SALA YA BABA YETU ULIYE MBINGUNI WAKRISTO WAITUMIA KUABUDIA MIUNGU!!!

[ad_1]

KIVIPI? SOMA


Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI, ambaye ndiye mwana wa MUNGU wa pekee na aliye hai mpaka leo. Mwana wa MUNGU huyu yeye ni mwana wa MUNGU na yeye siyo mwana wa miungu, na pia watu wengi mnajua ya kuwa yeye ni mwana wa MUNGU na alitoka kwa MUNGU akaja duniani kimwili na akarudi kwa BABA yake mbinguni. Aliponiita YESU na kunituma niukomboe ulimwengu, aliniambia ulimwengu umepotea, Hebron mwanangu wanadamu wanaona wapo sawa sawa ila hawapo sawa sawa kabisa na hii ni sababu niliwaita watumishi nao wamenisaliti na niliwaita watumishi wachache sana, na siyo kama unavyowaona wengi katika ulimwengu huu, wala mimi siwajui. Wapo wanaojifanya, wapo waliojiita, wapo wa mishahara na wapo walionisaliti, hawa wote ni wana wa shetani na mimi siyo BABA yao, hao wanaye baba yao ambaye ni shetani, na kama hawa wanaye baba yao ambaye ni shetani basi hata hao watu wote wanaowaongoza wanapelekwa kwa shetani.
Hebron akaniita YESU kwa jina langu, muda wangu wa kurudi umekaribia lakini sina furaha sababu shetani ndiye anao watu wengi katika ufalme wake na MUNGU ni kidogo sana. Kwa jinsi nilivyoona mimi juu ya idadi kwa siku hiyo kwa hesabu ya kibinadamu ni kama vile kila bara lina watu 20000 tu ambao majina yao yapo mbinguni ambao waliokuwa hai. Sasa ukigawanya figure hii kwa mahesabu ya jumla za nchi katika bara moja utakuta nchi zingine zina watu 500 tu na wengine 100 tu na nyingine 2000. Hii figure inatisha sana, na hii ni dalali ya kuwa injili inayohubiriwa katika ulimwengu wote kwa kiasi kikubwa siyo injili ya kweli au ni injili inayohubiriwa na watumishi ambao YESU hawajui na hawana YESU WA KWELI niwanafiki tupu wanaotumia jina la YESU kutafutia pesa na kunyanganya watu mali zao wakitumia jina la YESU na kumfanya YESU aitwe ni mnyang’anyi wengi ni wachawi, freemason. Muwe makini figure hii inatisha niliogopa sana, akanieleza kazi zao ni bure tu, wanawafungia watu wasije kwangu wakati wao wenyewe hawajui kwangu. Sasa sikiliza amua leo upya nikuongoze sala ya toba maana 90% ya sala zote za toba katika ulimwengu wote ni feki anayekuongoza unapokiri katika ulimwengu wa roho jina lako linaandikwa katika kitabu cha ufalme wa shetani ambacho anacho kristo wa uongo ambaye ndiye yesu wa uongo. Unashikiliwa hapo pasipo kujua, ila kama unashikiliwa huko leo unatoka utakapokiri sala ya toba.
YESU alipokuwa hapa uliwenguni, aliwafundisha wanafunzi wake jinsi ya kusali (Mathayo 6: 9-13) basi ninyi salini hivi, BABA yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama mbinguni. Utupe leo riziki yetu, utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amen.
Sala hii inayo nguvu kubwa sana kwa jinsi ukiyaangalia hata maneno yake au watu wengi mnaijua na hata mmeikariri na hata makanisani watu husali sala hii wakijua sala yao imesikilizwa na MUNGU aliye hai na kumbe imepokelewa na miungu, na ndiyo maana wakristo wamekuwa wakoma wa kiroho wala hawabadiliki ni sababu sala zao hazijaenda mbinguni bali zimeenda kwa miungu na bado hata mtakaoendelea katika maneno ambayo nitaifundisha bado na wewe utakuwa upo kwa miungu na umeabudu miungu pasipo kujua wala kupenda. Katika sala ya BABA yetu uliye mbinguni, inasema BABA yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe, sasa wewe unayekiri hivyo katika kanisa ulilopo wanaabudu sanamu, au ubatizo wa maji mengi ya kikombe, au kipaimara, kubusu misalaba, mnafanya ibada za wafu, mnafanya kanisa ni soko, harambee tu na michango katika nyumba ya sala. Je niwaulize kama yanafanywa hayo katika kanisa, je hayo ndiyo BABA yetu aliye mbinguni ameruhusu, na je ndiyo mapenzi yake, na je ndiyo nguvu yake na Baraka zake zipo katika mambo hayo?
