Close

TAIFA TEULE ISRAEL SASA KUANZA KUREJEA KATIKA NCHI YAO

[ad_1]

 TAIFA TEULE ISRAEL SASA KUANZA KUREJEA KATIKA NCHI YAO
Ndugu msomaji wa blog hii ninakusalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazarethi, aliye hai, BWANA wa Mabwana, Mfalme wa Wafalme, wala hakuna zaidi yake.
Leo hii unabii wa wana wa Israel kurudi Israel umetimia, kuanzia tarehe 11-02-2013 majira ya saa kumi na mbili jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki (Tanzania).
MUNGU amewafungua Waisraeli wote, na sasa watarudi na kukusanyika na pia watamwamini kama BWANA na mwokozi wa mataifa yote. Aliyekuwa amewafunga hata wakamkataa YESU na kumuita siyo Mfalme wa Wayahudi sasa akamatwa kuzimu na kuwaachia na sasa mtashangaa wakianza kurejea nchini kwao kama ilivyotabiriwa na kuanza kuja Tanzania, ambayo ndiyo Edeni ya sasa aliyoichagua MUNGU. Mtakapoyaona hayo, msishangae; mjue ni YESU wa Nazarethi ndiye anayeyafanya na hakuna wa kuzuia.
Nitakueleza kwa kifupi tu kuhusu huyu mfalme wa Wayahudi aliyekuwa kuzimu ni nani? Huyu ni mzimu wa Wayahudi wa kizazi cha kwanza, uliokuwa unamilikiwa na shetani na joka kuu, ulipewa nguvu na joka kuu yaani baba yake shetani ili kuwazuia Wayahudi wasiwamini YESU na kumkubali, na pia swali hili watu wengi wamekuwa wakijiuliza sana, kwa nini walimpinga; Ndugu msomaji, mahali popote na nchi yoyote, leo hii jibu umelipata . Ile roho imetolewa ya kumpinga, na sasa wataokoka na kwa spidi kubwa na nchi ya Israel itainuliwa sana kiuchumi na kijeshi kuliko ilivyo hivi sasa. Ni MUNGU amesema, na mimi naitoa kama alivyoniambia; sipunguzi wala siongezi neno langu.
NOTE:
Unabii wote nilioutoa soma katika blog hii, umeshaanza kutimia, na lazima utimie wote. Ni YESU mwenyewe yupo kazini, msishangae mnapoona mabadiliko, hata katika viongozi wa kanisa. Walio watumishi freemason watakufa wote ulimwengu mzima na wengine wataiacha hiyo kazi kwa ajili ya kuogopa kifo.
Miaka 1000 (elfu moja) ya utawala wa YESU umetimia, aliye na sikio na asikie asema BWANA wa majeshi, MUNGU wa Ibrahimu na Isaka. Mtayaona matukio yasiyo ya kawaida, anakuja kulichukua kanisa lake yaani wateule tu.
Ujumbe huu nimekufikishia wewe mimi Nabii Hebron.

[ad_2]