SAFARI YA MBINGUNI ILIYO SALAMA NI HII HAPA!!!

[ad_1]

Safari ya mbinguni ni maandalizi ya kupata ticket au visa ya kwenda mbinguni, visa hiyo ni YESU WA NAZARETI peke yake tu yeye ndiye njia ya uzima na ukweli ya kumfikisha mtu mbinguni katika neno la MUNGU yaani biblia. Pia imeandikwa ni YESU peke yake ndiye njia ya uzima na ukweli (Yohana 14:6), au maana nyingine katika safari hauwezi kuingia katika ndege au basi bila ticket. Ukiingia kwenye basi unaulizwa ticket yako uliyokata na kama hauna hushushwa na kuachwa hivyo hivyo, na kwenda mbinguni bila kuwa na YESU WA NAZARETI tena wa kweli yaani yeye ndiye ticket original hauendi. Na ukiwa na ticket feki ya YESU pia utashushwa na kuachwa sawa sawa na vile vile kimwili ukiwa na ticket feki ya basi fulani utakapoitoa utakataliwa utaambiwa hiyo ni feki na unaachwa.
                                                                                          
Ukisoma katika kitabu cha Ezra 8:21, inasema “Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili upate kijinyeyekeza mbele za MUNGU, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.” Hii inamaana kuwa njia  iliyonyooka watu wanaitafuta iliyo salama maana pia  zipo njia za uongo au ramani za uongo zikitoa direction ya safari ya mbinguni na kumbe ni wrong direction.
Ndugu msomaji, funguka ufahamu wako sasa ili ujue njia iliyo sahihi na ticket za salama za kwenda mbinguni pakuzipata. Katika safari ya mbinguni ticket original hupatikana kwa watumishi aliowaita YESU na siyo waliojiita au kutamani tu kufanya pasipo yeye kuwatuma. Ni sawa sawa katika basi, ili upate ticket original utamuona agent au wakala wa basi hilo original ndiye atakayekupatia ticket sahihi, ukienda tofauti na wakala asiyejulikana au tajiri huyo atakupatia ticket feki na muda wa basi kuondoka wakati wa ukaguzi wakiangalia ticket yako, wakiikuta siyo original yao watakushusha na kukuacha na pesa umeshatapeliwa.
Kama watu ilivyo kimwili wanayokatiwaga ticket feki sehemu mbali mbali katika miji mbali mbali, hubakia kulia na basi limeondoka. Watu wengi wanafikiria wanaenda mbinguni. Nilipokuwa ninaongea na YESU WA NAZARETI katika maongezi yangu mimi na yeye na kunifundisha, akanielezea kuhusu ticket feki za mbinguni na original. Sasa nakuja katika kanisa, watumishi 98% all over the world is fake, agent of the wrong Jesus, utaniuliza kivipi? Nitaelezea sababu chache ambazo utazichunguza kimwili;
·        Watumishi wote walio freemason member (angalia kwa internet).
·        Watumishi wote wanaobatiza ubatizo ambao haupo kwa biblia na hata katika kisima, na pia kubatiza kwa kutumia majina yao (huo ndio ufeki na hayo mnayashiriki mkijua ndio ticket za mbinguni na kumbe siyo, hayo siyo maelezo yaliyopo kutoka kwa mwenye kuandaa safari hiyo yaani YESU WA NAZARETI. Soma katiba yake hayo hayapo, onyo hao ni feki wakala ni wezi wanaotumiwa na shetani kuiba roho za wana wa MUNGU kwa kuwapa ticket za kwenda kuzimu badala ya mbinguni. Watu wengi hata wengi waliokufa wanajuta na kusaga meno, muda mwingi walioupoteza makanisani mpaka kifo hawakupewa ticket original bali ni feki.
Kivipi? Mtumishi wa jinsi hiyo hata ile sala ya toba anayokuongoza haipokelewi kwa sababu yeye siyo wakala wake haijalishi anatumia jina la YESU.
·        YESU aliye njia ya uzima na ukweli mawakala wake yaani watumishi ndio wakataji wa ticket za watu kwenda mbinguni, mtumishi yeyote anyefanya maombi kwa pesa ujue huyo ni fake agent, kubusu misalaba ni fake agent maana hayo maelezo ya kuruhusu hayo yafanyike siyo ya YESU WA NAZARETI ni ya yesu wa uongo na ukiambatana na yeye na wewe unakuwa mwana wa uongo. Ufunguke ufahamu wako ili uipate ticket original ya YESU WA NAZARETI. Sasa hivi 98% ya watumishi wote katika ulimwengu wote ni fake, na hii inaonyesha picha halisi jinsi walivyowapa watu wengi ticket feki na hawaendi mbinguni.
·        Mtumishi yeyote anayetoa stika zake na kuipiga saini yake halafu anawaambia watu inayo nguvu za MUNGU, huyo ni feki. Amekupa hirizi pasipo wewe kujua na hali yako itakua mbaya siku zote mpaka ufunguliwe na uichome. Hata stika zenye mikono ya watumishi zitupe, kupitia ile mikono ya stika zao inaiba uchumi wako, unaenda kwao. Au nieleze kirahisi ni jini chuma ulete.
·        Mtumishi anayechangisha pesa za harambee, au kukopa benki pesa kwa ajili ya kujenga kanisa, hayo yote siyo maelekezo ya mwenye ticket original ya mbinguni ni maelekezo ya mawakala feki ambao hajawaita wala kuwatuma bali kazi yao ni wizi tu wa mali za wana wa MUNGU. Kama ilivyo kimwili mawakala feki wa mabasi huchukua pesa na kukupa ticket feki na kukuacha umechanganyikiwa, haujijui, hivyo ndivyo ilivyo wakristo 98% katika ulimwengu hawaendi mbinguni pasipokujua.

Leo funguka, toka huko utajuta ule mwisho, kanisa limetekwa na shetani, na shetani amewatumia hawa hawa mawakala wake kuwapofusha watu wasubiri safari njema ya mbinguni. Siku ile YESU atakuambia sikujui sikujui wewe, ataangalia moyoni mwako je? Aliyekuongoza sala ya toba ni wakala wake? Ataangalia, akikuta ni safi utaenda, akikuta ni feki utatupwa motoni milele. SOMA VITABU VYA NABII HEBRON JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI, MKRISTO USIKUBALI KUWA MPUMBAVU, na watu wote katika ulimwengu huu msikubali kuwa wapumbavu mbele za MUNGU, muwe wajanja kama alivyo YESU. Chunguzeni ticket zenu, waliowaongoza sala za toba na mikao yao je inafanana na toba za YESU, ukikuta tofauti ujue umeangamia. Fanya haraka utafute mtumishi wa kweli aliye na YESU wa kweli akuongoze sala ya toba iingie ndani ya moyo wako tena original.
NOTE:
YESU anasema anawapenda wale wote wamtafutao kwa bidii na hakika watamuona, ila 98% all over the world bado hawajamuona yeye, je? Ni wewe? Jichunguze.

NABII HEBRON.

[ad_2]