Close

UNABII KUHUSU NCHI YA TANZANIA AMBAYO NDIYO EDENI YA SASA


1.   KUHUSU MADAWA YA KULEVYA NA BIASHARA HARAMU
2.   JESHI LA TANZANIA, USALAMA WA TAIFA
3.   UCHUMI WA NCHI HII.
Ndugu msomaji na mwananchi  mwenye nia njema juu ya nchi ya Tanzania pia hao wasio na nia njema  juu ya nchi ya Tanzania, nchi hii sasa hivi siyo ile Tanzania iliyokuwaga watu wanafanya uovu kwa jinsi wanavyotaka hata kuangamiza maisha ya watoto wa MUNGU na hawajulikani sasa hivi siyo tena nchii hii kama  nilivyowajulisha kupitia vipindi vyangu  vilivyorushwa katika redio Mlimani ya Dar es Salaam, Afya redio ya Mwanza,Moshi Fm ya Kilimanjaro na Sunrise redio ya Arusha.
Wengi waliniona nazungumza nisichokijua, nilisema madawa ya kulevya hayatapita tena katika viwanja vyetu vya ndege na watakamatwa wote na sasa mmeyaona. Kazi hii ni YESU wa NAZARETI ndiye  anayeifanya na sio kwa uwezo wa mwanadamu. Maana aliniambia YESU nchi  haiwezi kuinuka kiuchumi  wakati wanaotakiwa wauinue uchumi ndio wanaodhoofishwa na  kuangamizwa.
Hawa wauzaji hadi sasa wanashangaa imekuwaje wanaumbuka na wanapatikana, watu hawa walikuwa wamejizindika kiuchawi na zaidi kutoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa juu ila huu ndio mwisho,  uchawi haufanyi kazi tena katika nchi hii na bado yapo mengi  nitayasema atakaponituma YESU niyaseme.
Hiyo yote ni MUNGU ndiye amefichua uovu huo na hata jeshi la Tanzania limeinuliwa juu sana pia na usalama wa Taifa. Wala hakuna atakayeweza kuwauwa watumishi hao wanaofichua uovu maana wameshikwa mkono na YESU  na wapo imara wamewezeshwa na YESU wa Nazareti. Haya ni baadhi ya mambo  niliyoyasema kuhusu unabii wa Tanzania na sasa mumeyaona.
Nilisema  mwaka 2012 mawaziri wataachishwa kazi na mafisadi au wanaoibia pesa nchi hii watatajana na mliyaona. Sasa hivi uchawi haufanyi kazi nchi hii ipo mikononi mwa YESU. Maana YESU hauzi madawa ya kulevya , waliotumia jina lake kufanya uovu watafungwa jela wote na mtaona .
Inachosha jina la YESU kutukanwa na kutumiwa kama kivuli cha kutendea uovu. Muda sio mrefu  mtaona Air Tanzaniaikiwa na ndege nyingi. Na yote niliyoyasema mtayaona  na baada ya sakata la madawa ya kulevya, ni mafisadi wataibuliwa kwa njia wasiyoijua ni bora warudishe hizo pesa kwenye benk za nchi hii mapema. Njia za MUNGU sizo za mwanadamu na mipango yake na njia zake  hufichika , hazijulikani ni siri yake.
NOTE:
Polisi msiogope MUNGU anawalinda hakuna kitakachowadhuru, mawaziri wote, wabunge, makatibu, na watendaji wote. Pia hata Rais songa mbele usirudi nyuma. YESU AMESEMA HAMTADHURIKA NA LOLOTE. Amewashika mkono. Na  ninaendelea kuwaombea.
Nabii Hebron.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.