Close

Ujumbe wa maandalizi ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO

Ujumbe wa maandalizi ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO

[ad_1]

Ndugu msomaji wa blog hii, nakusalimu katika jina la YESU KRISTO ambaye ni BWANA na mwokozi wa mataifa yote.
Kwanza kabisa napenda kukukaribisha na kushiriki nawe neno la MUNGU alilompa Mtume na Nabii Hebron akueleze wewe msomaji wa blog hii upate kufahamu kweli ya MUNGU na ufunguke ufahamu wako. Katika siku hizi za maandalizi ya siku kuu ya kukumbuka kuzaliwa kwa MASIHI yaani Krismasi.
Neno ambalo MUNGU amempa Nabii ili likufungue nyakati hizi ni kutoka katika kitabu cha Marko Mtakatifu 11:20-26 
20  Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani.
21  Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.
22  Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.
23  Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
24  Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
25  Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
26  Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu
MUNGU anataka tusamehe. Kama hatujasamehe ni bure, hatutajibiwa maombi. Shetani anatuwekea mabango ya mashitaka kwenye ulimwengu wa roho kwa sababu, shetani anajua maadiko (usiposamehe, na wewe hutasamehewa). 
Faida za kusamehe:
MUNGU anakupigania
MUNGU anajibu maombi yako
Hasara za kutokusamehe:
Usiposamehe na MUNGU hakusamehi
Kutokusamehe kunazuia baraka zako
Usiposamehe, MUNGU anakuacha
Usiposamehe, ROHO MTAKATIFU anakuacha na MALAIKA wanakimbia.
Maana ya mtini kukauka:
Ni kwa sababu haukuzaa matunda, na haukuwa na faida, kwa hiyo lolote lisilozaa lazima likaushwe.
ONYO
Kanisa limeonywa wasisikilize nyimbo za MUNGU zenye mitindo ya bolingo au zenye midundo ya miziki ya kidunia, kwa sababu zina uvuvio wa kuzimu na zinakunajisi uzisikilizapo. Pia, nyimbo za mitindo ya ngoma za asili, tusisikilize maana zina najisi, zote zina asili ya kuzimu.

Nabii Hebron akifundisha kwa makini NENO kuhusu mtini uliovyolaaniwa na kukaushwa kwa NENO la YESU.

MATUKIO:

Mtini ambao ni Mapepo ndani ya dada huyu, ulikaushwa kwa NENO la MUNGU la leo kama linavyojieleza hapo juu, na alifunguliwa vifungo alivyokuwa akitumikishwa papo hapo. Tukio hili lilijiri katika ibada ya leo jumapili tarehe 09/12/2012.

Dada huyu akikatwa mzizi wa mtini ndani yake, ambao ni majini na mapepo, yaliyotesa na kusumbua ndoa yake kwa muda mrefu, lakini leo imekuwa mwisho wa mateso hayo baada ya Mtume na Nabii Hebron kutumia NENO la MUNGU kama YESU alivyolaani ule mtini, na ukakauka, ilikuwa vivyo hivyo kwa dada huyu kuachwa huru dhidi ya majini na mapepo hayo yaliyokuwa yakimtesa.

MENGINEYO

Picha nyinginezo wakati Mtume na Nabii Hebron na baadhi ya watumishi wa HUDUMA YA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE walipomtembelea baba wa kiroho Askofu Moses Kulola, mwanzoni mwa wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam.

Moses Kulola, alimzaa Mtume na Nabii Hebron katika mkutano wake uliofanyika jijini Arusha mwaka 1998, na Nabii huyu alikaa muda mrefu sana bila kumjua, na MUNGU alimficha kwa kipindi kirefu hadi MUNGU alipomfunulia Nabii Hebron na kumwambia kuwa, huyu ndiye baba yake wa kiroho. Kabla Nabii Hebron hajaonana naye, Mzee Kulola alishamjua na kumuona kiroho na kujua sura yake na alithibitisha alipomuona na alimbariki na kumfurahia sana, naye Mtume na Nabii Hebron alimfurahia sana baba yake wa kiroho mzee Moses Kulola.

Mtume na Nabii Hebron pamoja na mke wake Nancy, wakiwa na baba wa kiroho aliyemzaa Nabii Hebron
Mchungaji Dorcas na Mwalimu Dorcas Macrine wakiwa na baba wa kiroho
 
Moses Kulola akiongea jambo na Mchungaji Dorcas

PICHA NYINGINEZO:

  Kwa mawasiliano;

+ 255 759 610 820
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149

Email:

Imeandaliwa na Priscus & Dorcas Macrine,

KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

[ad_2]