Sasa mfunguke ulimwengu wote hapo watu walipigwa upofu wakiamini wakiitaja sala hii sala yao itafika mbinguni. Kumbe imekuwa kinyume unamtaja MUNGU katika madhabahu ambazo hazina uhusiano kabisa na yeye kimatendo na unaitumia sala hii katika kanisa ambalo linavunja mapenzi ya MUNGU na kuweka mapenzi yake ambayo hata katika kitabu cha biblia ambacho ndicho katiba kimekataza mambo haya. Sasa kama kimekataza mambo haya ya nini uyafanye hayo ambayo siyo ya MUNGU bali ni ya miungu, halafu unayatenda ya miungu unamuita MUNGU ndiye BABA yako. Hapo umejidanganya, baba yako wanakuwa ni miungu sababu unayatenda ya miungu, mfano unaabudu wanafunzi wa YESU, nyota, mwezi au viumbe alivyoviumba MUNGU na yeye ameonya aabudiwe yeye peke yake, ambao wanao umoja MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU basi, hayo mambo mengine unayoyatenda au kushiriki tayari na wewe unakuwa baba yako ni miungu. Na zaidi utakuwa unajipigia makelele tu na ndivyo ilivyo katika ulimwengu wote, watu wanapigwa upofu na sala hii ikitumika makanisani wakiamini ipo katika biblia ni ya MUNGU, na hata wakiabudu sanamu sala yao itafika. Nikueleze hakuna uhusiano wowote au shirika kati ya MUNGU na sanamu, au matendo yaliyokinyume na MUNGU umshirikishe MUNGU.
Sasa tazama ni mabilioni ya watu wanamkiri miungu ndio baba yao na inawezekana wewe ni mmoja wao. Jichunguze unaposali sala hii kama kanisa halipo sawa sawa na Neno la MUNGU hata kama sehemu nyingine inasema kweli na sehemu nyingine haliendi sawa sawa na Neno la MUNGU, na wewe umeshajua sasa MUNGU hachanganywi, mambo yake ni BLACK AND WHITE yamenyooka. Mfunguke shetani amewateka mabilioni kupitia sala hii maana katika structure ya shetani ametengeneza mfumo huu, ili kuwapiga upofu ili waabudu miungu badala ya MUNGU aliye hai pasipo kujua sasa elewa. Na zaidi cha ajabu wanafunzi wa YESU walikuwa wameokoka na ukishaokoka ndipo unafanyika kuwa mwana wa MUNGU sababu jina lako anakuwa nalo katika kitabu chake mbinguni. Sasa shetani akayapiga makanisa upofu na watumishi wake. Makanisa watu ambao hawajaokoka ndiyo wwanaosali sala hiyo ya BABA yetu uliye mbinguni kuliko sehemu yeyote katika ulimwengu huu.
Hata mimi nilifundishwa katika kipaimara lakini nilikuwa sijaokoka, hata wazazi wangu tulikuwa tunasali sala hii na hatujaokoka. Asante YESU WA NAZARETI unayenifundisha wewe ni mwalimu wa waalimu nakupenda sana, nilipoteza muda kusali sala hii kumbe sikuwa hata mwana wa MUNGU na hata sasa wengi hawajaokoka kumbe siyo watoto wa MUNGU bali ni watoto wa miungu, fungukeni mataifa yote, okokeni na mtoke huko hizo ni sehemu za miungu wala hawatamuona MUNGU huo ni ukweli, mmedanganyika hata mimi nilipotea, sasa naijua njia ya uzima wa milele na nyie ifuateni. Soma makala ya Nabii Hebron, YouTube, fuatilia vipindi vya Television na vipindi vya redio kila wakati utapona, na pia karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, utapona roho yako na utakuwa wana wa MUNGU na siyo wa miungu tena.
NOTE:
Ili uwe na kibali cha kumuita MUNGU ni BABA yako lazima uokoke, unapokuwa haujaokoka halafu unataja sala ya BABA yetu uliye mbinguni, ujue unajiunganisha kwa miungu haijalishi mnalitaja jina lake.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NAOMBA UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA ILI UWE BABA YANGU NA MUNGU WANGU, NAJITENGA NA miungu PALE NILIPOKIRI SALA YA BABA YETU ULIYE MBINGUNI KABLA SIJAOKOKA, NIONGOZE NIFUNGUE MACHO NA AKILI YANGU ISHIKE YESU WA NAZARETI NITAWALE WEWE SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU. AMEN.
Karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, utafunguliwa roho yako na mengi atakutendea bure, pasipo malipo yeyote, yeye anao upendo, yeye siyo maskini ila kristo wa uongo ndiye mnyang’anyi, maskini na atesaye watoto wa MUNGU makanisani. Uwatumie na wengine ujumbe huu wasome watoke kwa miungu. Usiogope.
NABII HEBRON.

[ad_2]