda chini, huko chini ni kuzimu hivyo mtu unapoingizwa katika kisima hicho linachoelekea chini kama vile shimo unakuwa unavuliwa vitu vyako vyote vinaenda kuzimu na unabakia empty kama vile boksi tupu. Hii ni njia ya shetani kuwateka watu kwa ubatizo wake kwa maji mengi. Pili na visima vyote ambavyo vimejengwa ndani ya kanisa, kisima hicho linatumiwa na shetani kama njia yake ya kufikia madhabahuni na ndiyo sababu kisima linachimbwa kuelekea chini. Utajiuliza mbona mto mto ni mrefu na unaweza ukazama unaelekea chini. Mto tofauti yake hauna mwisho na mto ni umbaji wa MUNGU peke yake (soma makala ya Nabii Hebron somo la ubatizo wa kikombe) nimeelezea utaona tofauti hapo. Hivyo hapo tayari ni feki, na pia wapo wachungaji ambao hapa ulimwenguni watu wanafikiri ni watumishi wa MUNGU wa kweli kumbe ni washetani. Ile huduma na nguvu anazopewa na shetani lazima afuate ubatizo wa kisima hayo ni masharti ili kuwapeleka watu kwa shetani, hapa ulimwenguni mtaona anahubiri biblia na ana onya dhambi, ila katika ulimwengu wa roho ni kinyume na mafundisho mnayoyasikiliza na kuyapokea yanawaua kiroho pasipo kujua. Sasa uelewe, mimi nasema ukweli na kweli itawaweka watu huru, imeandikwa atakayeongeza maneno ya kitabu cha MUNGU atahukumiwa au kuyapunguza. Sasa hiki kisima, swimming pool, tenki je hazijaongezwa kutoka katika biblia ya shetani, vikatae upone, ubatizwe upya.
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, uniandike katika kitabu chako cha uzima, uniongoze nibatizwe upya, maana nilidanganywa, asante kwa kujua ukweli wako, nishike mkono. Amen.

NABII HEBRON.

[ad_2]