Close

UBATIZO WA WATOTO WADOGO – MWISHO

[ad_1]

UBATIZO WA WATOTO WADOGO – MWISHO
MARKO 11:27-33

UJUMBE WA YESU KWA WATU WOTE WA MATAIFA YOTE:


Ujumbe huu mimi Hebronna kufikishia wewe kama alivyonielezea na mimi nina tii. Ujumbe huu ni kwa watu wote walioumbwa na MUNGU anayejulikana ambaye nimezisoma habari zake katika kitabu kitakatifu yani Biblia, MUNGU ambaye yeye ndiye anayeijua misingi ya dunia hii na yeye ndiye aliyeiweka, yeye aliyeumba mtu pamoja na wewe  iwe unampenda au humpendi ila atabakia kuwa MUNGU tu na kama humpendi ina maana ndani yako wewe unampenda shetani.

Ujumbe huu ameniambia tarehe 25.09.2013, muda wa saa nane mchana  majira ya saa za Africa Mashariki, Arusha Tanzania, mahali nilipokuwepo.

Ameniambia Hataki kusikia tena watoto wadogo wanabatizwa  ubatizo wa Mungu asiyejulikana, ikiwa ina maana kwa ubatizo ambao hajaugiza BABA yake, pia ubatizo ambao hata yeye  hakubatizwa  na maji ya kikombe, Alibatizwa ubatizo wa maji mengi ambao ndio ulioagizwa na MUNGU anayejulikana.

Wanaobatiza hivyo hao siyo wa MUNGU anayejulikana ni wa Mungu asiyejulikana yaani ( Baali) na mlio batizwa  ubatizo huo umeshakabidhiwa kwa shetani kwa kupigwa chapa ya  namba 666.

Soma Makala yangu Hebron katika blog yangu ya tarehe 26.09.2013. Utaelewa vizuri jinsi YESU alivyonieleza na utapona ukipenda maana siyo watu wote watakaopona ila ni wale watakaolifanyia  kazi na kutokushiriki hata ibada hizi na nyumba zao za sala, hii ni picha halisi wanamwabudu Mungu asiyejulikana, na wewe ukishiriki unakuwa hivyo hivyo, ila upone Toka utengwe nao utapona.

Wewe chunguza utaujua ukweli ( pia soma kitabu changu cha Nabii Hebron utaelewa zaidi. ( UBATIZO WA KWELI  KWA ULIMWENGU WOTE).

MATHAYO 18: 6-7, Na yeyote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo waaminio afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake na atupwe baharini (hao wanaowabatiza watu ubatizo tofauti Mathayo 18: 6 -7 inawahusu.

ONYO:  ONYO hili nalifikisha kama alivyonielekeza YESU wa Nazareti ambaye pia ndie Baba yangu,  watakao sikia wasikie watakao puuza au kutokusikia wasisikie asema BWANA WA MAJESHI.

Wote mnao batizwa ubatizo wa maji ya kikombe na watoto wadogo, hamtauona ufalme wake ambaye yeye YESU ndiye njia  ya uzima na ukweli, msikilize yeye tu ndio salama, usishiriki mafundisho ya uongo, sasa hivi watumishi 98% katika ulimwengu wote siyo watumishi wake, wengi ni wachawi, freemason, watumishi wakujiita, na pesa tu, na wengine ni wafanya mazingaubwe wa shetani.

Hii ni kwa mitume, manabii, wachungaji, wainjilisti, walimu. Wanaojiita kwa jina lake.Hakuna cha kujitetea tena, soma Biblia kuhusu ubatizo na vitabu vyangu  na pia endelea kusoma blog yangu  Hebron  ataujua ukweli zaidi hautakuwa kipofu, utauona mwanga na gizalitaondoka.


  • UBATIZO  KWA WATOTO  WADOGO – STOP

  • UBATIZO WA KIKOMBE – STOP


Nabii Hebron  kwa niaba ya YESU wa Nazareti
Nimetumwa  kwako ujumbe huu.

[ad_2]