TANZANIA NDIYO EDENI YA SASA

TANZANIA NDIYO EDENI YA SASA

[ad_1]

UTANGULIZI:
Ndugu msomaji, nakusalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti, ambaye pia ndiye BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, wala hakuna mwingine aliyewahi kutokea zaidi ya huyu. Huyu ndiye MASIHI wa MUNGU aliyeuumba ulimwengu wote ikiwamo wewe mwanadamu au kwa kukuelewesha watu wengine wanamtambua kwa kumuita Nabii ISSA kwa itikadi za dini zao! Na ndiye Nabii atakayekuja ile siku ya mwisho kuchukua waliomwamini yeye na kutenda matendo matakatifu na kufuata sheria zake sawasawa na neno la MUNGU linavyosema. Nabii huyu, kwa yeyote asiyemwamini hakika hatamchukua, atawachukua wale tu waliomkubali, na wale waliomkataa yeye atawakataa na mahali pao ni kwenye shimo la moto milele.
Natumaini mpaka sasa umemuelewa vizuri huyu YESU. Ewe mwanadamu, unayeishi mahali popote , kwa rangi yoyote na jinsia yoyote, nakushirikisha ujumbe huu, ni wa YESU sio mimi Hebron, mimi ninatii na kufikisha ujumbe sawasawa na anavyonieleza, siongezi neno, wala sipunguzi. Watu wote mumrudie YESU wa Nazareti ili mpone. Muda wake umetimia kurudi, mtaangamia. Muda na siku yake kurudi sijui, ni siri ya MUNGU tu, hata YESU haijui ila amenifunulia ya kuwa ni muda wowote. Yote aliyoyasema kupitia manabii wake katika kitabu kitakatifu yametimia. Imebakia muda na siku, uwe makini na tengeneza njia yako na yeye; ukweli 100% hakuna mtu yeyote anayekufa bila kumpokea YESU anakwenda Paradiso. Nimewaona mabilioni ya watu ambao hawajaokoka na pia waliookoka ambao hawakuwa wakweli na watakatifu walivyokuwa hapa ulimwenguni wanateseka sana! Ilikuwa ni November 2012. Hii ilikuwa ni kwa bara la Afrika, watu wote wanaokufa kwa siku moja kuanzia miaka 13 kuendelea, ni watu 15 tu, ndio wanaenda Paradiso. Niliogopa sana, inatisha watoto wenye umri kuanzia wakiwa tumboni mpaka umri wa miaka 12 ndio wanapokelewa bila tatizo, akaniambia YESU hao wengine wanavuna walichopanda kwa shetani (mfano wakilima mahindi, watavuna mahindi). Ukipanda dhambi, utavuna dhambi. Ukipanda mema, utavuna mema.
Kwenye mabara mengine hakuniambia, ila hali ni mbaya sana, hata kwenye mabara yaliyosalia, shetani ameliteka kanisa 98%. Imebakia 2% tu ulimwenguni mwote na zaidi, baadhi yao, ni watumishi wamemsaliti YESU 45% ni wachawi kiwango cha juu sana na 53% wengine hawajielewi wanafanya nini japo wapo waliojiita, waliojifanya, na wengine wameiacha Injili ya YESU, wengine freemason – hawa ndio viongozi vipofu wanaotumiwa na shetani kuwaangamiza wanadamu na ndio manabii wa uwongo (utawatambua kwa matendo yao). Imebakia 2% tu ya watumishi wa MUNGU wanaosema ukweli na kutumiwa na YESU KRISTO wa Nazareti aliye hai. Hii ni kwa ulimwengu wote! Ujumbe huu ni kweli 100% hata na wewe chunguza ndipo utajua ukweli kamili.
YESU KRISTO WA NAZARETHI ASHUKA NCHINI TANZANIA NA KUIFANYA NDIYO EDENI.
Ujumbe huu kwa mara ya kwanza, YESU aliniambia kuhusu Tanzania, sikumuelewa, kwa maana kibinadamu niliona labda kapenda kuiita  tu kwa jina na siyo Edeni, yaani bustani ya MUNGU mwezi wa tatu 2011. Alinieleza mambo mengi ya kufundisha kuhusu Edeni, na pia kuhusu nchi ya Tanzania. MUNGU aliiumba kwa kusudi lake yeye mwenyewe na alijua itafika wakati ndipo itageuka na kuwa Edeni, na haya yote ni kwa utukufu wake. Akaniambia, MUNGU alipomuumba mwanadamu alimuweka katika bustani ya Edeni (soma 2:4-14, Mwanzo 13:10) na Edeni wakati huo MUNGU alikuwa akishuka sana katika bustani na kusema na kuongea na mwanadamu, ila baadaye, ile bustani iliyokuwa katika upande wa mashariki pakatokea machafuko na nchi hiyo, hata pale MUNGU alipoichoma kwa moto yani Sodoma na Gomora. Ukisoma katika nyaraka za Mwanzo 13 yote, utaelewa vizuri. Hapo ndipo sura ya Edeni ilipotea na mpaka sasa imebakia jina tu, ila hayo yaliyokuwepo kwenye bustani hayapo tena, yaliungua wakati wa Sodoma na Gomora, ila kwa sasa YESU alivyoniambia ndivyo ilivyo na imekwisha kuwa na haitabadilika, na sasa ni yeye ndiye ameishikilia nchi hii na hakuna  ufisadi utakaofanyika na yote maovu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wabaya, atawafichua na kuwashughulikia peke yake. Atatumia watu na viongozi baadhi yao! Atauinua uchumi juu sana, na ndio taifa lililo tajiri kuliko yote ulimwenguni na kutagunduliwa madini ya thamani sana na yasiyopatikana nchi yoyote, ila anawaandaa Watanzania waweze kufanya wenyewe maana baadhi ya nchi ziliiba utajiri wa Watanzania na vitu vingi ambavyo siwezi kumaliza kueleza, ila kuanzia April 2012 ameanza YESU mwenyewe na hii yote ni maandalizi ya ujio wake na siku ya ujio wake kimwili atashukia Tanzania, ila sasa anashuka katika ROHO. Nilimuomba ashuke kimwili katika maongezi, akaniambia, nikishuka kimwili ulimwengu wote na milima itakuwa tambarare, kwa hiyo ni mpaka ile siku, ila natumia mwili wako kufanya maandalizi ya ujio wangu. Alisema kwa sauti ya uchungu, niliowatuma 98% wamenisaliti wananitaja tu midomoni ila ndani ya mioyo hawapo na mimi. Hadi watoto wake wanateseka na kuteswa na shetani. Akasema, sitakubali, ardhi itaongea, milima na kila kitu. Lazima watu wakombolewe. Hawaambiwi ukweli kuhusu mimi, sikuwatuma kufanya hivyo! Nimewapa bure, mtoe bure. Baraka za MUNGU hupewa bure, ila fomula ya shetani lazima ulipe. Akasema, amani ya Tanzania imeletwa na MUNGU, na siyo mwanadamu, watu wamshukuru MUNGU, ni mkono wake, ndio umezuia.
Kuhusu Tanzania, miundombinu yote itakuwa kwa haraka na pia muda si mrefu atafungulia petroli, gesi, na baadhi ya madin;i amefunika yasionekane mpaka atakapoamua yeye. Kilimo na viwanda vimeshafufuliwa kwenye ulimwengu wa roho na muda si mrefu, utayaona kimwili. Air Tanzania imesharejeshwa uthamani wake na uliibiwa na na shirika lililopo hapa Tanzania, na litaporomoka kwa sababu waliihujumu nchi, na kila mahali iwe ni nchi  au mtu binafsi aliyeihujumu nchi hii, ataporomoka, na ni YESU peke yake ndiye anafanya kazi hiyo katika bustani yake, yaani Tanzania.
Jeshi la Tanzania limeinuliwa juu sana nao watagundua baadhi ya silaha ambazo hazijaonekana ulimwenguni humu na wameshapewa hekima, japo hawajui, ila niliona wakipewa kila kitu. Nchi hii baadaye itakuwa ni nchi ya kifalme.
Nchi hii kuhusu Muungano kuvunjika hiyo ni ndoto. Haitakuwepo milele, wanaofanya kutumika kuvunja muungano waache wataadhibiwa na YESU! Akaniambia, haki ataifanya peke yake, maana ni mali ya MUNGU ila wapo mataifa wanaochochea vurugu; zimerudishwa kwao na mtayaona kwa macho ya mwili.
Ndugu msomaji, nimekujulisha kijuu juu tu, ila sikuruhusiwa na MUNGU kuyaeleza kwa watu wengine, hayo mengine ni kwa ajili ya nchi hii, na waliopata ujumbe wakadharau, hiyo ni shauri lao na MUNGU. Mimi kazi yangu ni kutoa na kutimiza tu, hayo mengine ni MUNGU mwenyewe.

