UCHAGUZI MKUU KENYA 2013

[ad_1]

UCHAGUZI MKUU WA KENYA 2013

Nawasalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazareth aliye hai, BWANA WA Mabwana, MUNGU wa Miungu, ambaye ndiye MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Ndugu Wakenya, MUNGU anawapenda sana. Niliyajua haya nilipowekewa mizigo moyoni mwangu kuombea nchi ya Kenya, hasa ni katika uchaguzi mkuu 2013. Wananchi wa Kenya, kwa rangi zote, makabila yote, na watu kwa jinsia zote; nyie wote ni yeye kawaumba na nyie ni mali ya MUNGU, na MUNGU anawawazia mema na siyo mabaya, ila shetani anaiwazia mabaya nchi yenu. Ila, mkitii haya niliyoelezwa na MUNGU, shetani atashindwa kuleta machafuko katika uchaguzi wa mwaka 2013.
MUNGU ameniambia watu wote na vyama vyote anawapenda sana, japo nitaendelea kuiombea tu ili kusudi la MUNGU lisimame. Watoto wa MUNGU, kuhusu suala la uchaguzi haswa la Urais, muombeni MUNGU awape kiongozi ambaye MUNGU ndiye atakayewapa awaongoze. Yeye anamjua yupi atawaongoza vema, na atakuwa mwema na mwenye hekima, YESU akaniambia, watu wanaomba tu kama wanavyotamania, ila siyo MUNGU anavyotaka na madhara ya kuomba unachotaka, utapewa ila usimlaumu MUNGU. Ila mkimuomba wape kiongozi wa kuongoza mzuri hakika atawapatia, hivyo baadhi wanaomba kwa kumpenda wanayemtaka, ila hawajui ndani ya moyo atafanyaje. Muache ukabila, kabila zote ni za MUNGU, nay eye ndiye muasisi wa lugha zote, wekeni ukabila mbali muwe na umoja, upendo na mshikamano. Nyakati hizi ingieni kwa maombi, mwachieni MUNGU awape rais yeye, hii ni siri ya MUNGU, japo ninajua kila kitu na matokeo ya uchaguzi wa nchi hii ila sijaruhusiwa kutamka.
Ujumbe:
Muombeni yeye awachagulie kiongozi mwema, maana wengine ndani yao hawaiwazii mema nchi, ila yote MUNGU ameyaona, na ameniambia kanisa lijipange upya kwa kumuomba MUNGU awape kiongozi kutoka kwake na si vinginevyo, na yeye atafanya. MUNGU ibariki Kenya, wafungue fahamu zao wale wasiojielewa kuhusu uchaguzi 2013.

[ad_2]