UNABII KUHUSU TANZANIA BARA 2014

[ad_1]

By Nabii Hebron.
Nawasalimu kwa jina la mwenyezi MUNGU aliye hai na siyo mungu mfu ambaye hajulikani na wala hajaumba chochote na hana chochote katika ulimwengu huu. MUNGU wa kweli ndiye BABA yake YESU WA NAZARETI, ambaye alikufa na kufufuka na katika ule mwisho ndiye MUNGU aliyemchagua kuja kuuhukumu ulimwengu na kwa jina lingine wanamwita Nabii Issa.
Leo tena ninawajulisha yale yatakayotokea Tanzania Bara 2014, kama nilivyokwisha kuwaeleza miaka miwili iliyopita mtaona mabadiliko katika uchumi, gesi itapatikana, na madini yatarudishwa kwa wananchi wa nchi hii na baadhi ya Mawaziri watatolewa katika uongozi wa serikali hii na mmeyaona yametimia na mengine mengi aliyonieleza YESU kuhusu kuiinua nchi hii sasa inajulikana zaidi, maana ilikuwa imefungwa kipepo na watu wenye nia mbaya kuhusu nchi hii.
Tokea 2012 nchi hii MUNGU ameishika kwa mikono yake mwenyewe na ataibadilisha kila siku apendavyo yeye na akaniambia Tanzania ndiyo Eden ya sasa. Viongozi wote wenye nia mbaya katika serikali hii na hata katika vyama vya siasa hawatadumu watajikuta kila wakati wakiondolewa katika uongozi na kukataliwa na Bunge, wananchi, na ni MUNGU ndiye afanyaye hayo nab ado ataendelea. Naelezea machache tu ambayo ameniruhusu niyaseme, hayo mengine mpaka kwa wakati wake.
Na pia bandari ya Dar Es Salaam itakuwa ndiyo bandari bora na kubwa kuliko zote kwa upande wa bahari ya Afrika mashariki mwa Bara la Afrika. Ndege tayari shirika limefufuka la ATC, RELI na pia mafuta ya petrol yapo Tanzania tena mengi sana, ila mpaka atakapotaka YESU ndipo yataonekana ili Watanzania wenyewe wafaidike, na siyo wezi wasio na nia njema katika nchi hii.
Nchi hii sasa hivi, kila kiongozi katika eneo lolote atende haki, na asitumie uchawi. Endapo atakuwa kinyume na haya niliyoeleza hata dumu katika kazi atatolewa, na mwaka huu 2014 uovu utafichuliwa zaidi na ni YESU mwenyewe ndiye afanyaye hayo.
·        Upande wa Mawaziri bado wengi watatolewa tena. Mtakapo yaona msiogope mjue ni YESU yupo kazini kuitengeneza nchi.
·        Watumishi waliomsaliti YESU wataporomoka mpaka zero.
·        Watumishi wanaotumia nguvu za shetani watakufa vifo vibaya kimwili.
·        Watumishi wanaouza madawa ya kulevya watajisema wazi wazi na Usalama wa Taifa MUNGU amewainua sana, watafanya kazi nzuri sana, na mtasikia ni mengi yalikuwa hayajulikani watayakamata, wataongozwa na YESU tena pasipo wao kujua. Hawatalogeka, hongeka, danganyika.
·        Mwaka 2015 katika uchaguzi viongozi wengi watalia machozi maana hawatapata tena nafasi katika nchi hii ya kuiongoza, na wote watakaotumia uchawi hawatapata nafasi na hata wakiiba kura, hawataishi.
·        Pesa zilizoibiwa za nchi hii zilizopo huko katika nchi za nje zitarejeshwa nchini, MUNGU ndiye atakaye yafanya hayo yote wala hakuna kitakacho pingika, akisema niamesema.
NOTE:
Yapo mengi sana katika nchi hii na mengine yatakuwa ni mabaya zaidi kwa jinsi wanavyochelewa kutii ujumbe wake na taarifa wanazo.  Kwa sababu ya viongozi kukaza shingo ngumu kumtii MUNGU na ujumbe wake kwa ajili ya nchi hii. Muonapo hayo yakitokea msiogope mjue ni MUNGU mwenyewe, ila wakitii ujumbe wake kila kitu kitakuwa salama. Maneno haya nimeelezwa na MUNGU peke yake na mimi nayaandika kama alivyonieleza, namtii BABA yangu na MUNGU wangu. Na mengine nitayatoa kila akiniruhusu maana ujumbe huu siyo kutoka kwa Nabii Hebron, ni MUNGU mwenyewe.
SOMA website ya Prophet Hebron www.prophethebron.blogspot.com na pia angalia video za Prophet Hebron kwenye YouTube.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
NABII HEBRON.

[ad_2]