Kupitia Edeni (Tanzania) mataifa yatapona, na viongozi wa nchi wataponywa na watu wao (kwa wale watakaotii).  Na nchi yoyote atakayonituma YESU, nayo itaponywa na watu wake, uchumi utainuka, yale yote yaliyoshindikana yataisha, hata nchi zenye vita ikifika wakati, kitendo cha kukanyaga tu, vita ni mwisho!

Ni YESU ndiye yupo ndani yangu, anayefanya kupitia mwili huu aliouumba yeye! Hakuna atakayeweza kuniua, kunizuia nisiseme ukweli kuhusu YESU, na ndivyo alivyoniambia. Ninao ulinzi kuliko mtu yeyote ulimwengu huu, nipo kwenye mkono wa MUNGU. Alichoniambia; niwapende, niwasaidie, niwaombee na niwaelekeze anavyotaka. Endelea kusoma ujumbe kwenye vitabu vya ujumbe wa Nabii Hebron, utayajua mengi.
Kuhusu nchi nyingine pia, YESU anazipenda, na tarehe 5.11.2012, ndio miaka 1,000 (elfu moja) ya utawala imeanza. Soma Ufunuo wa Yohana 20:1-3.
Ujumbe wa YESU kwa ulimwengu wote
Neema ya MUNGU ikufungue ufahamu
MUNGU zidi kuibariki Tanzania na yote kuhusu kuifanya Edeni yaonekane sasa. Amen.
Mtume na Nabii Hebron akiwa katika kazi ya utalii ambo alifanya kama Professional Driver Guide, kabla ya kuitwa na MUNGU kufanya kazi yake.
Mtume na Nabii Hebron akiwa katika moja ya safari zake katika mbuga za wanyama. Kabla ya kuitwa na MUNGU alikuwa akifanya kazi katika sekta ya utalii akiwa kama Professional Driver Guide.




 Kwa mawasiliano;

+ 255 759 610 820
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149


Email:

[email protected]


Imeandaliwa na Priscus & Dorcas Macrine,

KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

[ad_2]